Chimbuko La Watumwa Weusi

Sasa tumeona msimamo wa Uislamu kuhusu utumwa, hebu ngoja tuuangalie Ukristo na wafuasi wake, na tuone wali- fanya nini kuhusu suala hili. Inashangaza kuona kwamba Wakristo, ambao kwa sababu wanazo zijua wao, siku hizi wanajifanya kama mabingwa wa uhuru wa mwanadamu, kumbe wao ndiyo mawakala wa dhahiri na watetezi wakubwa wa mfumo huu wa utumwa. Walivumbua falsafa na uthibitisho wa kimaadili, kama sababu za kuwafanya watumwa watu “wasio staarabika.” Mojawapo ya hoja zao ni kwamba walikuwa wana waokoa watu hao (watumwa) kutoka kwa majirani zao wanaokula watu hapa duniani, na kutoka kwenye fedheha ya daima milele baada ya uhai wa hapa duniani.

Uislam na wafuasi wake kamwe hawakuwa na fikira kama hizo. Wingi mno wa maandiko ya Kiisilamu hauna kitu kama hicho, kutokana na aina hii ya jitihada ya uadilishi wa kusikitisha. Lakini waandishi wa Kikiristo kila mara hutaja biashara ya utumwa kama vile wao hawakuhusika kwa vyovyote vile na tatizo hili, na kwamba ni Uislam ndio ambao “ulihimiza na kuhalalisha utumwa” ambapo wao, Wakristo, kila mara walijaribu kukomesha mpango huu mbaya sana! Haya ndiyo maelezo ya waandishi wa Kikristo.

Ni jambo la kuvutia kuona kwamba wakati wanapo zungumzia kuhusu biashara ya watumwa ya Afrika ya Magharibi ambayo ilifanywa kikamilifu na Wakristo peke yao, waandishi na wanahistoria wa Kikristo, wameipa biashara hii jina la “West African Slave trade,” Yaani biashara ya utumwa ya Afrika ya Magharibi au “Atlantic Slave – Trade” yaani biashara ya utumwa ya Atlantic, lakini wanapotoa maelezo kuhusu suala hili kwa upande wa Afrika ya Mashariki, hubadili maneno na kuandika “Arab Slave Trade” yaani biashara ya utumwa ya Waarabu.

Ukristo, kwa kutumia propanganda ya udanganyifu wa jinsi hii, umefaulu kwa kiwango kikubwa kupanua uwanja wa athari zake miongoni mwa Waafrika ambao humo umeweka mkakati wa propaganda yake na wanafurahi sana lakini hawatambui ukweli kwamba makanisa ya Kikristo yalikuwa washiriki wenye bidii sana kwenye “African Slave Trade” (biashara ya utumwa ya Kiafrika). Sura zifuatazo zitaonye- sha picha ya kweli kwa wasomaji.

Mnamo mwaka wa 1492, ambapo Columbus, akiwakilisha ufalme wa Hispania aligundua “New World” (Dunia mpya), alianzisha mfululizo mrefu na mchungu wa ushindani wa kimataifa katika kujipatia makoloni, ambao hadi sasa baada ya karne nne na nusu, hakuna suluhu iliyopatikana. Ureno, ambayo ndio iliasisi kitendo cha kujipanua kimataifa, ilidai hizo nchi mpya kwa hoja ya kwamba zilikuwa kwenye eneo la madaraka ya amri ya baba mtakatifu (papal bull) wa 1455 inayowaruhusu wareno (ambao ni Wakristo) kuwafanya watumwa wapagani wote.

Katika kujaribu kuepuka ubishani, mamlaka hizi mbili, zilitafuta suluhisho, na kwa sababu zote zilikuwa katika madhehebu ya Ukatoliki, zilimwelekea Baba Mtakatifu – hatua ambayo ilikuwa ya kawaida na ya mantiki katika kipindi ambapo madai ya wakati wote ya Kipapa yalikuwa bado hayana upinzani ama kutoka kwa mtu binafsi au serikali ya nchi. Baada ya kuchunguza kwa makini madai ya washindani, Baba Mtakatifu, katika mwaka 1493, alitoa mfululizo wa amri za kipapa ambazo ziliweka mipaka ya kuaua kati ya makoloni yanayomilikiwa na dola hizo mbili za Ulaya: Mashariki ilichukuliwa na Ureno na Magharibi ilichukuliwa na Hispania. Mgawanyo huo, hata hivyo, haukukidhi matege- meo ya Ureno na mwaka uliofuata washindani hao wawili walifanikiwa kuhitimisha mwafaka wa maridhiano zaidi kwenye Mkataba wa Tordesillas ambao ulirekebisha uamuzi wa Baba Mtakatifu kuiruhusu Ureno kumiliki Brazili1 kama koloni lake.

Lakini maamuzi haya hayakuweza kuzifunga mamlaka zingine ambazo zilikuwa zina wania kunyakua makoloni mengi iwezekanavyo; Uingereza, Ufaransa, na hata Uholanzi zilianza kudai sehemu zao (makoloni) hapa duni- ani. Mtu mweusi, pia, alikuwa apate sehemu yake, licha ya kwamba hakuomba; ilikuwa uanzishwaji na upanukaji wa mashamba makubwa ya miwa, tumbaku na pamba ya ulimwengu Mpya.

“Kwa mujibu wa Adam Smith, maendeleo ya koloni jipya yalitegemea jambo moja rahisi la kiuchumi- ‘ardhi pana yenye rutuba.’ Hata hivyo, umiliki wa makoloni wa Uingereza hadi 1776, kwa ujumla unaweza kugawanywa katika aina mbili. Aina ya kwanza ni wakulima wadogo wanao jitosheleza na kushughulika na uchumi wa bidhaa mbalimbali.

Aina ya pili ni koloni ambalo limesheheni hali iwezeshayo mtu kuzalisha bidhaa kuu mbali mbali kwa wingi kwa madhumuni ya kuuza nje. Katika aina ya kwan- za, yalikuwemo makoloni ya Kaskazini ya bara la Marekani; katika aina ya pili, yalikuwepo makoloni ya tumbaku na visiwa vya miwa vya Caribbean. Kwenye makoloni; ardhi na mtaji havikuwa na manufaa bila ya kuwepo nguvu kazi ya musuli. Kibarua, lazima awepo wakati wote na lazima afanye kazi, au ahimizwe kufanya kazi, katika kundi moja.

Bila ya sharti hili, kibarua angeamua kuwa na mwelekeo wake binafsi na kufanya kazi katika ardhi yake mwenyewe. Hadithi moja inasimuliwa mara nyingi kuhusu kabaila mmoja wa Uingereza, Bwana Pell, ambaye alichukua pauni za Kiingereza elfu hamsini (50,000) na vibarua mia tatu akaenda nao kwenye koloni la Swan River huko Australia.

Mpango wake ulikuwa kwamba vibarua hao wangefanya kazi kwake, kama iliyvokuwa Uingereza. Bwana Pell akawasili Australia ambapo ardhi ilikuwa pana sana vibarua wakapendelea kufanya kazi kwenye mashamba yao madogo kwa manufaa yao kama wamiliki wadogo, badala ya kufanya kazi chini ya kabaila kwa kulipwa ujira. Austaralia haikuwa Uingereza, na kabaila huyo alibaki hana mtumishi wa kumtandikia kitanda au wa kumchotea maji.”2

  • 1. Williams, Dk. Eric, Capitalism and Slavery (London, 1964) P. 4.
  • 2. Ibid uk. 4-5