Zoezi – Siku 30

Njia yako ya kwanza ya mkato ni ile Takbir (Allah-u-Akbar) ambayo unaitamka kabla ya kuanza Swala yako. Hii ni ishara kwa akili yako kwamba sasa umesimama mbele ya Mola wako, Mwenye nguvu zaidi katika ulimwengu huu. Unalazimika kuukubali ukweli kwamba umesimama mbele ya Allah (s.w.t.) na Yeye anakutazama wewe.

Imam al-Sadiq (a.s.) anasimuliwa kwamba alisema: “Unaposema, Allahu Akbar, tweza kila kitu kilichopo kati ya anga ya juu na ardhi, ukiviona vyote chini ya Utukufu Wake, kwa sababu kama Allah (s.w.t.) ameangalia ndani ya moyo wa mja wakati anapoitamka Takbir, na akaona ndani yake kitu kinachopingana na Takbir yake, Yeye angesema, ‘Ewe muongo wee! Unanidanganya Mimi?

Kwa Uwezo Wangu na Utukufu Wangu, Nitakunyima wewe (muonjo) utamu wa kunikumbuka Mimi, na Nitakuondoa kutoka karibu Yangu na kwenye kupata furaha kutokana na maombi yako.”’ (Mustadrak al-Wasa’il, Mlango wa 2, Hadithi ya 9)

Uahidi kutamka SUBHANALLAH 5 kila wakati unapochanganyikiwa kwa dhahiri na ulichukue wazo hilo linalokuchanganya kwa sekunde chache. Deni hili ni lazima lirudiwe (kulipwa) kwa mara nyingi unapochanganywa na wakati wowote unapoweza kulipa deni hilo. Madeni yote yalipwe TU wakati wa hali ya Rukuu au Sajida.

Kwa mfano, wakati unaposoma Suratul Hamd, kisha unapata kugeuzwa mawazo mara mbili za dhahiri kabisa, basi katika Rukuu yako inayofuata, utalipa deni la SUBHANALLAH 10 kwanza na kisha uendelee na kusoma dhikiri ya kawaida ya Rukuu. Kama hilo wazo linalopotosha linapata kujitokeza wakati ukiwa kwenye Tashahud au Salaam, basi utalipa deni lako mara baada tu ya kukamilisha Swala yako.

Tahadhari

Deni hilo hapo juu na SUBHANALLAH vinakuwa sehemu ya Swala yako na unapaswa kuweka nia kabla na wakati wa Swala yako ya desturi.

Deni linapaswa kulipwa pale tu ukiwa katika hali ya kuinama (rukuu) au Sijida, nyongeza zaidi ya hapo, vinginevyo, itaifanya swala yako kuwa BATILI na iliyo tanguka, hata kama Swala yako ni iliyopitwa na wakati na sio Swala ya wajibu.

Kwa vyovyote vile, unazo Rukuu 4 na Sajida 8 katika Swala ya rakaa nne, za kuweza kulipia madeni unayodaiwa. Usizingatie ni mara ngapi unapata kugeuzwa mawazo wazi wazi kwa vile utatambua juu ya jambo hili pale linapotokea, na utalipa deni lako ndani ya Rukuu au Sajida inayofuatia.

Utaitumia kwa jumla amali hii wakati wote katika Swala yako ya rakaa 4. Baada ya kukamilisha ibada yako, utakumbuka ni mara ngapi imekubidi kurudia zile SUBHANALLAH 5 na ni mara ngapi imekupasa kulipa. Sasa unaahidi kusoma ASTAGHFIRULLAHA RABBI WA ATUBU ILAYH – 5 kwa kila deni.

Kama umelipa madeni 10 wakati wa swala yako, hii ina maana kwamba utasoma ASTAGHFIRULLAHA RABBI WA ATUBU ILAYH mara 50 mara tu baada ya kukamilisha Swala yako.

Sasa utaonyesha kwenye chati yako ile idadi ya mara ngapi ulipaswa kulipa deni wakati wa Swala yako, mara 5 au 10, au pengine 3. Huu ndio mwisho wa ZOEZI.

Tahadhari

Mazoezi hayo hapo juu ni zoezi tu la kuongeza umakini wako na halina dhima yoyote katika Swala yako ya wajibu ya kila siku.Vilevile, zoezi hili bila hisia nzito wakati wa Swala na kwa bidii zaidi tu baada ya Swala yako – kwa maana kwamba kama utamakinika sana katika deni, basi unaweza ukajikengeusha mwenyewe kutoka kwenye lengo kuu.