Sura Ya 32: Matukio Ya Mwaka Wa Tatu Hijiriya

Mwaka wa tatu wa hijiriyya ulianza na mapambano madogo madogo na vita vilivyotawanyika, zenye sura ya kujihami na zilizopiganwa kwa lengo la kukomesha njama za makabila ya wenye kuyaabudu masanamu katika hatua ya mwanzo kabisa. Hata hivyo, vita vya Uhud vyastahili kuzingatiwa mno miongoni mwa matukio ya mwaka wa tatu. Vita hivi ni mfano ung’arao wa kuihami dini takatifu ya Uislamu, itikadi ya upweke wa Allah na uhuru wa kuabudu.

Haitafaa hata kidogo kuipa jina la ‘Vita’ au ‘Ghazwah’ ile mihanga waliyoitoa Waislamu, kwa sababu hawakupanga wao kupigana vita bali walilazimika kuzishika silaha kwa ajili ya kuuhami Uislamu tu na kuhakikisha ya kwamba unapatikana uhuru wa kuabudu.

Waliwarudisha nyuma baada ya kuwatia hasara kubwa, wale watu waliokuja kutoka Makka na sehemu za jirani yake kuja kuushambulia mji wa Madina ili kuwaangamiza wenye kumwabudu Allah na watafutaji wa uhuru, na Waislamu hawakuwa na lolote jingine la kufanya isipokuwa kuwajibu wadhalimu katili na watesaji kwa jeshi na silaha kali.

Sababu Za Vita Ya Uhud

Mashambulizi ya pamoja yaliyofanywa na wenye kuabudu masanamu yalikuwa ni matokeo ya nyororo ya visababisho vya ndani na vya nje vilivyolileta jeshi kubwa mjini Madina ili kulipiza kisasi.

Mtu mmoja hatari sana aliyekuwa akiitwa Ka’ab bin Ashraf ndiye aliuwasha moto huu. Alikuwa Myahudi kwa mama yake, lakini yeye mwenyewe alikuwa muabudu masanamu. Alikuwa akiufaidi ulinzi wa Dola ya Kiislamu na hakupatwa na dhara lolote kwenye Vita vya Badr, lakini kutokana na uadui aliokuwa nao dhidi ya Mtume wa Uislamu (s.a.w.w.) alikwenda Makka na akamiminikwa na machozi ya mamba kwenye mikutano ya Waquraishi na kuwakumbusha jinsi machifu wao walivyouawa na kutekwa. Aliudhihirisha ubingwa kwenye kazi hii kiasi kwamba wazee na vijana wa Waquraishi wakawa tayari kwenda kupigana na Mtume (s.a.w.w.) na kuiangusha serikali ya Kiislamu.

Ili kuziibua hasira za watu wa Makka, Ka’ab aliusifu uzuri wa wanawake wa Kiislamu kwa jinsi ambavyo watu wa Makka wote waliidhihirisha nia yao ya kwenda kupigana dhidi ya Waislamu ili waweze kuwashinda na kuwateka wanawake wao na kuzitosheleza tamaa zao mbaya. Vile vile aliziimba beti fulani fulani za tenzi zihusianazo na jambo hili na ndani ya beti hizo aliweka bila ya aibu yoyote yale majina na maelezo ya wanawake fulani na kuwaeleza kwa maelezo yasiyo ya adabu njema juu yao. Baada ya kutekeleza mpango wake alirejea Madina na kukimbilia kwenye ngome yake.

Nini jukumu la Mtume (s.a.w.w.) na Waislamu kuhusiana na mtu huyu aliyeibua hasira za watu? Aliuwasha moto ambao miali yake iliwachoma hadi kuwa majivu askari mashujaa wa Uislamu sabini akiwamo Hamza, na ukasababisha kutiririka kwa damu ya wacha Mungu katika ardhi ya Uhud.

Watu wa kabila la Aws waliamua kuwaondolea Waislamu ufisadi wa Ka’ab. Watu wawili waitwao Muhammad bin Maslamah na Abu Naa’ilah waliwasili kwenye ngome yake kwa kujifanya marafiki na wakamlaumu Mtume (s.a.w.w.) na dini yake.

Waliongezea kusema kwamba tangu kufika kwa Mtume mjini Yathrib watu wote wamekuwa wakizungukwa na misiba na watu wao na mali zao vimeangamizwa. Wakaikuza mno maudhui hii kiasi kwamba Ka’ab akafikiria kwamba maoni yao juu ya maudhui ile yalikuwa sawa na yake. Kisha wakasema: “Sasa tumekuja kununua nafaka kutoka kwako na tunalazimika kuweka rehani kitu fulani, kwa sababu hivi sasa hatuna pesa.”

Ka’ab alikubali kuwauzia nafaka, lakini kuhusu kile kitu cha kuweka rehani, alitamka maneno yaliyodhihirisha tabia zake mbaya na chafu, kwa kuwa alitamka tena bila ya aibu, hivi: “Ni lazima wanawake na watoto wenu wabakie kwenye mamlaka yangu kwa njia ya rehani.” Maelezo yake yaliwashitua mno hawa watu wawili kiasi kwamba walimjibu wakisema: “Je, yawezekana?”

Kusema kweli watu hawa wawili hawakutaka kununua nafaka. Walirudi na kuunda makri ya kumwua. Hivyo basi, mara moja waliomba waziache silaha zao kwake ili ziwe kama dhamana. Lengo lao la kuomba hivyo lilikuwa kwamba, watu hawa wawili wenye silaha watakapoiendea ile ngome yake atadhania ya kwamba wamekuja kuziacha silaha zao kwake ili ziwe rehani na wala sio kwamba walikuwa wamepanga mpango mwovu dhidi yake.

Wakati wa usiku kikundi cha watu wa Aws wenye silaha walijikusanya kuizunguka ngome yake, wakijifanya kwamba wamekuja kununua nafaka. Muhammad bin Maslamah, aliyekuwa ndugu wa kambo wa Ka’ab alimwita Ka’ab, lakini mkewe alikataa mumewe asitoke nje kwenye giza la usiku, lakini kutokana na yale mazungumzo ambayo Ka’ab alikuwa tayari kaishayafanya nao, alitoka nje ya ile ngome kwa matumaini kamili wala hakuwa na shaka yoyote kutokana na kuwa kwao na silaha. Baada ya kumzunguka, walielekea kwenye bonde, kana kwamba walikuwa wakienda kuonyesha bidhaa au kwenda kuichukua.

Walikuwa bado hawajakwenda mbali zaidi kutoka kwenye ile ngome wakati wale watu wa Aws ghafla walipomvamia na kumkata vipande vipande. Kwa njia hii adui hatari, mpelelezi fisadi na mtu mwovu, ambaye tamaa yake kuu daima imekuwa ni kuwapiga pigo Waislamu, aliondolewa kutoka kwenye njia yao.

Mara baada ya kuuwawa kwa Ka’ab Myahudi mmoja aitwaye Abu Raafi, aliyezifuata nyayo za Ka’ab na wakati mmoja alikuwa pamoja naye kwenye jambo la upepelezi na uchochezi, naye aliuawa. Ibn Athir ameliandika tukio hili kwa kirefu kwenye historia yake.1

Waquraishi Waamua Kuzikabili Gharama Za Vita

Mbegu ya maangamizi na ghasia ilikuwa tayari imeshapandwa mjini Makka kwa kipindi kirefu hivi. Kule kupigwa marufuku kuwaomboleza waliouawa Badr kuliimarisha hisia ya kulipiza kisasi. Kufungwa kwa ile njia ya kibiashara ya watu wa Makka kupitia Madina na Iraq kumewafanya wakose raha kabisa. Ka’ab bin Ashraf aliongeza mafuta kwenye moto huu na kuuwasha.

Kwa sababu hii, Safwaan bin Umayyah na ‘Ikrimah bin Abu Jahl walimshauri Abu Sufyan kwamba, kwa vile machifu na askari wa Waquraishi wameuwawa kwa ajili ya kuhami msafara wa biashara wa Makka, ingalifaa kwamba kila mmoja wa wale waliokuwa na mafungu ya bidhaa zilizokamatwa katika msafara wao ule atoe fungu kwa ajili ya kuzikabili gharama za vita. Mpango huu ulipata idhini ya Abu Sufyan na ukatekelezwa upesi sana.

Machifu wa Waquraishi waliokuwa wakiitambua nguvu ya Waisilamu na kwa karibu zaidi wameuona ushujaa wao na kujitolea mhanga kwao kwenye Vita vya Badr, waliona kwamba ingalifaa kumkabili Muhammad kwa jeshi lililotayarishwa vizuri lenye watu wa makabila mbalimbali walio mashujaa na wenye uzoefu.

Amr bin Aas na mwengineo walitumwa kwenda kuonana na watu wa makabila ya Kinanah na Saqif na kuomba msaada wao. Walishauriwa waende wakawaalike mashujaa wao kupigana na Muhammad wakiwa wanazo silaha za kutosha kabisa, na kuwaahidi kwamba gharama za vita na mahitaji yoyote ya safari ile zitalipwa na Waquraishi.

Baada ya kufanya kazi vizuri walifaulu kuipata huduma ya baadhi ya watu mashujaa wa makabila
ya Kinanah na Tahaamah na katika kutayarisha jeshi lenye watu elfu tatu hadi nne kushiriki
kwenye vita vile.2

Tuliyoitaja hapo juu ni idadi ya wanaume tu walioshiriki kwenye vita vile, na kama idadi ya wanawake waliokuwapo pale inajumlishwa, basi idadi itaongezeka. Haikuwa desturi miongoni mwa Waarabu kuwachukua wanawake na kwenda nao kwenye uwanja wa vita lakini safari hii wanawake nao walishiriki kwenye vita hivi pamoja na wanaume. Mpango wao ulikuwa kwamba wanawake hawa wapite katikati ya safu za vikosi, wakipiga dufu, kuwahamasisha kulipiza kisasi, kusoma beti za tenzi na kutoa hotuba za kuhamasisha.

Wamewaleta wanawake pamoja nao ili kwamba njia za askari wanaokimbia kwenye uwanja wa vita ziweze kufungwa, kwa sababu kukimbia kutakuwa na maana ya kuwaacha wasichana na wanawake watekwe na maadui, na hisia za ushujaa za Waarabu zisingaliweza kuvumilia kulitenda jambo hili la fedheha.
Idadi kubwa ya watumwa walijiunga na jeshi hili la Waquraishi kutokana na ahadi za kutamanisha walizopewa. Wahshi bin Harb alikuwa mtumwa Mwethiopia wa Mut’am. Alikuwa na ustadi mkubwa wa matumizi ya mkuki naye alikuwa kaahidiwa kupewa uungwana kama akimwua yeyote kati ya watu wakuu watatu wa Uislamu (ambao ni Muhammad, Ali au Hamza). Kwa kifupi, baada ya kufanya kazi kwa juhudi mno, walitayarisha jeshi lililokuwa na watu mia saba waliovaa deraya, elfu tatu wapanda ngamia, askari wapanda farasi mia mbili, na kundi la askari waendao kwa miguu.

Taasisi Ya Upelelezi Ya Mtume (S.A.W.W) Yatoa Taarifa

Abbas, baba yake mkubwa wa Mtume (s.a.w.w.) ambaye kusema kweli alikuwa Mwislamu lakini alikuwa bado hajaitangaza waziwazi imani yake, alimwarifu Mtume (s.a.w.w.) ile mipango ya Waquraishi. Aliandika barua aliyoitia saini yake na akaifunga, kisha akampa mjumbe wa kabila la Bani

Ghifaar na kuichukua ahadi yake kwamba ataifikisha kwa Mtume (s.a.w.w.) ndani ya muda wa siku tatu. Yule mjumbe aliileta ile barua iliyofungwa kwa Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa kwenye bustani moja nje ya mji wa Madina na akampa barua ile baada ya kutoa heshima yake kwa Mtume (s.a.w.w.). Mtume (s.a.w.w.) aliisoma barua ile lakini hakuyataja yale yaliyomo kwenye barua ile kwa masahaba zake.3 Allamah Majlis ananukuu kutoka kwa Imamu Sadiq (a.s.)4 kwamba Mtume (s.a.w.w.) hakuweza kuandika lakini aliweza kusoma barua. Hatimaye ilikuwa muhimu kwa Mtume (s.a.w.w.) kuwaarifu masahaba zake juu ya mpango wa adui upesi upesi iwezekanavyo. Hivyo, aliporejea mjini, ile barua ilisomwa ili kuwapasha habari.

Jeshi La Waquraishi Laanza Safari

Jeshi la Waquraishi liliamua kuanza safari, na baada ya kwenda masafa fulani walifika Ab’wa alipozikwa mama yake Mtume (s.a.w.w.). Baadhi ya watu wapuuzi miongoni mwa Waquraishi walisisitiza kwamba mwili wake uchimbuliwe. Hata hivyo, waliokuwa wakiona mbali miongoni mwao walililaumu vikali wazo hili na wakaongeza kusema: “Inawezekana kwamba kitendo hiki kikawa ni desturi hapo baadae, na maadui zetu wa kabila la Bani Bakr na Bani Khuzaa’ah wanaweza kuyachimbua makaburi ya maiti wetu.”

Mtume (s.a.w.w.) aliwatuma Anas na Munis bin Fazalah kwenda kuleta taarifa juu ya Waquraishi. Watu hawa wawili walileta taarifa ya kwamba jeshi la Waquraishi limeshafika karibu na Madina nao wamewaachilia wanyama wao wa kupanda kulisha kwenye mashamba ya Madina. Habib bin Munzir alileta taarifa ya kwamba viongozi watanguliao wa jeshi lWaquraishi wameshafika karibu na Madina. Wakati wa alasiri wa siku ya Alhamisi ilithibitishwa kwamba sehemu kubwa ya jeshi la Waquraishi ilikuwa imeukaribia mji wa Madina. Waislamu waliogopa maadui wasije wakamdhuru Mtume (s.a.w.w.) kwa kufanya mashambulizi ya usiku. Hivyo basi, machifu wa Aws na Khazraji waliamua kuchukua silaha na kukesha usiku ule msikitini ili kuilinda nyumba ya Mtume (s.a.w.w.) na malango ya mji ule hadi walipopewa kazi nyinginezo kwa mujibu wa mipango ya kivita baada ya kuchomoza jua.

Ukanda Wa Uhud

Bonde kubwa na refu lililoungana na ile njia ya biashara iendayo Shamu na Yaman linaitwa Wadiul Qura. Makabila mbalimbali ya Waarabu na Wayahudi walifanya maskani yao kwenye sehemu yalimopatikana mahitaji ya maisha. Kwa hiyo, idadi ya vijiji ilikuwepo na pembezoni mwake vilizungushiwa uzio wa mawe. Yathrib (ambao baadae uliitwa Madinatul Rasuli – yaani Mji wa Rasuli) ulichukuliwa kuwa ndio mji mkuu wa vijiji hivi.
Yeyote yule aliyekuja Madina kutoka Makka alilazimika kuingia mjini mle kupitia upande wa kusini. Hata hivyo, kwa vile ukanda huu ulikuwa na mawe mengi, na ilikuwa vigumu kwa jeshi kuingia humo, jeshi la Waquraishi liliipinda njia yake na kwenda kutua kwenye sehemu ya kaskazini ya Madina kwenye bonde liitwalo ‘Aqiq’ lililoko chini ya mlima Uhud. Sehemu hii ilifaa kwa aina zote za harakati za kijeshi kwa kuwa haikuwako mitende kwenye sehemu hii na vile vile ardhi ilikuwa tambarare. Madina iliweza kushambuliwa vizuri zaidi kutoka upande huu kwa sababu vilikuwako vizuizi vya kimaumbile vichache mno kwenye upande huu.

Majeshi ya Waquraishi yalipiga kambi chini ya Mlima Uhud katika siku ya Alhamisi mwezi 5 Shawwal, mwaka wa 3 Hijiriya. Mtume (s.a.w.w.) alibakia mjini Madina siku ile na vile vile usiku wa kuchea Ijumaa. Aliunda halmashauri ya kijeshi siku ya Ijumaa na akawaomba maafisa na watu wengine walio na uzoefu kutoa maoni yao kuhusiana na ulinzi wa mji.

Kushauriana Kuhusu Ulinzi

Allah, Mwenye nguvu zote Alimwamrisha Mtume wa Uislamu (s.a.w.w.) kuomba ushauri wa masahaba zake katika mambo yaliyo muhimu na kuufikiria ushauri wao anapofanya uamuzi, na kwa kufanya hivyo alitoa mfano bora zaidi kwa wafuasi wake na kujenga moyo wa demokrasia, ukweli na uhakika miongoni mwao. Je, alifaidika kutokana na maoni yao au la? Ulamaa na wanachuoni wa theolojia wamelijibu swali hili. Hata hivyo, ni ukweli ukubalikao kwamba, mashauriano haya ni mifano iliyo hai ya kanuni za kikatiba zilizotufikia kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.). Njia yake hii ilikuwa yenye mafunzo na ya kuvutia mno kiasi kwamba makhalifa wa Uislamu nao waliifuata baada ya kufariki dunia kwake na kuyakubali kabisa maoni bora zaidi ya Imamu Ali, Amiri wa Waumini (a.s.) kuhusiana na mambo ya kijeshi na matatizo ya kijamii.

Kwenye mkutano mkubwa uliohudhuriwa na maafisa na askari mashujaa wa jeshi la Waislamu, Mtume (s.a.w) alisema: “Hebu nipeni maoni yenu” – Yaani aliwaomba wale maafisa na askari kutoa maoni yao kuhusiana na ulinzi wa Uislamu uliokuwa ukitishiwa na Waquraishi.

Abdullah bin Ubay aliyekuwa mmoja wa wanafiki wa mjini Madina, alishauri utumike ulinzi wa kwenye ngome. Ina maana ya kwamba Waislamu wasitoke mle Madina bali waitumie minara na majengo. Wanawake wampige mawe adui kutoka kwenye mapaa ya nyumba na minara na wanaume wapigane bega kwa bega kwenye mitaa ya mji. Alisema: “Zamani tulikuwa tukiitumia njia ya ulinzi wa ngome na wanawake walitusaidia kutoka kwenye mapaa ya nyumba na ni kwa sababu hii kwamba mji wa Yathrib umebakia katika hali ya kutoguswa.

Adui hakufaulu kuitumia njia hii. Kila tulipojihami kwa njia hii, tulishinda na kila tulipotoka nje ya mji, tulipata madhara.”

Wazee wazoefu kutoka miongoni mwa Muhajirin na Ansar waliliunga mkono wazo hili. Hata hivyo, vijana na hasa wale ambao hawakushiriki kwenye vita vya Badr nao walikuwa na shauku ya kupigana, walilipinga vikali wazo na wakasema:

“Njia hii ya ulinzi itamshawishi adui, nasi tutapoteza heshima tuliyoipata kwenye Vita vya Badr. Si aibu kwamba wenye kumwabudu Allah walio mashujaa na wenye kujitolea mhanga wajifiche majumbani mwao na kumruhusu adui afike pale? wakati wa Vita vya Badr nguvu yetu ilikuwa ndogo mno ikilinganishwa na hii ya hivi sasa, na ukiachilia mbali hayo, tulishinda. Tumekuwa tukisubiri kwa muda mrefu ili tupate nafasi na sasa tumeipata.”

Hamza, alisema: “Ninaapa kwa jina la Allah, Aliyeifunua Qur’ani, leo sitakula chakula changu mpaka nimepigana na adui nje ya mji.” Kundi hili lilishikilia kwamba jeshi la Waislamu litoke nje ya mji na kumpa kipigo yule adui.5

Kupiga Kura Ya Kuuwawa

Mzee mmoja mchamungu aliyeitwa Khaysamah alisimama na kusema: “Ewe Rasuli wa Allah! Waquraishi wamekuwa wakijishughulisha kwa mwaka mzima nao wamefaulu kuyaweka sawa pamoja nao makabila ya Waarabu. Kama hatutatoka hivi sasa kuihami sehemu hii, basi upo uwezekano wakauzingira mji wa Madina. Pia inawezekana kwamba wanaweza wakayaondoa kuzingira huko na kurudi Makka.

Hata hivyo, jambo hili litawatia moyo, nasi katika siku zijazo hatutakuwa na usalama kutokana na mashambulio yao. Nasikitika kwamba sikuweza kushiriki katika Vita vya Badr wakati mimi na mwanangu tulipenda sana kushiriki kwenye vita vile na kila mmoja wetu alitaka kumtangulia mwenziwe.

Wakati wa Vita vya Badr nilimwambia mwanangu: Wewe bado ni kijana na unayo tamaa ya kufanya mambo mengi na unaweza kuitumia nguvu ya ujana wako katika njia ambayo unaweza kuipata radhi ya Allah. Kwa kadiri mimi nihusikavyo, umri wangu hivi sasa karibuni ushakwisha na maisha yangu ya siku zijazo si yenye furaha. Hivyo basi, ni muhimu kwamba nishiriki kwenye jihadi hii takatifu (Vita vya Badr), nawe utapaswa kuyabeba majukumu yahusuyo wote wanaonitegemea.

Hata hivyo, mwanangu alipenda sana kushiriki kwenye vita ile kiasi kwamba tuliamua kupiga kura. Kura ilimwangukia yeye, na akafa kishahidi kwenye Vita vya Badr. Usiku wa jana kila mtu alikuwa akizungumzia juu ya kule kuzingirwa na Waquraishi, nami nikaenda kulala na fikira hizi akilini mwangu. Nilimwota mwanangu. Alikuwa akitembea kwenye bustani za peponi na alikuwa akiyafaidi matunda yake. Alizungumza nami kwa huba na akasema: “Baba yangu mpenzi! Ninakusuburi.” Ewe Mjumbe wa Allah! Ndevu zangu zimekuwa na mvi na mifupa yangu imepoteza nyama zake. Ninakuomba uniombee kufa kishahidi katika njia ya haki.”6

Utawaona watu wengi walio mashujaa na wenye kujitolea mhanga kama mtu huyu kwenye kurasa za historia ya Uislamu. Shule za mafunzo zisizoasisiwa juu ya itikadi na imani juu ya Mungu Muweza na Siku ya Hukumu, haziwezi kuwafunza askari wanaojitolea mhanga kama Khaysamah. Moyo huu wa kujitolea mhanga umfanyao askari kukitafuta kifo chake katika njia ya unyoofu huku machozi yakimdondoka machoni mwake, ni ari ambayo haiwezi kufundishwa kwenye shule yoyote ile isipokuwa kwenye shule ya uchamungu.

Katika nchi za viwanda za ulimwenguni huu, siku hizi umuhimu zaidi umewekwa kwenye hali za maisha ya maafisa na wakuu wengine wa majeshi. Hata hivyo, kwa vile lengo la vita za siku hizi ni kupata maisha bora na matengenezo yake, malengo yao makuu ni kuyaokoa maisha yao. Hata hivyo, kwenye shule ya wachamungu, lengo la kupigana ni kuitafuta radhi ya Allah, na kwa lengo hili laweza kufikiwa kwa kuuawa. Askari wa Allah huzikabili taabu zote kwa uimara bila kuyumba.

Matokeo Ya Ushauriano

Mtume (s.a.w.w.) aliyachukulia maoni ya walio wengi kuwa ndio yenye kukata shauri na akatayarisha kwenda nje ya mji badala ya kuitumia ile njia ya ulinzi wa ngomeni na mapigano ya bega kwa bega.
Haikufaa hata kidogo kwamba baada ya msisitizo wote wa maafisa kama vile Hamza na Sa’ad bin Ubaadah awe anaupendelea ushauri wa Abdullah Ubay, aliyekuwa mmoja wa wanafiki wa Madina.

Ingawa kwa mtazamo wa ulinzi na kanuni za vita, ushauri wake (Abdullah Ubay) ulithibitisha ushindi, au kwa uchache ulithibitisha ya kwamba Waislamu wasishindwe, lakini ulikuwa ni makosa kabisa kisaikolojia kwa sababu zifuatazo:

1. Mapigano yasiyo na utaratibu mwema ya bega kwa bega kwenye mitaa myembamba ya Madina na kuwaruhusu wanawake washiriki kwenye haya mapigano ya kiulinzi na kusalia kwenye maficho majumbani mwao na kuiacha njia ikiwa wazi kwa adui, ingalikuwa dalili ya unyonge na ujinga wa Waislamu na isingeliafikiana na ile nguvu waliyoionyesha kwenye Vita vya Badr.

2. Madina itakapozingirwa na maadui na barabara zake kumilikiwa na maadui na kikathibiti kimya cha askari wa Kiislamu mbele ya yote haya, kungeliuuwa kabisa moyo wa kupigana katika nafsi zao.

3. Je, isingeliwezekana kwamba Abdullah bin Ubayy aliyekuwa na mfundo dhidi ya Mtume (s.a.w.w.) alitaka kumpiga pigo kali kwa njia hii?

Mtume (S.A.W.W.) Achukua Uamuzi

Baada ya kuliandaa jeshi la ulinzi, Mtume (s.a.w.w.) aliingia nyumbani mwake. Alivaa deraya, akavaa upanga kiunoni, akaweka ngao mgongoni mwake, akaning’iniza upinde begani mwake, akaushika mkuki mkononi mwake, na baada ya kujiandaa kwa silaha kiasi hicho, alijitokeza mbele ya watu. Mandhari hii iliwapa Waislamu mshituko mkubwa.

Baadhi yao walifikiria kwamba kule kushikilia kwao kutoka nje ya mji hakukuafikiana na kanuni za Uislamu na walimshauri Mtume (s.a.w.w.) jambo lisilo la lazima kutoka nje kwenda kupigana. Hivyo basi, ili kusahihisha kosa hilo, walisema kwamba walikuwa tayari kufuata maoni yake na watakubaliana na uamuzi wowote ule atakaoutoa, yaani kama haifai kutoka nje basi wako tayari kubakia mle mjini. Hata hivyo, Mtume (s.a.w.w.) alijibu akisema: ‘Mtume anapovaa deraya haimfalii kuivua mpaka apigane dhidi ya adui.”7

Mtume (S.A.W.W.) Aenda Nje Ya Mji Wa Madina

Mtume (s.a.w.w.) alisali sala ya Ijumaa na kisha akatoka mjini Madina na kwenda Uhud akifuatana na jeshi lenye watu elfu moja. Hakwenda na watu kama vile Usama bin Zayd bin Haarith na Abdullah bin Umar kutokana na udogo wa umri wao, lakini vijana wawili ambao ni Samurah na Raafi, ambao umri wao haukuzidi miaka kumi na mitano, walishiriki kwenye vita hii kwa sababu, ingawa walikuwa bado wangali watoto, walikuwa wapiga mishale wazuri.

Walipokuwa njiani, baadhi ya Wayahudi waliokuwa washirika wa Abdullah bin Ubay walionyesha kupendelea kwao kushiriki katika ulinzi wa mji, lakini Mtume (s.a.w.w.) kutokana na sababu fulani fulani hakuona kuwa inafaa kuwaruhusu kufanya hivyo. Wakati huo huo Abdallah bin Ubay naye alikataa kushiriki mwenye jihadi kwa sababu ya kwamba Mtume (s.a.w.w.) ameukubali ushauri wa vijana na kuuacha wake. Hivyo basi, yeye alirudi baada ya kufika katikati ya safari ile pamoja na watu mia tatu wa kabila la Aws waliokuwa ndugu zake.

Mtume (s.a.w.w.) na masahaba zake walipendelea kuipitia njia iliyofupi zaidi ili waweze kufika kwenye sehemu ya kupigia kambi zao upesi. Kwa lengo hili walilazimika kupitia kwenye bustani ya mnafiki mmoja aliyeitwa Jumuh. Mtu huyu alionyesha kuudhika sana kwa ukaidi kwa sababu ya jeshi la Kiislamu kuingia kwenye konde yake na akamvunjia heshima Mtume (s.a.w.w.). Masahaba wa Mtume (s.a.w.w.) walitaka kumwua lakini Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Mwacheni mtu huyu aliyepotoshwa na mkaidi.”8

Askari Wawili Waliojitolea Mhanga

Walipofika mahali fulani Mtume (s.a.w.w.) aliwakagua askari wake. Moyo wao wa kujitolea mhanga na nyuso angavu zilikuwa ziking’aa kupitia mwanga wa panga zao. Jeshi alilolileta Mtume (s.a.w.w.) chini ya Mlima Uhud lilikuwa na watu ambao umri wao ulitofautiana mno. Wengi wao walikuwa wazee wenye vichwa na nyuso nyeupe, lakini vile vile waliweza kuonekana vijana mashujaa, ambao umri wao haukuzidi miaka kumi na mitano.

Jambo lililowahimiza watu hawa kushiriki kwenye vita hivi halikuwa lolote jingine ila huba ya ukamilifu ambao unaweza kupatikana tu chini ya msaada wa ulinzi wa Uislamu. Katika kuiunga mkono kauli hii tunasimulia hapa chini hadithi za watu wawili yaani mzee mmoja na kijana mmoja aliyekuwa ameoa usiku mmoja tu kabla ya hapo:

1. Amr bin Jumuh: Alikuwa ni mzee aliyekuwa na mgongo uliopinda, ambaye nguvu zake za mwili zilikuwa zimekwisha, na alikuwa mtu ambaye mmoja wa miguu yake ulijeruhiwa katika ajali. Alikuwa na wana wanne mashujaa aliowapeleka kwenye uwanja wa vita na alikuwa na furaha kwamba walikuwa wakipigana kwa ajili ya haki na ukweli.

Hata hivyo, alifikiria nafsini mwake kwamba haikuwa sahihi kukaa mbali kutoka kwenye vita vile na hivyo kuweza kupoteza rehema (za jihadi). Ndugu zake walikataa vikali kushiriki kwake kwenye vita vile na wakasema kwamba sheria ya Uislamu imemsamehe majukumu yote ya aina hii. Hata hivyo, maneno yao hayakumtosheleza hivyo yeye mwenyewe akamwendea Mtume (s.a.w.w.) na akasema: “Ndugu zangu wananizuia kushiriki kwenye jihadi. Nini maoni yako juu ya jambo hili?”

Mtume (s.a.w.w.) alimjibu akisema: “Allah Anakufikiria kuwa umesamehewa na hakuna jukumu lililo juu yako.” Hata hivyo, alimsisitiza na kumsihi alikubali ombi lake. Wakati ndugu zake wakiwa wamemzunguka, Mtume (s.a.w.w.) aliwageukia na kusema: “Msimzuie kufa kifo cha kishahidi katika njia ya Uislamu.” Alipotoka nje ya nyumba yake alisema: “Ee Allah! Nifanye mshindi katika kuuweka uhai wangu katika njia Yako na usinifanye nirudi nyumbani mwangu.”

Mtu aendaye kukutana na kifo kwa mikono miwili yu mwenye uhakika wa kuufikia mwishilizo wake. Mashambulizi ya kilema huyu yalikuwa yenye kushitusha. Alimshambulia adui vikali mno ingawa alikuwa na mguu uliolemaa, na akasema: “Mimi ninaitamani Pepo.” Mmoja wa wanawe naye alikuwa akisonga mbele pamoja naye. Matokeo yake ni kwamba wote wawili walipigana hadi wakaipata heshima ya kufa kishahidi.9

2. Hanzalah: Alikuwa yu kijana ambaye bado hajautimiza umri wa miaka ishirini na minne. Imesemekana hivi: ‘Anawatoa wana safi kutokana na wazazi wasio safi. Hanzalah alikuwa mwana wa Abu ‘Amr, adui wa Mtume (s.a.w.w.). Baba yake alishiriki kwenye vita vya Uhud katika upande wa Waquraishi naye alikuwa mmoja wa watu mafasiki waliowachochea Waquraishi kupigana vita dhidi ya Mtume (s.a.w.w.). Alijishughulisha na matendo yaliyo dhidi ya Uislamu hadi kwenye kifo chake na alikuwa mmoja wa waasisi wa Masjidi Dhiraar. Maelezo marefu juu ya msikiti yatatolewa kuhusiana na matukio ya mwaka wa tisa wa Hijiriya.

Hisia za utoto hazikumfanya Hanzalah akengeuke kutoka kwenye njia iliyonyooka. Usiku wa kuchea siku ya Vita vya Uhud ulikuwa usiku wa harusi yake. Alimwoa binti wa Abdullah bin Ubay mtu mashuhuri wa kabila la Bani Aws na alilazimika kuzifanya sherehe za ndoa usiku ule ule. Alipousikia mwito wa jihadi alitatanika. Hakuipata njia yoyote nyingine ila kuomba ruhusa kuto kwa yule Amir-jeshi Mkuu kuutumia usiku ule mjini Madina na kwenda kwenye uwanja wa vita siku iliyofuatia. Kama ilivyonukuliwa na Allamah Majlis,10 aya ifuatayo ilifunuliwa juu yake:

“Hakika wenye kuamini ni wale wamwaminio Allah na Mtume Wake, na wanapokuwa pamoja naye kwenye jambo linalohusiana na wote, hawaondoki mpaka wamwombe ruhusa, kwa hakika wale wakuombao ruhusa hao ndio wamwaminio Allah na Mtume Wake. Hivyo watakapokuomba ruhusa kwa ajili ya mambo yao, basi mruhusu umpendaye miongoni mwao na uwaombee msamaha kwa Allah, hakika Allah ni Mwingi wa kusamehe Mwenye kurehemu.” (Surah an-Nur 24:62).

Mtume (s.a.w.w.) alimpa ruhusa ya usiku mmoja kusherehekea ndoa yake. Asubuhi yake aliwasili kwenye uwanja wa vita hata kabla ya kuoga janaba. Alipotaka kutoka nyumbani mwake, machozi yalimchuruzika yule bibi harusi ambaye ndoa yake ilifanyika usiku mmoja tu kabla ya pale. Aliiweka mikono yake shingoni mwa mumewe kumwomba asubiri kidogo. Kisha akawaita watu wanne waliosalia mjini mle Madina kutokana na sababu fulani fulani, ili washuhudie ya kwamba ndoa ilifanyika baina yao usiku uliopita.

Hanzallah alipotoka, yule bibi harusi aliwageukia wale watu wanne waliotajwa hapo juu akawaambia: “Usiku uliopita niliota kwamba mbingu ilipasuka vipande viwili na mume wangu akaingia na baada ya hapo vile vipande viwili vya mbingu vikaungana tena. Kutokana na ndoto hii, ninaona kwamba mume wangu na roho yake watapaa kwenda Peponi.”

Hanzalah alijiunga na jeshi lile. Macho yake yakamwangalia Abu Sufyan aliyekuwa akitembea baina ya majeshi mawili. Alimshambulia shambulio la kishujaa dhidi yake kwa upanga wake lakini uliupiga mgongo wa farasi wa Abu Sifyan na yeye mwenyewe akaanguka chini.

Vilio vya Abu Sufyan viliibua mazingatio ya askari wa Waquraishi.Shaddad Dulaythi akamshambulia Hanzalah, na matokeo yake ni kwamba Abu Sufyan akatoroka. Askari wa mkuki kutoka miongoni mwa askari wa Waquraishi alimshambulia Hanzalah na kumchoma mkuki mwilini mwake. Ingawa alikuwa na jeraha kubwa, Hanzalah alimfuatia mtu yule na kumpiga dharuba ya upanga. Yeye naye akaanguka chini na akakata roho kutokana na lile jeraha alilotiwa na askari yule.

Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Nimewaona malaika wakimwosha Hanzalah.” Hii ndio sababu iliyomfanya aitwe ‘Ghasilul Malaa’ikah’ (yaani yule aliyeoshwa na malaika). Watu wa kabila la Aws walipokuwa wakizihesabu sababu za utukufu na heshima yao walikuwa wakisema: “Mmoja wetu alikuwa ni Hanzalah aliyeoshwa na malaika.”

Abu Sufyan alikuwa akisema: “Kama wamemwua mwanangu Hanzalah kwenye Vita vya Badr, mimi nami nimemwua Hanzalah wa Waislamu kwenye Vita vya Uhud.”

Hapana shaka kwamba fikara, uaminifu na imani ya wanyumba hawa vinashangaza, kwa sababu baba zao walikuwa maadui wakuu wa Uislamu. Baba wa bibi harusi alikuwa ni Abdallah bin Ubay bin Salul aliyekuwa chifu wa wanafiki wa Madina, na Hanzalah alikuwa mwana wa Abu Amr, aliyekuwa Mtawa katika zama za ujinga na baada ya kuingia kwa Uislamu alijiunga na wenye kuabudu masanamu wa Makka. Yeye ndiye aliyemkaribisha Hercules (mfalme wa Warumi wa Kigiriki) kuishambulia na kuiharibu Dola mpya ya Kiislamu.11

Safu Za Yale Majeshi Mawili

Asubuhi ya mwezi 7 Shawwal, mwaka 3 Hijiriya, jeshi la Kiislamu lilijipanga mkabala na jeshi la Waquraishi linaloshambulia na kuhujumu. Jeshi la Waislamu lilichagua sehemu ya kupigia kambi yao katika sehemu iliyokuwa na kizuizi na hifadhi ya kimaumbile nyuma yake ambayo ni Mlima Uhud. Hata hivyo, ilikuwako nafasi maalumu katikati ya mlima ule na ulikuwapo uwezekano kwamba majesahi ya adui yangaliweza kugeuka nyuma ya mlima ule na kutokea nyuma ya jeshi la Waislamu kwa kupitia kwenye nafasi ile na kuweza kuwashambulia kwa nyuma.
Ili kuiondoa hatari hii, Mtume (s.a.w.w.) aliweka makundi mawili ya askari wa mishale kwenye kilima kidogo na kumwambia kamanda wao Abdallah bin Jaabir hivi: “Muwafukuze maadui kwa kupiga mishale. Msiwaruhusu kuingia kwenye uwanja wa vita kwa kupitia nyuma na kutushambulia kwa kutushitukiza. Iwe tumeshinda au tumeshindwa, musiiitoke sehemu hii.”

Matukio ya Vita ya Uhud yanadhihirisha kwamba nafasi hii ilikuwa nyeti mno na kushindwa kwa Waislamu baada ya kupata ushindi kunatokana na ukweli kwamba, wale askari wa pinde walionyesha utovu wa nidhamu na wakaitoka hii sehemu iliyo muhimu mno na yule adui aliyekuwa kishashindwa na alikuwa kakimbia alishambulia shambulio la ghafla kupitia kwenye sehemu hii.

Ile amri kali aliyoitoa Mtume (s.a.w.w.) kuwapa askari wa pinde, ya kutoitoka sehemu ile ilikuwa ni ushuhuda wa ujuzi wake uliokamilika juu ya kanuni za vita. Hata hivyo, ujuzi wa kamanda wa kanuni za vita hauhakikishi kupata ushindi kama askari wataonyesha utovu wa nidhamu.

Kuimarisha Hamasa Za Askari

Mtume (s.a.w.w.) hakuacha kuimarisha hamasa za askari kwenye vita. Katika wakati huu, vile vile askari mia saba walipojifunga dhidi ya watu elfu tatu, aliziimarisha nyoyo zao kwa hotuba. Mwanahistoria mkuu wa Uislamu, Waaqidi, amesema: “Mtume (s.a.w.w.) aliweka askari wa kupiga mishale hamsini kwenye shingo ya mlima iitwayo Ainayn na kuuweka Mlima Uhud nyuma na mji wa Madina mbele ya majeshi ya Waislamu. Alipokuwa akitembea kwa miguu alivipanga vikosi na kuweka nafasi ya kila afisa. Alikiweka kikundi kimoja mbele na kingine nyuma. Alizipanga safu kwa uangalifu kiasi kwamba kama bega la askari yeyote yule lilikuwa mbele ya wenziwe, mara moja alimtaka askari yule kurudi nyuma.

Baada ya kuzipanga safu, Mtume (s.a.w.w.) aliwahutubia Waislamu kwa maneno haya: “Ninakushaurini kuyafuata yale mliyoamrishwa na Allah Mwenye nguvu zote kwenye Kitabu chake. Ninakukumbusheni kuzitii amri za Allah na jiepusheni na kumwasi.” Kisha aliongeza kusema hivi: “Ni jukumu gumu na zito kupigana na adui, na kuna watu wachache mno wawezao kubakia madhubuti mbele yao ila wale walioongozwa na kusaidiwa na Allah, kwa kuwa Allah Yu pamoja na wale wamtiio na shetani yu pamoja na wale wamwasio Allah. Juu ya kitu chochote kile lazima mbakie imara katika jihadi na kwa njia hii mtapata baraka aliyokuahidini Allah. Mjumbe, Malaika Mkuu Jibriil ameniambia kwamba hakuna yeyote afaye kwenye ulimwengu huu mpaka ameila ile chembe ndogo ya riziki yake ya kila siku aliyowekewa na Mola wake... Na mtu asianze kupigana mpaka pale itakapotolewa amri ya kupigana.”12

Adui Azipanga Safu Zake

Abu Sufyan aliligawa jeshi lake katika makundi matatu. Aliwaweka wale askari wa miguu wenye deraya katikati, kundi jingine lililokuwa chini ya uongozi wa Khalid bin Walid upande wa kulia, na kundi jingine chini ya uongozi wa Ikrimah upande wa kushoto. Vile vile aliweka kikosi maalum mbele ya jeshi kwa namna ya watangulizi, na vile vile kwenye kundi hili walikuwemo wale washika bendera, wote wakitokana na kabila la Abdud Daar. Kisha akawahutubia akasema: “Ushindi wa jeshi lolote lile hutegemeana na umadhubuti na uvumilivu wa washika bendera. Katika siku ya Badr tulishindwa kwenye uwanja huu. Kama kabila la Abdud Daar halionyeshi ustadi katika kuihami bendera, inawezekana kwamba heshima ya kuishika bendera inaweza kuhamishiwa kwenye kabila jingine.” Talhah bin Abi Talhah aliyekuwa mtu shujaa na mshika bendera wa kwanza kabisa, aliyahisi maneno haya. Alipiga hatua moja mbele upesi sana akasai akamwita mpinzani aje kupigana.

Vichocheo Vya Kisaikolojia

Kabla ya kuanza kwa vita Mtume (s.a.w.w.) alishika upanga mkononi mwake, na ili kuichemsha damu ya askari mashujaa, aliwageuzia uso wake na kusema: “Ni nani mtu yule atakayeushika upanga huu mkononi mwake na kuupa haki yake?” Baadhi ya watu walisimama lakini Mtume (s.a.w.w.) hakuwapa upanga ule. Kisha Abu Dujaanah, aliyekuwa askari shujaa alisimama na akauliza akisema: “Ni ipi haki ya upanga huu na ni vipi tunaweza kuitoa?” Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Unapaswa kupigana sana ukiwa nao kiasi kwamba mpaka upate kupinda.” Abu Dujanah akasema: “Mimi niko tayari kuulipa haki yake.” Kisha akajifunga leso nyekundu kichwani mwake aliyoiita leso ya kifo” na akauchukua ule upanga kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.). Hivyo, kwa kukifunga kile kitambaa kichwani mwake alikuwa na maana ya kwamba atapigana hadi pumzi zake za mwisho. Alitembea kama chui mwenye kujiona na alikuwa na furaha mno kuipata ile heshima aliyoipata, na ile leso nyekundu iliiongeza heshima yake.13

Hakuna shaka kwamba mikogo hii ni kichocheo bora zaidi cha kulishawishi jeshi linalopigana kwa ajili ya kuuhami ukweli na mambo ya kiroho na lisilokuwa na nia yoyote nyingine ila kuueneza uhuru wa kuabudu, na halina madhumuni mengine ila huba ya ustawi. Labda kitendo hiki cha Mtume (s.a.w.w.) hakikuwa tu kwa ajili ya kuichochea nafsi ya Abu Dujaanah, kwa kuwa, kwa njia hii vile vile aliwashawishi wale wengine na kuwahamasisha kwamba ushujaa wao na nia zao nazo ni lazima ziwe kwenye kipimo kama hiki kiasi kwamba wastahiki kuzipata medali za kijeshi.

Zubayr bin Awaam, ambaye yeye mwenyewe alikuwa ni askari shujaa, alijikuta akiwa si mwenye raha, kwa sababu Mtume (s.a.w.w.) hakumpa ule upanga. Hivyo, alijisemea mwenyewe: Nitamfuatilia Abu Dujanah ili nikione kiwango cha ushujaa wake.” Anasema: “Nilimfuatilia mle kwenye uwanja wa vita. Alimkatilia mbali kila shujaa aliyemkabili..” Kisha akasema: ‘Alikuwako shujaa mmoja miongoni mwa Waquraishi, ambaye upesi upesi alivikata vichwa vya Waislamu waliojeruhiwa. Nami nilishitushwa mno kutokana na hiki kitendo chake kisicho cha kawaida. Kwa bahati njema shujaa yule alikuja uso kwa uso na Abu Dujaanah. Walibadilishana mapigo machache na hatimaye yule shujaa wa Waquraishi aliuawa mikononi mwa Abu Dujaanah.”

Abu Dujaanah alisema: “Nilimwona mtu mmoja akiwashawishi Waquraishi kupigana. Nilimwendea na alipouona upanga ukining’inia kichwani mwake alianza kuomboleza na kulia. Mara kwa ghafla nilitambua ya kwamba alikuwa ni mwanamke (Hind mkewe Abu Sufyan) na nikauchukulia upanga wa Mtume (s.a.w.w.) kuwa ni safi mno kiasi cha kutostahili kupigwa kichwani mwa mwanamke (kama Hind).”14

Vita Vyaanza

Ibn Hisham anaandika hivi:15 “Vita vilianza kupitia kwa Abu ‘Amr aliyekuwa mmoja wa wale waliokimbia kutoka Madina. Yeye alitokana na kabila la Bani Aws, lakini kutokana na uadui wake dhidi ya Uislamu, alikimbilia Makka na watu kumi na watano wa Bani Aws walikuwa pamoja naye. Alikuwa akifikiria ya kwamba kama watu wa kabila la Bani Aws wakimwona watamtoka Mtume (s.a.w.w.). Hivyo basi, alijitokeza mbele ili kulifikia lengo hili. Hata hivyo alipowakabili Waislamu ilimbidi kuzikabili dhihaka na matusi yao.16 Hivyo basi, baada ya mapigano mafupi alitoka kwenye mstari wa mbele.
Kujitolea mhanga kwa baadhi ya mashujaa kwenye Vita vya Uhud kunatambulika vyema miongoni mwa wanahistoria, na kujitolea mhanga kulikofanywa na Sayyidna Ali (a.s.) kunafaa kutajwa. Ibn Abbas anasema: “Kwenye vita vyote Ali alikuwa mshika bendera na daima mshika bendera alikuwa akiteuliwa kutoka miongoni mwa watu wenye uzoefu na uthabiti, na kwenye Vita vya Uhud bendera ya Muhajiriin ilikuwa mikononi mwa Ali.” Kufuatana na kauli ya wengi wa wanahistoria, baada ya Mus’ab bin Umayr, mshika bendera wa Waislamu kuuliwa kishahidi, Mtume (s.a.w.w.) alimpa Sayyidna Ali (a.s.) bendera ile, na sababu iliyomfanya Mus’ab aishike bendera ile pale mwanzoni labda ni kwa sababu alikuwa anatokana na familia ya Abdud Daar na mshika bendera wa Waquraishi naye alitokana na familia hii hii.” (maoni haya yamechukuliwa kutoka Balazari).

Talhah Abi Talhah, aliyekuwa akiitwa Kabshul Katibah (mtu aliyesawa na kikosi kizima cha mbele cha jeshi) akaingia katika uwanja wa vita huku akipiga makelele, akisema: “Enyi masahaba wa Muhammad! Mnaamini ya kwamba watu wetu wanaouawa, wanakwenda Motoni ambapo wenu wanakwenda Peponi. Katika hali hiyo, je, yuko yeyote miongoni mwenu ambaye ninaweza nikampeleka huko Peponi au anipeleke Motoni?” Sauti yake ilikuwa ikivuma katika ule uwanja wa vita. Sayyidna Ali (a.s.) alijitokeza mbele na baada ya kubadilishana mapigo kadhaa hivi, Talhah alianguka chini.

Baada ya Talhah kuuawa, ndugu zake wawili wakawa washika bendera, mmoja baada ya mwingine. Hata hivyo, wote wawili waliuawa kwa mishale iliyopigwa na Aasim bin Thaabit.

Tunajifunza kutokana na hotuba aliyoitoa Sayyidna Ali (a.s.) mbele ya kamati ya ushauri iliyoundwa ili kumteua Khalifa baada ya kifo cha Khalifa wa pili kwamba, jeshi la Waquraishi liliwaweka akiba watu tisa kwenye nafasi ya mshika bendera na iliamuliwa ya kwamba waishike bendera ile kwa zamu, mtu kwanza akiuawa wa pili aishike ile bendera na kuendelea hadi waishe wote. Washika bendera wote hawa watokanao na kabila la Bani Abdud Daar waliuawa mikononi mwa Sayyidna Ali (a.s.). Baadda yao, mtumwa Mwethiopia, aliyeitwa Sawaab, aliyekuwa na umbo la kuogofya na sura ya kutisha aliiokota ile bendera na akasai. Yeye naye alianguka kutokana na dharuba ya Sayyidna Ali (a.s.).

Kwenye mkutano mkuu, ambao masahaba zake Mtume (s.a.w.w.) walihudhuria, Sayyidna Ali (a.s.) alisema: “Je, mnakumbuka kwamba nilikuondoleeni ufisadi wa watu tisa wa kabila la Bani Abdud Daar, ambapo kila mmoja wao aliishika ile bendera kwa zamu na akasai?” Wale wote waliokuwapo pale waliyathibitisha maneno ya Sayyidna Ali, Amiri wa Waumini (a.s.).17

Aliongeza kusema: “Je, mnakumbuka kwamba baada ya wale watu tisa, yule mtumwa Mwethiopia, Sawaab aliingia katika uwanja wa vita na hakuwa na lengo lolote ila kumwua Mtume wa Allah! Alikuwa mwenye ghadhabu kali mno kiasi kwamba alitokwa na povu kinywani na macho yake yalikuwa mekundu. Mlipomwona shujaa yule nyote mlishikwa na bumbuwazi na mkarudi nyuma, ambapo mimi nilikwenda mbele na baada ya kumpiga dharuba mgongoni mwake, nikamwangusha chini?” Wale waliokuwapo pale waliyathibitisha maneno haya pia.18

Nani Waliokuwa Wakipigana Kwa Ajili Ya Tamaa?

Tunajifunza kutokana na beti za mashairi alizokuwa akizisoma Hindi na wanawake wengine huku wakipiga dufu ili kuwahamasisha mashujaa wa Kiquraishi na kuwachochea katika umwagaji wa damu na kulipiza kisasi kwamba, watu hawa hawakuwa wakipigana kwa ajili ya mambo ya kiroho, usafi, uhuru na tabia njema. Kinyume na hayo, wao walikuwa wakisukumwa na mambo ya ngono na dunia. Ule wimbo waliouimba wale wanawake kwa dufu na sauti maalum katikati ya safu za jeshi ulikuwa: “Sisi ni mabinti wa Taariq. Tunatembea kwenye mazulia ghali. Kama mkimkabili adui, tutalala pamoja nanyi, lakini kama mkimwonyesha adui migongo yenu na kukimbia, tutajitenga nanyi.”

Ni ukweli ukubalikao kwamba kuna kutoafikiana kwa dhahiri kabisa na tofauti kubwa baina ya watu, ambao mambo yao ya kivita yanasukumwa na tamaa za kingono na wasio na lengo lolote jingine ila kujitosheleza katika faida za kiulimwengu na anasa za kimwili na wale watu wapiganao kwa lengo takatifu la kiroho kama vile kudumisha uhuru, kuinua kiwango cha fikara na kumwondolea mwanadamu ibada ya mti na jiwe. Kutokana na hivyo vichocheo viwili tofauti viliyomo akilini mwa makundi mawili haya, haikuchukua muda mrefu kabla ya kutoa matokeo ya kujitolea mhanga kwa maafisa wa Uislamu kama vile Sayyidna Ali (a.s.), Hamza, Abu Dujaanah, Zubayr na wengineo. Jeshi la Waquraishi lilizitupa chini silaha na vyakula vyao na wakakimbia kwa fedheha kutoka kwenye uwanja wa vita. Utukufu mwingine ulifikiwa kwa namna hiyo na wale mashujaa wa Uislamu.19

Kushindwa Baada Ya Ushindi

Tunaweza kutaja hapa kwa nini mashujaa wa Uislamu walishinda. Ilitokana na ukweli kwamba hadi katika dakika ya mwisho ya ushindi wao hawakuwa na lengo jingine lile ila jihadi katika njia ya Allah, kuitafuta radhi Yake, kuubalighisha ujumbe wa Allah na kuondoa kila kizuizi njiani mwake.

Basi vipi walishindwa baada ya hapo? Ilikuwa ni kwa sababu baada ya kuupata ushindi, nia na lengo la wengi wa Waislamu lilipatwa na mabadiliko. Mwelekeo wa nyoyo zao kwenye ngawira zilizotupwa na jeshi la Waquraishi kwenye uwanja wa vita na wao wenyewe kukimbia, ziliathiri uaminifu wa kundi kubwa na wakaiasi amri waliyopewa na Mtume (s.a.w.w.).

Haya yafuatayo ni maelezo ya tukio hili kwa kirefu: “Tulipokuwa tukiielezea hali ya kijiografia ya Uhud tulieleza ya kwamba kilikuwapo kipenyo maalum katikati ya Mlima Uhud, na Mtume (s.a.w.w.) aliwapa wapiga mishale hamsini chini ya uongozi wa Abdullah Taabar jukumu la kulilinda bonde lililokuwapo nyuma ya mstari wa mbele wa uwanja wa vita, na alimpa kamanda wa kikundi hiki amri hii: “Mzuieni adui asipitie kwenye kipenyo hiki cha mlima kwa kumpiga mishale na msiitoke sehemu hii kwa vyovyote vile itakavyokuwa, tuwe tumeshindwa au tumeshinda.” Moto wa vita uliwaka katika pande zote mbili.

Kila wakati maadui walipotaka kupitia kwenye bonde hili walirudishwa nyuma na wale wapiga mishale. Jeshi la Waquraishi lilipozitupa chini silaha zao na kukiacha kila kitu ili kuokoa uhai wao, maofisa mashujaa wachache wa Uislamu ambao viapo vyao vya utii vilikuwa vyenye uaminifu kamili waliwafuata wale maadui nje ya ule uwanja wa vita. Lakini wengi waliacha kule kuwafuatilia wale maadui na wakaziweka chini silaha zao na kuanza kukusanya ngawira na wakadhania kwamba vita imemalizika.

Wale watu wanaolilinda lile bonde lililokuwako nyuma ya mstari wa mbele wa vita nao waliamua kuitumia fursa ile na wakaambiana: “Hakuna faida yoyote kwetu kubakia hapa na ni jambo lenye faida kwamba sisi nasi tukusanye ngawira.” Hata hivyo, kamanda wao aliwakumbusha kwamba Mtume (s.a.w.w.) aliamrisha ya kwamba jeshi la Waislamu lipate ushindi au kushindwa wasitoke kwenye sehemu yao ile. Wengi wa askari wa mishale waliokuwa wakikilinda kipenyo kile, walimpinga kamanda wao na kusema: “Kukaa kwetu hapa hakuna faida na Mtume alikuwa na maana tu ya kwamba tukilinde kipenyo hiki vita ilipokuwa ikiendelea lakini hivi sasa mapigano yamekwisha.”

Kwa msingi wa dhana hii potovu, watu arobaini walishuka kutoka kwenye ile sehemu ya doria na watu kumi tu ndio waliobakia pale. Khalid bin Walid, aliyekuwa shujaa na mzoefu na alijua tangu mwanzoni kwamba kinywa cha kipenyo kile kilikuwa ufunguo wa ushindi, na kwa mara nyingi sana alijaribu kufika katika ule mstari wa mbele wa vita kupitia kwenye kipenyo hiki, lakini alikabiliwa vikali na wale wapiga mishale. Wakati huu alijinufaisha kutokana na ile idadi ndogo ya walinzi.

Aliwaongoza askari wake kuelekea ule upande wa nyuma wa jeshi la Waislamu na kufanya mashambulizi ya kushtusha na hatimaye alifika kwenye kundi la Waislamu. Mara baada ya hapo wale Waislamu wasio na silaha na wazembe walishambuliwa vikali mno kwa nyuma.
Baada ya kuikamata ile sehemu nyeti Khalid aliomba ushirikiano wa lile jeshi la Waquraish lililoshindwa lililokuwa kwenye hali ya kukimbia, na wakauimarisha moyo wa upinzani na uvumilivu wa Waquraishi, kwa makelele na vilio vya kurudia rudia. Kutokana na mfarakano na rabsha zilizokuwako kwenye safu za Waislamu, mara moja jeshi la Waquraish likawazunguka mashujaa wa Kiislamu na mapigano yakaanza tena baina yao.

Kushindwa huku kulitokana na kutojali kwa wale watu waliokitoka kile kipenyo kwa ajili ya faida zao za kidunia na bila ya kudhamiria wakawafungulia njia maadui kwa jinsi ambayo askari wapanda wanyama waliokuwa chini ya uongozi wa Khalid bin Walid waliingia katika uwanja wa vita kutokea nyuma ya Waislamu.

Mashambulizi ya Khalid yalisaidiwa na mashambulizi ya Ikrimah bin Abi Jahl na mvurugiko wa utaratibu usio na kifani na wa kushtusha ulitokea kwenye safu za Waislamu. Waislamu hawakuwa na lolote jingine ila kujihami katika hali ya vikundi vilivyotawanyika. Hata hivyo, kwa vile mawasiliano na kamanda nayo yamekatwa hawakufaulu katika kujihami na walipatwa na msiba mkubwa mno kiasi kwamba baadhi ya askari wa Kiislamu waliuawa na Waislamu wenzao kwa uzembe.

Mashambulizi ya Khalid na Ikrimah yaliuimarisha moyo wa jeshi la Waquraishi. Wale askari waliokuwa wakirudi nyuma na kukimbia waliingia tena kwenye uwanja wa vita na kuwapa msaada. Waliwazingira Waislamu pande zote na kuua idadi fulani miongoni mwao.

Tetesi Juu Ya Kuuwawa Kwa Mtume (S.A.W.W) Zaenea

Shujaa mmoja wa Waquraishi aitwaye Layth alimshambulia Mas’ab bin Umayr, yule mshika bendera jasiri wa Uislamu, na baada ya kubadilishana idadi fulani ya dharuba yule mshika bendera wa Uislamu aliuawa. Kwa kuwa wale mashujaa wa Kiislamu walikuwa wamezificha nyuso zao, Layth alifikiri kwamba yule mtu aliyeuawa alikuwa ni Mtume wa Uislam (s.a.w.w.).

Hivyo alipiga ukelele na kuwajulisha wale machifu wa jeshi kwamba Muhammad ameuawa. Tetesi hii ilienea toka kwa mtu hadi kwa mtu mwingine kwenye jeshi la Waquraish. Machifu wao walifurahi mno kiasi kwamba sauti zao zilivuma mle kwenye uwanja wakisema: “Enyi watu! Muhammad ameuawa! Enyi watu! Muhammad ameuawa!”

Kuenea kwa taarifa za uwongo kulimhamasisha adui na jeshi la Waquraishi likaja kuendelea na vita. Kila mmoja wao alipendelea kushiriki katika kukata viungo vya Muhammad ili kwamba aweze kukipata cheo kikubwa kwenye ule ulimwengu wa washirikina.

Taarifa hizi zilizidhoofisha nyoyo za mashujaa wa Kiislamu zaidi ya vile zilivyozipa nguvu nyoyo za jeshi la maadui. Kwa kiasi kwamba idadi fulani miongini mwa Waislamu waliacha kupigana na wakakimbilia mlimani na hakuna yeyote aliyebakia kwenye uwanja wa vita ila wachache tu ambao waliweza kuhesabiwa katika vidole vya mikono.

Je, Yawezekana Kukana Kule Kukimbia Kwa Baadhi Ya Watu?

Haiwezekani kukana kwamba baadhi ya masahaba walikimbia kutoka kwenye uwanja wa vita, na hivyo ukweli wa kwamba walikuwa ni masahaba wa Mtume (s.a.w.w.) au kwamba baadae walijipatia vyeo na heshima miongoni mwa Waislamu usituzuie kuukubali ukweli huu ulio mchungu.

Ibn Hisham, mwanahistoria maarufu, anaandika hivi: “Anas bin Nazr, ami yake Anas bin Malik anasema: “Jeshi la Waislamu lilipoelemewa, na taarifa za kuuwawa kwa Mtume zilipoenea, wengi wa Waislamu waliufikiria uhai wao wenyewe na kila mtu alikimbilia kwenye pembe moja au nyingine.” Anaongeza kusema: “Nililiona kundi la Muhajiriin na Ansar wakiwamo Umar bin Khattab na Talhah bin Ubaydullah Taymi, waliokuwa wamekaa kwenye pembe na walikuwa na hofu ya hatari juu yao wenyewe.
Niliwauliza kwa sauti ya kutopendelea: “Kwa nini mnakaa hapa?” Walijibu: “Mtume ameuwawa na hivyo basi, hakuna faida yoyote ya kupigana.” Niliwaambia: “Kama Mtume ameuwawa, basi hakuna faida ya kuishi. Simameni na mkutane na kufa kishahidi kwenye njia ile ile aliyofia.”20

Kwa mujibu wa kauli ya wanahistoria wengi, Anas alisema: “Kama Muhammad ameuwawa Mola wake yupo hai.” Na kisha akaongeza kusema: “Niliona kwamba maneno yangu hayakuwa na athari yoyote kwao. Nilikiweka kiganja changu kwenye silaha yangu na nikaanza kupigana kwa ushupavu.” Ibn Hishamu anasema kwamba, Anas alipata majeraha makubwa kwenye vita hivi na hakuna aliyeweza kuitambua maiti yake ila dada yake tu.21

Kikundi fulani cha Waislamu walikuwa wamedhoofishwa mno kiasi kwamba ili kuhakikisha usalama wao, walipanga kumwendea Abdullah bin Ubay ili aweze kuwapatia usalama kutoka kwa Abu Sufyan.22

Qur’ani Tukufu Yafichua Baadhi Ya Mambo

Aya za Qur’ani Tukufu zinalipasua pazia la ushabiki wa kidini na ujinga na zinadhihirisha vya kutosha kwamba baadhi ya masahaba walifikiria kwamba, ahadi aliyoiahidi Mtume (s.a.w.w.) juu ya ushindi na kufuzu haikuwa na msingi, na Allah Mwenye nguvu zote anasema hivi kuhusiana na kundi hili: “..... Na kundi jingine limeshughulishwa na nafsi zao, wakimdhania Mwenyezi Mungu lisilokuwa haki, dhana ya kikafiri. Husema: Tuna kitu katika jambo hili? ... . .” (Surah Aali Imran 3:154).

Unaweza kuzitambua habari zilizojificha juu ya vita hivi kwa kuzisoma aya za Sura Aali Imran. Aya hizi zinaunga mkono kikamilifu mambo wanayoyaamini Mashi’a. Wao wanaamini kuwa sio kweli kwamba masahaba wote walikuwa wenye kujitolea mhanga au wapenzi wa Uislamu.

Baadhi ya watu miongoni mwao walikuwa wanafiki. Na wakati ule ule miongoni mwa masahaba lilikuwemo kundi kubwa la waumini wa kweli na wachamungu na watu waaminifu. Siku hizi kikundi cha waandishi wa Kisunni wanajaribu kulitanda pazia juu ya mengi ya matendo yasiyo na thamani ya masahaba (mifano yao umeiona kwenye maelezo yanayohusu vita hivi). Wamevihami vyeo vyao wote kwa kutoa maelezo ya kweli yaonyeshayo ushupavu wao wa kidini tu, lakini nayo hayawezi kuzificha habari halisi za historia.

Ni nani awezaye kukikana kiini cha aya hii ambayo wazi wazi inasema hivi: “Kumbukeni mlipokuwa mkikimbia mbio wala hamkumtazama yeyote na hali Mtume akiwaiteni kwa nyuma yenu.....” (Surah Aali Imran, 3:153).

Aya hii inazungumzia juu ya watu wale wale aliowaona Anas bin Nazr kwa macho yake walipokuwa wameketi kwenye pembe, nao walikuwa wakiyahofia maisha yao ya baadaye. Aya ifuatayo inaelezea zaidi kuliko ile tuliyoimukuu hapo juu:

إِنَّ الَّذِينَ تَوَلَّوْا مِنْكُمْ يَوْمَ الْتَقَى الْجَمْعَانِ إِنَّمَا اسْتَزَلَّهُمُ الشَّيْطَانُ بِبَعْضِ مَا كَسَبُوا ۖ وَلَقَدْ عَفَا اللَّهُ عَنْهُمْ ۗ إِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ حَلِيمٌ {155}

“Hakika wale waliokimbia miongoni mwenu siku (ya Uhud) yalipokutana majeshi mawili, hakika ni shetani ndiye aliyewatelezesha kwa sababu ya baadhi ya waliyoyachuma.
Na Allah Amekwisha wasamehe, hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mvumilivu.” (Surah Aali Imran, 3:155).

Katika Aya ifuatayo Allah anawakaripia wale watu waliozifanya taarifa za kuuawa kwa Mtume (s.a.w.w.) kuwa ni udhuru wa kuacha kupigana, nao walikuwa wakifikiria kumwendea Abu Sufyan kupitia kwa Abdullah bin Ubayy ili awathibitishiye usalama wao:

وَمَا مُحَمَّدٌ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِنْ قَبْلِهِ الرُّسُلُ ۚ أَفَإِنْ مَاتَ أَوْ قُتِلَ انْقَلَبْتُمْ عَلَىٰ أَعْقَابِكُمْ ۚ وَمَنْ يَنْقَلِبْ عَلَىٰ عَقِبَيْهِ فَلَنْ يَضُرَّ اللَّهَ شَيْئًا ۗ وَسَيَجْزِي اللَّهُ الشَّاكِرِينَ {144}

“Na hakuwa Muhammad ila ni Mtume aliyepitiwa na Mitume kabla yake. Basi je, akifa au akiuliwa mtarudi nyuma kwa visigino vyenu? Na atakayerudi nyuma kwa visigino vyake hatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu atawalipa wanaoshukuru.”
(Surah Aali Imran, 3:144).

Uzoefu Mchungu

Tunapochunguza matukio ya Uhud ukweli fulani wenye uchungu na mtamu hupatikana; nguvu ya uthabiti na uvumilivu wa kundi moja na utovu wa uthabiti wa kundi jingine unaweza kuonekana waziwazi. Wanahistoria, wachanganuzi wa mambo na wengineo ambao huandika habari za matukio, unaposoma taarifa zao, inakuwa dhahiri kabisa kwamba masahaba wote hawawezi kuchukuliwa kuwa ni wachamungu kabisa na waadilifu, eti kwa sababu tu kwamba wao walikuwa ni masahaba, hivyo miongoni mwa wale watu waliokitoka kile kilima cha wapiga mishale, na wale walioupanda ule mlima katika wakati ule nyeti na kuuacha mwito wa Mtume (s.a.w.w.) walikuwamo masahaba walewale wanaoheshimiwa.

Mwanahistoria mashuhuri wa Uislamu, Waaqid anasema: “Katika siku ya Uhud watu wanane walikula kiapo cha utii kwa Mtume (s.a.w.w.) wakimthibitishia kuyatoa maisha yao kwa ajili yake. Miongoni mwao watatu walikuwa Muhajiriin (Ali, Talhah na Zubayr) na wale watano waliosalia walikwua Ansar na ukiwachilia mbali hawa watu wanane, watu wote walikimbia katika wakati ule nyeti.”

Ibn Abil Hadid anaandika hivi:23 “Katika mwaka wa 608 Hijiriya nili- hudhuria kwenye mkutano mmoja mjini Baghdad ambao watu fulani walikuwa wakikisoma kitabu cha Maghaazil-Waaqidi mbele ya mwanachuoni mkuu Muhammad bin Ma’ad Alawi. Walipoifikia hatua ambayo Muhammad bin Maslamah anasimulia waziwazi kuwa: “Katika siku ya Uhud niliona kwa macho yangu kwamba Waislamu walikuwa wak- iupanda mlima na Mtume alikuwa akiwaita kwa majina yao maalum na alikuwa akisema: “Ewe fulani! Ewe fulani!” Lakini hakuna hata mmoja wao aliyeitika mwito ule wa Mtume.” Mwalimu aliniambia: “Maneno ‘fulani na fulani’ yalikuwa na maana ya walewale watu waliojipatia vyeo na nafasi baada ya Mtume. Huyu msimuliaji hakuyataja majina halisi kutokana na hofu, na kwa sababu ya heshima ambayo alitegemea kuwapa.”

Katika tafsiri yake vilevile amesimulia kwamba wengi wa wasimuliaji wanapatana juu yake kwamba Khalifa wa tatu alikuwa mmoja wa watu wale ambao hawakuwa imara na thabiti kwenye uwanja wa vita katika wakati ule nyeti.

Baadae utaisoma sentensi ya Mtume (s.a.w.w.) juu ya mwanamke wa Uislamu aliyejitolea mhanga aliyeitwa Nasibah aliyemhami Mtume (s.a.w.w.) kwenye uwanja wa vita wa Uhud. Kwenye sentensi ile, vilevile kuna dokezo la kushuka daraja na sifa za wale waliokimbia. Hatuna haja ya kutoa taarifa za yeyote miongini mwa masahaba wa Mtume (s.a.w.w.). Lengo letu ni kuleta hali halisi kwenye mwanga na kuelezea ukweli. Tunakulaumu kukimbia kwao sawa kabisa na vile tunavyosifu uthabiti na uvumilivu wa lile kundi jingine na kuichukulia tabia yao kuwa ni nzuri sana.

Watu Watano Wapanga Kumuua Mtume (S.A.W.W)

Wakati ule ambao jeshi la waislamu lilikabiliwa na mvurugiko wa utaratibu na ghasia, Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akishambuliwa kutoka pande zote. Watu watano wabaya kutoka miongoni mwa Waquraishi walidhamiria kuyamalizia mbali maisha ya Mtume (s.a.w.w.) kwa vyovyote vile iwavyo. Watu hawa walikuwa ni:

1. Abdullah bin Shanaab aliyelijeruhi paji la uso la Mtume (s.a.w.w.).

2. ‘Utbah bin Abi Waraqa, ambaye kwa kumtupia mawe manne alimvunja meno yake ya upande wa kulia.24

3. Ibn Qumi’ah Laythi aliyemjeruhi Mtume (s.a.w.w.) usoni. Jeraha hili lilikuwa kali sana kiasi kwamba pete za kofia yake ya chuma zilimchoma kwenye mashavu yake! Pete hizi zilichomolewa na Abu Ubaydah Jarraah kwa meno yake naye alipoteza meno yake manne katika kufanya hivyo.

4. Abdullah bin Hamid, aliyeuawa mikononi mwa shujaa wa Uislamu Abu Duj?nah wakati wa kushambulia.

3. Abi Khalf. Alikuwa mmoja wa watu wale waliokufa mikononi mwa Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe. Alimkabili Mtume (s.aw.w) wakati yeye (Mtume s.a.w.w) alipofaulu kulifikia lile bonde huku baadhi ya masahaba wakiwa wamemkusanyikia baada ya kumtambua. Abu Khalf alimsogelea Mtume (s.a.w.w.) ndipo Mtume (s.a.w) akauchukua mkuki kutoka kwa Hasis bin Simmah na kuuchoma shingoni mwa Abi Khalf na matokeo yake ni kwamba Abi Khalf alianguka chini kutoka kwenye farasi wake.

Ingawa lile jeraha alilotiwa Abi Khalf lilikuwa dogo tu, alipatwa na hofu mno kiasi kwamba marafiki zake walipomfariji hakuweza kutulia akasema: “Nilimwambia Muhammad kule Makka kwamba nitamwua naye alinijibu akisema kwamba ataniua, naye katu hasemi uongo.”

Yote yalimalizika kwake kutokana na lile jeraha na woga, na baada ya muda fulani alikufa alipokuwa njiani akienda Makka.25

Hakuna shaka yoyote kwamba tukio hili laonyesha udhaifu wa mbali kabisa wa washirikina. Ingawa upo ukweli kwamba walikubali kwamba Mtume (s.a.w.w.) alikuwa mkweli na katu hakusema uwongo, lakini walitaka kuimwaga damu yake.

Mtume (s.a.w.w.) hakusonga kutoka mahali alipokuwa. Alisalia kuwa thabiti kama mwamba na akaendelea kujihami yeye mwenyewe na Uislamu. Ingawa ulikuwepo ukweli kwamba umbali baina ya maisha yake na kifo umekuwa mfupi sana na aliweza kuona vizuri kwamba jeshi la adui lilikuwa likimgeukia kama wimbi, lakini hakusogea kutoka pale alipokuwa, wala hakutamka neno lolote lile ambalo lingaliweza kuisaliti hofu yoyote ile au maumivu kwa upande wake.

Na pale alipokuwa akiipangusa damu kutoka kwenye paji la uso wake alisema: “Vipi watu wataweza kuupata wokovu kama wanaupaka uso wa Mtume wao damu anapowaita kwenye ibada ya Allah?” Na hii yaonyesha upole mwingi na huruma hata kwa maadui zake.

Sayyidna Ali, Amiri wa Waumini (a.s.) anasema: “Mtume alikuwa karibu sana na adui kwenye uwanja wa vita na akatupatia kimbilio wakati mambo yalipokuwa magumu.” Hivyo, moja ya sababu zilizomwezesha Mtume (s.a.w.w.) kubakia salama ni kule kujihami kwake yeye mwenyewe na Uislamu, lakini vilevile ilikuwako sababu yingine iliyomthibitishia uhai wake, nayo ni kujitolea mhanga kwa marafiki zake wachache walio waaminifu na wakweli na masahaba walioyanunua maisha yake kwa gharama ya maisha yao wenyewe, na kuubakisha salama mshumaa uwakao kutokana na kuzimishwa. Mtume (s.a.w.w.) alipigana pigano kali mno katika siku ile ya Uhud na alitupa mishale yote iliyokuwamo kwenye podo lake, kiasi kwamba upinde wake ulivunjika na kamba yake nayo ikakatika.26

Idadi ya wale waliomhami Mtume (s.a.w.w.) haikuzidi ile ya watu wachache.27 Hata hivyo, umadhubuti wao wote haukaniki, lakini ni dhahiri kutokana na historia isemavyo, la uhakika na lenye kukata maneno miongoni mwa wanahistoria ni ule uthabiti wa kundi dogo mno. Taarifa za ulinzi walioufanya zinatolewa hapa.

Ulinzi Ulioandamana Na Kufuzu Na Kushinda Upya.

Haitakuwa vibaya kama hii sehemu ya historia ya Uislamu tukiipa jina la “ushindi uliopatikana upya.’ Maana ya ushindi huu ni kwamba, kinyume na mategemeo ya maadui, waislamu walifaulu kumwokoa Mtume (s.a.w.w.) kutokana na kifo. Huu ndio ule ushindi uliopatikana tena ulio- liangukia kura ya jeshi la Waislamu.

Kama tukiushirikisha ushindi huu na lile jeshi zima la Waislamu tutakuwa tunafanya hivyo ikiwa ni dalili ya heshima kwa wale mashujaa wa Uislamu. Hata hivyo, kwa kweli ule mzigo mzito wa ushindi huu umean- gukia mabegani mwa watu wachache walioweza kuhesabiwa katika vidole vya mkono. Hawa walikuwa wale watu waliomhami Mtume (s.a.w.w.) kwa kuyahatarisha maisha yao wenyewe, na hakika ilikuwa ni kutokana na kujitolea mhanga kwa hili kundi la watu wachache kwamba Dola ya Kislamu ilibakia kuwa na ujuzi wa utendaji wa mambo katika wakati wa shida, na hivyo ule mshumaa uangazao ukaendelea kuwaka badala za kuzimika.

Yafuatayo hapa chini ni maelezo ya matendo ya ujasiri ya hawa watu waliojitolea mhanga:

1. Sayyidna Ali bin Abi Twalib (a.s.): Mtu wa kwanza mwaminifu na madhubuti alikuwa ni afisa shujaa, ambaye wakati ule alikuwa kaumaliza mwaka wa ishirini na sita tu wa maisha yake, na aliyekuwa akimhudumia Mtume (s.a.w.w.) tangu utotoni mwake hadi katika wakati wa kifo cha Mtume (s.a.w.w.), naye hakuacha kujitolea mhanga na kumsaidia japo kwa muda mfupi tu. Afisa huyu mkuu na mchamungu halisi alikuwa ni Imamu Ali, Sayyidi wa wachamungu na Amiri wa Waumini, ambaye huduma na kujitolea kwake katika njia ya Uislamu vimeandikwa kweye historia.

Kimsingi huu ushindi uliopatikana tena ulifikia kama ule ushindi wa kwanza kwa njia ya ushujaa na kujitolea mhanga kwa yule mtu mwaminifu, kwa sababu ni dhahiri kwamba sababu ya kukimbia kwa Waquraishi kwenye ile hatua ya awali kabisa ya vita vile ni kwamba washika bendera wao wali- uwawa, mmoja baada ya mwingine, na wote waliuwawa mikononi mwa Sayyidna Ali (a.s.), na matokeo yake ni kwamba jeshi la Waquraishi lili- tishwa mno kiasi kwamba waliipoteza nguvu yao ya kubakia pale uwanjani na kuzuia mashambulizi ya Waislamu. Waandishi wa Kimisri wa zama zetu hizi walioliachanganua tukio hili, hawakumtendea haki Sayyidna (a.s.) kulingana na kile cheo chake au habari halisi zilizoandikwa kwenye historia na wamezichukulia huduma za Amiri wa Waumini (a.s.) kuwa sawa na zile za wale wengine. Hivyo basi, tunaona kuwa ni muhimu kutoa hapa taarifa fupi za kujitolea kwake na mihanga aliyoitoa.

Ibn Athir anasema:28 “Mtume akawa shabaha ya mashambulizi ya kila kisehemu cha jeshi la Waquraishi kutoka pande zote. Ali alishambulia kufuatana na maamrisho ya Mtume kila kisehemu cha jeshi lile kili- chomshambulia (Mtume), na akawatawanya au akawaua baadhi yao, na jambo hili lilitokea kwa mara kadhaa pale Uhud. Wakati huo huo, Malaika mkuu Jibriil alikuja na akakusifu kujitolea kwa Ali mbele ya Mtume na akasema: “Haki ni kilele cha kujitolea mhanga ambacho afisa huyu anakionyesha.”
Mtume akayathibitisha yale maelezo ya Jibriil na akasema: “Mimi ninatokana na Ali na Ali anatokana na mimi.” Kisha ilisikika sauti mle kwenye uwanja wa vita ikisema: “La Saifa ila Dhulfiqar, La Fataa illa Ali” Yaani “Hakuna upanga utoao huduma ila Dhulfiqar iliyokuwamo mkononi mwa Ali na hakuna mtu aliye shujaa ila Ali.”

Ibn Abil Hadid ametoa maelezo marefu zaidi ya tukio hili na anasema: “Kila kimoja cha vile visehemu vya jeshi vilivyokuwa vikijaribu kumwua Mtume kilikuwa na watu hamsini, na ingawa alikuwa hana mnyama wa kupanda lakini alivitawanyisha vyote.”

Kisha akatoa maelezo ya kuja kwa Jibril na akasema: “Ukiuachilia mbali ukweli uliopo kwamba tukio hili ni jambo likubaliwalo kwa maoni ya his- toria, nimesoma taarifa za kuja kwa Jibriil kwenye kitabu cha Muhammad Bin Is’haq kiitwacho ‘Kitaabul Ghazwaat’ na siku moja nikabahatika kuulizia kuhusu usahihi wake kutoka kwa mwalimu wangu Abdul Wahhaab Sakinah. Alisema: ‘Ni sahihi’. Kisha nikauliza: ‘Kwa nini Hadith hii haikuandikwa na wakusanyaji wa Sihah?’29Akajibu akisema: “Tunayo idadi ya Hadith Sahihi ambazo wakusanyaji wa Sihah wameziacha kuziweka kwenye vitabu vyao.”30

Katika hotuba ndefu aliyoitoa Sayyidna Ali (a.s.) kwa ajili ya ‘Raas al- Yahud’ mbele ya kikundi cha wafuasi wake, anarejelea kwenye kujitolea kwake mhanga kwa maneno haya: “... Jeshi la Maquraishi lilitushambulia kama jeshi moja tu, Ansar na Muhajiriin walikimbilia majumbani mwao nami nilipata majeraha makubwa nikimhami Mtume.”

Kisha yeye (Ali ) akalivutia kando vazi lake na akazionyesha zile sehemu ambazo alama za majeraha (kovu) zilikuwa bado zinaonekana.31 Zaidi ya hapo, kama ilivyoandikwa mwenye ‘Ilalusha Sharaa’i32 Ali (a.s.) alipokuwa akimhami Mtume (s.a.w.w.), alionyesha ushujaa mwingi na kujitolea mhanga kiasi kwamba upanga wake ulikatika vipande viwili. Hapo Mtume (s.a.w.w.) alimpa upanga wake uitwao ‘Dhulfiqaar’ na kwa upanga huu aliendeleza jihadi katika njia ya Allah.

Kwenye kitabu33 chake chenye thamani, Ibn Hishamu ameitaja idadi ya wale waliouawa kutoka miongoni mwa wenye kuabudu masanamu kuwa ni ishirini na wawili na vilevile imeyataja majina na sifa zao na akitoa pia jina la kabila n.k. Miongoni mwa hawa watu ishirini na wawili, kumi na wawili waliuawa na Sayyidna Ali (a.s.) na wale kumi waliobakia waliuawa na Waislamu wengine. Waandishi wa wasifu wa maisha ya Mtume (s.a.w) tuliowataja, wameyataja waziwazi majina na sifa za wale waliouawa.

Tunakubali kwamba haikuwezekana kwetu sisi kutoa kwenye kurasa hizo, sura halisi ya huduma alizozitoa Sayyidna Ali (a.s.) kama ilivyoelezwa kwenye vitabu vya madhehebu zote mbili, hasa kwenye kitabu kiitwacho Bihaarul Anwaar.34

Inatambulika kutokana na kuchunguza maelezo na Hadith mbalimbali kwamba, pale Uhud hakuna aliyekuwa kama vile alivyokuwa Sayyidna Ali (a.s.) na hata Abu Dujaanah aliyekuwa afisa wa Uislamu hodari na shujaa hakuweza kuwa sawa naye katika suala la ulinzi.

2. Abu Dujaanah: Baada ya Amiri wa Waumini, Abu Dujaanah alikuwa afisa wa pili aliyeihami nafsi ya Mtume (s.a.w.w.) katika hali ambayo ali- jifanya kuwa kofia ya chuma kwa ajili yake. Mishale ilikuwa ikimkaa mgongoni na kwa njia hiyo alikuwa akimhami Mtume (s.a.w.w.) kutokana na kuwa shabaha yao.

Marehemu Sipahr, ameandika sentensi moja juu ya Abu Dujaanah kwenye kitabu chake kiitwacho ‘Nasikhut Tawaarikh,35 hatukuweza kuipata asili yake. Anaandika hivi: “Mtume na Ali walipozungukwa na wenye kuyaabudu masanamu macho ya Mtume yalimwangukia Abu Dujaanah na akamwambia: “Ewe Abu Dujaanah! Ninakutoa kwenye kiapo chako. Hata hivyo Ali yu wangu na mimi ni wake.” Abu Dujaanah alilia sana na akasema: “Mimi niende wapi? Je, niende kwa mke wangu ambaye hana budi kufa? Je niende kwenye nyumba yangu itakayobomoka? Je, niuendee utajiri wangu na mali zangu zitakazoharibiwa? Je, nikimbilie kifo ambacho ni lazima kije?”

Mtume alipoyaona machozi machoni mwa Abu Dujaanah alimruhusu kupigana, na wote wawili, yeye na Ali walimhami Mtume (s.a.w.w.) kutokana na mashambulizi makali ya Waquraishi.

Kwenye vitabu vya Historia tunaona majina ya watu wengine kama vile Aasim bin Thaabit, Sahl Hunayf Talhah bin Ubaydullah n.k. katika nyadhifa za wa wale waliobakia kuwa madhubuti, na baadhi ya wanahistoria wameitaja idadi ya watu hao kuwa ni karibuni thelathini na sita. hata hivyo, kile kilicho dhahiri kutokana na historia ni kule kutobadilika kwa Sayyidna Ali (a.s.), Abu Dujaanah, Hamza, na Bibi aitwaye Ummi Amir. Ama uimara wa watu wengine wenyewe ni wenye kutuhumiwa, ila kwa hawa wanne na katika hali nyingine ni wenye kutiliwa mashaka.

3. Hamza bin Abdul Muttalib: Yeye ni mfano wa kujitolea mhanga kwa afisa shujaa. Kumekuwako idadi fulani ya maofisa shujaa na wenye kujitolea mhanga na mashujaa wenye nguvu na uwezo kwenye jeshi la Uislamu lakini ushujaa wa Hamza bin Abdul Muttalib umeandikwa kwenye kurasa za historia, na kwa hakika unatoa majani ya dhahabu ya historia ya vita vya Uislamu.

Hamza ami yake Mtume wa Uislamu (s.a.w.w.) alikuwa mmoja wa watu waliokuwa mashujaa zadi barani Arabu na afisa maarufu wa Uislamu. Ni yeye aliyeshikilia kwa uaminifu kwamba jeshi la Uislamu liende nje ya Madina na kupigana dhidi ya Waquraishi. Ni yeye Hamza aliyemhami Mtume (s.a.w.w.) mjini Makka kwenye ule wakati nyeti kwa nguvu zake zote na ili kulipiza kisasi cha matusi na madhara aliyofanyiwa Mtume (s.a.w.w.) na Abu Jahl, alikivunja kichwa cha Abu Jahl kwenye mkutano mkuu wa Waquraishi na hakuna yeyote aliyethubutu kumpinga. Alikuwa afisa mkuu na shujaa aliyemwua yule mtetezi shujaa wa Waquraishi aliyeitwa Shaybah na wengineo. Vile vile akakijeruhi kikundi cha maadui kwenye Vita vya Badr. Hakuwa na lengo lolote akilini mwake ila kuuhami ukweli na maadili na kudumisha uhuru katika maisha ya wanadamu.

Hind, mkewe Abu Sufyan alikuwa bint yake Utbah. Mwanamke huyu alikuwa na mfundo dhidi ya Hamza na alikusudia kumlipizia kisasi baba yake katika upande wa Waislamu kwa gharama yoyote ile. Wahshi, shujaa wa Kiethiopia alikuwa mtumwa wa Jaabir bin Mut’am na ami yake Jaabir naye aliuawa kwenye Vita vya Badr. Yeye (Wahshi) aliteuliwa na Hind kumsaidia katika kulifikia lengo lake kwa vyovyote vile. Alimwomba auwe miongoni mwa watu watatu (ambao ni Mtume s.a.w, Ali au Hamza) ili kwamba aweze kulipiza kisasi cha kifo cha baba yake. Yule shujaa wa Kiethiopia akamjibu akisema: “Siwezi kabisa kumkabili Muhammad, kwa sababu masahaba zake wako karibu zaidi naye kuliko yeyote mwingine.

Ali naye yu mwangalifu mno awapo kwenye uwanja wa vita. hata hivyo, Hamza yu mwenye ghadhabu mno kiasi kwamba anapopigana haangalii upande wowote mwingine, na inawezekana kwamba nikiweza kumwan- gusha kwa njia fulani au kwa kumshtukizia.”

Hind alitosheka na maneno haya na akamwahidi kwamba kama akifaulu kuifanya kazi ile atampa uungwana. Baadhi ya watu wanaamini kwamba Jaabir ndiye aliyeitoa ahadi hii kwa huyu mtumwa wake (Wahshi) kwa kuwa ami yake (Jaabir) aliuawa kwenye vita vya Badr.

Wahshi, yule mtumwa anasema: “Katika siku ya Uhud nilikuwa nikimfuatia Hamza. Alikuwa kama simba aliyeghadhibika. Alimwua kila mmoja aliyeweza kumfikia. Nilijificha kiasi kwamba hakuweza kuniona. Alikuwa akijishughulisha mno na mapigano.
Nilitoka kutoka kwenye yale maficho. Nilikuwa ni Mwethiopia, nilikuwa na desturi ya kuitupa silaha yangu kama wao (yaani kama Waethiopia) na mara chache sana niliikosa shabaha niliyo kusudia. Hivyo, nilimtupia mkuki wangu kutoka kwenye umbali maalumu baada ya kuutayarisha mtupio kwa jinsi maalumu. Silaha ile ilimchoma ubavuni na ikatokea baina ya miguu yake miwili. Alitaka kunishambulia lakini maumivu makali yalimzuia kufanya hivyo. Alibakia kwenye hali hiyo hadi roho yake ilipotoka mwili wake. Kisha nilimwendea kwa uangalifu na baada ya kuichomoa silaha yangu kutoka mwilini mwake, nilirejea kwenye jeshi la Waquraishi na kuusubiri ungwana wangu.

Baada ya vita ya Uhud niliendelea kuishi mjini Makka kwa muda mrefu sana hadi Waislamu walipouteka mji wa Makka. Kisha nilikimbilia Taa’if, lakini upesi sana Uislamu ulifika sehemu ile pia. Nilisikia ya kwamba vyovyote vile ubaya wa jinai la mtu uwezavyo kuwa, Mtume alimsamehe mtu huyo. Hivyo nilimwendea Mtume na ‘Shahaadatayn’ midomoni mwangu (yaani nilishuhudia kwamba hakuna mungu ila Allah na vile vile nikashuhudia ya kwamba Muhammad yu Mtume).

Mtume aliniona na akasema: “Wewe ndiwe Wahshi Mwethiopia?” Nikajibu: “Ndio.” Baaada ya hapo akasema: “Ulimwuaje Hamza?” Nilitoa maelezo ya tukio lile. Mtume (s.a.w.w.) alihuzunika sana na akasema: “Nisione uso wako kwa kadiri uwavyo hai, kwa sababu msiba wenye kuupasua moyo ulimwan- gukia ami yangu mikononi mwako.”

Ni moyo mkuu uleule wa Mtume wa Uislamu uliomfanya amwachie huru mtu huyu ingawa angeweza kumnyonga kutokana na makosa mengi. Wahshi anasema: “Kwa kadri Mtume alivyokuwa hai nilijificha kutoka machoni pake. Baada ya kifo chake ilitokea Vita dhidi ya Musaylimah Kazzaab. Nilijiunga na jeshi la Waislamu na nikaitumia silaha ileile dhidi ya Masaylimah na nikafaulu kumwua kwa msaada wa mmoja wa Ansar. Kama nilimwua mtu aliyekuwa bora zadi miongoni mwa watu, (yaani Hamzah) kwa silaha hii, mtu mwovu naye hakuweza kukiepuka kitisho chake kikuu.”

Kushiriki kwa Wahshi kwenye vita dhidi ya Musaylimah ni jambo analol- idai yeye mwenyewe, lakini Ibn Hisham anasema: “Kwenye siku za mwis- honi mwa uhai wake Wahshi alikuwa kama kunguru mweusi aliyekuwa daima akichukiwa na Waislamu kutokana na ulevi wake na aliadhibiwa mara mbili kutokana na kunywa mvinyo. Kutokana na tendo hili baya, jina lake lilifutwa kwenye kumbukumbu za kijeshi na Umar bin Khattab alikuwa akisema: Mwuwaji wa Hamza hastahili kusamehewa huko kwenye ulimwengu wa Akhera.”36

4. Nasibah bint Kaab: Mwanamke mwenye kujitolea mhanga. Hakuna apingaye kwamba jihadi ni haramu kwa wanawake katika dini ya Uislamu. Kuhusiana na jambo hili tunaweza kusema hapa kwamba mwak- ilishi wa wanawake wa Madina aliyepata heshima ya kufika mbele ya

Mtume (s.a.w.w.) akazungumza naye kuhusu huku kunyimwa jihadi na kulalamika kwa maneno haya: “Tunawapatia waume zetu mahitaji yote ya maisha, nao wanashiriki kwenye jihadi wakiwa kwenye amani ya kiakili, ambapo sisi wanawake tunanyimwa baraka hii kuu.”

Hapo ndipo Mtume (s.a.w.w.) aliwapelekea wanawake wote wa Madina ujumbe ufuatao kupitia kwake: “Kama mmenyimwa baraka hii kuu kutokana na sababu za kimaumbile na kijamii, mnaweza kujipatia baraka za jihadi kwa kuyatekeleza majukumu ya maisha ya ndoa.”

Kwenye uhusiano huu, vile vile aliitamka sentensi ya kihistoria ifuatayo: “(Mwanamke) kuyatekeleza majukumu ya maisha ya ndoa kwa jinsi itakikanavyo ni sawa na jihadi katika njia ya Allah.”

Hata hivyo wakati fulani, baadhi ya wanawake wazoefu walitoka nje ya mji wa Madina pamoja na Mujahidiin (ambao hasa walikuwa ni wana wao, kaka zao na ndugu zao) ili kwenda kuwasaidia,
nao waliwasaidia Waislamu katika kupata ushindi kwa kuwapa maji wenye kiu, kufua nguo za mashujaa na kuyafunga majeraha ya wale waliojeruhiwa.

Ummi Aamir, ambaye jina lake hasa lilikuwa Nasibah, anasema: “Nilijiunga na vita ya Uhud ili kuwapatia maji mashujaa na niliona kwam- ba hewa yenye kunukia vizuri ya ushindi ilikuwa ikivuma kuwaelekea Waislamu. Lakini upesi baada ya hapo, meza zilipinduliwa upesi sana na wale Waislamu walioshindwa wakaanza kukimbia. Vile vile niliona kwam- ba maisha ya Mtume yalikuwa hatarini, na nilifikiria kwamba ni jukumu langu kuyaokoa maisha yake japo iwe kwa gharama ya maisha yangu. Hivyo nilikiweka chini kiriba changu cha maji na kuanza kuyarudisha nyuma mashambulizi ya adui kwa upanga uliopata kufika mkononi mwan- gu. Wakati mwingine vile vile nilipiga mishale.”

Kisha alilitaja jeraha alilolipata begani mwake, na akasema: “Kwenye wakati ambao watu wamewageuzia migongo yao maadui, huku wakiwa wanakimbia, macho ya Mtume yalimwangukia mtu mmoja aliyekuwa kwenye hali ya kukimbia na akamwambia: “Hivyo sasa unakimbia, itupe chini ngao yako.” Alifanya hivyo nami nikaiokota ili niitumie. Ghafla nilimwona mtu aitwaye Ibn Qumi’ah akipiga ukelele na kusema: “Yuko wapi Muhammad?”

Alimtambua Mtume na akamkimbilia huku akiwa na upanga uliofutwa. Mas’ab na mimi tulimzuia dhidi ya kulitimiza lengo lake. Ili kunirudisha nyuma, alinipiga dhoruba begani mwangu. Ingawa mimi nami nilimpiga dharuba, lakini dharuba yake ilikuwa na athari kubwa kwangu, iliendelea kwa mwaka mzima ambapo kwa kuwa alikuwa kavaa deraya mbili dharuba yangu haikuwa na athari kwake. Ile dharuba niliyoipata begani mwangu ilikuwa kubwa mno. Mtume aliona kwamba damu ilikuwa ikichuruzika kwa wingi kutoka jerahani mwangu. Mara moja alimwita mmoja wa wanangu akamwomba alifunge kitambaa jeraha langu! mwanangu alifanya hivyo na nikaenda kupigana tena.

Wakati ule nilifahamu ya kwamba, mmoja wa wanangu alikuwa kajeruhiwa. Mara moja niliokota vipande vya nguo nilivyokuja navyo kwa ajili ya kufungia majeraha ya watu waliojeruhiwa ikiwa ni pamoja na lile jeraha la mwanangu. Hata hivyo, kwa kuwa maisha ya Mtume yalikuwa hatarini basi kila mara nilikuwa nikimgeukia mwanangu na kumwambia: “Mwanangu! Amka na upigane.”

Mtume alishangazwa mno kuuona uhodari na ushujaa wa mwanamke huyu ajitoleaye mhanga. Hivyo basi, alipomwona yule mtu aliyempiga dharuba mwanawe mara moja alimsoza akimwonyesha yule mwanamke na kuse- ma: “Huyu ndiye mtu aliyempiga dharuba mwanao.”

Mama yule aliyekuwa akirukaruka kumzunguka Mtume (s.a.w.w.) kama vile arukavyo nondo kando kando ya mshumaa, mara moja alimshambulia mtu yule kama simba mwenye ghadhabu na akampiga dharuba kwenye shavu la mguu wake iliyombwaga chini. Wakati huu kule kushangaa kwa Mtume juu ya ushujaa wa mwanamke yule kuliongezeka zaidi na alicheka kutokana na jambo hili mpaka meno yake ya nyuma zaidi (magego) yakaonekana na kisha akamwambia yule mwanamke: “Umelipiza kisasi cha shambulio aliloshambuliwa mwanao.”

Kwenye siku iliyofuatia, Mtume alipoviunda vikundi vidogo vidogo vya jeshi lake kutembea kuelekea Hamraa’ul Asad, Nasibah alitaka kwenda na jeshi lile, lakini lile jeraha kubwa alilotiwa halikumruhusu kufanya hivyo. Baada ya kurejea kutoka Hamraa’ul Asad, Mtume (s.a.w.w.) alimtuma mtu mmoja kwenda nyumbani kwa Nasibah kwenda kumtazama na alifurahi sana kusikia kwamba hali yake ilikuwa nzuri.

Ikiwa ni zawadi kwa kujitolea mhanga kwake kote, Bibi huyu alimwomba Mtume (s.a.w.w.) kumwombea kwa Allah ili aweze kuruhusiwa katika kumhudumia Mtume (s.a.w.w.) huko Peponi. Mtume (s.a.w.w.) alimwombea na akasema: “Ee Mola Wangu! Wafanye kuwa masahaba zangu huko Peponi.”37

Jinsi Bibi huyu alivyopigana, ilikuwa yenye kupendeza sana kwa Mtume (s.a.w.w.) kiasi kwamba alisema kuhusiana naye: “Leo cheo cha Nasibah bint Ka’ab ni bora kuliko kile cha watu fulani na fulani.”

Ibn Abil Hadid anasema: “Msimuliaji wa Hadith hii hakuwa mwaminifu kwa Mtume, kwa sababu hakuwataja dhahiri wale watu wawili ambao Mtume aliwataja kwa majina kwenye tukio hili.”38

Hata hivyo, nafikiri kwamba maneno fulani na fulani ni watu wale wale waliojipatia nafasi kubwa miongoni mwa Waislamu baada ya kufariki Mtume, na msimuliaji hakuwataja kwa wazi kwa sababu ya heshima na woga utokanao na nafasi zao.

Alama Za Matukio Kule Uhud

Maisha ya Mtume yaliokolewa kutoka kwenye hatari halisi kwa njia ya kujitolea mhanga ya watu wachache. Kwa bahati wengi wa maadui wali- jua kwamba Mtume alikuwa ameuawa na walikuwa wakiitafuta maiti yake miongoni mwa wale mashahidi. Na kuhusu wale wachache miongoni mwa maadui ambao walikuwa wakitambua kuapo kwake hai, mashambulizi yao yalikuwa yakirudishwa nyuma na Sayyidna Ali (a.s.), Abu Duj?nah na wengineo.

Wakati ule iliamuliwa ya kwamba taarifa za kifo cha Mtume (s.a.w.w.) zisingeweza kukataliwa na watu wakaziamini, hivyo Mtume aende kwenye lile bonde pamoja na masahaba zake. Alipokuwa njiani akielekea kwenye lile bonde alitumbukia kwenye shimo lililochimbwa na Abu Aamir kwa ajili ya Waislamu. Sayyidna Ali (a.s.) akamshika mkono upesi sana na kumtoa shimoni mle. Mtu wa kwanza kumtambua Mtume (s.a.w.w.) alikuwa ni Ka’ab bin M?lik. Aliyaona macho ya Mtume (s.a.w.w.) yaking’ara kutoka chini ya kofia yake ya chuma na kupiga ukelele mara moja: “Enyi Waislamu! Mtume yuko hapa! Yu hai! Allah amemwokoa kutokana na madhara ya maadui.”

Kutokana na kwamba kutangazwa kwa taarifa za Mtume kuwa hai kungeweza kuzaa mashambulizi mapya kutoka kwa maadui, Mtume alimshauri Ka’ab kulifanya jambo hili kuwa siri. Hivyo akanyamaza hadi Mtume alipowasili kwenye bonde.

Wakati huo huo Waislamu waliokuwa jirani na sehemu ile walifurahia sana kumwona Mtume (s.a.w.w.) akiwa hai na wakaona aibu walipokuwa mbele yake. Abu Ubaydah Jarraah alizing’oa pete mbili za kofia ya chuma zilizodidimia usoni mwa Mtume (s.a.w.w.) ambapo Sayyidna Ali (a.s.) aliijaza maji ngao yake ili kumwezesha Mtume (s.a.w.w.) kuosha uso wake. Alipokuwa akiuosha uso wake (Mtume s.a.w.w) aliyatamka maneno haya: “Ghadhabu ya Allah imekuwa kali zaidi juu ya watu walioupaka damu uso wa Mtume wao.”

Wenye Kufuata Maslahi Miongoni Mwa Maadui

Waislamu walipokabiliwa na kushindwa kubaya mno pale Uhud, maadui waliinyakua fursa hii na wakaanzisha namna ya mbinu dhidi ya maoni ya Kiislamu ya Upweke wa Allah ambazo zikawa na athari za haraka mno miongoni mwa watu wajinga. Mwandishi wa zama zetu hizi anasema hivi: “Hakuna nafasi ifaayo zaidi kwa kuziathiri itikadi na fikara za watu kuliko wakati ule wanapokabiliwa na kushindwa, msiba, huzuni na dhiki. Wakati wa taabu kali nyoyo za watu wanaotaabika huwa dhaifu mno na zisizotu- lia kiasi kwamba busara zao hupoteza uwezo wa kuamua na kuyatathmini mambo, na ni katika wakati huu kwamba propaganda zenye uovu huziathiri fikara za watu walioshindwa.”

Abu Sufyani, Ikrimah na wengineo waliokuwa wakiyashika masanamu makubwa mikononi mwao na walikuwa wakijihisi kuwa na shangwe, wali- itumia fursa hii kikamilifu na wakapiga kelele wakisema: “Naatukuzwe Hubal! Naatukuzwe Hubal.” (Hubal lilikuwa ni jina la sanamu). Kwa kusema hivi walitaka kuwaambia Waislamu kwamba ushindi wao ulitokana na kuyaabudu kwao masanamu na kama angalikuwako mungu yeyote mwingine, na ibada ya Allah Mmoja tu ingalikuwa ndiyo dini ya kweli, basi Waislamu wangalishinda.
Mtume (s.a.w.w.) alitambua kwamba maadui walikuwa wakihubiri mambo yaliyo hatari sana katika nyakati hizo zilizo nyeti na walikuwa wakijinu- faisha kikamilifu kutokana na fursa waliyoipata wakati ule. Hivyo basi, alizisahau taabu zake zote na upesi sana akamwamrisha Sayyidna Ali (a.s.) na Waislamu wengine kujibu tangazo hili la ibada ya masanamu kwa maneno haya: “Allah Yu Mkubwa na Mwenye nguvu zote.” (Yaani kushindwa huku tulikokupata hakutokani na ule ukweli wetu wa kumwabudu Allah bali ni matokeo ya baadhi ya watu kuziasi amri za kamanda).

Hata hivyo, Abu Sufyan hakukoma kuzitangaza fikra zake zenye sumu, na akasema: “Tunalo sanamu kama vile Uzza ambapo ninyi hamna mfano wake.” Mtume akaitumia nafasi hii na akawaamrisha Waislamu wajibu wakisema: “Allah Yu Mola wetu, nanyi hamna mola kama Yeye.” (Yaani kama mwalitegemea sanamu lisilo chochote ila kipande cha jiwe au mti, sisi twamtegemea Allah Aliye Mkuu na Mwenye nguvu zote).

Watangazaji wa ibada ya masanamu wakasema kwa mara ya tatu: “Siku hii ni siku ya kulipizia kisasi Siku ya Badr.” kwa dai hili Waislamu walijibu kufuatana na amri za Mtume (s.a.w.w.), wakisema: “Hizi siku mbili hazilingani, kwa sababu ndugu zetu waliouawa wako Peponi, ambapo wale wenu wako Motoni!”

Abu Sufyan alighadhibishwa mno na majibu haya makali yaliyokuwa yak- ija kutoka makooni mwa mamia ya Waislamu. Hivyo basi, baada ya kusema: “Tutakutana tena mwaka ujao” alitoka ule uwanja wa vita na kuamua kurudi Makka.39

Waislamu ambao miongoni mwao watu sabini waliuawa na wengi wao wakajeruhiwa, hata hivyo waliwajibika kutekeleza wajibu wa ki-Mungu (kusali sala ya Adhuhuri na ya Alasiri). Kutokana na udhaifu uliokithiri, Mtume (s.a.w.w.) alisali sala ya jamaa akiwa amekaa, na kisha akafanya kafani (kuvika sanda ) na mazishi ya mashahidi.

Mwisho Wa Vita

Miali ya vita ilizimishwa na yale makundi mawili yalitengana. Idadi ya wale waliojeruhiwa katika upande wa Waislamu ilikuwa mara tatu ya wale wa Waquraish. Ilikuwa muhimu kwao kulitimiza jukumu la kidini (kusali) na kuwazika wapenzi wao mapema iwezekanavyo.

Kabla ya Waislamu kuzizika maiti zao, wanawake wa Kiquraishi ambao waliuona uwanja wa vita ukiwa huru kutokana na aina zote za matendo ya kijinai, waliamua kuyatenda majinai makubwa mno baada ya ule ushindi, tena majinai yasiyo na kifani katika historia ya mwanadamu.

Hawakutosheka na ule ushindi wao wa dhahiri, bali ili kulipiza zaidi kisasi walivikata viungo, masikio, na pua za Waislamu waliokuwa wamelala chini wakiwa wameshakufa, na hivyo kuliweka doa la aibu kubwa juu ya tabia zao. Kwenye mataifa yote ya ulimwengu, maiti za maadui zisizo na msaada wowote na zisizolindwa, hupewa heshima. Hata hivyo, mkewe Abu Sufyan alitengeneza kidani na heleni za viungo vya Waislamu. Vile vile alilipasua tumbo la yule afisa mtiifu wa Uislamu, Hamzah, na kulitoa ini lake! Alijaribu kwa kadiri ya uwezo wake wote kulitafuna na kulila, lakini alishindwa!

Kitendo chake hiki kilikuwa cha aibu sana na chenye kuchukiza kiasi kwamba hata Abu Sufyan alisema: “Ninakikana kitendo hiki nami sikuamrisha kwamba kifanywe. Hata hivyo, wala mimi sichukizwi sana na jambo hili.”

Kutokana na kitendo hiki kichafu, Hind alifahamika miongoni mwa Waislamu kwa jina la ‘Hind mla ini’ na baadaye wanawe nao walifahamika kwa jina la ‘wana wa mwanamke mla ini.’

Waislamu waliwasili kwenye uwanja wa vita wakifuatana na Mtume (s.a.w.w.) ili kuzizika maiti zao. Macho ya Mtume (s.a.w.w.) yaliangukia kwenye maiti ya Hamza naye alichukizwa mno kuiona hali yake ya kuhuzunisha. Dhoruba ya ghadhabu iliibuka akilini kwake na akasema: “Hasira na ghadhabu ninayoihisi nafsini mwangu hivi sasa haina kifani maishani mwangu.”

Wanahistoria na wafasiri wa Qur’ani wanaandika kwa makubaliano ya pamoja kwamba Waislamu waliweka ahadi neno lao (na wakati mwingine walimjumlisha Mtume s.a.w.w miongoni mwao) kwamba, kama wakipata mamlaka juu ya waabudu masanamu watawatendea maiti wao namna ile ile na watakata viungo vya maiti zao thelathini kwa kila Mwislamu mmoja. Mara tu baada ya nia yao ya kufanya hivyo, Aya ifuatayo ilifunuliwa:

“Na kama mkitaka kulipiza kisasi, basi fanyeni sawa na vile mlivyoonewa. Lakini kama mkisubiri, hakika itakuwa bora kwenu.” (Surah al-Nahl, 16:126).

Kwa njia ya Aya hii, ambayo yenyewe ni msingi wa uadilifu wa Kiislamu, kwa mara nyingine tena Uislamu umedhihirisha mwelekeo wake wa kiroho na kihisia na ukathibitisha ya kwamba Dini hii Tukufu (Uislamu) si dini ya kulipiza kisasi. Haipuuzi misingi ya uadilifu na upole hata kwenye wakati mgumu mno, wakati mtu anapozidiwa nguvu na ghadhabu; na huutekeleza uadilifu kwenye matukio yote.

Safiyah dada yake Hamzah, alishikilia kutaka kuiona maiti ya kaka yake lakini, kama alivyoamrisha Mtume (s.a.w.w.), mtoto wake Zubayr alimzuia asiikaribie. Alimwambia mwanawe: “Ninafahamu kwamba wamevikatakata viungo vya mwili wake. Ninaapa kwa jina la Allah kwamba kama nikimkaribia sitadhihirisha kukereka kwangu na nitauvumilia msiba huu katika njia ya Allah.” Bibi huyu aliyefunzwa aliikaribia ile maiti ya kaka yake kwa utulivu ustahilio heshima, akamwombea dua, akam- wombea wokovu na akarejea.

Bila shaka nguvu ya imani ndio nguvu iliyo kuu zaidi. Inadhibiti ghadhabu kali zaidi na shinikizo na inatoa heshima na utulivu kwa mtu aliyeathirika. Jambo hili lenyewe ni maudhui tofauti iliyojadiliwa na wanachuoni kuhu- siana na Utume na misingi ya imani.

Baada ya hapo Mtume (s.a.w.w.) aliwasalia wale mashahidi wa Uhud na kisha akawazika mmoja mmoja au wawili wawili. Aliamrisha hasa kwamba ‘Amr bin Jumuh na Abdullah bin ‘Amr wanaweza kuzikwa kwenye kaburi moja, kwa kuwa walikuwa marafiki walipokuwa hai, na ingalikuwa bora kama wangalibakia pamoja vilevile baada ya kifo.40

Neno La Mwisho La Sa’ad Bin Rabi’

Sa’ad bin Rabi’ alikuwa mmoja wa wafuasi waaminifu wa Mtume (s.a.w.w.). Moyo wake ulikuwa umejaa imani na utiifu. Alipoanguka chini baada ya kupata majeraha kumi na mawili, mtu mmoja alipita karibu naye na akasema: “Wanasema kwamba Muhammad ameuwawa.”

Sa’ad akamwambia mtu yule: “Hata kama Muhammad kauwawa Mola wa Muhammad Yu hai, nasi tunafanya jihadi ili kuieneza itikadi ya Upweke wa Allah.”

Wakati miali ya vita ilipozimika, Mtume (s.a.w.w.) alimfikiria Sa’ad bin Rabi’ na akasema: “Ni nani awezaye kunipatia taarifa juu ya Sa’ad.” Zayd bin Thabit alilichukua jukumu la kuleta taarifa sahihi kwa ajili ya Mtume (s.a.w.w.) kuhusu Sa’ad kama yu hai au kauwawa. Alimkuta Sa’ad akiwa miongoni mwa wale waliolala na akamwambia: “Mtume amenituma ili nithibitishe juu ya hali yako na nimpelekee taarifa sahihi juu yako.”

Sa’ad akamjibu akasema: “Zifikishe salam zangu kwa Mtume na mwambie kwamba si zaidi ya muda kidogo tu wa maisha ya Sa’ad uliosalia na Ewe Rasuli wa Allah! Allah na Akulipe malipo yaliyo mema zaidi yamstahikiyo Mtume.” Vile vile aliongeza kusema:
“Zifikishe salam zangu kwa Ansar na kwa masahaba wa Mtume (s.a.w.w.) na waambie kwamba, kama Mtume akipatwa na dhara lolote lile wakati wao wakiwa hai, hatawapozwa na Allah.” Yule mtu aliyetumwa na Mtume (s.a.w.w.) alikuwa bado hajaondoka pale alipo Sa’ad wakati yeye Sa’ad alipokata roho.41

Huba ya mwanadamu juu na nafsi yake ina nguvu zaidi kiasi kwamba katu haisahau nafsi yake na hukitoa kila kitu kilicho chake kwa ajili ya kuihifadhi. Hata hivyo, nguvu ya itikadi na huba ya lengo na maslahi ya mtu katika fikara zake, ni kitu chenye nguvu zaidi, kwa sababu kama ilivyoelezwa dhahiri kwenye historia, huyu askari shujaa alijisahau mwenyewe katika wakati ule mgumu zaidi alipokuwa hayupo mbali kutoka kwenye kifo na alimkumbuka Mtume (s.a.w.w.), ambaye ulinzi wake ulikuwa njia kuu ya kulifikia lengo lake. Na ujumbe pekee alioupeleka kupitia kwa Zayd bin Thabit ulikuwa kwamba masahaba wa Mtume wasiwe wazembe wa usalama na ulinzi wake japo kwa kitambo kidogo tu.

Mtume (S.A.W.W.) Arejea Madina

Jua linasogea kuelekea magharibi na linaitupia miyonzi yake ya dhahabu kwenye ule upande wa pili wa nusu ya duinia. Sasa Uhud imetulia na kunyamaza kabisa.

Waislamu ambao baadhi ya wenzao wameuawa na wengine wamejeruhiwa, sasa wanalazimika kurejea majumbani mwao ili kwenda kuipata tena nguvu na kuvifunga vidonda vya wale waliojeruhiwa. Yule kamanda mkuu aliwaamrisha watu wake kuondoka na kuelekea madina. Mtume (s.a.w.w.) pamoja na Muhajiriin na Ansar baadae waliwasili mjini Madina. Mji ule ule ambao baadhi ya nyumba zake vilisikika vilio vya mama wa watoto na vya wake waliofiwa, waliowapoteza wana na waume zao.

Mtume (s.a.w.w.) alifika kwenye nyumba ya Bani Abdul Ashhal. Vilio vya wanawake wao vilimhuzunisha. Machozi yakaanza kumtiririka machoni mwake na akasema kwa sauti ndogo: “Ninapatwa na maumivu makali kwamba hakuna amliliaye Hamza.”42

Sa’ad bin Mu’aaz na wengineo walipotambua alichokitamani Mtume (s.a.w.w.), waliwaomba baadhi ya wanawake kufanya maombolezo kwa ajili ya Hamza, yule askari mwaminifu wa Uislamu. Mtume (s.a.w.w.) alipotambua hivyo aliwaombea wale wanawake na akasema: “Daima nimekuwa nikiufaidi msaada wa kiroho na kidunia wa Ansar.” Kisha aliwaomba wale wanawake kurudi majumbani mwao.

Kumbukumbu Zenye Kusisimua Za Mwanamke Mwaminifu

Maisha ya kujitolea mhanga ya wanawake kwenye kipindi cha awali cha Uislamu ni jambo la kushangaza na kutia moyo. Wakati tunaposema kwamba jambo la kushangaza, ni kwa sababu ni kwa nadra sana tunawaona wanawake walio mfano wao kwenye historia ya kisasa.

Siku hizi, kaulimbiu za ujasiri na ushujaa hutoka kwenye makoo ya wanawake wa ulimwengu huu na wanadai kuwa na nguvu na uthabiti utoshelezao kuyakabili matukio ya kutetemesha ya zama hizi, lakini hawawezi kuwa sawa na wale wanawake waumini na wenye kujitolea mhanga wa siku za awali za Uislamu. Nguvu na ufanisi wa wanawake wale ilikuwa ni matokeo ya moja kwa moja ya imani zao katika hukumu ya Allah na mategemeo yao juu ya malipo ya huko Akhera.

Bibi mmoja wa kabila la Bani Din?r, aliyempoteza mumewe, baba yake na kaka yake alikuwa ameketi miongoni mwa wanawake wengine na kulia huku akitiririkwa na machozi, na wale wanawake wengine walikuwa wakiomboleza. Mara ghafla Mtume (s.a.w.w.) alipita karibu na kile kikun- di cha wanawake. Huyu mwanamke aliyefiwa aliwauliza watu waliokuwa karibu naye kuhusu Mtume (s.a.w.w.). Wote wakamjibu: “Shukurani zimwendee Allah, yeye Mtume yu mzima kabisa.”
Yule mwanamke akasema: “Mimi ninapenda kumwona kwa karibu.” Mahali alipokuwa kasima- ma Mtume (s.a.w.w.) hapakuwa mbali. Hivyo wakamsoza kidole Mtume (s.a.w.w.). Yule mwanamke alipouona uso wa Mtume (s.a.w.w.), upesi sana aliisahau misiba yake yote na akalisema jambo litokalo kwenye kiini cha moyo wake, lililozaa mapinduzi akilini mwa wale wote waliokuwapo pale.

Alisema: “Ewe Mtume wa Allah! Mambo yote yasiyopendeza na misiba huwa rahisi katika njia yako.” (Yaani, kama wewe uko hai, tunachukulia kila msiba utukumbao kuwa jambo dogo mno, na tunalibeua).

Nausifiwe uimara huu na isifiwe imani hii ambayo humuweka mtu salama kutokana na kutokutengemaa kama vile nanga iwekavyo jahazi katika hali ya usalama kutokana na mawimbi inaposafiri baharini.43

Mfano Mwingine Wa Mwanamke Aliyejitolea Mhanga

Katika kurasa zilizotangulia tumemtaja kwa kifupi ‘Amr bin Jumuh. Ingawa bwana huyu alikuwa mlemavu, na haikuwa wajibu juu yake kufanya jihadi, alishikilia kushiriki, na baada ya kuruhusiwa na Mtume (s.a.w.w.) alijiunga na mujahidiin (askari wa Uislamu) watanguliao mbele. Sio tu kwamba alijiunga na safu za Mujahidiin, bali mwanawe Khallad na shemeji yake Abdullah bin Amr nae alishiriki kwenye hii jihadi takatifu na wote walikufa kishahidi.

Mkewe Hind bint Amr bin Hazm aliyekuwa shangazi yake Jabir bin Abdullah Ansar, alikuja pale Uhud. Alizikusanya maiti za mashahidi na wapenzi wake kutoka kwenye uwanja wa vita, akazipakia kwenye ngamia na akaondoka kwenda Madina.

Tetesi zilienea mle mjini Madina kwamba Mtume (s.a.w.w.) ameuawa. Wanawake walitoka kwenda Uhud ili kwenda kupata taarifa sahihi juu ya Mtume (s.a.w.w.). Akiwa njiani, Hind alikutana na wakeze Mtume (s.a.w.w.) waliomwuliza juu ya hali ya Mtume (s.a.w.w.).

Ingawa alikuwa kachukua maiti za mumewe, kaka yake na mwanawe katika ngamia, ali- waambia kwa utulivu kamili, kana kwamba hakuna msiba wowote uliomkumba: “Ninayo taarifa ya furaha kwa ajili yenu. Mtume yu hai na unapoifikiria baraka hii, misiba yote huwa kitu kidogo sana. Pili, Allah amewarudisha makafiri wakiwa wamejawa na hasira na ghadhabu.”44

Kisha aliulizwa kuhusu zile maiti alizozichukua kwenye ngamia. Alijibu: “Ni ndugu zangu. Mmoja wao ni mume wangu, mwingine ni mwanangu, na wa tatu ni kaka yangu. Ninawapeleka Madina nikawazike huko.”

Hapa tunaona kwenye historia ya Uislamu moja ya maelezo bora zaidi ya imani (yaani kule kuifikiria misiba yote kuwa rahisi, na kuzivumilia huzuni na matatizo kwa ajili ya kulifikia lengo la kiroho). Itikadi za kimaada haziwezi kuwafunza wanaume na wanawake kujitolea mhanga kwa kiwango hiki. Watu hawa wanapigana kwa ajili ya kulifikia lengo la kiroho na wala si kwa ajili ya faida za kidunia au kwa kujipatia vyeo.

Sehemu ya baadae ya kisa hiki ni yenye kustaajabisha zaidi na haiafikiani hata kidogo na kipimo cha kimaada na misingi iliyowekwa na walimwen- gu kwa ajili ya uchanganuzi wa matatizo ya kihistoria. Ni wale watu wa Mungu tu na wale wenye itikadi madhubuti juu ya Allah na msaada wake wawezao kuichanganua hadithi ifuatayo na wawezao kuichukulia kuwa ni kweli kabisa.
Yule mama (Hind) alikuwa kashika hatamu ya ngamia mikononi mwake na alikuwa akimwelekeza mjini Madina. Hata hivyo, yule ngamia alikuwa akisogea kwa taabu sana. Mmoja wa wakeze Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Kwa hakika mzigo ulioko juu ya ngamia huyu ni mzito sana” Hind akajibu: “Ngamia huyu yu mwenye nguvu mno naye anao uwezo wa kuchukua mzigo wa ngamia wawili na bila shaka iko sababu nyingine inayomfanya afanye hivi, kwa sababu kila ninapomgeuzia Uhud anatembea kwa urahisi sana, lakini kila nikimgeuzia Madina huwa anasogea kwa shida au anapiga magoti.

Hind akaamua kurudi Uhud na kumwarifu Mtume (s.a.w.w.) jambo hili. Hivyo akaja Uhud pamoja na yule ngamia na zile maiti na akamwarifu Mtume (s.a.w.w.) juu ya hali ya yule ngamia. Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Je, mumeo amemwomba nini Allah katika du’a yake pale alipokuwa akienda vitani?” Hind akajibu: “Amesema: “Ewe Mola wangu! Usinifanye nirejee nyumbani kwangu.” Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Sababu ya kukataa kwa ngamia kwenda Madina imedhihirika. Du’a ya mumeo imetakabaliwa. Allah hapendi kwamba maiti hii iende nyumbani kwa Amr. Ni muhimu kwamba uzizike maiti zote tatu kweye hii ardhi ya Uhud nawe huna budi kutambua kwamba watu hawa watatu watabakia kuwa pamoja huko kwenye ulimwengu mwingine pia.” Hind akiwa anachuruzikwa na machozi kutoka machoni mwake, alimwomba Mtume amwombee kwa Allah ili naye aweze kuwa pamoja nao.45

Mtume (s.a.w.w.) alifika nyumbani kwake. Macho ya binti wake mpenzi Fatimah Zahrah yaliangukia kwenye ule uso wake uliojeruhiwa na akaanza kutiririkwa na machozi machoni mwake. Mtume (s.a.w.w.) alimpa binti yake upanga wake ili ausafishe.

Ali bin Isa Arbali mwanahadithi na mwanahistoria wa karne ya saba Hijiriya anaandika hivi: “Binti yake Mtume alileta maji ili kuisafisha damu kutoka usoni mwa baba yake.

Amiri wa Waumini (a.s.) alimwagia maji na Zahrah akaisafisha ile damu kutoka pande zote, lakini kwa vile lile jeraha mle usoni lilichimbika sana, damu haikukoma kutoka. Mwishowe kipande cha mkeka kilichomwa na majivu yake yakapakwa kwenye kile kidonda na hapo ile damu ikakoma kutiririka kutoka mle kwenye jeraha la usoni mwake46

Ni Lazima Adui Afuatiliwe

Usiku ambao Waislamu walipumzika majumbani mwao mjini Madina baada ya tukio la Uhud, ulikuwa usiku nyeti mno. Wanafiki, Wayahudi na wafuasi wa Abdallah bin Ubayy walikuwa na shangwe kutokana na yale yaliyotokea kule Uhud. Vilio na maombolezo ya wale waliofiwa yaliweza kusikika kutoka kwenye nyumba nyingi. Zaidi ya yote hayo, ilikuwako hatari kwamba wanafiki na Wayahudi wangaliweza kuasi dhidi ya Waislamu, au kwa uchache tu wangaliweza kuuharibu ule umoja na utulivu wa kisiasa wa yale makao makuu ya Uislamu kwa kujenga tofauti na mifarakano miongoni mwa wakazi wake.

Uovu unaofanywa na tofauti za ndani ni mkubwa kuliko ule ufanywao na mashambulizi ya maadui wa nje. Hivyo basi, ilikuwa muhimu kwamba Mtume (s.a.w.w.) awaonye maadui wa ndani na kuwafanya waelewe kwamba nguvu ya Uislamu haiwezi kudhoofishwa kwa njia ya machafuko na ghasia, na kila kitendo cha propaganda chenye kuutishia msingi wa Uislamu kitakomeshwa tangu mwanzoni mwake kabisa kwa nguvu yote.

Mtume (s.a.w.w.) aliamrishwa na Allah kumuandama yule adui katika siku iliyofuatia usiku ule. Hivyo, alimteuwa mtu kutangaza katika sehemu zote za mji maneno haya: “Wale watu waliokuwa Uhud jana wajitayarishe kum- fuatilia adui kesho. Hata hivyo, wale wasioshiriki kwenye vita ile hawana haki ya kuungana nasi kwenye jihadi hii.”47
Hakuna shaka kwamba sharti hili liliwekwa kwa lengo zuri tu, lisiloweza kufichikana kwa mtu mwenye fikira za kisiasa; kwanza sharti hili ni aina ya shambulio kwa wale watu walioshindwa kushiriki kwenye Vita vya Uhud. Kwa hakika lilikuwa ni kukana mashindano na kundi lile ambalo halistahili ulinzi na kushiriki katika vita. Pili, ilikuwa ni adhabu kwa wale walioshiriki katika vita vya Uhud. Kwa kuwa Uislamu umepata pigo hili kutokana na utovu wao wa nidhamu, hivyo ilikuwa muhimu kwamba wafanye masahihisho kwa kushindwa huku ili kwamba hapo baadae wasionyeshe tena utovu wa nidhamu.

Tangazo lililotangazwa na yule mpiga mbiu wa Mtume (s.a.w.w.) lilifika masikioni mwa mtu mmoja wa kabila la Bani Ashhal, alipokuwa amelala pamoja na ndugu yake huku mwili umejeruhiwa.

Tangazo hili liliwa- tetemesha wote wawili kiasi kwamba, ingawa wote wawili hawakuwa na usafiri ila mnyama mmoja wa kupanda, na vile vile kuondoka kwao kulikuwa kwa taabu kutokana na sababu fulani fulani, waliambiana: “Si sahihi hata kidogo kwamba Mtume aende kwenye jihadi nasi tubakie nyuma.” Ingawa iliwalazimu ndugu hawa kuifanya safari hii kwa kupanda yule mnyama kwa kubadilishana, walifaulu kujiunga na askari wa Uislamu.48

Mtume (S.A.W.W) Aenda Hadi Hamraa’ul Asad

Mtume (s.a.w.w.) alimteuwa Ibn Ummi Maktum kuwa mwakilishi wake mjini Madina, na akaenda akapiga kambi Hamraa’ul Asaad mahali palipo umbali wa maili nane (kilometa kumi na tatu hivi) kutoka Madina. Ma’abad bin Khuzaa’, chifu wa kabila la Khuzaa’ah, ingawa alikuwa mwenye kuabudu masanamu, alionyesha huruma kwa Mtume (s.a.w). Watu wa kabila la Khuzaa’ wakiwemo Waislamu na wasio Waislamu, daima wamekuwa wakiwasaidia Waislamu.

Ili kumhudumia Mtume (s.a.w.w.) Ma’abad alikwenda kutoka pale Hamraa-ul Asad hadi Rawhah, makao makuu ya jeshi la Waquraishi na akakutana na Abu Sufyan. Aligundua kwamba Abu Sufyan alidhamiria kurudi Madina na kuiharibu ile nguvu ya Waislamu iliyobakia.

Ma’abad akamzuia asifanye hivyo na akasema: “Ewe Abu Sufyan! Jihadhari na Muhammad, ambaye hivi sasa yuko Hamraa-ul Asad. Ametoka Madina na jeshi kubwa, na wale wasioshiriki kwenye vita jana leo wako pamoja naye pia. Nimeziona nyuso zilizogeuka kutokana na ghadhabu na katu sijapata kuziona nyuso kama hizo maishani mwangu mwote. Wanasikitika mno kwa utovu wa nid- hamu uliotokea jana.” Aliielezea kwa maneno mengi mno ile nguvu ya Waislamu na moyo wao wa juu kiasi kwamba Abu Sufyan aliitupilia mbali ile dhamira yake.

Mtume (s.a.w.w.) pamoja na masahaba zake walikaa hapo Hamr?-ul Asad katika sehemu ya kwanza ya usiku, na akaamrisha kwamba uwashwe moto kwenye sehemu mbalimbali mle jangwani ili kwamba adui adhanie kwam- ba nguvu ya Waislamu ilikuwa kubwa kuliko ile waliyoiona kule Uhud. Safwaan Umayyah alimwambia Abu Sufyan hivi: “Waislamu wana hasira na wamekasirika. Ni bora kwamba tutosheke na kile tulichokipata tayari na turejee Madina.49

Muumini Wa Kweli Hadanganywi Mara Mbili

Sentensi hiyo hapo juu ni marudio ya maelezo ya Mtume (s.a.w.w.) aliyesema: “Muumini wa kweli haumwi mara mbili kwenye shimo moja.” Abu Azza Jumahi alipomwomba Mtume (s.a.w.w.) katika vita vya Badr amwachie huru, Mtume (s.a.w.w.) alimwachia huru, naye akamwahidi kwamba hatajiunga na wenye kuabudu masanamu katika matendo yao dhidi ya Uislamu. Hata hivyo, aliivunja ahadi yake kwa kushiriki katika Vita ya Uhud dhidi ya Uislamu, na hatimaye alipokuwa akirejea kutoka Hamraa’ul Asad, Waislamu wakamteka tena.
Mara hii, vile vile alimwomba Mtume (s.a.w.w.) amsamehe na amwachilie. Hata hivyo Mtume (s.a.w.w.) hakulisikiliza ombi lake na kwa kuitamka sentensi hiyo hapo juu (yaani ile isemayo ‘Muumini wa kweli haumwi mara mbili kwenye shimo moja) aliamrisha anyongwe. Kwa haya, ule msiba wa Uhud ambao ulikuwa ni wenye mafunzo kamili ulimalizikia.50

 • 1. Maghaazil-Waqidi, Juzuu 1, uk. 184-190; Tabaqaat, Juzuu 2, uk. 31-34; na Tarikhul Kamil, Juzuu 2, uk. 101.
 • 2. Wafasiri wa Qur'ani na wanahistoria kama vile Ali bin Ibrahim, Shaykh Tabrasi, (A'laamul wara') na Ibn Hisham, wanatofautiana juu ya suala la idadi ya askari. Hata hivyo, idadi hiyo tuliyoitaja hapo juu yaelekea kuwa ndio ya kweli.
 • 3. Maghaazil-Waaqidi, Juzuu 1, uk. 203-204, na baadhi ya wanahistoria wanaamini kwamba yule mjumbe aliileta ile barua mjini Madina Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa msikitini na Abi bin Ka'ab alimsomea.
 • 4. Bihaarul Anwaar, Juzuu 20, uk. 111.
 • 5. Maghaazil-Waaqidi, Juzuu 1, uk. 211.
 • 6. Bihaarul Anwaar, Juzuu 2, uk. 125.
 • 7. Maghaazil-Waaqidi, Juzuu 1, uk. 214; na Tabaqaatul-Kubra, Juzuu 2, uk. 38.
 • 8. Siiratu Ibn Hisham, Juzuu 2, uk. 65.
 • 9. Siiratu Ibn Hisham, Juzuu 2, uk. 9
 • 10. Bihaarul Anwaar, Juzuu 20, uk. 57.
 • 11. Usudul Ghabah, Juzuu 2, uk. 59; na Bihaarul Anwaar, Juzuu 20, uk. 57.
 • 12. Maghaazil-Waaqid, Juzuu 1, uk. 221-222.
 • 13. Siiratu Ibn Hisham, Juzuu 2, uk 66.
 • 14. Siiratu Ibn Hisham, Juzuu 2, uk. 68-69.
 • 15. Siiratu Ibn Hisham, Juzuu 2, uk. 12.
 • 16. Hakusudii kwamba waisilamu walikuwa wakiwatusi watu pale, bali ina- maana kuwa ile hali halisi iliyokuwa dhidi ya adui kwake yeye adui aliichukulia kuwa ni matusi, ukizingatia kuwa adui alikuwa akijiona ni jeshi lenye nguvu na heshima katika Rasi ya Uarabu, hivyo mashujaa wake wanapogaragazwa kwa namna ile ni sawa na tusi kwao - Mhariri
 • 17. Taarifa ya washika bendera tisa waliouawa na Sayyidna Ali (a.s.) imenukuli- wa mwenye Bihaarul Anwaar, Juzuu 2, uk. 51.
 • 18. Khisaal, Juzuu 2, uk. 121. 220
 • 19. Siiratu Ibn Hisham, Juzuu 2, uk. 68; na Tarikhut-Tabari, Juzuu 2, uk. 194.
 • 20. Siiratu Ibn Hisham, Juzuu 2, uk. 83.
 • 21. Sisi bado tuna shaka na kauli ya Ibnu Hishamu ifidishayo kuwa Anas alifia viwanja vile, pale aliposema: "Anas alipata majeraha makubwa kwenye vita hivi na hakuna aliyeweza kuitambua maiti yake ila dada yake tu." Kwa sababu yanapingana na masimulizi ya Anas mwenyewe, hivyo tunalazimika kujiuliza: Je Anas alisimulia yale masimulizi yake pale uwanjani vitani au baadaye? Na kama ni baadaye basi aliwezaje kusimulia wakati alikuwa kishakufa? Na kama alisimulia pale vitani basi nalo akili haikubali kwani hali halisi ya kivita haikuruhusu kuanza kusimulia hayo pale, na hasa ukizingatia hekaheka yake pale. Na zaidi ya hapo ni kuwa simulizi zake zaonyesha kuwa yeye Anasi alikuwa akisimulia mambo yaliyotokea vitani, hivyo ni lazima itakuwa alisimulia baada ya vita - Mhariri.
 • 22. Tarikhul Kamil, Juzuu 2, uk. 109.
 • 23. Ibn Hadid, Sharhun- Nahjul Balaghah, Juzuu 15, uk. 23-24.
 • 24. Ruba'iyat ni yale meno (manne kwa idadi) ambayo yako kati ya meno ya mbele na meno ya kukatia.
 • 25. Siiratu Ibn Hisham, Juzuu 2, uk. 84; na Maghaazil-Waaqidi, Juzuu 1, uk. 244.
 • 26. Tarikhul Kamil, Juzuu 2, uk. 107.
 • 27. Ibn Abi Hadid, Sharhun-Nahjul- Balaghah, Juzuu 5, uk. 21.
 • 28. Tarikhul Kamil, Juzuu 2, uk. 107.
 • 29. Vile vitabu sita vya Hadith vilivyo sahihi miongoni mwa Ahlil Sunna.
 • 30. Ibn Abil Hadid, Sharhun-Nahjul Balaghah, Juzuu 14, uk. 251
 • 31. Khasaal, Juzuu 2, uk. 15.
 • 32. Siiratu Ibn Hishamu, Juzuu 2, uk. 14.
 • 33. Siiratu Ibn Hisham, Juzuu 2, uk. 18.
 • 34. Bihaarul Anwaar, Juzuu 20, uk. 84 na kuendelea.
 • 35. Nasikhut-Tawaarikh, juzuu 1, uk. 357.
 • 36. Siiratu Ibn Hisham, Juzuu 2, uk. 69-72.
 • 37. Mlolongo wa huduma za mwanamke huyu aliyejitolea mhanga haukumal- izikia hapa. Baadae alishiriki pamoja na mwanawe kwenye kampeni dhidi ya Musaylimah Kadhab (Mdanganyifu) na akapoteza mkono kwenye vita vile.
 • 38. Abil Hadid, Sharhun-Nahjul Balaghah, Juzuu 14, uk. 265-267.
 • 39. Bihaarul Anwaar, Juzuu 20, uk. 44-45.
 • 40. Siiratu Ibn Hisham, Juzuu 2, uk. 498; Bihaarul Anwaar, Juzuu 20, uk. 131.
 • 41. Siiratu Ibn Hisham, Juzuu 2, uk. 95.
 • 42. Siiratu Ibn Hisham, Juzuu 2, uk. 99.
 • 43. Siiratu Ibn Hisham, Juzuu 2, uk. 99.
 • 44. Kufuatana na ilivyonakiliwa na Ibn Abil Hadid, Hind aliisoma Aya ya Qur'ani isemayo:
  "Na Allah amewarudisha waliokufuru na ghadhabu yao; hawakupata faida yoyote; na Allah amewatoshea waumini katika mapigano; na Allah Yu Mwenye uwezo, Mwenye nguvu."(Surah al-Ahzaab, 33:25). Kisha anasema: "Hakika ameitaja maana ya sehemu ya kwanza ya Aya, kwa sababu Aya hii ilifunuliwa wakati wa Vita vya Handaq (Ahzaab), iliyopiganwa baada ya Vita vya Uhud." (Sharhun- Nahjul Balaghah, Juzuu 14, uk. 262).
 • 45. Maghaazil-Waaqidi, Juzuu 1, uk. 265.
 • 46. Kashful Ghummah, uk. 54.
 • 47. Siiratu Ibn Hisham, Juzuu 2, uk. 101.
 • 48. Siiratu Ibn Hisham, Juzuu 2, uk. 101.
 • 49. Tabaqaatul Kubra, Juzuu 2, uk 49.
 • 50. Siiratu Ibn Hisham, Juzuu 2, uk. 104.