Sura Ya 32.: Maelezo Mafupi Juu Ya Wafungwa Watokanao Na Familia Ya Husein.

Maelezo yamekwishatolewa katika Sura ya nyuma kuhusu kila shahidi wa Karbala. Sasa zinafuata taarifa fupifupi juu ya wale walio mashuhuri mion- goni mwa watu wa Husein waliosalimika vitani ambao walishikiliwa mateka:

1. Ali bin Husein alikuwa mtoto mkubwa wa Husein alizaliwa mwaka wa 38 A.H wakati babu yake Ali alipokuwa ndiye Khalifa, na alikuwa chini ya umri wa miaka mitatu wakati Ali alipouawa katika mwaka wa 40 A.H. Alikuwa zaidi kidogo ya miaka 22 umri wake wakati alipofuatana na baba yake katika safari ya kwenda Iraq. Haijulikani lini haswa alipatwa na maradhi, lakini mwezi 10 ya Muharram mwaka wa 61 A.H alikuwa mnyonge sana kiasi cha kushindwa hata kukaa tu, na kwa hivyo hakuweza kushiriki katika jihadi hiyo ya Karbala.

Baada ya kuuawa wafuasi wote, marafiki na ndugu wa Husein, na yeye Husein mwenyewe, Ali bin Husein alichukuliwa mateka na akafungwa minyororo.Alilazimika kuchukua safari iliyo na maumivu na udhalilishaji kutoka Karbala hadi Kufa, na kutoka hapo kwenda Syria kwa miguu pamoja na wanawake wa familia yake.

Hali yake lazima haikuwa ya kutweza kudogo ya kuhudhuria baraza ya Ibn Ziyad kule Kufa na ile ya Yazid mjini Damascus, ambako yeye, mama zake, shangazi na wanawake wengine wa familia yake walifikishwa mbele ya baraza hizo kama wafungwa.

Baada ya kuachiwa huru huko Syria, yeye alikwenda Madina kutumia muda uliobakia wa maisha yake katika Sala. Alifariki katika mwaka wa 96 A.H. Majina yake yanayofahamika sana ni Zayn al-Abidin na Sayyid al- Sajjad na ameacha mkusanyiko wa maombi yake mwenyewe na dua kwa kitabu kifahamikacho kama al-Sahifa al-Kamila ambacho ni kitabu kinachotukuzwa sana. Kaswida (taabini) ya al-Farzdaq kumhusu yeye ni sanaa kubwa katika fasihi ya Kiarabu.

2. Zainab alikuwa binti mkubwa wa Ali na Fatimah, binti ya Mtume. Alikuwa ameshika nafasi ya kuonekana wazi mno miongoni mwa watu wa Husein waliopona katika vita. Alikuwa bado mdogo sana wakati mama yake alipofariki dunia. Baba yake alimlea na kumkuza na alimwoza kwa Abdallah, mtoto wa ndugu yake Ja’far. Alifuatana na Husein kutoka Madina hadi Karbala na wakati huo alikuwa na umri wa miaka kama 50 hivi.

Wakati mmoja, aliposikia kutoka kwa Husein hapo Karbala kwamba hati- mae amejiandaa mwenyewe kwa ajili ya kifo, kwani kulikuwa hakuna njia mbadala iliyobaki kwake, wakati Zainab alipojipiga uso wake na kupasua nguo zake kutokana na huzuni iliyozidi kiwango, al-Husein alimuapisha asitatue vazi lake au kujiparura uso wake au kunyanyua sauti kubwa ya maombolezo kwa ajili yake baada ya kifo chake.

Zainab aliyatia moyoni maelekezo haya na katika hali zilizokuwa na mitihani mkali sana hakuzisaliti ishara zozote za hofu isiyofaa na ikaweza kuleta kufurahia miongoni mwa maadui kwa mateso apatayo. Alikuwa ni yeye Zainab ambaye alimpa Husein nguo ya kuvaa ndani kati ya nguo zake zote nyingine za ndani, na aliipasuapasua katika sehemu nyingi mbalimbali ili kuifanya isifae kwa makusudio ya kuporwa baada ya kifo chake.

Baada ya tarehe 10 ya Muharram, msafara wa watu wa Husein waliopona vita uliondoka Karbala, ukitanguliwa na vichwa vya mashahidi vilivyoinuliwa kwenye mikuki, pamoja na Ali bin Husein, dhaifu na aliyefungwa minyororo, akifuatia kwa miguu ngamia waliowabeba wanawake na watoto na wakawasili Kufa, makao ya serikali ya Ubaydullah bin Ziyad, mji ulikuwa umewekwa katika hali nzuri, sehemu ya sokoni ilipambwa na watazamaji walisongamana sehemu zote zenye kufaa kutazamia mambo ili kuuangalia msafara wa wale ambao, kama walivyoambiwa, walikuwa ni maadui wa Waislamu.

Katika mazingira haya ambayo yalikuwa siyo ya kirafiki kabisa na katika hali zenye kuvunja moyo kupita kiasi na kuhuzunisha, Zainab alitoa hotuba nzito, ambayo ndani yake hakuelezea hali yake ya kuhuzunisha na kusikitisha, wala hakuomba afanyiwe huruma bali kwa lawama kali kabisa aliyapitia tena yale matendo ya kihaini ya maadui zake na kuwataka kuzichunguza nyoyo zao na kutafakari juu ya makosa yao mabaya.

Macho yote yaliyokuwa yameamshwa kushuhudia taabu na mateso ya wafungwa hao yaliinamishwa chini kwa aibu. Ufasaha huohuo ulikuwemo kwenye hotuba yake ndani ya baraza ya Yazid huko Damascus.
3. Umm Kulthumu alikuwa bint wa pili wa Ali na Fatimah, mdogo kuliko Zaynab. Jina lake lilikuwa Zaynab al-Sughra na Umm Kulthumu lilikuwa ndiyo ‘Kuniyat’ yake. Aliolewa na binamu yake aitwaye Muhammad bin Ja’far bin Abi Talib na alifanywa mjane wakati baba yake akiwa yungali hai. Baada ya kifo cha mume wake, aliishi na ndugu (kaka) zake. Alifuatana na Husein wakati alipoondoka Madina kwenda Makkah na akabaki naye mpaka kuuawa kwake kishahidi. Yeye pia alitoa khutba ya kusisimua sana katika sehemu ya sokoni hapo Kufa baada ya khutba ya Zainab.
4. Rukaya alikuwa bint ya Ali bin Abi Talib kwa mke wake Umm Wahb, bint ya Rabia. Rukaya na kaka yake mmoja aitwaye Umar walizaliwa mapacha. Aliolewa na Muslim bin Aqil.

Yeye pamoja na mumewe walifuatana na Husein kutoka Madina, na aliendelea kubakia naye wakati mume wake alipotumwa kwenda Kufa kutoka Makkah. Katika mwendo wa safari ya Husein kutoka Makkah taarifa ziliwasili za kuuawa kishahidi kwa mume wake, aliendelea kusafiri na kaka yake mpaka alipokwishafika Karbala alimtoa mhanga mwanawe, Abdallah bin Muslim kwa ajili ya Husein mnamo mwezi 10 Muharram mwaka wa 61. A.H. Alishiriki pamoja na Zainab na Umm Kulthumu, dada zake, katika taabu zote kubwa na za huzuni zilizowakuta watu wa Husein waliopona vita, na hatimaye alirejea pamoja nao Madina.

5. Layla al-Thaqafiyya alikuwa mama wa Ali al-Akbar bin Husein. Uhusiano wake na Mu’awiyah na Yazid kumetajwa katika maelezo yenye kumhusu Ali al-Akbar. Alikuwa pamoja na Husein hapo Karbala na alishiriki katika matatizo na dhiki za kuchukuliwa mateka pamoja na dada zake Husein.

6. Rabab bin Imru al-Qays alikuwa ndiye mama yake Sakina bint Husein na ndugu yake wa kiume, Ali al-Asghar bin Husein (Abdallah). Alikuwa hapo Karbala, akiwa amefautana na Husein kutoka Madina. Alipitia miti- hani yote ambayo wanawake waliosalimika wa familia ya Husein walikabiliana nayo, lakini badala ya kurejea pamoja nao Madina wakati waliporejeshwa uhuru wao alibakia Karbala katika hema lililoko karibu na kaburi la Husein kwa mwaka mmoja, na akawa anakusanya makundi ya watu, mchana na usiku kuomboleza mauaji ya bint ya Husein. Rabab alirejea Madina baada ya mwaka na hapo napo pia aliutumia wakati wake katika kumlilia Husein, na tendo hili lilichukua muda mrefu.

7. Mama wa Fatimah bint Husein alikuwa Umm Ishaaq bint Talha bin Ubaydullah al-Taymi. Hasan al-Muthanna, mtoto wake Imam Hasan alim- womba ami yake, Husein kumpa mmoja wa bint zake amwoe. Hata hivyo, alizuiliwa na adabu kuonyesha chaguo lake. Husein alimchagua Fatimah kwa ajili ya ndoa hiyo iliyopendekezwa kwa vile yeye alifanana sana na mama yake mwenyewe, Fatimah, bint ya Mtume.

Wakati Husein alipokuwa anaondoka kwenda kwenye jihadi ya mwisho alikabidhi wasia wake na nyaraka nyingine muhimu kwa Fatimah zije kutolewa kwa Ali bin Husein wakati atakaporejewa na fahamu zake. Alibakia hai kwa miaka mingi baada ya msiba wa Karbala na anatambuli- ka kama msimuliaji wa hadith. Mtoto wake wa kiume Abdallah bin al- Mahd alikuwa akisimulia hadithi kutoka kwake. Wakati mume wake, Hasan bin al-Hasan, alipofariki dunia, alifunga wakati wa mchana na aliu- tumia usiku wote katika Sala mara kwa mara kwa kipindi cha mwaka mzima katika hema lililosimamishwa karibu na Kaburi lake. Kisha alirejea Madina.

8. Sakina bint Husein alikuwa dada kamili wa Ali al-Asghar. Alikuwa mdogo sana wakati vita vya Karbala vilipopiganwa. Maelezo ya maisha yake, baada ya tukio hilo yamekosa uthibitisho wa kutegemeka. Sasa yanafuata maelezo mafupi ya wanawake ambao kwa namna fulani maalum walihusika na matukio ya Karbala ingawaje hawakuwa pamoja na Husein katika tarehe 10 ya Muharram.

(1) Umm Salama alikuwa mwanamke mwenye tabia njema za kipekee sana miongoni mwa wake za Mtume, ambaye alimwoa katika mwaka wa pili baada ya kuhama Makkah. Alikuwa amebakia hususan hasa katika kuwapenda watu wa Nyumba ya Mtume hata baada ya kifo cha Mtume.

Al-Tirmidhi ameelezea kwamba tarehe 10 ya Muharram aliona katika ndoto Mtume akilia, kichwa chake na ndevu vyote vimefunikwa na vumbi, na alimwambia kwamba Husein ni hivi karibuni tu amekwishauawa.
(2) Umm al-Banin Fatimah bint Hizaam bin Khalid alikuwa amechaguliwa na Aqil kwa ombi la ndugu yake Ali bin Abi Talib, kama mwanake aliyetoka kwenye familia ifahamikayo waziwazi kwa ushujaa na ujasiri, ili kwam- ba kizazi chake kutokana naye (mwanamke huyu) kiweze pia kuwa jasiri sana na kujaaliwa kupata sifa za kijeshi. Alikuwa na watoto wanne wa kiume majasiri ambao katika hao Abbas alikuwa ndiye mkubwa na wote hao waliojitolea mhanga maisha yao kwa ajili ya Husein mnamo mwezi 10 ya Muharram.

Haiwezekani kueleza hisia nzito za huzuni zilizohisiwa na mama ambaye alipoteza vijana wanne mashujaa katika siku moja ndani ya masaa machache tu! Imesimuliwa kwa uaminifu kabisa kwamba, baada ya kupa- ta taarifa za msiba wa Karbala, Umm al-Banin alitumia kwenda kila siku kwenye maeneo ya makaburi ya al-Baqi na mtoto mdogo wa kiume wa Abbas, aliyeitwa Ubaydullah, ili kusoma hapo mashairi ya maombolezo kuhusu Abbas ambayo yalikuwa ni yenye kuumiza sana nyoyo yaliyoweza kuvuta watu, siyo wa Madina tu bali pia wakati mwingine hata yule adui mkubwa wa watu wa nyumba ya Mtume kama vile Marwan kuyasikiliza yakisomwa.

Ingefaa kuongeza maelezo mafupi hapa kuhusu wale wanawake pia ambao walikuwa wamehusiana na baadhi ya wafuasi wa Husein, na walifanya kitu chenye umuhimu maalum kuhusiana na matukio ya Karbala. Maelezo haya ni kama ifuatavyo:

1. Dalham bint Amr alikuwa mke wa Zuhayr bin al-Qayn. Alikwenda pamoja na mumewe kutekeleza ibada ya Hijja katika mwaka wa 60 A.H na katika kurudi kwao walitokea kukaa Zaruud mahali ambapo Husein alikuwa naye pia akikaa akiwa katika safari yake ya kutoka Makkah kwenda Iraq. Zuhayr bin al-Qayn alikuwa wakati huo ni miongoni mwa kundi la Waislamu la Uthman na alikuwa na mshughuliko mdogo sana na familia ya watu wa nyumba ya Mtume (Ahlil Bait). Husein alimtuma mtu mmoja kwenda kwa Zuhayr kumtaka Zuhayr amwone.

Zuhayr hakupenda kuonana na Husein, na ilikuwa ni mke wake Dalhan, aliyemwonyesha ni kuchukiza kusikofaa kiasi gani, kwa yeye kukataa kwenda kuonana na mjukuu wa Mtume. Hivyo Zuhayr akihimizwa na mke wake alikwenda kuonana na Husein na alirejea akiwa ni mtu aliyekwishabadilika kabisa, akiwa kipenzi cha Husein ambaye alijitoa mhanga maisha yake kwa ajili ya Husein.

Zuhayr alimtaliki Dalham na kumrudisha kwa mama yake, na yeye mwenyewe akafuatana na Husein kwenda Karbala.

2. Umm Wahb bint Ma’bad alikuwa mke wa Abdallah bin Umayr al-Kalbi. Waliishi Kufa. Wakati Abdallah bin Umayr alipotambua maandalizi ya hali ya kivita ya Ubaydullah bin Ziyad pale Nukhayla, na kuwasili kwa Husein Karbala, aliwasilisha nia yake ya kwenda kumsaidia Husein kwa mke wake ambaye mara moja, bila ya kupinga alikubali na akamwomba amchukue pamoja naye pia kwenda Karbala.

Kwa hiyo, wote wawili waliondoka kwenda Karbala usiku mmoja na kuungana na Husein na wafuasi wake. Alikuwa ni mwanamke pekee aliyeuawa hapo Karbala na damu isiyo na hatia ya mwanamke huyu asiye na ulinzi iliyomwagika hapo Karbala iliongeza sura mpya kwenye maovu yaliyotendwa hapo.

3. Mke wa Muslim bin Awsaja alikuja na mume wake mpaka Karbala. Alimpeleka mke wake kukaa katika hema zilizokuwa zikitumiwa na wanawake wa familia ya Husein.

4. Bahriyya bint Mas’ud, alikuwa mke wa Janaada bin Ka’b al-Ansari. Alifuatana na Husein pamoja na mume wake kutoka Makkah. Alimtuma kijana wake, Amr bin Janaada kwenda kujitoa mhanga maisha yake kwa ajili ya Husein, baada ya Janaada mwenyewe alipokwisha kutana na kifo cha kishahidi. Mama huyo alikitupa kuwarudishia maadui kichwa cha yule mwanawe ambaye maadui hao walikuwa wamekitupia kwenye jeshi la Husein na mama huyo akamshangilia mwanawe kwa mhanga wake ulio- tukuka ambao ulimfanya awe na furaha isiyo na kifani.