Aya 53: Nafsi
Mwanadamu ni mnyama mwenye akili na dini. Yeye kwa unyama wake au kwa nafsi yake anapondokea sana kwenye matamanio na starehe, hajali akili wala dini. Lakini kwa dini yake na akili yake anaizuia nafsi yake na akili yake isipetuke mipaka ya sharia.
Kwa hiyo mwenye kuiachia nafsi yake ifanye vile itakavyo, basi yeye ni mnyama katika sura ya binadamu, bali ni afadhali mnyama, kwa vile binadamu ana majukumu na ataulizwa, lakini mnyama hana majukumu yoyote. Ndio maana Mwenyez Mungu akasema:
إِنْ هُمْ إِلَّا كَالْأَنْعَامِ ۖ بَلْ هُمْ أَضَلُّ سَبِيلًا {44}
Ni kweli kwamba wakati mwingine mtu anaweza kuwa dhaifu mbele ya matamanio, lakini muumin mwenye akili anarudi kwenye uongofu wake na kutubia; Mwenyezi Mungu naye humsamehe, kwa sababu ni Mwingi wa Maghufira, Mwenye kurehemu.
Kauli yake Mwenyezi Mungu: “Ispokuwa ile ambayo Mola wangu ameirehemu.” Maana yake ni kuwa nafsi yoyote haiwezi kusalimika na kasoro isipokuwa ile aliyoihifadhi Mwenyezi Mungu kutokan na makosa na madhambi (isma) kama nafsi za mitume na maimamu. Muhimu ni kutong’ang’ania mkosaji na kuachana kabisa na Mola wake. Imam Ali (a.s.) anasema: “Dhambi kubwa ni ile ambayo mwenyewe ameipuuza” yaani ameing’ang’ania na wala asiombe msamaha.
وَقَالَ الْمَلِكُ ائْتُونِي بِهِ أَسْتَخْلِصْهُ لِنَفْسِي ۖ فَلَمَّا كَلَّمَهُ قَالَ إِنَّكَ الْيَوْمَ لَدَيْنَا مَكِينٌ أَمِينٌ {54}
قَالَ اجْعَلْنِي عَلَىٰ خَزَائِنِ الْأَرْضِ ۖ إِنِّي حَفِيظٌ عَلِيمٌ {55}
وَكَذَٰلِكَ مَكَّنَّا لِيُوسُفَ فِي الْأَرْضِ يَتَبَوَّأُ مِنْهَا حَيْثُ يَشَاءُ ۚ نُصِيبُ بِرَحْمَتِنَا مَنْ نَشَاءُ ۖ وَلَا نُضِيعُ أَجْرَ الْمُحْسِنِينَ {56}
وَلَأَجْرُ الْآخِرَةِ خَيْرٌ لِلَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ {57}