Aya 58-62: Wakaja Nduguze Yusuf
Wakaja ndugu zake Yusuf wakaingia kwake. Yeye akawajua na wao hawakumjua.
Kahati ilienea mpaka miji ya jirani, ikiwemo Palestina na Kanani aishipo Nabii wa Mungu, Ya’qub. Ikawa imeenea habari kwamba waziri wa Misr amejiandaa vizuri kuikabili njaa na kwamba yeye anagawanya chakula kwa uadilifu bila ya kumbagua yeyote.
Nyumbani kwa Ya’qub kukawa na shida, kama iliyoko katika majumba mengine. Hivyo akawaamrisha wanawe waende Misr kuhemera chakula.
Basi wakaondoka kuelekea Misr wakiwa ni watu kumi. Walipofika huko waliingia makao ya waziri wakamkuta Yusuf, kwa sababu alikuwa akisimamia kazi yeye mwenyewe. Yusuf akawatambua, lakini wao hawakumatambua.
Alipowatengenezea mahitaji yao
Baada ya kuwaandalia mahitaji yao yote pamoja na yale ya safari, aliwaambia: “Nileteeni ndugu yenu kwa baba.”
Wafasiri wanasemakuwaYusufaliwakirimusananduguzakempaka wakawa hawana wasiwasi naye; wakazungumza naye kuhusu maisha yao na ya baba yao na kwamba wao wana ndugu yao mdogo wa baba mmoja. Ndipo Yusuf akawaambia basi nileteeni huyo ndugu yenu mdogo.
Katika Aya hakuna linalofahamisha kuwa walizungumza naye, lakini kuhusu kuwakirimu kunafahamishwa na kauli:
Je hamuoni kuwa mimi ninatimiza kipimo na kwamba mimi ni mbora wa wakaribishao?
Msiponiletea basi hampati kipimo chochote kwangu wala msinikurubie
Maana yako wazi. Kwa mnasaba wa Aya hii, wamekongamana mafakihi kwamba inafaa kwa muuzaji na mnunuzi kuweka sharti lolote apendalo katika biashara, maadam haliharamishi halali wala kuahalalisha haramu. Na sharti la Yusuf ni katika aina hii.
Wakasema: “Tutamrairai baba yake; na hakika sisi tutafanya.”
Wao walikuwa wanajua kuwa baba yao si rahisi kumtoa, ndio maana wakasema kuwa watamrairai; yaani watajitahidi na kumbembeleza baba yao; pamoja na ugumu wa jambo lenyewe.
Akawaambia watumishi wake: “Tieni bidhaa zao katika mizigo yao Yusuf aliwaamrisha watumishi wake warudishe vile vitu walivyonunulia chakula kwenye mizigo yao, bila ya wao kutambua.
Ili wazione watakaporudi kwa watu wao wapate kurejea tena kwa kuwa na tamaa ya ukarimu wa Yusuf. Sio mbali kuwa lengo la Yusuf ni kumtuliza baba yake ili asione uzito kumwachia ndugu yake aje kwake.
فَلَمَّا رَجَعُوا إِلَىٰ أَبِيهِمْ قَالُوا يَا أَبَانَا مُنِعَ مِنَّا الْكَيْلُ فَأَرْسِلْ مَعَنَا أَخَانَا نَكْتَلْ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ {63}
قَالَ هَلْ آمَنُكُمْ عَلَيْهِ إِلَّا كَمَا أَمِنْتُكُمْ عَلَىٰ أَخِيهِ مِنْ قَبْلُ ۖ فَاللَّهُ خَيْرٌ حَافِظًا ۖ وَهُوَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ {64}
وَلَمَّا فَتَحُوا مَتَاعَهُمْ وَجَدُوا بِضَاعَتَهُمْ رُدَّتْ إِلَيْهِمْ ۖ قَالُوا يَا أَبَانَا مَا نَبْغِي ۖ هَٰذِهِ بِضَاعَتُنَا رُدَّتْ إِلَيْنَا ۖ وَنَمِيرُ أَهْلَنَا وَنَحْفَظُ أَخَانَا وَنَزْدَادُ كَيْلَ بَعِيرٍ ۖ ذَٰلِكَ كَيْلٌ يَسِيرٌ {65}
قَالَ لَنْ أُرْسِلَهُ مَعَكُمْ حَتَّىٰ تُؤْتُونِ مَوْثِقًا مِنَ اللَّهِ لَتَأْتُنَّنِي بِهِ إِلَّا أَنْ يُحَاطَ بِكُمْ ۖ فَلَمَّا آتَوْهُ مَوْثِقَهُمْ قَالَ اللَّهُ عَلَىٰ مَا نَقُولُ وَكِيلٌ {66}