Aya 94-98: Nasikia Harufu Ya Yusufu
Na ulipoondoka msafara, baba yao alisema: “Hakika mimi ninasikia harufu ya Yusuf, lau kama hamtanipuuza.”
Kuondoka msafara ni kuondoka pale ulipokuwa, ambapo ni Misr na kuelekea nchi ya Kanani alipokuwa akikaa Ya’qub. Kupuuza ni kumtuhumu na upotofu.
Dhahiri ya Aya inafahamisha kuwa Ya’qub alinusa harufu ya kanzu ya Yusuf kwa mbali mara tu msafara ulipoanza kuondoka, kabla ya kumaliza nchi ya Misr; ingawaje masafa yalikuwa marefu.
Aliyechukua kanzu ya Yusuf alikuwa masafa ya mwendo wa siku nane, na imesemekana ni siku kumi. Wafasiri wamelibakisha neno na dhahiri yake, wakasema kuwa Ya’qub alipata harufu ya Yusuf hasa pamoja na umbali wa masafa na wakazingatia huo ni muujiza aliomuhusisha nao Mwenyezi Mungu Ya’qub.
SiombalikuwaharufuyaYusufnifumbolamakisioyakutokatatamaa amabayo, huwapata baadhi ya watu; hasa wale wenye nyoyo safi. Na kwamba moyo wa Ya’qub ulihisi kukurubiana kukutana na Yusuf, kwa hiyo akalifasiri hilo kwa harufu.
Maana hayo yanatiwa nguvu na kwama Ya’qub hakukata tamaa ya kukutana na Yusuf hata mara moja. Hilo linatolewa ushahidi na kauli zake katika Sura hii; kama ifuatavyo:
“Enyi wanangu! Nendeni mkamtafute Yusuf na nduguye wala msikate tamaa na faraja ya Mwenyezi Mungu. “ Aya 87 “Huenda Mwenyezi Mungu akaniletea wote pamoja.” Aya 83 “Ewe mwanangu! Usiwasimulie ndugu zako ndoto yako wasije wakakufanyia vitimbi.” Aya 5, Juz.12 “Na kadhalika Mola wako atakuteua na atakufundisha tafsiri ya mambo na atatimiza neema yake juu yako.” Aya 6, Juz.12 “Mimi ninajua kutoka kwa Mwenyezi Mungu yale msiyoyajua” Aya 96.
Wakasema: “Wallah hakika wewe bado uko katika upotevu wako wa zamani.”
Waliosema ni wale waliokuwepo alipokaa Ya’qub aliposema nasikia harufu ya Ya’qub. Maana ni kuwa waliokuwepo walimwambia Ya’qub kuwa wewe unakosea katika kung’ang’ania kwako kumngoja Yusuf ambaye amekwishakwenda, kama walivyokwenda wengine waliokufa.
Alipomfikia mbashiri aliitupa kanzu usoni pake akarejea kuona
Ya’qub hakukosea katika hisia zake. Mbashiri (Mwenye kuleta habari njema) alimjia akiwa amechukua kanzu ya Yusuf; mara tu, ile kanzu ilipogusa uso wa Ya’qub, neema ya kuona ikarudi na furaha ya maisha. Inasemekana kuwa aliyechukua kanzu ya Yusuf ni yule yule aliyechukua kanzu iliyotapakazwa damu ya uwongo, miaka arubaini iliyopita, ili afute uovu kwa wema. Vile vile inasemekana kuwa hakuna ajabu ya Ya’qub kurudiwa na macho kwa furaha, kwani mara nyingi raha na furaha huponyesha magonjwa. Majaribio ya tiba yanathibitisha hilo.
Akasema: “Je, sikuwaambia kuwa mimi ninajua kutoka kwa Mwenyezi Mungu yale msiyoyajua?”
Hii inaashiria kauli yake katika Aya 86 ya Sura hii: “Akasema: Majonzi yangu na huzuni yangu ninamshtakia Mwenyezi Mungu Na ninajua kwa Mwenyezi Mungu yale msiyoyajua”
Wakasema: “Ewe baba yetu tuombee maghufira kwa dhambi zetu, hakika sisi tulikuwa wenye hatia.”
Ndugu zake Yusuf walijuta kwa kitendo chao, wakatubia makosa yao, na wakamuomba baba yao awaombee kwa Mwenyezi Mungu kuwatakabalia toba yao na awaghufurie dhambi zao na wakajiwekea sharti la kutorudia maasi.
Akasema: “Nitawaombea msamaha kwa Mola wangu. Hakika yeye ni Mwingi wa msamaha, Mwenye kurehemu.”
Mmojawapo wa wafasiri wa kisasa anasema: “neno ‘nita’ haliepuki kuwa kwenye moyo wa mtu aliyejeruhiwa” anamaanisha kuwa moyo wa Ya’qub bado una kitu kwa watoto wake, pamoja na toba yao na kuomba kwao masamaha.
Lakini huku ni kutatizika na kufanya makisio kwa nyoyo za mitume na za watu wengine. Ilivyo hasa ni kuwa Ya’qub, aliahirisha kuwaombea dua mpaka awe faragha katika mkesha wenye giza aweze kumwomba Mola wake awatakabalie toba. Kwa sababu hilo linapelekea kukubaliwa dua. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anasema:
وَبِالْأَسْحَارِ هُمْ يَسْتَغْفِرُونَ {18}
وَالْمُسْتَغْفِرِينَ بِالْأَسْحَارِ {17}
فَلَمَّا دَخَلُوا عَلَىٰ يُوسُفَ آوَىٰ إِلَيْهِ أَبَوَيْهِ وَقَالَ ادْخُلُوا مِصْرَ إِنْ شَاءَ اللَّهُ آمِنِينَ {99}
وَرَفَعَ أَبَوَيْهِ عَلَى الْعَرْشِ وَخَرُّوا لَهُ سُجَّدًا ۖ وَقَالَ يَا أَبَتِ هَٰذَا تَأْوِيلُ رُؤْيَايَ مِنْ قَبْلُ قَدْ جَعَلَهَا رَبِّي حَقًّا ۖ وَقَدْ أَحْسَنَ بِي إِذْ أَخْرَجَنِي مِنَ السِّجْنِ وَجَاءَ بِكُمْ مِنَ الْبَدْوِ مِنْ بَعْدِ أَنْ نَزَغَ الشَّيْطَانُ بَيْنِي وَبَيْنَ إِخْوَتِي ۚ إِنَّ رَبِّي لَطِيفٌ لِمَا يَشَاءُ ۚ إِنَّهُ هُوَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ {100}
رَبِّ قَدْ آتَيْتَنِي مِنَ الْمُلْكِ وَعَلَّمْتَنِي مِنْ تَأْوِيلِ الْأَحَادِيثِ ۚ فَاطِرَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ أَنْتَ وَلِيِّي فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ ۖ تَوَفَّنِي مُسْلِمًا وَأَلْحِقْنِي بِالصَّالِحِينَ {101}
ذَٰلِكَ مِنْ أَنْبَاءِ الْغَيْبِ نُوحِيهِ إِلَيْكَ ۖ وَمَا كُنْتَ لَدَيْهِمْ إِذْ أَجْمَعُوا أَمْرَهُمْ وَهُمْ يَمْكُرُونَ {102}