read

Aya 1: Hizo Ni Aya Za Kitab

Maana:

Alif Laam Raa.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 1 mwanzo wa Sura Baqara.

Hizo ni Aya za Kitabu.

Yaani Aya za Sura hii ni katika Qur’an Tukufu. Lengo la kutoa habari hii ni kubainisha kuwa sura hii ni haki kwa sababu ni katika Qur’an. Kwa vile Qur’an ni haki basi nayo ni haki. Haya ndiyo makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

Na uliyoteremshiwa kutoka Mola wako ni haki.

Hapa linakuja swali: Kuna dalili gani kuwa Qur’an ni haki? Jibu utalipata Juz. 1 (2:23-25) Imam Ali (a.s.) anasema : “Hakika Qur’an dhahiri yake ni safi na undani wake ni wa kina, maajabu yake hayaishi wala giza haliondoki ila kwayo.”

Lakini watu wengi hawaamini Qur’an wala kauli nyingine ya haki na uadilifu ila yule anayeona heri yake ni heri ya watu na shari yake ni shari yao pia.

Mtu mmoja katika watu wa Mungu aliambiwa kuwa soko limeungua lakini duka lako halikuungua, akasema: Alhamdullilah. Kisha akatanabahi kuwa ameasi kwa kujitakia yeye binafsi heri kuliko watu wengine, akatubia dhambi yake na akaomba msamaha.

Mfano wa watu hawa ni wachache ambao wanawafikiria wengine, ndio aliowakudia Mwenyezi Mungu kwa kusema: ‘Lakini watu wengi hawaamini”.

اللَّهُ الَّذِي رَفَعَ السَّمَاوَاتِ بِغَيْرِ عَمَدٍ تَرَوْنَهَا ۖ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۖ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ ۖ كُلٌّ يَجْرِي لِأَجَلٍ مُسَمًّى ۚ يُدَبِّرُ الْأَمْرَ يُفَصِّلُ الْآيَاتِ لَعَلَّكُمْ بِلِقَاءِ رَبِّكُمْ تُوقِنُونَ {2}

Mwenyezi Mungu ndiye aliyeziinua mbingu bila ya nguzo mnazoziona; kisha akatawala kwenye Arshi na amelitiisha Jua na Mwezi, kila kimoja kinaendelea mpaka muda uliotajwa. Anayapanga mambo Anazipambanua ishara, ili mpate kuwa na yakini ya kukutana na Mola wenu.

وَهُوَ الَّذِي مَدَّ الْأَرْضَ وَجَعَلَ فِيهَا رَوَاسِيَ وَأَنْهَارًا ۖ وَمِنْ كُلِّ الثَّمَرَاتِ جَعَلَ فِيهَا زَوْجَيْنِ اثْنَيْنِ ۖ يُغْشِي اللَّيْلَ النَّهَارَ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ {3}

Na yeye ndiye aliyeitandaza ardhi. Na akaweka humo milima na mito. Na katika kila matunda akafanya humo viwili viwilidume na jike. Huufunika usiku kwa mchana. Hakika katika hayo zimo ishara kwa watu wanaofikiri.

وَفِي الْأَرْضِ قِطَعٌ مُتَجَاوِرَاتٌ وَجَنَّاتٌ مِنْ أَعْنَابٍ وَزَرْعٌ وَنَخِيلٌ صِنْوَانٌ وَغَيْرُ صِنْوَانٍ يُسْقَىٰ بِمَاءٍ وَاحِدٍ وَنُفَضِّلُ بَعْضَهَا عَلَىٰ بَعْضٍ فِي الْأُكُلِ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِقَوْمٍ يَعْقِلُونَ {4}

Na katika ardhi mna vipande vilivyokaribiana. na zipo bustani za mizabibu na mimea mingine na mitende ichipuayo kwenye shina na isiyochipua kwenye shina moja inayonyweshwelezwa maji yale yale Na tunaifanya bora baadhi yake kuliko mingine katika kula. Hakika katika hayo kuna ishara kwa watu wanotia akilini (mambo).