Aya 26-29: Hukunjua Riziki
Mtu Na Riziki
Katika Juz.6 (5:66) Tumelielezea suala hili. Pia katika Juz. 7 (5:100), tumefafanua zaidi katika kifungu ‘Je riziki ni bahati au majaliwa.’ Hivi sasa tunarudia maudhui haya kwa mfumo mwingine kwa kuangalia umuhimu wake.
Mtu ana sifa nyingi, zikiwemo za kidhati na ulazima anazokuwa nazo bila ya kubanduka; kwa mfano kuwa mrefu au mfupi kuwa ni mtoto wa tajiri au fukara. Nyingine, sio za dhati ni za kutafuta; mfano kuwa mkulima, mfanyabiashara, tabibu au mwajiriwa n.k.
Utajirinaounasababuzake;zikiwemonasabu;yaaniurithi.Huounatambuliwa na kukubaliwa na dini, hata kama haukupatikana kwa jasho. Sababu nyingine ni ulanguzi na unyang’anyi; kama vile riba, ghushi, wizi, biashara ya haramu n.k. Huu ni haramu, hilo halina shaka. Sababu nyingine ya utajiri ni jasho la mtu na bidii; kama vile ukulima, viwanda n.k. Sababu hii ndio bora zaidi kiakili na kisharia.
Kwa hiyo basi, inatubainikia kuwa ufukara na utajiri unatokana na sanaa ya ardhini sio ya mbinguni. Lakini wako wanaotoka nje ya hayo na kuziita sababu za hayo kuwa ni tawfiki ya Mungu, wengine wakaita bahati, lakini hakuna hata mmoja wao anayethubutu kusema kuwa kadhaa na kadari inaingilia juhudi za mtu na kazi yake na kwamba inawaunga mkono wengine kwa kuwasaidia na kuwaacha wengine. Hakuna anayeweza kuthibitisha hilo. Vinginevyo ingelikuwa sababu zote ni bure tu, na kufanya kazi kungelikuwa ni maneno tu yasiyokuwa na maana.
Unaweza kuuliza: Kauli yako hii si inapingana na kauli ya Mwenyezi Mungu.
Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye na humkunjia.
Jibu: Maisha ya watu yako makundi mawili: kuna wale walio na riziki pana na wale walio na riziki finyu. Kila moja kati ya utajiri na ufukara unatokana na sababu zake maalum ambazo tumekwisha zidokeza. Kauli yake Mwenyezi Mungu: ‘Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye na humkunjia’ ni wasifu na kuelezea hali halisi ya watu; kana kwamba anasema watu ni makundi mawili mafukara na matajiri. Mwenyezi Mungu ameutegemeza ufukara na utajiri kwake ili kutanabahisha kuwa Yeye mtukufu ndiye muumba wa ulimwengu ambao una tabu na raha.
Ikiwa mtu atasema kwa nini basi Mwenyezi Mungu asingeumba ulimwengu usiokuwa na dhiki? Majibu yake yako kwenye Juz. 5 (4:78), ‘Kifungu cha Haiwezekani kuongeza zaidi ya ilivyo.’
Wamefurahia maisha ya dunia na maisha ya dunia kwa kulingana na Akhera si kitu ila ni starehe.
Mfano wa Aya hii umekwishapita mara nyingi, ikiwemo ile ya Juz.4 (3:185). Kuongezea na tuliyoyazungumza huko, ni kwamba kuna aina ya watu wanafurahia mali kwa sababu inasitiri aibu yao na uovu wao. Wengi katika wao hawaoni kitu isipokuwa kwenye mali na utajiri. Ni maarufu kwa wamarekani kwamba wao hawaangalii kitu chochote ila kupitia dola (pesa). Hicho ndicho kipimo cha hadhi ya mtu, hata wataalamu na wenye vipaji, thamani yao ni vile vilivyo katika mifuko yao sio vilivyo vichwani mwao.
Na husema wale ambao wamekufuru: “Kwa nini hakuteremshiwa Ishara kutoka kwa Mola wake?”
Umepita mfano wake katika Juz. 1 (2: 118), Juz. 7 (6:37), Juz. 11 (10:20) na kwa herufi zake hizihizi katika Juzu na sura hii tunayoendela nayo Aya 7 .
Sema: Mwenyezi Mungu humpoteza amtakaye na humuongoa anayeelekea kwake.
Angalia kifungu cha ‘Uongofu na upotevu’ kwenye Juz. 1 (2: 26) na kifungu ‘Upotevu’ katika Juz.5 (4:88).
Wale ambao wameamini na zikatua nyoyo zao kwa kumdhukuru Mwenyezi Mungu. Ehe! Kwa kumdhukuru Mwenyezi Mungu nyoyo zinatua.
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alipotaja watu wa mali na furaha yao inayotokana na kutulizana kwao kwenye maisha yao, anawataja waumini kwamba ni wale wanaotulizana kwa dhikri ya Mwenyezi Mungu. Kutua au kutulizana moyo maana yake ni kuzidi asili ya imani; yaani uthabiti wa imani na utulivu wake. Kuna Aya inayosema:
قَالَ أَوَلَمْ تُؤْمِنْ ۖ قَالَ بَلَىٰ وَلَٰكِنْ لِيَطْمَئِنَّ قَلْبِي ۖ {260}
وَقَلْبُهُ مُطْمَئِنٌّ بِالْإِيمَانِ {106}
Makusudio ya Dhikr sio kutamka maneno tu; isipokuwa ni dhikri ambayo inamzidisha yakini ya Mwenyezi Mungu yule mwenye kudhukuru na akawa ana mategemeo ya ahadi na miadi yake Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo dhikri ya matamshi tu na tasbihi sio dhikr ya kiuhakika. Dhikri inayozidisha yakini ni ile aliyoisema Mwenyezi Mungu:
فَاذْكُرُونِي أَذْكُرْكُمْ {152}
Wale ambao wameamini na wakafanya matendo mema, raha ni yao na marejeo mazuri.
Makusudio ya raha ni Pepo. Aya hii inaoana na ile isemayo:
وَبَشِّرِ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ أَنَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۖ {25}
كَذَٰلِكَ أَرْسَلْنَاكَ فِي أُمَّةٍ قَدْ خَلَتْ مِنْ قَبْلِهَا أُمَمٌ لِتَتْلُوَ عَلَيْهِمُ الَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ وَهُمْ يَكْفُرُونَ بِالرَّحْمَٰنِ ۚ قُلْ هُوَ رَبِّي لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْهِ مَتَابِ {30}
وَلَوْ أَنَّ قُرْآنًا سُيِّرَتْ بِهِ الْجِبَالُ أَوْ قُطِّعَتْ بِهِ الْأَرْضُ أَوْ كُلِّمَ بِهِ الْمَوْتَىٰ ۗ بَلْ لِلَّهِ الْأَمْرُ جَمِيعًا ۗ أَفَلَمْ يَيْأَسِ الَّذِينَ آمَنُوا أَنْ لَوْ يَشَاءُ اللَّهُ لَهَدَى النَّاسَ جَمِيعًا ۗ وَلَا يَزَالُ الَّذِينَ كَفَرُوا تُصِيبُهُمْ بِمَا صَنَعُوا قَارِعَةٌ أَوْ تَحُلُّ قَرِيبًا مِنْ دَارِهِمْ حَتَّىٰ يَأْتِيَ وَعْدُ اللَّهِ ۚ إِنَّ اللَّهَ لَا يُخْلِفُ الْمِيعَادَ {31}