read

Sura Ya Kumi Na Nne: Ibrahim

Imeshuka Makka Ina Aya 52. Imesemekana kuwa Aya mbili katika hizo zimeshuka Madina.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

الر ۚ كِتَابٌ أَنْزَلْنَاهُ إِلَيْكَ لِتُخْرِجَ النَّاسَ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِ رَبِّهِمْ إِلَىٰ صِرَاطِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ {1}

Hiki ni Kitabu tulichokiteremsha kwako ili uwatoe watu gizani uwapeleke kwenye nuru, kwa idhini ya Mola wao, uwafikishe kwenye njia ya Mwenye nguvu, Mwenye kusifiwa.

اللَّهِ الَّذِي لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَوَيْلٌ لِلْكَافِرِينَ مِنْ عَذَابٍ شَدِيدٍ {2}

Ni Mwenyezi Mungu ambaye ni vyake vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini. Na ole wao makafiri kwa adhabu kali.

الَّذِينَ يَسْتَحِبُّونَ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا عَلَى الْآخِرَةِ وَيَصُدُّونَ عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ وَيَبْغُونَهَا عِوَجًا ۚ أُولَٰئِكَ فِي ضَلَالٍ بَعِيدٍ {3}

Wale ambao wamestahabu maisha ya dunia kuliko Akhera na wakawazuilia watu na njia ya Menyezi Mungu na wanataka kuipotosha, hao wamepotelea mbali.

وَمَا أَرْسَلْنَا مِنْ رَسُولٍ إِلَّا بِلِسَانِ قَوْمِهِ لِيُبَيِّنَ لَهُمْ ۖ فَيُضِلُّ اللَّهُ مَنْ يَشَاءُ وَيَهْدِي مَنْ يَشَاءُ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ {4}

Na hatukumtuma Mtume ila kwa ulimi wa watu wake ili apate kuwabainishia. Basi humpoteza amtakaye na humwongoza amtakaye na Yeye ni Mwenye nguvu mwenye hekima.