read

Aya 5-8: Tulimtuma Musa

Hakika tulimtuma Musa pamoja na miujiza yetu kuwa watoe watu wako kutoka gizani kwenda kwenye nuru.

Maneno yamerudi tena kwa Musa (a.s.) na Waisrail ambao walimtoa roho. Mazungumzo yamewarudia wao na yamekaririka mara kadhaa. Mimi sijui siri ya kukaririka mazungumzo yanayowahusu wao kuliko wengine isipokuwa ni kwamba wao wamevuka mipaka ya kiutu kitabia na kivitendo; kama nilivyodokeza mwanzoni. Mimi sifichi kuwa ninaona uzito sana nikifasiri Aya zilizo na jina la Waisrail.

Na uwakumbushe siku za Mwenyezi Mungu.

Siku zilizo dhahiri zaidi na zenye neema juu yao ni zile walizookolewa na adhabu ya Firauni na kukombolewa kutoka utumwani.

Hakika katika hayo kuna ishara kwa kila mwenye kusubiri mwenye kushukuru.

“Vumilia mitihani yako kwa kutumaini nusura yako.”

Makusudio ya hayo ni hayo ya ukumbusho. Na makusudio ya ishara hapa ni mazingatio na mawaidha. Ilivyo ni kuwa mwenye kuzingatia na akawaidhika ndiye mumin wa kweli anayeshukuru wakati wa raha na kuvumilia wakati wa balaa pamoja na kujitahidi kufanya ikhlas.

Na Musa alipowaambia watu wake: “Kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu, alipowaokoa na watu wa Firauni, walipowapa adhabu mbaya na wakiwachinja watoto wenu wa kiume na wakiacha hai watoto wenu wa kike. Na katika hayo ulikuwa mtihani mkubwa kutoka kwa Mola wenu.

Musa (a.s.) aliwakumbusha wana wa Israil aliyowafanyia Firauni-kuwachinja watoto wao wa kiume na utumwa. Na akawakumbusha neema ya kuepukana na hayo na akawaamrisha wamkumbuke Mwenyezi Mungu na wamshukuru. Lakini wao hawakumshukuru wala kumkumbuka; bali walimkufuru Mwenyezi Mungu na wakaikana neema yake wakamuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wao Musa kwa kumwambia: Tuonyeshe Mungu waziwazi, Nenda wewe na Mola wako mkapigane.

Walipowapitia watu wakiabudu masanamu wakamwambia Musa tufanyie Mungu kama huyu wao; kisha wakaabudu ndama.

Hayo ndiyo malipo ya kumlipa Mungu aliyewaokoa na adhabu ya Firauni. Musa alipokata tamaa nao na kuona dhiki kubwa alimwelekea Mwenyezi Mungu na kusema:

رَبِّ إِنِّي لَا أَمْلِكُ إِلَّا نَفْسِي وَأَخِي ۖ فَافْرُقْ بَيْنَنَا وَبَيْنَ الْقَوْمِ الْفَاسِقِينَ {25}

“Ewe Mola wangu! Hakika mimi similiki ila nafsi yangu na ndugu yangu; basi tutenge na watu hawa mafasiki” Juz.6 (5:25)

Kuna maajabu gani baada ya hayo ikiwa Mayahudi wataikana neema ya waislamu kwao siku walipokataliwa na ulimwengu, ambapo hakukuwa na Amerika wala Uingereza au Ujerummani ya magharibi kuwafanya wao ni madalali na mbwa wa kulinda ukoloni na u-Nazi. Umepita mfano wake katika Juz.1 (2:49).

Na alipotangaza Mola wenu: Mkishukuru nitawazidishia na mkikufuru basi adhabu yangu ni kali.

Makusudioyakukufuruhapanikumuudhiyulemneemeshajinakuzikana neema zake, kwa sababu mazungumzo yanahusiana na waisrail kukana neema za Mwnyezi Mungu. Wamesema wafasiri wengi kuwa Mwenyezi Mungu akimneemesha mja wake na akashukuru na akamkiri Mwenyezi Mungu kwazo, basi Mwenyezi Mungu atamdumisha nayo na kumzidishia. Wamesema hivi kwa kuchukulia kauli mashuhuri: “Shukrani zinadumisha neema.”

Tuonavyo sisi ni kwamba makusudio ya kuzidi neema ni kuzidi hiyo neema Akhera si duniani, kwa sabubu ni uhakika kuwa makusudio ya adhabu kali ya kukufuru neema ni adhabu ya Akhera, kwa hiyo malipo ya kushukuru vilevile yatakuwa ni Akhera. Imethibiti kutoka kwa Mtume kwamba yeye alifanya sawa kumpa mwema na muovu. Imam Ali amesema: “Mali ingelikuwa yangu ningelifanya sawa; vipi isiwe hivyo na mali yote ni ya Mwenyezi Mungu”

Zaidi ya hayo tunashuhudia mali nyingi inarundikana kwa mataghuti kadiri wanvyozidi uasi na kupetuka mipaka. Ndio! Kama ingelikuwa makusudio ya kushukuru ni kuichunga mali, kuipangia vizuri na kuizalisha, basi wafasiri wangelikuwa na njia ya kusemea, lakini hiyo ni kinyume na dhahiri ya Aya ilivyo na wala hakuna aliyewahi kusema hivyo, hata hao wafasiri wenyewe.

Na alisema Musa: “Mkikufuru nyinyi na waliomo duniani wote, hakika wenyezi Mungu ni mkwasi mwenye kusifiwa.”

Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu si mwingine, na kujitosheleza ni kwake Yeye si mwingine. Musa alisema kauli hii kutokana na kukata kwake tamaa ya kuongoka Waisrail.

أَلَمْ يَأْتِكُمْ نَبَأُ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكُمْ قَوْمِ نُوحٍ وَعَادٍ وَثَمُودَ ۛ وَالَّذِينَ مِنْ بَعْدِهِمْ ۛ لَا يَعْلَمُهُمْ إِلَّا اللَّهُ ۚ جَاءَتْهُمْ رُسُلُهُمْ بِالْبَيِّنَاتِ فَرَدُّوا أَيْدِيَهُمْ فِي أَفْوَاهِهِمْ وَقَالُوا إِنَّا كَفَرْنَا بِمَا أُرْسِلْتُمْ بِهِ وَإِنَّا لَفِي شَكٍّ مِمَّا تَدْعُونَنَا إِلَيْهِ مُرِيبٍ {9}

Je haziukuwafikia habari za walio kabla yenu: Kaumu ya Nuh na A’d na Thamud na walio baada yao? Hakuna awajuaye illa Mwenyezi Mungu. Waliwajia mitume wao kwa hoja zilizo wazi. Wakarudisha mikono yao kwenye vinywa vyao. Na wakasema: “Hakika sisi tumeyakataa hayo mliyotumwa na hakika sisi tuna shaka kubwa ya mnayotuitia.”

قَالَتْ رُسُلُهُمْ أَفِي اللَّهِ شَكٌّ فَاطِرِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ يَدْعُوكُمْ لِيَغْفِرَ لَكُمْ مِنْ ذُنُوبِكُمْ وَيُؤَخِّرَكُمْ إِلَىٰ أَجَلٍ مُسَمًّى ۚ قَالُوا إِنْ أَنْتُمْ إِلَّا بَشَرٌ مِثْلُنَا تُرِيدُونَ أَنْ تَصُدُّونَا عَمَّا كَانَ يَعْبُدُ آبَاؤُنَا فَأْتُونَا بِسُلْطَانٍ مُبِينٍ {10}

Mitume wao wakasema: “Je kuna shaka na Mwenyezi Mungu, Muumba wa mbingu na ardhi? Anawaita ili apate kuwaghufiria dhambi zenu na anawapa muhula mpaka muda uliowekwa.” Wakasema: “Nyinyi si chochote ila ni watu kama sisi. Mnataka kutuzuwia na waliyokuwa wakiyaabudu baba zetu. Basi tuleteeni hoja iliyo wazi.”

قَالَتْ لَهُمْ رُسُلُهُمْ إِنْ نَحْنُ إِلَّا بَشَرٌ مِثْلُكُمْ وَلَٰكِنَّ اللَّهَ يَمُنُّ عَلَىٰ مَنْ يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۖ وَمَا كَانَ لَنَا أَنْ نَأْتِيَكُمْ بِسُلْطَانٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّهِ ۚ وَعَلَى اللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ {11}

Mitume wao wakawaambia: “Sisi si chochote ila ni wanadamu kama nyinyi, lakini Mwenyezi Mungu humneemesha amtakaye katika waja wake. Wala sisi hatuwezi kuwaletea dalili isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu.

وَمَا لَنَا أَلَّا نَتَوَكَّلَ عَلَى اللَّهِ وَقَدْ هَدَانَا سُبُلَنَا ۚ وَلَنَصْبِرَنَّ عَلَىٰ مَا آذَيْتُمُونَا ۚ وَعَلَى اللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُتَوَكِّلُونَ {12}

Na tuna nini hata tusimtegemee Mwenyezi Mungu na hali yeye ametuongoza kwenye njia yetu na hakika sisi tutavumilia mnayotuudhi; na kwa Mwenyezi Mungu nawategemee wenye kutegemea.”