Aya 18-21: Matendo Yao Ni Kama Majivu
Mfano wa wale ambao wamemkufuru Mola wao vitendo vyao ni kama majivu yanayopeperushwa kwa nguvu za upepo katika siku ya kimbunga.
Wafasiri wengi wamesema kuwa makusudio ya Aya ni kwamba kafiri hapati malipo yoyote kwa kufanya jambo jema; kama vile sadaka n.k. Lakini tuoanavyo sisi ni kuwa mwenye kufanya heri kwa msukumo wa kiutu basi atakuwa amefanya kwa jili ya Mwenyezi Mungu awe amekusudia hivyo au la.
Na hakuna mwenye shaka kwamba mwenye kufanya jambo kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, basi ujira wake uko kwa Mwenyezi Mungu kwa vile yeye ni mwadilifu, na hakimu na atamlipa kwa namna yoyote ile; iwe ni duniani au akhera kwa kupunguziwa adhabu; na si lazima kwamba asimwingize motoni kabisa. Hiyo ni kwa sababu neema za Mwenyezi Mungu hazidhibitiwi kwa kiwango wala ki namna. Tumeyazungumzia hayo kwa ufanuzi zaidi tulipofasiri Juz. 4 (3:178).
Kwa hiyo basi, maana ya Aya ni kwamba mtu yeyote atakayefanya matendo ya kheri kwa lengo la kibiashara, sio kibinadamu, kama yule anayefanya mambo ya kheri siku za uchaguzi, basi vitendo vyake huyo si chochote mbele ya Mwenyezi Mungu; sawa na hewa ndani ya wavu au majivu kwenye upepo; ni sawa awe aliyefanya hayo ni Mwislamu au si mwislamu. Imam Ali (a.s.) anasema:
“Fanyeni mambo bila ya ria wala kusikika; kwani anayefanya kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu, basi Mungu Humwachia huyo aliyemfanyia”.
Unaweza kuuliza: Ikiwa hukumu inawaenea makafiri na wasiokuwa makafiri kwa nini Aya imetaja makafiri peke yake?
Jibu: Kutajwa makafiri hakukanushi hukumu kwa wengine; isipokuwa wamehusishwa kutajwa hapa kwa kuwa ndio dhahiri zaidi.
Hawana uwezo wa chochote juu ya walichokichumma. Huko ndiko kupotelea mbali.
Walichokichumma ni kwa maana ya walichokifanya. makusudio ya ambao hawana uweza, kimatamshi, ni makafiri na kimaana ni kila mwenye kufanya wema kwa lengo la kibiashara.
Na makusudio yake ni kwamba anayefanya matendo kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu wala kwa ajili ya ubinadamu, hakika yeye hatanufaika kesho kwa amali yake; kwani ni sawa na majivu yanayopeperuka hewani na mwenyewe atakuwa amepotea kwa sababu matendo yake yameepukana na kila sababu inayo muunganisha na Mwenyezi Mungu na ubinadamu.
Je, huoni kuwa Mwenyezi Mungu ameziumba mbingu na ardhi kwahaki na akitaka atawaondoa na alete viumbe wapya! Na hilo kwa Mwenyezi Mungu si gumu.
Maana ya je, huoni ni je, hujui. Msemo unaelekezwa kwa kila mwenye kuisoma Qur’an na mwenye kuisikia. Neno ‘Haki’ linaashiria kuwa Yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu, hakuumba kitu chochote isipokuwa kwa hekima iliyopitisha hivyo.
وَمَا خَلَقْنَا السَّمَاءَ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا بَاطِلًا ۚ ذَٰلِكَ ظَنُّ الَّذِينَ كَفَرُوا ۚ {27}
Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kuwataja wale wanaofanya matendo kwa asiyekuwa Yeye, hapa anasema kuwa hana haja na watu na matendo yao; na kama angetaka angeliwamaliza wote na kuleta umma mwingine watakaotenda kwa ajili yake peke yake, bila ya kumshirikisha na kitu chochote; kwa sabu Yeye ni muweza wa kila kitu. Hakuna kitu kinachofa- hamisha zaidi hivyo kuliko kuumba ulimwengu na maajabu yake.
Dhalimu Na Mdhulumiwa
Na wamehudhuria kwa Mwenyezi Mungu wote.
Limekuja tamko la muda uliopita, lakini makusudio ni muda ujao; yaani watahudhuria. Kwa sababu ni uhakika kuwa litatokea hilo1. Maana ni kuwa watu, majini, malaika na mashetani wote hawa watajitokeza mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ya kiyama.
Hakuna yeyote katika wao ila ana yakini kuwa Mwenyezi Mungu ataifichua hakika yake, hata wale wanaomkufuru na kukana ufufuo.
Na wanyonge watawaambia wale waliotakabari: “Sisi tulikuwa wafuasi wenu, je mtatuondolea chochote katika adhabu ya Mwenyezi Mungu?”
Kila mwenye akili ana majukumu ya matendo yake awe na nguvu au mny- onge, kiongozi au mwenye kuongozwa:
عَمَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ {93}
مَا يَلْفِظُ مِنْ قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ {18}
Kwa hiyo mfuasi ataulizwa: Je, alifuata uongofu au upotevu? Je, aliwafuata na kuwategema wema au wafisadi? Vile vile aliyefuatwa naye ataulizwa, na majukumu yake yake yatakuwa makubwa zaidi, kwa vile ataulizwa kuhusu yeye mwenyewe, kisha aulizwe kuhusu wale waliomfuata: Je, atabeba mizigi yake na mizigo yao?
Mimi sijui kama kuna mwenye mzigo mzito zaidi, kuliko yule aliyefuata na akamsaidia kwenye dhulma, huku akiwa anajua uhakika wake. Hakika dhulama ya dhalimu sio mbaya sana, mbele ya Mwenyezi Mungu, kuliko uvumilivu wa mwenye kudhulumiwa.
Kuuliwa mwenye kudhulumiwa katika kuitetea haki ni kufa shahidi, na mashahidi, wako hai mbele ya Mola wao, wakiruzukiwa.
Dhalimu hathubutu kufanya dhulma ila kwa kunyamaza mdhulumiwa. Lau dhalimu anajua kuwa ndani ya mwili wa anayetaka kumdhulumu kuna nafsi ya ki-Hussein,2basi atamwogopa tu.
Kwa vyovyote iwavyo, makusudio ya wanyonge ni wale wadhaifu wa nafsi ambao wanamfuata dhalimu mpotevu huku wakijua dhulma yake na upotevu wake kwa tamaa ya jaha au mali, au woga wa kutaka raha na usalama.
Wanaingia kwenye hukumu hii ya majukumu na hatia wale wanofuata kwa upofu na kufuata mkumbo, marafiki au ndugu.
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amaeleta picha ya wafuasi wa upotevu, kwa kujua au kwa kutojua kiupofu, siku ya hisabu pamoja na mataghuti kwa namna hiyi:
Wadhaifu wa nafsi na wa hima watawambia wale viongozi wa dunia na wadanganyifu katika viongozi wa dini: tulikuwa tukifanya kwa amri zenu na tukiacha kwa makatazo yenu; sasa hivi, kama mnavyoona, tuko mbele ya Mwenyezi Mungu hatuna hila wala uwezo, atatuhisabu na kutuadhibu kutokana na kuwatii nyinyi katika kuwakadhibisha mitume na kumwasi Mwenyezi Mungu. Je mtaweza kutukinga na adhabu ya Mwenyezi Mungu, angalau kidogo?
Watasema: “Lau angelituongoza Mwenyezi Mungu tungeliwaongoza.”
Makusudio ya kuongozwa hapa ni kuokoka na adhabu ya Mwenyezi Mungu, kwa sabubu jawabu linakuja kulingana na swali lenyewe.
Wameuliza wafuasi kupunguziwa adhabu na wale wanaowafuata na wao wanajibu kuwa lau tungeliweza kujiokoa basi tungeliwaokoa na nyinyi. Hayo ndio makusudio ya kuongoka hapa; wala hakuna maana nyingine inayoafikiana nayo ila hiyo.
Ni mamoja kwetu tukipapatika au tukisubiri; hatuna pa kukimbilia, kwani kila kitu kimekwisha, hakuna faida ya kujadiliana wala kusutana, kwani hapa tulipo ni nyumba ya hisabu na adhabu si nyumba ya kauli na vitendo.
وَقَالَ الشَّيْطَانُ لَمَّا قُضِيَ الْأَمْرُ إِنَّ اللَّهَ وَعَدَكُمْ وَعْدَ الْحَقِّ وَوَعَدْتُكُمْ فَأَخْلَفْتُكُمْ ۖ وَمَا كَانَ لِيَ عَلَيْكُمْ مِنْ سُلْطَانٍ إِلَّا أَنْ دَعَوْتُكُمْ فَاسْتَجَبْتُمْ لِي ۖ فَلَا تَلُومُونِي وَلُومُوا أَنْفُسَكُمْ ۖ مَا أَنَا بِمُصْرِخِكُمْ وَمَا أَنْتُمْ بِمُصْرِخِيَّ ۖ إِنِّي كَفَرْتُ بِمَا أَشْرَكْتُمُونِ مِنْ قَبْلُ ۗ إِنَّ الظَّالِمِينَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ {22}
وَأُدْخِلَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِمْ ۖ تَحِيَّتُهُمْ فِيهَا سَلَامٌ {23}