read

Aya 22-23: Miadi Ya Mwenyezi Mungu

Hotuba Ya Shetani

Tumezungumzia kwa ufafanuzi kuhusu fikra ya Iblisi na Shetani, mwan- zoni mwa Juzuu ya kwanza na katika Juz.5 (4:38) na katika Aya nyingine zinazozungumzia shetani tumezungumzia kwa ujumla.

Hapa tunarudia kwa upana zaidi; kwa sababu Aya tuliyo nayo ndiyo iliyowazi zaidi kuonyesha dalili za kuweko shetani na kwamba ni hakika yenye kuthibiti; ingawaje haikueleza vile alivyo. Tutaeleza njia zinazoambatana na Aya hii, kama ifuatavyo:

1- Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amemtaja shetani, katika Kitabu chake Kitakatifu, kwa ibara mbali mbali. Mara nyingine anasema, Mtukufu, kuwa shetani ni katika aina ya watu na majini; kama pale aliposema:

شَيَاطِينَ الْإِنْسِ وَالْجِنِّ يُوحِي بَعْضُهُمْ إِلَىٰ بَعْضٍ زُخْرُفَ الْقَوْلِ غُرُورًا ۚ {112}

“Mashetani watu na majini Baadhi yao wanawapa wenzao maneno ya kupambapamba kuwahadaa.” Juz.8 (6:112).

Aya hii inaashira kwamba kila kauli ambayo dhahiri yake ni rehema na undani wake ni adhabu, basi hiyo ni kazi ya shetani, hata ikiwa imesemwa na nani.

Mara nyingine anasema Mwenyezi Mungu kuwa shetani ana askari na ana kabila; kama ilivyo katika Aya hizi:

وَجُنُودُ إِبْلِيسَ أَجْمَعُونَ{95}

“Na majeshi ya ibilisi yote” (26:95)

يَا بَنِي آدَمَ لَا يَفْتِنَنَّكُمُ الشَّيْطَانُ كَمَا أَخْرَجَ أَبَوَيْكُمْ مِنَ الْجَنَّةِ يَنْزِعُ عَنْهُمَا لِبَاسَهُمَا لِيُرِيَهُمَا سَوْآتِهِمَا ۗ إِنَّهُ يَرَاكُمْ هُوَ وَقَبِيلُهُ مِنْ حَيْثُ لَا تَرَوْنَهُمْ ۗ {27}

“Enyi wanaadamu! shetani asiwatie katika fitina, kama alivyowatoa wazazi wenu katika Bustani (Pepo) akiwavua nguo zao ili kuwaonyesha tupu zao. Hakika yeye na kabila lake anawaona, na nyinyi hamuwaoni.” Juz.8 (7:27).

Aya hizi zinafahamisha kuwa mashetani hawana idadi kwa wingi na kwamba wao hawaonekani kwa macho wala kuguswa kwa mkono.

Mara ya tatu Mwenyezi Mungu anasema mashetani wana marafiki na wasimamizi; kama ilivyo katika Aya hizi:

وَمَنْ يَكُنِ الشَّيْطَانُ لَهُ قَرِينًا فَسَاءَ قَرِينًا {38}

“Na ambaye shetani amekuwa ndiye rafiki yake, basi ana rafiki mbaya.” Juz.5 (4:38)

فَقَاتِلُوا أَوْلِيَاءَ الشَّيْطَانِ ۖ إِ{76}

“Basi piganeni na marafiki wa shetani” Juz.5 (4:76)

Tamko hili peke yake linafahamisha kuwa kupigana jihadi na wapotufu ni lazima na wajib, wajapokuwa ni waislamu. Mara ya nne, Mwenyezi Mungu, ambaye imetukuka hekima yake na maneno yake, anasema:

هَلْ أُنَبِّئُكُمْ عَلَىٰ مَنْ تَنَزَّلُ الشَّيَاطِينُ {221}

تَنَزَّلُ عَلَىٰ كُلِّ أَفَّاكٍ أَثِيمٍ {222}

“Je, niwaambie nani wanawashukia Mashetani? Wanamshukia kila mzushi mkubwa mwingi wa dhambi” (26: 221-222).

Inafahamisha Aya hii kuwa Mashetani ni wale waongo wazushi.

Ama wadhifa wa shetani na askari wake, kama ulivyoelezwa, ni kupoteza na kudanganya ili kuzuia njia ya haki na kheri, kwa nguvu na kulazimisha; isipokuwa ni kwa wasiwasi, kupambapamba na kudanganya.

Kwa ajili hii, tunasema na tunaendelea kusema kwamba jambo lolote linalompambia mtu kufanya uovu na kumuhimiza shari na ufisadi kwa njia ya hadaa na shauku, basi hilo ni shetani aliyefukuzwa na ibilisi mlaanifu ni sawa iwe ni mtu, mali, jaha, kitabu, gazeti, wasiwasi, mazungumzo ya ndani ya nafsi au kitu chochote kingine kinachoonekana au kisichoonekana.

Hii ndio picha ya shetani iliyoakisi katika akili zetu, tukiwa tunafuatilia na kuzifikiria Aya za Mwenyezi Mungu katika Kitabu chake, tukiziamini pamoja na mitume wa Mwenyezi Mungu.

Mengineyo yasiyokuwa hayo, katika aina na ufafanuzi, tunaiachia elimu ya Mwenyezi Mungu; wala sisi hatukalifiwi nayo au kuulizwa nayo. La wajibu kwetu ni kutohadaika, kutojiingiza katika matamanio na kuacha kuwasikiliza wadanganyifu na wapotevu. Kikitutokea kitu katika hayo, basi tumkumbuke Mwenyezi Mungu kwa ahadi na miadi yake: “Na kama uchochezi wa shetani ukikuchochea, basi jikinge kwa Mwenyezi Mungu; hakika yeye ndiye asikiaye na ajuaye. Hakika wale wanye takua zinapowagusa pepesi za shetani huzinduka.” Juz.9 (7:200-201). Rudia huko.

2- Katika nafsi ya binadamu kuna matamanio na silika, navyo ni vitenda- kazi vinavyopelekea kumuasi Mwenyezi Mungu na kuhalifu amri zake, kwa sababu vinakuja kutoka ndani sio nje na kutoka batini sio dhahiri. Kwa hiyo ikiwa ndani mwa mtu hamna nguvu kubwa na ngumu itakayomzuia kupondokea kwa ashetani na kudhibiti ukaidi wake, basi mtu bila shaka atakuwa amepigwa mwereka na matamanio.

3- Na shetani atasema itakapokatwa hukumu.

Kila kitu, isipokuwa Mwenyezi Mungu, kina mwanzo na mwisho. Inawezekana mwanzo wenyewe ukaonekana, kwa dhahiri, ni heri na mwisho ukaonekana, kiuhakika, ni shari na kinyume chake. Kwa ajili hii haifai kukihukumu kitu kwa dhahiri yake na mwanzo wake, maadamu mwisho wake uko kwenye elimu ya ghaibu.

Watu walimfurahia Qarun alipowatokea na kipambo chake na wakasema: Hakika yeye ni mwema na mtu adhimu. Ardhi ilipommeza yeye na nyumba yake, walisema ni mtu mbaya na muovu.

Dunia ni mwanzo na Akhera ni mwisho. Huko zitafunuka pazia na vifuniko; atajulikana kila mtu mwishilio wake, ambapo hakutakuwa na kombokombo wala kufungwafungwa. Hiyo ndiyo maana ya kauli yake Mwenyezi Mungu: ‘Itakapokatwa hukumu’

4- Hakika Mwenyezi Mungu aliwaahidi ahadi ya kweli nami nikaawahidi sikuwatimizia.

Ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ufufuo, hisabu na malipo:

فَوَرَبِّكَ لَنَسْأَلَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ {92}

عَمَّا كَانُوا يَعْمَلُونَ {93}

“Kwa haki ya Mola wako! Tutawauliza wote yale waliyokuwa wakiyatenda” (15:92-93).

Ama ahadi ya shetani ni kupinga ahadi ya Mwenyezi Mungu kuwa haku- na hisabu wala ufuo wala Pepo na moto. “Hakuna kingine ila maisha yetu ya dunia, wala sisi hatutafufuliwa.” Jz.7 (7:29).

Haya ndiyo anayoyasema shetani kuwaambia marafiki zake hapa duniani, palipo na kupindisha pindisha mambo na kudanganya, lakini huko Akhera hakuna kitu isipokuwa haki na uadilifu; hata shetani mwenyewe ataji- tokeza wazi na uongo wake, akiri mwenyewe kwa kauli yake kuwa mwanzo alikuwa akiwafundisha watu uongo na uzushi.

5- Na sikuwa na mamlaka juu yenu, isipokuwa niliwaita mkaniitikia.

Kabisa! Shetani anakubali mwenyewe kuwa hana uwezo wala nguvu yoy- ote isipokuwa vitimbi na hadaa. Wala hawamwitikii isipokuwa wale wad- haifu wa akili, nafsi na imani. Kauli yake hiyo shetani ni ile aliyoambiwa na Mwenyezi Mungu:

إِنَّ عِبَادِي لَيْسَ لَكَ عَلَيْهِمْ سُلْطَانٌ إِلَّا مَنِ اتَّبَعَكَ مِنَ الْغَاوِينَ {42}

“Hakika waja wangu wewe hutakuwa na mamlaka nao, isipokuwa wale wapotofu waliokufuata” (15:42).

6- Basi msinilaumu mimi, bali jilaumuni wenyewe.

IkiwaniolewakeyulealiyekufurishwanaNamrudi,itakuwajekwayule aliyekufurishwa na Iblisi? Ikiwa watu wanajilinda na shetani itakuwaje yule anyemtaka huyo shetani amlinde.

Huu ndio mwisho wa yule anayeidharau haki na watu wema kusaidia ufisadi na wafisadi na mwenye kufuata mlio. Tumewaona wengi katika mashetani watu wakiwahadaa walio wadhaifu, wanawaghuri kwa kueneza vurugu. Hata yakiwapata yale waliyoyafanya wenyewe, mashetani wao huwaambia yale yale atakayowaambia Ibilisi wafuasi wake siku ya hisabu na malipo.

7- Mimi siwezi kuwa mtetezi wenu wala nyinyi hamuwezi kuwa watetezi wangu

Yaani shetani kesho atawaambia wafuasi wake: mimi siwatoshelezi na kitu chochte, wala nyinyi pia hamnitoshelezi. Mimi na nyinyi hatuna mawasiliano yoyote.

Mimi nilikataa tangu zamani kunishirikisha.

Ibilisi anawaambia wale wale waliotikia mwito wake: mlinitii katika yale niliyowalingalia, mkanifanya ni mshirika wa Mwenyezi Mungu katika wajibu wa twaa, na mimi ninajiepusha na shirki na yale mliyoyashirikisha; hata kama mtanifanya ni mshirika wa Mwenyezi Mungu.

Hakika madhalimu wana adhabu chungu.

Hii ni jumla nyingine inayoanza, si katika maneno ya Ibilisi, ikiwa na maana ya kutoa miadi. Inawezekana kuwa ni mwishilio wa hotuba ya Ibilisi.

Ajabu ni yaliyoelezwa na baadhi ya wafasiri kwamba Ibilisi atatoa hotuba yake hii kwa watu wa motoni kwenye mimbari atakyowekewa huko! Kama ni hivyo basi, itabidi awekewe spika kubwa, kwa sababu wasikilizaji, ambao ni jeshi lake, ni wengi kuliko idadi ya mchanga.

Na wale ambao wameamini na wakatenda mema wataingizwa katika Mabustani (Pepo) ambayo hupita mito chini yake.

Baada ya Mwenyezi Mungu kutaja wapotevu na adhabu yao, sasa anataja waongofu wenye msimamo na malipo yao; kama iilvyo kawaida ya Qur’an. Umepita mfano wake katika Juz. 11 (10:9).

أَلَمْ تَرَ كَيْفَ ضَرَبَ اللَّهُ مَثَلًا كَلِمَةً طَيِّبَةً كَشَجَرَةٍ طَيِّبَةٍ أَصْلُهَا ثَابِتٌ وَفَرْعُهَا فِي السَّمَاءِ {24}

Je, hukuona jinsi Mwenyezi Mungu alivyopiga mfano wa neno zuri; kama mti mzuri, mizizi yake ni imara na matawi yake yako mbinguni.

تُؤْتِي أُكُلَهَا كُلَّ حِينٍ بِإِذْنِ رَبِّهَا ۗ وَيَضْرِبُ اللَّهُ الْأَمْثَالَ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ {25}

Hutoa matunda yake kila wakati kwa idhini ya Mola wake. Na Mwenyezi Mungu huwapigia watu mifano ili wapate kukumbuka.

وَمَثَلُ كَلِمَةٍ خَبِيثَةٍ كَشَجَرَةٍ خَبِيثَةٍ اجْتُثَّتْ مِنْ فَوْقِ الْأَرْضِ مَا لَهَا مِنْ قَرَارٍ {26}

Na mfano wa neno ovu ni kama mti muovu uliong’olewa juu ya ardhi, hauna uimara.

يُثَبِّتُ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۖ وَيُضِلُّ اللَّهُ الظَّالِمِينَ ۚ وَيَفْعَلُ اللَّهُ مَا يَشَاءُ {27}

Mwenyezi Mungu huwaimarisha wale walioamini kwa kauli thabiti katika maisha ya dunia na katika Akhera, na anawapoteza madhalimu; na Mwenyezi Mungu hufanya apendavyo.