read

Sura Ya Arubaini Na Sita: Al-Ahqaf

Imeshuka Makka. Ina Aya 35

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ 

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

حم {1}

Haa miim.

تَنْزِيلُ الْكِتَابِ مِنَ اللَّهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ {2}

Uteremsho wa Kitabu umetoka kwa Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hikima.

مَا خَلَقْنَا السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا إِلَّا بِالْحَقِّ وَأَجَلٍ مُسَمًّى ۚ وَالَّذِينَ كَفَرُوا عَمَّا أُنْذِرُوا مُعْرِضُونَ {3}

Hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyomo baina yake ila kwa haki na kwa muda uliowekwa. Na wale waliokufuru wanayapuuza yale wanayoonywa.

قُلْ أَرَأَيْتُمْ مَا تَدْعُونَ مِنْ دُونِ اللَّهِ أَرُونِي مَاذَا خَلَقُوا مِنَ الْأَرْضِ أَمْ لَهُمْ شِرْكٌ فِي السَّمَاوَاتِ ۖ ائْتُونِي بِكِتَابٍ مِنْ قَبْلِ هَٰذَا أَوْ أَثَارَةٍ مِنْ عِلْمٍ إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ {4}

Sema: Je, mnawaona wale mnaowaomba badala ya Mwenyezi Mungu? Nionyesheni wameumba nini katika ardhi; au wana shirika katika mbingu? Nileteeni Kitabu kilicho kuwa kabla ya hiki, au athari yoyote ya ilimu, ikiwa mnasema kweli.

وَمَنْ أَضَلُّ مِمَّنْ يَدْعُو مِنْ دُونِ اللَّهِ مَنْ لَا يَسْتَجِيبُ لَهُ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ وَهُمْ عَنْ دُعَائِهِمْ غَافِلُونَ {5}

Na ni nani mpotofu mkubwa kuliko yule anayeomba asiyekuwa Mwenyezi Mungu, ambaye hatamjibu mpaka Siku ya Kiyama, Na wala hawatambui maombi yao.

وَإِذَا حُشِرَ النَّاسُ كَانُوا لَهُمْ أَعْدَاءً وَكَانُوا بِعِبَادَتِهِمْ كَافِرِينَ {6}

Na watakapokusanywa watu watakuwa maadui zao, na wataikataa ibada yao.