Aya 17 – 20: Aliyewaambia Wazazi Wake Akh!
Maana
Na ambaye amewaambia, wazazi wake Ah! Nanyi! na akawaambia: Je, mnanitisha kuwa nitafufuliwa, na hali vizazi vingi vimekwishapita kabla yangu!
Ni nani mtoto huyu anayezungumziwa na Qur’an na kusema kuwa ni kafiri mwenye kuwaudhi wazazi wake?
Jibu: Mwenyezi Mungu hakumtaja mtu hasa. Dhahiri ya Aya inaonyesha kwamba makusudio yake ni kila mtoto anayeikanusha siku ya mwisho, naye akiwa na wazazi wanaojitahidi kumpa nasaha, kumwongoza na kumhadharisha na ghadhabu za Mwenyezi Mungu na adhabu yake, lakini bado anaona kusumbuliwa na kuwaambia: Poteleeni mbali! Vipi mtu ataweza kutoka kaburini na hali amekuwa mchanga? Je, ameshawahi kutokewa na hivyo mwingine asiyekuwa mimi katika zama zozote?
Aya hii inawaelekea vijana wengi wa kisasa, kama vile imewashukia wao. Lau kama watauliza na kujadiliana kwa kukusudia maarifa na kuongoka kwenye uhakika, basi itakuwa ni wajibu wetu tuwakaribishe na maswali na majadiliano yao; na tufanye bidii kubwa kadiri tunavyoweza ili tuwakinaishe, kwa kuifanyia kazi kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
لَتُبَيِّنُنَّهُ لِلنَّاسِ وَلَا تَكْتُمُونَهُ {187}
Na pia kuwa wao wana haja zaidi ya kuongozwa na kubainishiwa.
Na hao wazazi humwomba msaada Mwenyezi Mungu na humwambia mtoto wao: Ole wako! Amini! Hakika miadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli.
Wanamwomba msaada Mwenyezi Mungu kutokana na kufuru ya mtoto wao na kumsisitiza kwamba ufufuo ni kweli. Mara nyingi mwito wa wazazi kwa mtoto unakuwa kama kawaida tu, lakini neno ‘humwomba msaada Mwenyezi Mungu,’ linaonyesha jinsi wanavyoona uchungu na masikitiko kwa kufuru ya mtoto wao aliyewaasi na ujeuri wake. Lakini pamoja na yote hayo anang’ng’nia upotevu na yeye husema:
Hayakuwa haya ila ni ngano za watu wa kale.
Anawajibu wazazi wake pamoja na huruma zao kwake na nasaha zao: Maneno yenu haya hayana maana yoyote ispokuwa porojo tu. Hivi ndivyo vijana wengi wa kileo wanavyowangalia baba zao na mama zao. Ajabu ni kuwa kijana lau atayasikia haya kutoka kwa kijana mwenzake asingelikuwa na msimamo huu wa dharau.
Hao ndio ambao imehakikishwa kauli juu yao kama mataifa yaliyok- wishapita kabla yao miongoni mwa majini na watu.
‘Hao,’ ni kila mwenye kuifanyia inadi haki na akapinga mwito wa wenye ikhlasi. Kuhakikishiwa kauli juu yao ni neno la adhabu. Hii ni desturi ya Mwenyezi Mungu katika uma zilizotangulia, wawe maji- ni au watu.
Hakika hao wamekuwa wenye kuhasirika, kwa vile waliuacha mwito wa haki na wakamzibia masikio mtoa nasaha aliyemwaminifu.
Na wote watakuwa na daraja zao mbali mbali kwa waliyoyatenda, na ili awalipe kwa vitendo vyao, na hawatadhulumiwa.
Daraja za watu, siku ya Kiyama, zitatofautiana kulingana na matendo yao yalivyokuwa duniani. Tafisiri wazi zaidi inayofafanua Aya hii, ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:
يَوْمَ تَجِدُ كُلُّ نَفْسٍ مَا عَمِلَتْ مِنْ خَيْرٍ مُحْضَرًا وَمَا عَمِلَتْ مِنْ سُوءٍ {30}
Na siku wale waliokufuru watakapoonyeshwa Moto; yaani watakapoadhibiwa, na Malaika wa adhabu watawaambia:
Nyinyi mlitwaa vitu vyenu vizuri katika maisha yenu ya dunia, na mkastarehe navyo.
Mlikusanya mamilioni ya pesa mlizozipora kisha mkazirundika, mkajijengea viwanda na majumba marefu kwa hisabu ya wanyonge, mkatumia yote kwenye raha na starehe, bila ya kuiwekea akiba siku hii ya leo.
Basi leo mnalipwa adhabu ya fedheha kwa mlivyokuwa mkitakabari katika ardhi bila ya haki, na kwa mlivyokuwa mkifanya ufuska.
Mlionyeshwa haki mkaifanyia kiburi, mkajitukuza na mkaijaza ardhi dhulma na ufisadi. Basi onjeni uchungu wa ubaya wenu kama mlivyoonja utamu wake jana.
Katika Tafsir ya Sheikh Al-Maraghi, kuna maelezo kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alipokuwa akitaka kusafiri, mtu wa mwisho kumuaga katika familia alikuwa ni Fatima, na mtu wa kwanza kumjulia hali, anaporudi safirini, alikuwa ni Fatima. Siku moja aliporudi kutoka katika vita alikwenda nyumbani kwa Fatima, kama desturi yake.
Akaona pazia ya sufu nzito mlangoni na akawaona Hasan Na Husein wamevishwa vikuku vya fedha, basi akarudi bila ya kuingia. Fatima akaona kuwa hakuingia kutokana na aliyoyaona. Basi akaiondoa ile pazia na vikukuu akavipeleka kwa baba yake naye akawapa masikini na akasema: “Hawa ndio watu wa nyumba yangu – akiwashiria Fatima na waliomo nyumbani mwake – wala sipendi wale vizuri vyao katika maisha yao ya dunia.”
وَاذْكُرْ أَخَا عَادٍ إِذْ أَنْذَرَ قَوْمَهُ بِالْأَحْقَافِ وَقَدْ خَلَتِ النُّذُرُ مِنْ بَيْنِ يَدَيْهِ وَمِنْ خَلْفِهِ أَلَّا تَعْبُدُوا إِلَّا اللَّهَ إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ {21}
قَالُوا أَجِئْتَنَا لِتَأْفِكَنَا عَنْ آلِهَتِنَا فَأْتِنَا بِمَا تَعِدُنَا إِنْ كُنْتَ مِنَ الصَّادِقِينَ {22}
قَالَ إِنَّمَا الْعِلْمُ عِنْدَ اللَّهِ وَأُبَلِّغُكُمْ مَا أُرْسِلْتُ بِهِ وَلَٰكِنِّي أَرَاكُمْ قَوْمًا تَجْهَلُونَ {23}
فَلَمَّا رَأَوْهُ عَارِضًا مُسْتَقْبِلَ أَوْدِيَتِهِمْ قَالُوا هَٰذَا عَارِضٌ مُمْطِرُنَا ۚ بَلْ هُوَ مَا اسْتَعْجَلْتُمْ بِهِ ۖ رِيحٌ فِيهَا عَذَابٌ أَلِيمٌ {24}
تُدَمِّرُ كُلَّ شَيْءٍ بِأَمْرِ رَبِّهَا فَأَصْبَحُوا لَا يُرَىٰ إِلَّا مَسَاكِنُهُمْ ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِي الْقَوْمَ الْمُجْرِمِينَ {25}
وَلَقَدْ مَكَّنَّاهُمْ فِيمَا إِنْ مَكَّنَّاكُمْ فِيهِ وَجَعَلْنَا لَهُمْ سَمْعًا وَأَبْصَارًا وَأَفْئِدَةً فَمَا أَغْنَىٰ عَنْهُمْ سَمْعُهُمْ وَلَا أَبْصَارُهُمْ وَلَا أَفْئِدَتُهُمْ مِنْ شَيْءٍ إِذْ كَانُوا يَجْحَدُونَ بِآيَاتِ اللَّهِ وَحَاقَ بِهِمْ مَا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ {26}
وَلَقَدْ أَهْلَكْنَا مَا حَوْلَكُمْ مِنَ الْقُرَىٰ وَصَرَّفْنَا الْآيَاتِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ {27}
فَلَوْلَا نَصَرَهُمُ الَّذِينَ اتَّخَذُوا مِنْ دُونِ اللَّهِ قُرْبَانًا آلِهَةً ۖ بَلْ ضَلُّوا عَنْهُمْ ۚ وَذَٰلِكَ إِفْكُهُمْ وَمَا كَانُوا يَفْتَرُونَ {28}