read

Sura Ya Arubaini Na Saba: Muhammad

Ina Aya 38. Aya zote au nyingi zimeshuka Madina.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَنْ سَبِيلِ اللَّهِ أَضَلَّ أَعْمَالَهُمْ {1}

Wale waliokufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu, Yeye atavipotoa vitendo vyao.

وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ وَآمَنُوا بِمَا نُزِّلَ عَلَىٰ مُحَمَّدٍ وَهُوَ الْحَقُّ مِنْ رَبِّهِمْ ۙ كَفَّرَ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ وَأَصْلَحَ بَالَهُمْ {2}

Na wale walioamini, na wakatenda mema, na wakaamini aliyoteremshiwa Muhammad - nayo ni Haki iliyotoka kwa Mola wao - atawafutia maovu yao na ataitengeneza hali yao.

ذَٰلِكَ بِأَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا اتَّبَعُوا الْبَاطِلَ وَأَنَّ الَّذِينَ آمَنُوا اتَّبَعُوا الْحَقَّ مِنْ رَبِّهِمْ ۚ كَذَٰلِكَ يَضْرِبُ اللَّهُ لِلنَّاسِ أَمْثَالَهُمْ {3}

Hayo ni kwa sababu wale waliokufuru wamefuata upotovu, na walioamini wamefuata Haki iliyotoka kwa Mola wao. Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowapigia watu mifano yao.

فَإِذَا لَقِيتُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا فَضَرْبَ الرِّقَابِ حَتَّىٰ إِذَا أَثْخَنْتُمُوهُمْ فَشُدُّوا الْوَثَاقَ فَإِمَّا مَنًّا بَعْدُ وَإِمَّا فِدَاءً حَتَّىٰ تَضَعَ الْحَرْبُ أَوْزَارَهَا ۚ ذَٰلِكَ وَلَوْ يَشَاءُ اللَّهُ لَانْتَصَرَ مِنْهُمْ وَلَٰكِنْ لِيَبْلُوَ بَعْضَكُمْ بِبَعْضٍ ۗ وَالَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَلَنْ يُضِلَّ أَعْمَالَهُمْ {4}

Basi mnapokutana na waliokufuru wapigeni shingo, mpaka mkiwadhoofisha wafungeni pingu. Tena waachilieni kwa hisani au wajikomboe, mpaka vita vitue mizigo yake. Ndio hivyo. Na lau angelitaka Mwenyezi Mungu angeliwashinda mwenyewe, lakini haya ni kwa sababu awatie katika mitihani nyinyi kwa nyinyi. Na waliouliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu hatazipoteza amali zao.

سَيَهْدِيهِمْ وَيُصْلِحُ بَالَهُمْ {5}

Atawaongoza na awatengezee hali yao.

وَيُدْخِلُهُمُ الْجَنَّةَ عَرَّفَهَا لَهُمْ {6}

Na atawaingiza katika Pepo aliyowajulisha.