Aya 1 – 6: Aminini Tuliyomteremshia Muhammad
Maanaa
Wale waliokufuru na wakazuilia njia ya Mwenyezi Mungu, Yeye atavipotoa vitendo vyao.
Neno ‘kuzuilia’ tumelifasiri kutokana na neno la kiarabu ‘swaddu’ lenye maana ya kupinga na pia lina maana ya kuzuuilia. Likifasiriwa kwa maana ya kwanza, itakuwa kukufuru na kupinga ni kwa maana moja na uungan- ishi utakuwa ni wa kitafsiri. Ikiwa litafasiriwa ‘kuzuiliwa’ maana yake itakuwa wao hawakuamini na pia wamewazuia watu wengine wasiamini. Hii ndio dhahiri inayofahamishwa na Aya.‘Kuvipotoa vitendo vyao,’ ni kuvibatilisha; kama kwamba havikuwaokoa.
Maana ni kuwa mwenye kuupinga Uislamu na akawazuia watu wengine wasiuamini, Mwenyezi Mungu hatamkubalia chochote. Kwa sababu Uislamu ni sharti la msingi la thawabu za Akhera. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:
وَمَا مَنَعَهُمْ أَنْ تُقْبَلَ مِنْهُمْ نَفَقَاتُهُمْ إِلَّا أَنَّهُمْ كَفَرُوا بِاللَّهِ وَبِرَسُولِهِ {54}
Na wale walioamini, na wakatenda mema, na wakaamini aliyoteremshiwa Muhammad - nayo ni Haki iliyotoka kwa Mola wao - atawafutia maovu yao na ataitengeneza hali yao.
Neno hali hapa tumelifasiri kutokana na neno la kiarabu ‘bal’ ambalo pia lina maana ya moyo.
Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kusema kuwa hatawakubalia makafiri, sasa anasema kuwa mwenye kufanya amali njema akiwa anamwamini Mwenyezi Mungu na Qur’an isiyo na shaka, atamkubalia na atamsamehe dhambi zake akitubia na pia atamtengenezea vizuri mambo yake duniani kwa tawfiki na heri na Akhera atamtia Peponi.
Hayo ni kwa sababu wale waliokufuru wamefuata upotovu, na walioamini wamefuata Haki iliyotoka kwa Mola wao.
‘Hayo’ ni hayo ya thawabu za watenda mema na adhabu ya watenda uovu. Maana ni kuwa haki ina wenyewe na batili ina wenyewe. Na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) atamlipa kila mmoja stahiki yake, hakika yeye ana habari ya wanayoyafanya.
Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowapigia watu mifano yao akibainisha thawabu za mtenda mema na mfano wa watenda mema wenzake, ili awe na yakini ya wema wake na uongofu wake na kumbainishia muovu mfano wa adhabu ya waovu wenzake, ili aweze kujikanya na kuongoka.
Basi mnapokutana na waliokufuru wapigeni shingo mpaka mkiwadhoofisha wafungeni pingu. Tena waachilieni kwa hisani au wajikomboe, mpaka vita vitue mizigo yake.
Aya hii ni miongoni mwa mama wa Aya na katika Aya zilizo wazi wazi na maudhui yake ya vita ni muhimu. Kwa hiyo kwanza tutafsiri misamiati yake kisha tubainishe maana yanayopatikana:
Makusudio ya kukutana ni kupamabana na maadui wa Uislamu katika vita. Kupiga shingo ni kinaya cha kuua; iwe ni kwa kukata shingo au vinginevyo. Mwenyezi Mungu amehusisha kutaja shingo kwa vile ni katika viungo muhimu. Kuwadhoofisha ni kuwaua sana na kuwakamata.
Kufunga pingu ni kuwafunga imara au kutia jela ili wasikimbie wakawarudishia mpira nyinyi. Kuwachilia kwa hisani ni kuwaachilia kwa fidia au bila ya kutoa fidia. Kutua vita mizio yake ni adui kusalimu amri na kutupa silaha. Kwa sababu mizigo ya vita ni silaha.
Maana ya Aya kwa ujumla ni maadui wa dini waking’ang’ania kufuru na mkapambana nao kwa vita, basi wapigeni ili isiwashike huruma na mpambane nao kwa uimara mpaka muwakamate.
Mkishawakamata basi muwazuie barabara ili wasiwaponyoke wasije wakawageukia. Baada ya hapo mwenye hiyari atakuwa ni Mtume au naibu wake, kuwaachia mateka kwa fidia au bila fidia kulingana na masilahi yalivyo wakati huo.
Ilivyo hasa maana ya Aya hii na ile simayo:
مَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَنْ يَكُونَ لَهُ أَسْرَىٰ حَتَّىٰ يُثْخِنَ فِي الْأَرْضِ ۚ {67}
Juz. 10 (8:67),
Ni moja tu; yaani hakuna mateka ila baada ya kuwashinda vitani.
Ndio hivyo. Na lau angelitaka Mwenyezi Mungu angeliwashinda mwenyewe, lakini haya ni kwa sababu awatie katika mitihani nyinyi kwa nyinyi.
‘Ndio hivyo,’ ni ishara ya aliyoyabainisha Mwenyezi Mungu – kupigana na maaduia wa Mwenyezi Mungu na kuwachukua mateka. Maana ni kuwa lau Mwenyezi Mungu angelitaka kuwatesa maadui zake katika dunia bila ya vita angeliweza kuwaangamiza kwa askari wa kutoka mbinguni, lakini Mwenyezi Mungu amewaamuru waumini kupigana jihadi na kuwajaribu kwa makafiri, ili vidhihirike vitendo vya yule mwenye kustahiki thawabu na adhabu.
Na waliouliwa katika njia ya Mwenyezi Mungu hatazipoteza amali zao.
Mwenyezi Mungu anapigana vita na mwenye kumuasi kwa kumtumia mwenye kumtii. Akiuliwa mtiifu, damu yake haiendi bure. Vipi isiwe hivyo na hali atakuwa shahidi wa njia ya Mwenyezi Mungu na kwa ajili yake? Ni nani anayemtekelezea Mwenyezi Mungu kuliko yule aliyemafanyia ikhlasi na akafanya kwa ajili yake?
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amebainisha ujira wa waliofanya kwa ajili yake kwa kusema: “Hatapoteza amali zao,” bali itawarudia wao heri. Hiyo ni kwa kuwa Atawaongoza peponi kwenye mashukio yao, sawa na walivyokuwa wakiongoka kwenye nyumba zao za duniani na awatengezee hali yao, siku ile mtu atakapomkimbia ndugu yake na mama yake na wanawe.
Na atawaingiza katika Pepo aliyowajulisha mito yake, matunda yake, makasri yake, mahurilaini wake na mengineyo yanayotamaniwa na nafsi na yale yanayoburudisha macho.
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ تَنْصُرُوا اللَّهَ يَنْصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ {7}
وَالَّذِينَ كَفَرُوا فَتَعْسًا لَهُمْ وَأَضَلَّ أَعْمَالَهُمْ {8}
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَرِهُوا مَا أَنْزَلَ اللَّهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ {9}
أَفَلَمْ يَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَيَنْظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ ۚ دَمَّرَ اللَّهُ عَلَيْهِمْ ۖ وَلِلْكَافِرِينَ أَمْثَالُهَا {10}
ذَٰلِكَ بِأَنَّ اللَّهَ مَوْلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَأَنَّ الْكَافِرِينَ لَا مَوْلَىٰ لَهُمْ {11}
إِنَّ اللَّهَ يُدْخِلُ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ۖ وَالَّذِينَ كَفَرُوا يَتَمَتَّعُونَ وَيَأْكُلُونَ كَمَا تَأْكُلُ الْأَنْعَامُ وَالنَّارُ مَثْوًى لَهُمْ {12}
وَكَأَيِّنْ مِنْ قَرْيَةٍ هِيَ أَشَدُّ قُوَّةً مِنْ قَرْيَتِكَ الَّتِي أَخْرَجَتْكَ أَهْلَكْنَاهُمْ فَلَا نَاصِرَ لَهُمْ{13}
أَفَمَنْ كَانَ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِنْ رَبِّهِ كَمَنْ زُيِّنَ لَهُ سُوءُ عَمَلِهِ وَاتَّبَعُوا أَهْوَاءَهُمْ {14}