read

Sura Ya Arubaini Na Nane: Al-Fath

Imeshuka Makka. Ina Aya 29.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

إِنَّا فَتَحْنَا لَكَ فَتْحًا مُبِينًا {1}

Hakika tumekupa ushindi wa dhahiri

لِيَغْفِرَ لَكَ اللَّهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِكَ وَمَا تَأَخَّرَ وَيُتِمَّ نِعْمَتَهُ عَلَيْكَ وَيَهْدِيَكَ صِرَاطًا مُسْتَقِيمًا {2}

Ili Mwenyezi Mungu akughufirie dhambi yako iliyotangulia na ijayo, na akutimizie neema zake, na akuongoze katika njia iliyonyooka.

وَيَنْصُرَكَ اللَّهُ نَصْرًا عَزِيزًا {3}

Na Mwenyezi Mungu akunusuru nusura yenye nguvu.

هُوَ الَّذِي أَنْزَلَ السَّكِينَةَ فِي قُلُوبِ الْمُؤْمِنِينَ لِيَزْدَادُوا إِيمَانًا مَعَ إِيمَانِهِمْ ۗ وَلِلَّهِ جُنُودُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَكَانَ اللَّهُ عَلِيمًا حَكِيمًا {4}

Yeye ndiye aliyeteremsha utulivu katika nyoyo za waumini ili wazidi imani juu ya imani yao. Na Mwenyezi Mungu ana majeshi ya mbingu na ardhi; na Mwenyezi Mungu ni Mwenye ujuzi, Mwenye hikima.

لِيُدْخِلَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِنْ تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَيُكَفِّرَ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عِنْدَ اللَّهِ فَوْزًا عَظِيمًا {5}

Ili awaingize waumini wanaume na waumini wanawake katika Bustani zipitiwazo na mito chini yake, wadumu humo, na awafutie maovu yao. Na huko ndiko kufuzu kukubwa mbele ya Mwenyezi Mungu.