Aya 6 – 9: Na Awaadhibu Wanafiki
Maana
Na awaadhibu wanafiki wanaume na wanafiki wanawake, na washirikina wanaume na washirikina wanawake, wanaomdhania Mwenyezi Mungu dhana mbaya. Utawafikia mgeuko mbaya, na Mwenyezi Mungu awakasirikie, na awalaani, na awaandalie Jahannamu. Na hayo ni marudio maovu kabisa.
Ubaya ni shari na ufisadi. Makusudio ya dhana mbaya kwa Mwenyezi Mungu ni kudhani kuwa, ambaye imetukuka hekima yake, hatafufua walio katika makaburi na kwamba hataunusuru uislamu na Nabii wa uislamu na mengineyo wanayoyadhania wanafiki na washirikina.
Maana kwa ujumla ni kuwa Mwenyezi Mungu, kama alivyowaandalia watu wa imani Peo yenye neema, vile vile amewaandalia wale waliomdhania vibaya, kama waanafiki na washirikana, shari itakayowazunguka kila upande, hasira, laana na mwisho mbaya – moto wa Jahannam usiokwisha wakafa wala hautapunguzwa.
Na Mwenyezi Mungu ana majeshi ya mbingu na ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye ujuzi, Mwenye hikima.
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) aliitaja Aya hii alipowaashiria watu wa imani na malipo yao katika Aya iliyotangulia. Hapa tena ameitaja akiwaashiria wanafiki na washirikina. Lengo la kukaririka huku ni kutanabahisha kwamba Yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu ni muweza wa kuwaneemesha na kuwaadhibu, ili mja amtii Mwenyezi Mungu kwa kutarajia thawabu zake na ajiepushe na kumuasi kuhofia adhabu yake.
Hakika tumekutuma uwe shahidi na mbashiri na muonyaji.
Kesho Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) atashuhudia mbele ya Mwenyezi Mungu kwamba yeye amewafikishia waja yale aliyopewa wahyi, akawabashiria watiifu kuokoka na akawaonya waasi na maangamizi.
Imetangulia kwa herufi zake katika Juz. 22 (33:45).
Ili mumwamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na mumsaidie, na mumhishimu, na mumsabihi asubuhi na jioni.
Mumsaidie na mumhishimu ni Mtume. Imesemekana kuwa ni Muisaidie na muihishimu dini, lakini maana yote ni sawa. Mumsabihi Mwenyezi Mungu. Makusudio ya tasbihi ya asubuhi na jioni ni swala tano.
Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu alimtuma Muhammad kwa viumbe ili wamwamini Mwenyezi Mungu na risala ya Muhammad (s.a.w.) wamsaidie kwa kupigana jihadi katika njia yake Mwenyezi Mungu na wamuhishimu kwa kuhishimu hukumu za Mwenyezi Mungu kwa kuzitii na kuzitumia na pia wadumu kwenye Swala tano.
إِنَّ الَّذِينَ يُبَايِعُونَكَ إِنَّمَا يُبَايِعُونَ اللَّهَ يَدُ اللَّهِ فَوْقَ أَيْدِيهِمْ ۚ فَمَنْ نَكَثَ فَإِنَّمَا يَنْكُثُ عَلَىٰ نَفْسِهِ ۖ وَمَنْ أَوْفَىٰ بِمَا عَاهَدَ عَلَيْهُ اللَّهَ فَسَيُؤْتِيهِ أَجْرًا عَظِيمًا {10}
سَيَقُولُ لَكَ الْمُخَلَّفُونَ مِنَ الْأَعْرَابِ شَغَلَتْنَا أَمْوَالُنَا وَأَهْلُونَا فَاسْتَغْفِرْ لَنَا ۚ يَقُولُونَ بِأَلْسِنَتِهِمْ مَا لَيْسَ فِي قُلُوبِهِمْ ۚ قُلْ فَمَنْ يَمْلِكُ لَكُمْ مِنَ اللَّهِ شَيْئًا إِنْ أَرَادَ بِكُمْ ضَرًّا أَوْ أَرَادَ بِكُمْ نَفْعًا ۚ بَلْ كَانَ اللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا {11}
بَلْ ظَنَنْتُمْ أَنْ لَنْ يَنْقَلِبَ الرَّسُولُ وَالْمُؤْمِنُونَ إِلَىٰ أَهْلِيهِمْ أَبَدًا وَزُيِّنَ ذَٰلِكَ فِي قُلُوبِكُمْ وَظَنَنْتُمْ ظَنَّ السَّوْءِ وَكُنْتُمْ قَوْمًا بُورًا {12}
وَمَنْ لَمْ يُؤْمِنْ بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ فَإِنَّا أَعْتَدْنَا لِلْكَافِرِينَ سَعِيرًا {13}
وَلِلَّهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ يَغْفِرُ لِمَنْ يَشَاءُ وَيُعَذِّبُ مَنْ يَشَاءُ ۚ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَحِيمًا {14}