read

Sura Ya Hamsini na Mmoja: Adh-Dhariyat

Imeshuka Makka. Ina Aya 60.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu

وَالذَّارِيَاتِ ذَرْوًا {1}

Naapa kwa zinazotawanya sana.

فَالْحَامِلَاتِ وِقْرًا {2}

Na zinazobeba mizigo.

فَالْجَارِيَاتِ يُسْرًا {3}

Na zinazokwenda kwa wepesi.

فَالْمُقَسِّمَاتِ أَمْرًا {4}

Na zinazogawanya amri.

إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَصَادِقٌ {5}

Hakika mnayoahidiwa bila ya shaka ni kweli.

وَإِنَّ الدِّينَ لَوَاقِعٌ {6}

Na kwa hakika dini bila ya shaka itatokea.

وَالسَّمَاءِ ذَاتِ الْحُبُكِ {7}

Naapa kwa mbingu zenye umbile zuri.

إِنَّكُمْ لَفِي قَوْلٍ مُخْتَلِفٍ {8}

Hakika nyinyi bila ya shaka mko katika kauli inayokhitalifiana.

يُؤْفَكُ عَنْهُ مَنْ أُفِكَ {9}

Anageuzwa nayo mwenye kugeuzwa.

قُتِلَ الْخَرَّاصُونَ {10}

Wazushi wameangamizwa.

الَّذِينَ هُمْ فِي غَمْرَةٍ سَاهُونَ {11}

Ambao wameghafilika katika ujinga.

يَسْأَلُونَ أَيَّانَ يَوْمُ الدِّينِ {12}

Wanauliza: Ni lini hiyo siku ya malipo?

يَوْمَ هُمْ عَلَى النَّارِ يُفْتَنُونَ {13}

Ni siku watakayojaribiwa Motoni.

ذُوقُوا فِتْنَتَكُمْ هَٰذَا الَّذِي كُنْتُمْ بِهِ تَسْتَعْجِلُونَ {14}

Onjeni fitna yenu! Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyahimiza.