Aya 1 – 14: Naapa Kwa Zinazotawanya
Maana
Naapa kwa zinazotawanya sana, na zinazobeba mizigo, na zinazokwenda kwa wepesi, na zinazogawanya amri.
Katika kufasiri sifa hizi nne kuna rai kadhaa: Kuna waliosema kuwa Makusudio ya zinazotawanya ni pepo, zinazobeba ni mawingu zinazokwenda kwa wepesi ni jahazi na zinazogawanya ni malaika.
Kauli yenye nguvu ni kuwa zote hizi ni sifa za pepo. Ndizo zinazotawanya kwa vile zinatawanya mchanga nk. Akitumia neno hilo, Mwenyezi Mungu Mtufu anasema:
هَشِيمًا تَذْرُوهُ الرِّيَاحُ ۗ {45}
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameapa kwa upepo kuashiria manufaa yake, pia kuwa Mwenyezi Mungu anaweza kuapa na kila anachokitaka katika viumbe vyake. Tazama Juz. 23 (37:1-10)
Sifa ya pili ni ‘Na zinazobeba mizigo,’ Makusudio yake hapa ni kuwa pepo zinabeba mzigo wa mawingu. Anasema Mwenyezi Mungu Mtufu:
سُقْنَاهُ لِبَلَدٍ مَيِّتٍ {57}
Sifa ya tatu: ‘Na zinazokwenda kwa wepesi,’ ni kuwa pepo zinakwenda kwa wepesi zikiwa zinabeba mawingu. Sifa ya nne: ‘Na zinazogawanya amri.’ Pepo zinatawanya mvua katika ardhi; kama ilivyoelezwa kwenye Juz. 8 (7:57).
Hakika mnayoahidiwa bila ya shaka ni kweli, Na kwa hakika dini bila ya shaka itatokea.
Hili n jawabu la kiapo. Makusudio ya mnayoahidiwa ni uhai baada ya mauti. Na dini ni hisabu na malipo.Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu atawafufua tu walio makaburini, hilo halina shaka. Na kwamba Yeye atamlipa mtu kwa matendo yake. Yakiwa heri basi ni heri na yakiwa shari basi ni shari.
Naapa kwa mbingu zenye umbile zuri.
‘Umbile zuri’ tumelifasiri kutokana na neno la kiarabu ‘Hubuk’ ambalo wafasiri wamelitolea kauli nyingi. Lakini iliyo na nguvu ni hii tuliyoifasiri; kwa maana ya kuwa katika maumbile ya mbingu kuna mpangilio, nidhamu, uzuri na kupendeza.
Hakika nyinyi bila ya shaka mko katika kauli inayokhitalifiana.
Msemo unaelekezwa kwa wale wanaomkadhibisha Mtume (s.a.w.) na kauli zao zote ni za mgongano, mkorogano, uwongo na njozi; kama vile kusema kuwa Mtume ni mshairi, mara mwendawazimu na mara nyingine ni mchawi. Na kuhusu Qur’an wakasema ni vigano vya watu wa kale au imetungwa na Muhammad (s.a.w.) n.k.
Anageuzwa nayo mwenye kugeuzwa.
Yaani anageuzwa na dini na haki yule anayeigeuka kwa hawa na ujinga; mfano wake ni sawa na kauli: “Hapofuki na hilo ila kipofu.”
Wazushi wameangamizwa.
Hao ni wale aliowabainisha Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa kusema:
Ambao wameghafilika katika ujinga.
Ujinga na upotevu umewavaa kuanzia kichwani hadi unyayoni, wakazipeleka dhana zao ovyoovyo na bila ya msingi wowote, kwenye ardhi na mbinguni na kwenye ufufuo na malipo. Wakasema kuwa Mwenyezi Mungu ana washirika katika mawe na ana mabinti katika Malaika na wengine aliozaa na majini. Ama ufufuo na hisabu kwao ni upotevu.
Wanauliza: Ni lini hiyo siku ya malipo?
Wenye dharau wanauliza, huo ufufuo utakuwa lini? Mwenyezi Mungu (s.w.t.) naye anawajibu:
Ni siku watakayojaribiwa Motoni.
Ufufuo utakuwa siku watakayoonyeshwa moto na kuunguzwa humo. Husemwa kuwa kitu kimejaribiwa, ili kutoa kilichoghushiwa, kikiunguzwa motoni. Malaika wa Motoni watawaambia:
Onjeni fitna yenu! Haya ndiyo mliyokuwa mkiyahimiza.
Hii ndio adhabu mliyokuwa mkihimiza na kuifanyia dharau jana. Je, mmeionaje ladha yake?
إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ {15}
آخِذِينَ مَا آتَاهُمْ رَبُّهُمْ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَبْلَ ذَٰلِكَ مُحْسِنِينَ {16}
كَانُوا قَلِيلًا مِنَ اللَّيْلِ مَا يَهْجَعُونَ {17}
وَبِالْأَسْحَارِ هُمْ يَسْتَغْفِرُونَ {18}
وَفِي أَمْوَالِهِمْ حَقٌّ لِلسَّائِلِ وَالْمَحْرُومِ {19}
وَفِي الْأَرْضِ آيَاتٌ لِلْمُوقِنِينَ {20}
وَفِي أَنْفُسِكُمْ ۚ أَفَلَا تُبْصِرُونَ {21}
وَفِي السَّمَاءِ رِزْقُكُمْ وَمَا تُوعَدُونَ {22}
فَوَرَبِّ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ إِنَّهُ لَحَقٌّ مِثْلَ مَا أَنَّكُمْ تَنْطِقُونَ {23}
هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ ضَيْفِ إِبْرَاهِيمَ الْمُكْرَمِينَ {24}
إِذْ دَخَلُوا عَلَيْهِ فَقَالُوا سَلَامًا ۖ قَالَ سَلَامٌ قَوْمٌ مُنْكَرُونَ {25}
فَرَاغَ إِلَىٰ أَهْلِهِ فَجَاءَ بِعِجْلٍ سَمِينٍ {26}
فَقَرَّبَهُ إِلَيْهِمْ قَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ {27}
فَأَوْجَسَ مِنْهُمْ خِيفَةً ۖ قَالُوا لَا تَخَفْ ۖ وَبَشَّرُوهُ بِغُلَامٍ عَلِيمٍ {28}
mwenye ilimu.
فَأَقْبَلَتِ امْرَأَتُهُ فِي صَرَّةٍ فَصَكَّتْ وَجْهَهَا وَقَالَتْ عَجُوزٌ عَقِيمٌ {29}
قَالُوا كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِ ۖ إِنَّهُ هُوَ الْحَكِيمُ الْعَلِيمُ {30}