read

Sura Ya Arubaini Na Mbili: Ash-Shura

Ina Aya 53.

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

حم {1}

Haa Mim.

عسق {2}

A’yn Siin Qaaf.

كَذَٰلِكَ يُوحِي إِلَيْكَ وَإِلَى الَّذِينَ مِنْ قَبْلِكَ اللَّهُ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ {3}

Hivyo ndivyo Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu na Mwenye hikima anavyokuletea Wahyi wewe na walio kabla yako.

لَهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۖ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ {4}

Ni vyake vilivyomo mbinguni, na vilivyomo ardhini. Na Yeye ndiye Mtukufu, Mkuu.

تَكَادُ السَّمَاوَاتُ يَتَفَطَّرْنَ مِنْ فَوْقِهِنَّ ۚ وَالْمَلَائِكَةُ يُسَبِّحُونَ بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَيَسْتَغْفِرُونَ لِمَنْ فِي الْأَرْضِ ۗ أَلَا إِنَّ اللَّهَ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ {5}

Zinakaribia mbingu kutatuka juu yao. Na Malaika wakimsabihi Mola wao kwa kumhimidi na wakiwaombea maghufira waliomo kwenye ardhi. Ehe! Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwingi wa maghufira Mwenye kurehemu.

وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مِنْ دُونِهِ أَوْلِيَاءَ اللَّهُ حَفِيظٌ عَلَيْهِمْ وَمَا أَنْتَ عَلَيْهِمْ بِوَكِيلٍ {6}

Na wale waliowafanya mawalii wengine badala yake Yeye, Mwenyezi Mungu ni Mwangalizi juu yao; wala wewe si wakili juu yao.

وَكَذَٰلِكَ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لِتُنْذِرَ أُمَّ الْقُرَىٰ وَمَنْ حَوْلَهَا وَتُنْذِرَ يَوْمَ الْجَمْعِ لَا رَيْبَ فِيهِ ۚ فَرِيقٌ فِي الْجَنَّةِ وَفَرِيقٌ فِي السَّعِيرِ {7}

Na namna hivi tumekupa wahyi Qur’an kwa kiarabu ili uwaonye watu wa Mama wa miji na walio pembezoni mwake. Na uhadharishe na Siku ya Mkutano, haina shaka hiyo. Kundi moja litakuwa Peponi, na kundi jengine Motoni.

وَلَوْ شَاءَ اللَّهُ لَجَعَلَهُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَلَٰكِنْ يُدْخِلُ مَنْ يَشَاءُ فِي رَحْمَتِهِ ۚ وَالظَّالِمُونَ مَا لَهُمْ مِنْ وَلِيٍّ وَلَا نَصِيرٍ {8}

Na Mwenyezi Mungu angelipenda angewafanya umma mmoja. Lakini anamwingiza katika rehema yake amtakaye. Na madhalimu hawana walii wala msaidizi.