Aya 9 – 14: Simamisheni Dini Wala Msifarikiane
Maana
Au wamechukua mawalii wengine badala yake! Lakini Mwenyezi Mungu ndiye walii hasa. Na Yeye ndiye anayehuisha wafu. Na Yeye ni Muweza wa kila kitu.
Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kusema katika Aya ya 6: ‘Na wale waliowafanya mawalii wengine badala yake Yeye, Mwenyezi Mungu ni Mwangalizi juu yao,’ hapa amerudia tena kauli hii na kuzidisha kuwa Yeye peke yake ndiye Mwenye kunusuru, Mwenye kusaidia, Mwenye kuhuisha, Mwenye kufisha na Muweza wa kila kitu.
Amerudia pamoja na ziada hii ili kumpinga anayemfanyia washirika; kwamba asiyekuwa Yeye hawezi kuleta uhai wala mauti au kusaidia, kwa vile hawezi kila kitu.
Na mkikhitalifiana katika jambo lolote, basi hukumu yake iko kwa Mwenyezi Mungu.
Huyo Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu ninayemtegemea na kwake Yeye narejea.
Haya ni masimulizi ya maneno ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) akiwaambia watu wote kwamba kila kitu watakachikhitalifiana kuwa ni haki au batili, basi rejea ni Qur’an; kauli yake ni ya upambanuzi na hukumu yake ni ya uadilifu.
Mfano wa Aya hii ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Na kama mkipingana katika jambo, basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake mkiwa mwamwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho. Hilo ni bora zaidi na mwisho mzuri.” Juz. 5 (4:95).
Muumba mbingu na ardhi.
Ameziumba na akazipangilia, wala hakuna tofauti kwa Mwenyezi Mungu baina ya kuumba mbingu na ardhi na kuumba mdudu chungu. Amempangilia vizuri hivi, kama alivyoupangilia ulimwengu.
Amewajaalia mke na mume katika nafsi zenu, ili mpate utulivu:
وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُمْ مِنْ أَنْفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُمْ مَوَدَّةً وَرَحْمَةً ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ {21}
Na katika wanyama howa dume na jike, anawazidisha namna hii.
Yaani Mwenyezi Mungu amewafanya watu na wanyama waume na wake ili wazidi kuwa wengi. Na kuzidi huku ni neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Hakuna chochote kama mfano wake, si katika dhati yake wala sifa zake, kwa vile Yeye ni zaidi ya kila kitu. Hakuna Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu mmoja Mwenye nguvu. Naye ni Mwenye kusikia Mwenye kuona, anasikia kauli zote na kuona matendo yote.
Yeye ndiye Mwenye funguo za mbingu na ardhi. Humkunjulia riziki amtakaye, na humpimia amtakaye. Hakika Yeye ni Mjuzi wa kila kitu.
Riziki za mbinguni na ardhini ziko mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Humpanulia amtakaye na humfinyia amtakaye kutokana na hekima yake inavyotaka. Hakuna mwenye shaka kwamba uchache wa mali pamoja na afya, amani, dini na utengenevu ni bora mara elfu kuliko kuwa na mali nyingi pamoja na hofu, ugonjwa, ukafiri na ufisadi. Tumezungumzia rizi kwa anuani ya: ‘Riziki na ufisadi’ Juz. 6 (5:66), ‘Je, riziki ni bahati au majaliwa’ Juz. 7 (5:100) na ‘Mtu na riziki’ Juz. 13 (13:26)
Amewapa sharia ya Dini aliyomuusia Nuh na tuliyokupa wahyi wewe, na tuliyowausia Ibrahim na Musa na Isa, kwamba simamisheni Dini wala msifarikiane kwayo.
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) aliwatuma mitume wote kwa tamko la Tawhid, kuamini siku ya mwisho, kusimaisha Swala na kutoa Zaka. Vile vile kuharamisha dhulma, ghushi, uongo na zina. Pia kuharamisha kuoa mama, binti, dada na mengineyo ya misingi ya dini na sharia, lakini sio matawi ya dini ambayo yanatofautiana kulingana na wakati na masilahi; kama alivyoashiria Mwenyezi Mungu kwa kusema:
لِكُلٍّ جَعَلْنَا مِنْكُمْ شِرْعَةً وَمِنْهَاجًا ۚ {48}
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amemuhusisha kumtaja Nuh, Ibrahim, Musa, Isa na Muhammad, kwa vile tu wao ni mitume ulul-azm, vinginevyo ni kuwa huyo anayeusiwa ni mmoja kwa mitume wote.
Ikiwa Mungu ni mmoja, dini ni moja na mwito ni mmoja, basi kuna haja gani ya uadui na kuchinjana katika dini? Kuna sababu gani ya vita vilivyosajiliwa na historia kwa herufi za fedheha na aibu?
Tumezungumza kwa ufafanuzi zaidi kuhusu mwito wa mitume na kwam- ba wao wako kwenye dini moja katika Juz. 3 (3:18–20) kifungu cha ‘Dini ya Mwenyezi Mungu ni uislamu’ na tukafuatishia kuzungumzia tofauti baina ya dini na madhehebu kwenye kifungu ‘Vikundi sabini na tatu.’
Vile vile tumezungumzia kwenye Juz.1(2:111) kifungu cha ‘Ualanguzi wa Pepo’ na tukafuatishia na kifungu cha: “Kila mmoja avutia kwake’
Ni magumu kwa washirikina hayo unayowaitia ewe Muhammad, kwa sababu kwanza, wewe si mfalme wala huna mali. Pili, wewe unalingania kwenye haki, wala hakuna kitu kizito zaidi kuliko hicho kwa watu wa matamanio na wabatilifu. Tatu, kuwa wewe umewaita mababa zao wajinga na wapotevu.
Mwenyezi Mungu humteua kwake amtakaye, na amekuchagua wewe ewe Muhammad kuwa ni mtu wa risala yake na akakuishilizia kwa mitume wote, ambapo huna kifani na yeyote kuanzia wa kwanza hadi wa mwisho.
Na humwongoa kwake aelekeaye.
Kila anayekimbilia kwa Mwenyezi Mungu kwa ukweli na ikhlasi basi Mwenyezi Mungu humwitikia na kumwongoza:
وَمَنْ يُؤْمِنْ بِاللَّهِ يَهْدِ قَلْبَهُ ۚ {11}
Na hawakufarikiana ila baada ya kuwajia ilimu kwa sababu ya uhasidi baina yao.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 2 (2:213) na Juz. 3 (3:19)
Na lau si neno lililokwishatangulia kutoka kwa Mola wako mpaka muda uliowekwa, basi bila ya shaka palingelihukumiwa baina yao.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 11 (10:19), Juz. 12 (11:110), Juz. 16 (20:110) na Juz. 24 (41:45)
Na hakika waliorithishwa Kitabu baada yao wanamtilia shaka inayowahangaisha.
Makusudio ya waliorithishwa kitabu ni mayahudi na manaswara. Baada yao ni mtume au uma zilizotangulia na wanayemtilia shaka ni Muhammad kutokana na inavyofahamisha kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: ‘Mwenyezi Mungu humteua kwake amtakaye.’ Maana ni kuwa watu wa Kitabu walipinga aliyokuja nayo Muhammad (s.a.w.) pamoja na ushahidi wazi wa utume wake na ukweli wa risala yake.
فَلِذَٰلِكَ فَادْعُ ۖ وَاسْتَقِمْ كَمَا أُمِرْتَ ۖ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَهُمْ ۖ وَقُلْ آمَنْتُ بِمَا أَنْزَلَ اللَّهُ مِنْ كِتَابٍ ۖ وَأُمِرْتُ لِأَعْدِلَ بَيْنَكُمُ ۖ اللَّهُ رَبُّنَا وَرَبُّكُمْ ۖ لَنَا أَعْمَالُنَا وَلَكُمْ أَعْمَالُكُمْ ۖ لَا حُجَّةَ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمُ ۖ اللَّهُ يَجْمَعُ بَيْنَنَا ۖ وَإِلَيْهِ الْمَصِيرُ {15}
وَالَّذِينَ يُحَاجُّونَ فِي اللَّهِ مِنْ بَعْدِ مَا اسْتُجِيبَ لَهُ حُجَّتُهُمْ دَاحِضَةٌ عِنْدَ رَبِّهِمْ وَعَلَيْهِمْ غَضَبٌ وَلَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ {16}
اللَّهُ الَّذِي أَنْزَلَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ وَالْمِيزَانَ ۗ وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّ السَّاعَةَ قَرِيبٌ {17}
يَسْتَعْجِلُ بِهَا الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِهَا ۖ وَالَّذِينَ آمَنُوا مُشْفِقُونَ مِنْهَا وَيَعْلَمُونَ أَنَّهَا الْحَقُّ ۗ أَلَا إِنَّ الَّذِينَ يُمَارُونَ فِي السَّاعَةِ لَفِي ضَلَالٍ بَعِيدٍ {18}