read

Sura Ya Arubaini Na Tatu: Az-Zukhruf

Ina aya 89 Imeshuka Makka. Imesemekana isipokuwa Aya moja haikushuka Makka

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu

حم {1}

Haa-miim.

وَالْكِتَابِ الْمُبِينِ {2}

Naapa kwa Kitabu kinachobainisha.

إِنَّا جَعَلْنَاهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ {3}

Hakika tumeifanya Qur’an kwa kiarabu ili mfahamu.

وَإِنَّهُ فِي أُمِّ الْكِتَابِ لَدَيْنَا لَعَلِيٌّ حَكِيمٌ {4}

Na hakika hiyo imo katika mama wa Kitabu kilichoko kwetu, ni tukufu na yenye hiki- ma.

أَفَنَضْرِبُ عَنْكُمُ الذِّكْرَ صَفْحًا أَنْ كُنْتُمْ قَوْمًا مُسْرِفِينَ {5}

Je, tuache kuwakumbusha kwa kuwa ni watu mliopita mipaka?

وَكَمْ أَرْسَلْنَا مِنْ نَبِيٍّ فِي الْأَوَّلِينَ {6}

Na manabii wangapi tuliwatuma kwa watu wa zamani!

وَمَا يَأْتِيهِمْ مِنْ نَبِيٍّ إِلَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ {7}

Na hakuwajia nabii yeyote ila walikuwa wakimkejeli.

فَأَهْلَكْنَا أَشَدَّ مِنْهُمْ بَطْشًا وَمَضَىٰ مَثَلُ الْأَوَّلِينَ {8}

Na tuliwaangamiza waliokuwa na nguvu kushinda wao, na mfano wa watu wa zamani umekwishapita.

وَلَئِنْ سَأَلْتَهُمْ مَنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ لَيَقُولُنَّ خَلَقَهُنَّ الْعَزِيزُ الْعَلِيمُ {9}

Na ukiwauliza: Nani aliyeumba mbingu na ardhi? Bila ya shaka watasema: Kaziumba Mwenye nguvu, Mjuzi.

الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ مَهْدًا وَجَعَلَ لَكُمْ فِيهَا سُبُلًا لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ {10}

Ambaye amewafanyia ardhi kuwa tandiko, na akawafanyia ndani yake njia mpate kuongoka.

وَالَّذِي نَزَّلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً بِقَدَرٍ فَأَنْشَرْنَا بِهِ بَلْدَةً مَيْتًا ۚ كَذَٰلِكَ تُخْرَجُونَ {11}

Na ambaye ameteremsha kutoka mbinguni maji kwa kiasi, na kwa hayo tukaifufua nchi iliyokufa. Na hivyo ndivyo mtakavyotolewa.

وَالَّذِي خَلَقَ الْأَزْوَاجَ كُلَّهَا وَجَعَلَ لَكُمْ مِنَ الْفُلْكِ وَالْأَنْعَامِ مَا تَرْكَبُونَ {12}

Na ambaye ameumba aina zote, na akawafanyia jahazi na wanyamahowa mnaowapanda.

لِتَسْتَوُوا عَلَىٰ ظُهُورِهِ ثُمَّ تَذْكُرُوا نِعْمَةَ رَبِّكُمْ إِذَا اسْتَوَيْتُمْ عَلَيْهِ وَتَقُولُوا سُبْحَانَ الَّذِي سَخَّرَ لَنَا هَٰذَا وَمَا كُنَّا لَهُ مُقْرِنِينَ {13}

Ili mkae vizuri migongoni mwao. Kisha mkumbuke neema za Mola wenu mnapokaa sawa sawa juu yao hao mnaowapanda na mseme: Ametakasika aliyemfanya huyu atutumikie, na tusingeliweza kufanya haya wenyewe.

وَإِنَّا إِلَىٰ رَبِّنَا لَمُنْقَلِبُونَ {14}

Na hakika sisi tutarudi kwa Mola wetu Mlezi.