read

Aya 15 – 25:Au Amejichukulia Watoto Wanawake

Maana

Na wanamfanyia katika waja wake fungu. Kwa hakika mwanadamu ni mwenye kukufuru waziwazi. Au amejichukulia watoto wakike katika vile alivyoviumba, na akawachagulia nyinyi watoto wa kiume?

Makusudio ya fungu hapa ni mtoto, kwa sababu ni sehemu ya mzazi wake. Ama kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: Watoto wa kike katika vile alivyoviumba, inaonyesha dalili ya uharibifu wa madai yao kuwa Mwenyezi Mungu ana mtoto, kwa sababu muumbwa hawezi kuwa ni sehemu ya aliyeumba; kama ambavyo nyumba haiwezi kuwa ni sehemu ya mjenzi.

Washirikina hawakutosheka na uzushi huu, mpaka wakamhusisha Mwenyezi Mungu na wale watoto wasiowapenda wao.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 7 (6:100), Juz. 15 (17:40) na Juz. 23 (37:149-153).

Na mmoja wao akibashiriwa kwa yale aliyompigia mfano Mwingi wa rehema, uso wake husawijika naye amejaa chuki.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kuwasifu washirikina na ukafiri ulio waziwazi, sasa anawashutumu wale wanaohuzunika na kukasirika wakipata wasichana, wakati huohuo wanamzulia Mwenyezi Mungu na kusema kuwa ana watoto wasichana.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 14 (16:58).

Ati aliyelelewa katika mapambo, na katika mabishano hawezi kusema bayana?

Ewe mshirikina mjinga! Unamnasibishia Mwenyezi Mungu wanawake wanojipamba, na kama ukihojiwa kwenye hilo utashindwa na hoja na dalili? Wafasiri wamesema wamemnasibishia Mwenyezi Mungu wanawake ambao hawawezi hoja na kubishana DhahiriyaAyainarudiakwenyetafsirihii.

Na wakawafanya Malaika, ambao ni waja wa Mwingi wa Rehema, ni wanawake! Kwani wameshuhudia kuumbwa kwao?

Vipi wanajasiri washirikina kusema kuwa Malaika ni mabinti wa Mwenyezi Mungu. Je, walikuwako kwa Mwenyezi Mungu wakati akiwaumba Malaika au aliwapa habari ya hilo? Amesema kweli aliyesema: “Mtu amesema uwongo juu aliye mfano wake, juu ya Mola wake, juu ya Mitume wake na Malaika wake, vile vile amesema uwongo juu ya nafsi yake.”
Mfano wa Aya hii ni kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

أَمْ خَلَقْنَا الْمَلَائِكَةَ إِنَاثًا وَهُمْ شَاهِدُونَ {150}

“Au tumewaumba malaika kuwa ni wanawake na wao wakashuhudia? Juz. 23 (37:150).

Ushahidi wao utaandikwa na wataulizwa!

Kwa Mwenyezi Mungu hakufichiki chochote, Yeye anajua uzushi wao kwake na kwa Malaika wake na kesho atawauliza na kuwahisabu

Na husema: Angelipenda Mwingi wa Rehema tusingeliwaabudu.

Wanadai kuwa Mwenyezi Mungu yuko radhi wao kuabudu Malaika na masanamu; vinginevyo angeliwazuia kwa nguvu. Wamesahau kama Mwenyezi Mungu angelifanya hivyo, mtu angelikuwa sawa na mawe, asingelistahiki thawabu wala adhabu.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 8 (6:148).

Hawana ujuzi wowote wa hayo! Hawana ila kusema uwongo tu!

Wamenasibisha shirki yao na upotevu wao kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu! Hawajui kuwa Yeye, ambaye imetukuka enzi yake, anaamrisha na anakataza kitaklifa na kimongozo, akaacha utekelezaji uwe kwa matakwa ya aliyekalifishwa, ili yadhihiri matendo yake yatakayomfanya astahiki thawabu au adhabu.

Au tuliwapa Kitabu kabla ya hiki, wakawa wameshikamana nacho?

Hapana! Hawana dalili ya akili wala ya nakili kwa madaia yao, isipokuwa dalili hii:

Bali wanasema: “Hakika sisi tuliwakuta baba zetu juu ya desturi na tunaongoza nyayo zao.

Kwa hiyo kuwaiga mababa ndio kimbilio la kwnza na la mwisho. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameisimulia kauli yao hii katika Aya kadha; miongoni mwazo ni: Juz. 2 (2:170), Juz. 7 (5:104), Juz.17 (21:53), Juz.21 (31:21) na nyinginezo. Tumeweka kifungu kuhusu kuiga na mafungu yake katika Juz. 2 (2:170).

Na kadhalika hatukumtuma mwonyaji kwenye mji wowote ila wapenda anasa wake walisema: Hakika sisi tuliwakuta baba zetu juu ya des- turi na tunafuata nyayo zao.

Haya ndio mantiki ya wanaotaka manufaa yao tu, tangu walipoanza kupatikana hadi siku ya mwisho. Tazama kifungu ‘Fikra ya mataghuti’ katika Juz. 13 (13:30-31), Juz. 15 (17:16-21) na kifungu ‘Mantiki ya watu wa pesa ni benki na ardhi.’ katika Juz. 18 (25:7-16).

Akasema: Hata nikiwaletea yenye muongozo bora kuliko mliowaku- ta nayo baba zenu? Wakasema: Sisi tunayakataa hayo mliyotumwa nayo.

Tunalolifahamu kutokana na kauli yao hii ni kuwa wao wanaikataa haki popote na vyovyote iwavyo; hata kama ingelitoka kwa mababa zao, na kwamba wao hawaamini chochote isipokuwa manufaa na chumo lao tu.

Ama kujiingiza kwenye desturi ya mababa ni visingizio tu, wakihofia kujulikana uhakika wao na watu. Tumewawona wengi wakiwabeza mababa zao, si kwa lolote ila kuwa wanagongana na masilahi na mapendeleo yao. Hakuna malipo kwa mwenye kuipinga haki isipokuwa kumtumilia nguvu:

Basi tukawalipizia. Angalia ulikuwaje mwisho wa waliokadhibisha!

Bila shaka ni fedheha na moto wa Jahannam.

وَإِذْ قَالَ إِبْرَاهِيمُ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ إِنَّنِي بَرَاءٌ مِمَّا تَعْبُدُونَ {26}

Na pale Ibrahim alipomwambia baba yake na kaumu yake: Hakika mimi ninajitenga mbali na hayo mnayoyaabudu.

إِلَّا الَّذِي فَطَرَنِي فَإِنَّهُ سَيَهْدِينِ {27}

Isipokuwa yule aliyeniumba, kwani Yeye ataniongoza.

وَجَعَلَهَا كَلِمَةً بَاقِيَةً فِي عَقِبِهِ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ {28}

Na akalifanya liwe neno lenye kubaki katika vizazi vyake ili warejee.

بَلْ مَتَّعْتُ هَٰؤُلَاءِ وَآبَاءَهُمْ حَتَّىٰ جَاءَهُمُ الْحَقُّ وَرَسُولٌ مُبِينٌ {29}

Bali tuliwastarehesha hawa na baba zao mpaka ikawafikia Haki na Mtume anayebainisha.

وَلَمَّا جَاءَهُمُ الْحَقُّ قَالُوا هَٰذَا سِحْرٌ وَإِنَّا بِهِ كَافِرُونَ {30}

Na ilipowafikia Haki wakasema: Huu ni uchawi, na sisi hakika tunaukataa.

وَقَالُوا لَوْلَا نُزِّلَ هَٰذَا الْقُرْآنُ عَلَىٰ رَجُلٍ مِنَ الْقَرْيَتَيْنِ عَظِيمٍ {31}

Na walisema: Kwa nini Qur’an hii haikuteremshwa kwa mtu mkubwa katika miji miwili hii?

أَهُمْ يَقْسِمُونَ رَحْمَتَ رَبِّكَ ۚ نَحْنُ قَسَمْنَا بَيْنَهُمْ مَعِيشَتَهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۚ وَرَفَعْنَا بَعْضَهُمْ فَوْقَ بَعْضٍ دَرَجَاتٍ لِيَتَّخِذَ بَعْضُهُمْ بَعْضًا سُخْرِيًّا ۗ وَرَحْمَتُ رَبِّكَ خَيْرٌ مِمَّا يَجْمَعُونَ {32}

Kwani wao ndio wanaogawa rehema za Mola wako? Sisi tumewagawanyia baina yao maisha yao katika uhai wa duniani, na tukawainua baadhi yao juu ya wengine kwa daraja nyingi; kwa hivyo baadhi yao wanawafanya wengine wawatumikie. Na rehema za Mwenyezi Mungu ni bora kuliko hayo wanayoyakusanya.

وَلَوْلَا أَنْ يَكُونَ النَّاسُ أُمَّةً وَاحِدَةً لَجَعَلْنَا لِمَنْ يَكْفُرُ بِالرَّحْمَٰنِ لِبُيُوتِهِمْ سُقُفًا مِنْ فِضَّةٍ وَمَعَارِجَ عَلَيْهَا يَظْهَرُونَ {33}

Na lau isingekuwa watu watakuwa kundi moja tungeliwajaalia wanaomkufuru Mwingi wa rehema nyumba zao zina dari ya fedha, na ngazi zao pia wanazopandia.

وَلِبُيُوتِهِمْ أَبْوَابًا وَسُرُرًا عَلَيْهَا يَتَّكِئُونَ {34}

Na milango ya nyumba zao na vitanda wanavyoegemea juu yake.

وَزُخْرُفًا ۚ وَإِنْ كُلُّ ذَٰلِكَ لَمَّا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۚ وَالْآخِرَةُ عِنْدَ رَبِّكَ لِلْمُتَّقِينَ {35}

Na mapambo. Na hayo yote si chochote ila ni starehe ya maisha ya dunia tu, na Akhera iliyoko kwa Mola wako ni ya wenye takua.