Aya 67 – 80: Siku Hiyo Marafiki Watakuwa Ni Maadui
Maana
Siku hiyo marafiki watakuwa maadui, wao kwa wao, isipokuwa wenye takua.
Makusudio ya maadui ni kukatika muungano; iwe ni kwa chuki na kulaaniana au bila chuki. Maana ni kuwa muungano wa mapenzi na urafiki uliokuwa duniani, baina ya watu, siku ya kiyama utaondoka na kukatika; ila ukiwa chimbuko lake ni udugu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kusaidiana kwenye twaa yake.
Kwani huo utadumu bila ya kuwa na kikomo, bali unazidi na kukua kila muda unavyorefuka, kwa sababu yaliyoko kwa ajili ya Mwenyezi Mungu yanazidi.
Zaidi ya hayo ni kwamba watu wa Peponi watakuwa ni familia moja, hata kama walikuwa wanatofautiana duniani: Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:
وَنَزَعْنَا مَا فِي صُدُورِهِمْ مِنْ غِلٍّ إِخْوَانًا عَلَىٰ سُرُرٍ مُتَقَابِلِينَ {47}
Juz.14 (15:47).
Enyi waja wangu! Leo hamtakuwa na khofu, wala hamtahuzunika.
Hii ni amani ya Mwenyezi Mungu kesho kwa wale waliomwamini Mwenyezi Mungu na wakawa na takua.
Ambao waliziamini Ishara zetu na wakawa Waislamu: Ingieni kwenye Bustani (Pepo), nyinyi na wake zenu katika hali ya kufurahishwa.
HuuniubainifunatafsiriyawajawaMwenyeziMungunakwambawao ni wale waliomwamini Mwenyezi Mungu na wakanyenyekea twaa yake na malipo yao mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni kuwaingiza Peponi pamoja na wake zao walio wema.
Maana ya ‘kufurahishwa’ ni kuwa thawabu zao haziishii kwenye amani na kukosa hofu tu; bali zinavuka hadi kwenye shangwe na furaha. Vile vile Watapitishiwa sahani za dhahabu na vikombe; sahani ni za chakula na vikombe ni vya kinywaji.
Na vitakuwamo ambavyo nafsi zinavipenda katika starehehe za kimaada na za kiroho, na macho yanavifurahia, katika mandhari mazuri. Na nyinyi mtakaa humo milele bila ya kuwa na mwisho.
Na hiyo ni Bustani (Pepo) mliyorithishwa kwa hayo mliyokuwa mkiyafanya. Pepo ni haki yenu enyi waumini mlioifanyia kazi; sawa na mirathi. Kwa sababu nyinyi mliifanyia kazi duniani.
Mnayo humo matunda mengi mtakayoyala. Chakula, kinywaji na matunda pia. Vinavyotamaniwa na nafsi havina idadi, kwa sababu matamanio ya nafsi hayana udhibiti. Vile vile ladha ya jicho.
Hakika wakosefu watakaa milele katika adhabu ya Jahannamu. Hawatapumzishwa nayo na humo watakata tamaa.
Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kutaja walioongoka, sasa anataja waliopotea na kwamba wao watakuwa katika adhabu ya daima wakiwa hawana matumaini yoyote ya kwisha wala kupungua.
Wala Sisi hatukuwadhulumu, bali wao ndio waliokuwa madhalimu. Kwa sababu Allah (s.w.t.) aliwahadharisha na kawaonya, lakini wakakataa isipokuwa kufuru. Na watapiga kelele waseme: Ewe Malik! Na atufishe Mola wako! Naye atasema: Hakika nyinyi mtakaa humo humo!
Watamuomba Malik, mtunzaji wa Moto, awaombee kwa Mwenyezi Mungu awape mauti, ili waepukane na adhabu. Naye Malik atawajibu kuwa hakuna kuokoka, nyinyi mtakua humo humo tu. Haya ndiyo mliyozifanyia nafsi zenu. Basi onjeni yale mliyokuwa mkiyafanya.
Unaweza kuuliza: Mwenyezi Mungu (s.w.t.), katika Aya iliyotangulia amewaelezea kuwa wao watakata tamaa hata ya kupunguziwa adhabu, sikwambii kukatika. Vipi hapa anawatolea habari kwamba wao watataka mauti ili waondokewe na adhabu? Hii inafahamisha matarajio ambayo yanapingana na kukata tamaa.
Jibu: Watu wa motoni watakuwa na hali ya kukata tamaa na mara nyingine kuwa na matumaini. Zaidi ya hayo inawezekana kuwa mwito wao kwa Malik ni kiasi cha kuelezea shida yao tu.
Kwa yakini tuliwaletea Haki, lakini wengi katika nyinyi mlikuwa mnaichukia Haki.
Wanaoipinga haki wako aina mbili: Kwanza, ni wale wanaopinga kwa kutoijua. Pili, ni wale wanaoipinga kwa vile inagongana na masilahi yao na matamanio. Aina hii ndio nyingi zaidi.
Kila atakayeingia motoni kesho atauingia kwa sababu aliipinga haki na kutoitumia, lakini wachache miongoni mwao watastahiki adhabu kwa vile wamezembea kuijua haki. Na wengi watastahiki adhabu kwa vile wameiacha kwa kuwa inagongana na matamanio yao; sio kwa kutoijua.
Au wamekata shauri? Bali ni Sisi ndio tunaopitisha.
Yaani hao makuraishi. Maana ni kuwa washirikina hawakufanya njama zozote kwa Mtume ila Mwenyezi Mungu huvunja njama zao; kama alivyowafanyia makuraishi, pale walipopanga njama ya kumuua mtume akiwa amelala kitandani mwake.
Au wanadhani kwamba hatusikii siri zao na minong’ono yao? Wapi! Na wajumbe wetu wapo karibu nao, wanayaandika.
Wao wanapanga njama kwa siri wakidhani kuwa hilo linafichika kwake Mwenyezi Mungu Mtukufu, lakini Yeye anajua siri na yaliyofichika, naye haviongozi vitimbi vya wahaini.
قُلْ إِنْ كَانَ لِلرَّحْمَٰنِ وَلَدٌ فَأَنَا أَوَّلُ الْعَابِدِينَ {81}
سُبْحَانَ رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ رَبِّ الْعَرْشِ عَمَّا يَصِفُونَ {82}
فَذَرْهُمْ يَخُوضُوا وَيَلْعَبُوا حَتَّىٰ يُلَاقُوا يَوْمَهُمُ الَّذِي يُوعَدُونَ {83}
وَهُوَ الَّذِي فِي السَّمَاءِ إِلَٰهٌ وَفِي الْأَرْضِ إِلَٰهٌ ۚ وَهُوَ الْحَكِيمُ الْعَلِيمُ {84}
وَتَبَارَكَ الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا وَعِنْدَهُ عِلْمُ السَّاعَةِ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ {85}
وَلَا يَمْلِكُ الَّذِينَ يَدْعُونَ مِنْ دُونِهِ الشَّفَاعَةَ إِلَّا مَنْ شَهِدَ بِالْحَقِّ وَهُمْ يَعْلَمُونَ {86}
وَلَئِنْ سَأَلْتَهُمْ مَنْ خَلَقَهُمْ لَيَقُولُنَّ اللَّهُ ۖ فَأَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ {87}
وَقِيلِهِ يَا رَبِّ إِنَّ هَٰؤُلَاءِ قَوْمٌ لَا يُؤْمِنُونَ {88}
فَاصْفَحْ عَنْهُمْ وَقُلْ سَلَامٌ ۚ فَسَوْفَ يَعْلَمُونَ {89}