read

Sura Ya Arubaini Na Nne: Ad-Dukhan

Imeshuka Makka. Ina Aya 59

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

حم {1}

Haa Mim.

وَالْكِتَابِ الْمُبِينِ {2}

Naapa kwa Kitabu kinachobainisha.

إِنَّا أَنْزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةٍ مُبَارَكَةٍ ۚ إِنَّا كُنَّا مُنْذِرِينَ {3}

Hakika tumekiteremsha katika usiku uliobarikiwa. Hakika Sisi ni waonyaji.

فِيهَا يُفْرَقُ كُلُّ أَمْرٍ حَكِيمٍ {4}

Katika huo hubainishwa kila jambo la hikima.

أَمْرًا مِنْ عِنْدِنَا ۚ إِنَّا كُنَّا مُرْسِلِينَ {5}

Ni amri itokayo kwetu. Hakika Sisi ndio wenye kutuma.

رَحْمَةً مِنْ رَبِّكَ ۚ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ {6}

Ni rehema itokayo kwa Mola wako. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.

رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ إِنْ كُنْتُمْ مُوقِنِينَ {7}

Mola wa mbingu na ardhi na vilivyomo kati yake, ikiwa nyinyi mna yakini.

لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۖ رَبُّكُمْ وَرَبُّ آبَائِكُمُ الْأَوَّلِينَ {8}

Yeye Hakuna mungu ila Yeye; anahuisha na anafisha - Mola wenu na Mola wa baba zenu wa mwanzo.

بَلْ هُمْ فِي شَكٍّ يَلْعَبُونَ {9}

Lakini wao wamo katika shaka wakicheza.