read

Aya 1 – 9: Tumeiteremsha Usiku Uliobarikiwa

Maana

Haa Mim.

Umetangulia mfano wake katika Juz. 1 (2:1)

Naapa kwa Kitabu kinachobainisha. Hakika tumekiteremsha katika usiku uliobarikiwa.
Umebarikiwa kwa kuteremkiwa na Qur’an. Tukiunganisha Aya hii na ile isemayo:

إِنَّا أَنْزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ {1}

“Hakika tumeiteremsha katika usiku wa heshima (Laylatul-qadr.) (97:1)

Na pia ile isemayo:

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنْزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ {185}

“Ni mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa ndani yake Qur’an.” Juz.2 (2:185),

Tukiunganisha Aya hizi tatu, tunapata maana kuwa usiku uliobarikiwa ni Laylatul-qadr, na kwamba uko ndani ya mwezi wa Ramadhani uliobarikiwa.

Katika Juz. 2 (2: 183-185), Tumesema kwamba mwanzo wa kushuka Qur’an ulikuwa kwenye Layaltul-qadr, sio kuwa ilishuka Qur’an yote usiku huo. Kwa maelezo zaidi rudia huko.

Hakika Sisi ni Waonyaji wa adhabu kali kwa atakayeasi na kufanya ufisadi katika ardhi. Onyo hili limekuja katika Qur’an iliyoteremshwa kwenye moyo wa Muhammad (s.a.w.).

Katika usiku huu hubainishwa kila jambo la hikima. Ni amri itokayo kwetu.

Wafasiri wametofautiana kuhusu ‘jambo la hikima.’ wengi wameonelea ni kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anagawanyia waja wake riziki na muda wa kifo katika usiku huu. Pia anasamehe makosa mengi kwa anayemtaka.

Wengine wakasema kuwa Makusudio ya jambo la hikima ni ubainifu wa kila jambo la dini uliokuja katika Qur’an. Lakini ikumbukwe Mwenyezi Mungu amesema katika huu, na hakusema katika hii. Ubainifu zaidi utaku- ja katika Juz. 30 (97).

Hakika Sisi ndio wenye kutuma. Ni rehema itokayo kwa Mola wako.

Yaani Mwenyezi Mungu alimtuma Muhammad kuwa ni rehema kwa viumbe vyote; kama ilivyoelezwa katika Juz. 17 (21:107).

Hakika Yeye ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.

Anasikia kauli na anajua yaliyo kwenye nia.

Mola wa mbingu na ardhi na vilivyomo kati yake, ikiwa nyinyi mna yakini.

Mwenye akili akiuangalia ulimwengu kwa mtazamo safi na kutilia maanani, atashuhudia kwa ikhlasi na yakini kwamba Mwenyezi Mungu ndiye mmiliki wa ulimwengu na vilivyomo ndani yake na kwamba Yeye Hakuna mungu ila Yeye; anahuisha na anafisha.

Hakuna yeyote anayeleta uhai isipokuwa Yeye. Na muda ukifika hakuna kinachoweza kuusogeza mbali wala karibu.

Mola wenu na Mola wa baba zenu wa mwanzo. Vipi basi mnaabudu mizimu na kumtii shetani badala ya Mwenyezi Mungu?

Lakini wao wamo katika shaka wakicheza.

Wametia shaka ya kutumwa Muhammad (s.a.w.) pamoja na dalili na ubainifu na wanafanya mchezo na mwisho wao na yale wanayotakiwa kuyafanya.

فَارْتَقِبْ يَوْمَ تَأْتِي السَّمَاءُ بِدُخَانٍ مُبِينٍ {10}

Basi ingoje siku ambayo mbingu italeta moshi ulio dhahiri.

يَغْشَى النَّاسَ ۖ هَٰذَا عَذَابٌ أَلِيمٌ {11}

Utakaowafunika watu. Hii ni adhabu chungu!

رَبَّنَا اكْشِفْ عَنَّا الْعَذَابَ إِنَّا مُؤْمِنُونَ {12}

Mola wetu! Tuondolee adhabu hii. Hakika tutaamini.

أَنَّىٰ لَهُمُ الذِّكْرَىٰ وَقَدْ جَاءَهُمْ رَسُولٌ مُبِينٌ {13}

Kutafaa nini kukumbuka kwao? Na alikwishawafikia Mtume mwenye kubainisha.

ثُمَّ تَوَلَّوْا عَنْهُ وَقَالُوا مُعَلَّمٌ مَجْنُونٌ {14}

Kisha wakamgeuzia uso, na wakasema: Amefunzwa, mwenda wazimu.

إِنَّا كَاشِفُو الْعَذَابِ قَلِيلًا ۚ إِنَّكُمْ عَائِدُونَ {15}

Hakika tutaiondoa adhabu kidogo, (lakini) nyinyi kwa yakini mtarudia.

يَوْمَ نَبْطِشُ الْبَطْشَةَ الْكُبْرَىٰ إِنَّا مُنْتَقِمُونَ {16}

Siku tutakayowashika kwa mashiko makubwa, hakika sisi ni wenye kutesa.

وَلَقَدْ فَتَنَّا قَبْلَهُمْ قَوْمَ فِرْعَوْنَ وَجَاءَهُمْ رَسُولٌ كَرِيمٌ {17}

Na hakika kabla yao tuliwajaribu watu wa Firauni, na aliwafikia Mtume Mtukufu.

أَنْ أَدُّوا إِلَيَّ عِبَادَ اللَّهِ ۖ إِنِّي لَكُمْ رَسُولٌ أَمِينٌ {18}

Nipeni waja wa Mwenyezi Mungu; kwa hakika mimi kwenu ni Mtume mwaminifu.

وَأَنْ لَا تَعْلُوا عَلَى اللَّهِ ۖ إِنِّي آتِيكُمْ بِسُلْطَانٍ مُبِينٍ {19}

Na msijitukuze mbele ya Mwenyezi Mungu; hakika mimi nitawaletea uthibitisho ulio wazi.

وَإِنِّي عُذْتُ بِرَبِّي وَرَبِّكُمْ أَنْ تَرْجُمُونِ {20}

Nami najikinga kwa Mola wangu na Mola wenu, ili msinirujumu.

وَإِنْ لَمْ تُؤْمِنُوا لِي فَاعْتَزِلُونِ {21}

Na ikiwa hamniamini, basi jitengeni nami.