Aya 10 – 21: Siku Ambayo Mbingu Italeta Moshi
Maana
Basi ingoje siku ambayo mbingu italeta moshi ulio dhahiri, utakaowafunika watu.
Maneno yanatoka kwa Mwenyezi Mungu kwenda kwa Nabii wake mtukufu Muhammad (s.a.w.) akimwahidi kumkubalia dua yake. Hiyo ni baada ya Makuraishi kuzidi sana kumuudhi Mtume (s.a.w.). Akawaombea dua mbaya, akasema: “Ewe Mola wangu wafanyie miaka kama ya Yusuf.” Basi mvua ikakatika na ardhi ikawa kame, makuraishi wakapatwa na njaa mpaka wakawa wanakula mifupa na mizoga. Kutokana na njaa mtu alikuwa akiona kama moshi mbinguni.
Wakasema: Hii ni adhabu chungu! Mola wetu! Tuondolee adhabu hii. Hakika tutaamini.
Walimjia Mtume (s.a.w.) na kumwambia: Muombe Mwenyezi Mungu (s.w.t.) atuondolee adhabu hii na sisi tutaamini risala yako.
Kutafaa nini kukumbuka kwao? Na alikwishawafikia Mtume mwenye kubainisha. Kisha wakamgeuzia uso, na wakasema: Amefunzwa, mwendawazimu.
Walitoa ahadi ya kuwaidhika na kukumbuka kama Mwenyezi Mungu atawaondolea adhabu, lakini wao hawatubii wala hawatekelezi ahadi. Kwani hawakushuhudia dalili za Tawhid, lakini pamoja na hayo wakamshirikisha Mwenyezi Mungu? Je, hakuwajia Mtume na hoja zilizo wazi wakamkadhibisha? Wakasema ni mwendawazimu, anafundishwa baadhi ya matamshi na jinni au mtu, kisha anakuja kutusomea?
Hakika tutaiondoa adhabu kidogo, (lakini) nyinyi kwa yakini mtarudia.
Makusudio ya adhabu hapa ni adhabu ya kahati na njaa. Kurudia, ni kuvunja ahadi kwa kurudia makosa. Maana ni kuwa tutawaondolea shida waliyo nayo, katika baadhi ya wakati, lakini sisi tunajua wazi kuwa watavunja ahadi. Lakini hiyo ni katika upande wa kutimiza na kuondoa visababu.
Siku tutakayowashika kwa mashiko makubwa, hakika sisi ni wenye kutesa.
Hili ni tishio kuwa Mwenyezi Mungu siku ya kiyama atawashika kwa adhabu ya kufedhehesha kutokana na uasi na jeuri yao.
Kwa ufupi ni kuwa makuraishi walimuudhi Nabii (s.a.w.), naye akawombea dua mbaya. Ilipowapata shida walimkimbilia Mtume na kumwahidi kutubia, lakini walivunja ahadi baada ya kupata faraja, ndio Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akawatishia kwa Jahannam na makazi mabaya.
Na hakika kabla yao tuliwajaribu watu wa Firauni, na aliwafikia Mtume Mtukufu.
Yaani kabla ya makuraishi. Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu aliwapa mtihani watu wa Firauni kwa neema na kumakinishwa katika ardhi; kama walivyopewa mtihani makuraishi kwa kuondolewa adhabu. Mwenyezi Mungu alimtuma Musa kwa watu wa Firauni; kama alivyomtuma Muhammad kwa makuraishi. Wote wakaasi amri ya Mwenyezi Mungu.
Na Musa akamwambia Firauni na watu wake: Nipeni waja wa Mwenyezi Mungu; kwa hakika mimi kwenu ni Mtume mwaminifu.
Firauni alikuwa akiwakandamiza wana wa Israil kwa kuwachinja watoto wa kiume na kuwabakisha wa kike kwa ajili ya utumishi. Kwa hiyo Musa akamtaka Firauni amwachie ili aende nao anapotaka. Mfano wake ni kauli yake Mwenyezi Mungu:
فَأَرْسِلْ مَعَنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ وَلَا تُعَذِّبْهُمْ ۖ {47}
Na msijitukuze mbele ya Mwenyezi Mungu; hakika mimi nitawaletea uthibitisho ulio wazi.
Haya ni maneno ya Musa kwa watu wa Firauni. Maana ni kuwa msijiweke juu ya twaa ya Mwenyezi Mungu, kwani mimi nina hoja za kutosha za kuthibitisha haki.
Nami najikinga kwa Mola wangu na Mola wenu, ili msinirujumu. Najilinda na ninakimbilia kwake ikiwa mtanikusudia ubaya.
Na ikiwa hamniamini, basi jitengeni nami. Achaneninamimi,kamahamtakikunisadikinakuitikiamwitowangu.
فَدَعَا رَبَّهُ أَنَّ هَٰؤُلَاءِ قَوْمٌ مُجْرِمُونَ {22}
فَأَسْرِ بِعِبَادِي لَيْلًا إِنَّكُمْ مُتَّبَعُونَ {23}
وَاتْرُكِ الْبَحْرَ رَهْوًا ۖ إِنَّهُمْ جُنْدٌ مُغْرَقُونَ {24}
كَمْ تَرَكُوا مِنْ جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ {25}
وَزُرُوعٍ وَمَقَامٍ كَرِيمٍ {26}
وَنَعْمَةٍ كَانُوا فِيهَا فَاكِهِينَ {27}
كَذَٰلِكَ ۖ وَأَوْرَثْنَاهَا قَوْمًا آخَرِينَ {28}
فَمَا بَكَتْ عَلَيْهِمُ السَّمَاءُ وَالْأَرْضُ وَمَا كَانُوا مُنْظَرِينَ {29}
وَلَقَدْ نَجَّيْنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ مِنَ الْعَذَابِ الْمُهِينِ {30}
مِنْ فِرْعَوْنَ ۚ إِنَّهُ كَانَ عَالِيًا مِنَ الْمُسْرِفِينَ {31}
وَلَقَدِ اخْتَرْنَاهُمْ عَلَىٰ عِلْمٍ عَلَى الْعَالَمِينَ {32}
وَآتَيْنَاهُمْ مِنَ الْآيَاتِ مَا فِيهِ بَلَاءٌ مُبِينٌ {33}