Aya 34 – 42: Je, Wao Ni Bora Au Watu Wa Tubbaa’
Maana
Hakika hawa wanasema: Hapana ila kufa kwetu mara ya kwanza tu, wala sisi hatufufuliwi.
‘Hawa’ ni ishara ya washirikina wa Makka, walisema hakuna uhai wala ufufuo baada ya mauti na wakatoa hoja kwa kusema: Basi warudisheni baba zetu, ikiwa mnasema kweli. Wao hawaamini kuwa Mwenyezi Mungu anaweza kuwafufua wafu ila wakiona hilo kwa macho; wakasahau umbile la kwanza, kwamba yule aliyeleta mwanadamu, aliyekuwa hayuko, ndiye huyo huyo mwenye uweza wa kufufua mifupa iliyosagika.
Je, wao ni bora au watu wa Tubbaa’ na walio kuwa kabla yao? Tuliwaangamiza. Hakika hao walikuwa wakosefu.
Watubba’ walikuwa na dola yenye nguvu katika Yemen, na walikuwa na mali na hali nzuri zaidi kuliko makuraishi. Walipoasi amri ya Mola wao, Mwenyezi Mungu aliwakamata na akawaangamiza; kama alivyowaangamiza watu wa Nuh, A’d na Thamud kutokana na kufuru na ufisadi. Lau wangelizingatia wangeliona na wakaamini, lakini wao ni watu wasiofahamu.
Na hatukuziumba mbingu na ardhi na viliomo kati yake kwa mchezo. Hatukuviumba ila kwa haki.
Mwenyezi Mungu ni mwenye hikima na mwenye hikima hawezi kufanaya mchezo. Kwa hiyo haumbi kitu ila kwa masilahi yanayorudia kuumba. Lengo la kuumbwa mtu ni kuishi maisha mema ya milele yasiyokuwa na mwisho. Kwa hiyo basi hakuna budi kuweko na ufufuo; vinginevyo itakuwa kuumbwa mtu ni kwa mchezo tu. Tazama Juz. 21 (31:33-34) kifungu cha: ‘Kwa nini Mungu akamuumba mtu?’
Lakini wengi wao hawajui kwamba Mwenyezi Mungu ameumba ulimwengu na vilivyomo ndani yake kwa hikima na malengo sahihi.
Hakika siku ya Upambanuzi ni wakati uliowekwa kwa wao wote.
Siku ya upambanuzi ni siku ya Kiyama ambayo Mwenyezi Mungu atawakusanya watu wote kwa ajili ya kuangalia hisabu na malipo. Kuwekewa wakati kwa wote ni ahadi ya huko kukusanywa kwa hisabu na malipo.
Siku ambayo rafiki hatamfaa rafiki yake kwa chochote, wala hawatanusuriwa.
Si cheo, mali, nasabu, urafiki wala chochote kitakachoweza kufaa siku hiyo, isipokuwa matendo mema. Hayo peke yake ndiyo yatakayoweza kusaidia mbele ya Mwenyezi Mungu.
Isipokuwa yule ambaye Mwenyezi Mungu atamrehemu, lakini Mwenyezi Mungu atamrehemu yule anayestahiki kurehemiwa; kama yule mwenye vitangulizi vya kumkurubisha kwa muumba wake.
Hakika Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu. Hakuna mwenye kunusuru wala kurehemu kesho isipokuwa Mwenyezi Mungu. Yeye ni mwenye nguvu na rehema, viumbe wananyenyekea nguvu yake na wanahitajia rehema yake.
إِنَّ شَجَرَتَ الزَّقُّومِ {43}
\
طَعَامُ الْأَثِيمِ {44}
كَالْمُهْلِ يَغْلِي فِي الْبُطُونِ {45}
كَغَلْيِ الْحَمِيمِ {46}
خُذُوهُ فَاعْتِلُوهُ إِلَىٰ سَوَاءِ الْجَحِيمِ {47}
ثُمَّ صُبُّوا فَوْقَ رَأْسِهِ مِنْ عَذَابِ الْحَمِيمِ {48}
ذُقْ إِنَّكَ أَنْتَ الْعَزِيزُ الْكَرِيمُ {49}
إِنَّ هَٰذَا مَا كُنْتُمْ بِهِ تَمْتَرُونَ {50}
إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي مَقَامٍ أَمِينٍ {51}
فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ {52}
يَلْبَسُونَ مِنْ سُنْدُسٍ وَإِسْتَبْرَقٍ مُتَقَابِلِينَ {53}
كَذَٰلِكَ وَزَوَّجْنَاهُمْ بِحُورٍ عِينٍ {54}
يَدْعُونَ فِيهَا بِكُلِّ فَاكِهَةٍ آمِنِينَ {55}
لَا يَذُوقُونَ فِيهَا الْمَوْتَ إِلَّا الْمَوْتَةَ الْأُولَىٰ ۖ وَوَقَاهُمْ عَذَابَ الْجَحِيمِ {56}
فَضْلًا مِنْ رَبِّكَ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ {57}
فَإِنَّمَا يَسَّرْنَاهُ بِلِسَانِكَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ {58}
فَارْتَقِبْ إِنَّهُمْ مُرْتَقِبُونَ {59}