Aya 7- 15: Ole Wake Kila Mtunga Uongo Mwenye Dhambi!
Maana
Ole wake kila mtunga uongo mwenye dhambi! Anayesikia Aya za Mwenyezi Mungu akisomewa, kisha anang’ng’ania huku akijivuna, kama kwamba hakuzisikia. Basi mbashirie adhabu chungu! Na anapokijua kitu katika Aya zetu hukifanyia mzaha.
Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kuweka wazi dalili za kihisia zinazofahamisha, kwa mkato na kwa yakini, kuweko Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa mwenye akili, na kusema kuwa asiyeziamini hizo basi hawezi kuamini dalili nyingine zozote, sasa anampa onyo na kumwahidi yule asiyezitilia manani dalili hizi na kunufaika nazo kwa kumwita mzushi mwenye dhambi na kumpa kiaga cha adhabu chungu.
Vile vile ammempa sifa ya mpinzani wa haki na kujitia ukubwa, na kwamba hakutosha na hayo bali ameidharau na kuifanyia mzaha haki.
Kafiri huyu mwenye kuidharau haki na watu wake hana tofauti, siku ya hisabu, na yule anayeiamini haki kwa kauli tu, bila ya kufanya, na kwa nadharia tu bila ya matendo. Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema:
وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ قَالُوا سَمِعْنَا وَهُمْ لَا يَسْمَعُونَ {21}
Imam Ali (a.s.) anasema: “Mwenye busara ni yule anayesikia akatafakari, akachunguza akaona na akanufaika na mazingatio.”
Hao ndio watakaokuwa na adhabu ya kufedhehesha. Nyuma yao ipo Jahannamu. Na waliyoyachuma hayatawafaa kitu, wala mawalii waliowashika badala ya Mwenyezi Mungu. Na watapata adhabu kubwa.
‘Hao’ ni kila mtunga uwongo. Makusudio ya waliyoyachuma ni watoto wao, mali zao na vyeo vyao. Na waliyoyashika ni masanamu na mizimu yao.
Maana ni kuwa wale walioifanyia kiburi haki na wakaidharau, marejeo yao ni kuingia Jahannam; hakuna atakayewaokoa na adhabu hiyo – si masanamu wala watoto wala mali au vyeo.
Hii ni mwongozo.
‘Hii’ ni ishara ya Qur’an. Hakuna mwenye shaka kuwa Qur’an ni mwongozo kwa mwenye kuiamini na ni nguvu kwa mwenye kuitegemea.
Na wale waliozikataa Ishara za Mola wao watapata adhabu yenye maumivu iliyo chungu.
Makusudio ya Ishara hapa ni dalili za kilimwengu za kuwako Mwenyezi Mungu na ukuu wake. Neno adhabu, maumivu na uchungu, yanarudiana au yanakaribiana. Lengo la kukaririka huku ni kusisitiza adhabu atakayokutana nayo mzushi mwenye dhambi ambaye ameikalia juu haki na kuidharau.
Mwenyezi Mungu ndiye aliyeifanya bahari iwatumike, ili humo yapite majahazi kwa amri yake, na ili mtafute fadhila yake, na mpate kushukuru.
Fadhila za Mwenyezi Mungu ziko bara, baharini na angani. Miongoni mwa neema zake Mwenyezi Mungu Mtukufu baharini ni chakula, chumvi, mawe ya thamani, mawasiliano, matembezi na hata michezo nk. Umetangulia mfano wake katika Aya kadhaa, ikiwemo Juz.15 (17:66) na Juz.21 (30:46).
Na amefanya viwatumikie viliomo mbinguni na vilivyo katika ardhi, vyote kutoka kwake. Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu wanaotafakari.
Katika ulimwengu huu mpana kuna manufaa na nyenzo zisizokuwa na idadi. Pamoja na kuendelea kwa elimu katika zama zetu hizi, lakini nyenzo zilizofichikana ni nyingi zaidi kuliko zilizobainika, lakini Mwenyezi Mungu amempa mtu maandalizi kamili ya kugundua nguvu na nyenzo zilizomo ulimwenguni na kufaidika nazo, kama atakuwa na mweleko wa elimu ya kibinadamu sio ya kibiashara, na pia kama atafanya juhudi kubwa.
Neno ‘Vyote,’ linaashiria kwamba mtu anayo maandalizi ya kumwezesha kufika mwezini na kwengineko. Tazama Juz. 20 (29:19-27) kifungu cha ‘Qur’an na fikra.’ Pia Umetangulia mfano wake katika Juz. 21 (31:20)
Waambie walioamini wawasamehe wale wasiozitaraji siku za Mwenyezi Mungu, ili awalipe kwa waliyokuwa wakiyachuma.
Makusudio ya siku za Mwenyezi Mungu hapa ni siku za adhabu yake. Wale wasiozitarajia siku za Mwenyezi Mungu ni washirikina wa kiarabu. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimwamrisha Mtume wake awaombe waumini wawasamehe washirikina ubaya waliowafanyia na wawalipize wema. Mwenyezi Mungu ndiye mwenye hisabu ya muovu na malipo yake.
Anayetenda mema basi anajitendea mwenyewe, na anyetenda uovu basi ni juu yake; kisha mtarudishwa kwa Mola wenu.
Maanayakowazi.UmetanguliamfanowakekatikaJuz.7(6:104)nakwa Herufi zake katika Juz. 24 (41:46).
وَلَقَدْ آتَيْنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ وَرَزَقْنَاهُمْ مِنَ الطَّيِّبَاتِ وَفَضَّلْنَاهُمْ عَلَى الْعَالَمِينَ {16}
وَآتَيْنَاهُمْ بَيِّنَاتٍ مِنَ الْأَمْرِ ۖ فَمَا اخْتَلَفُوا إِلَّا مِنْ بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْعِلْمُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ ۚ إِنَّ رَبَّكَ يَقْضِي بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ {17}
ثُمَّ جَعَلْنَاكَ عَلَىٰ شَرِيعَةٍ مِنَ الْأَمْرِ فَاتَّبِعْهَا وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَاءَ الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ {18}
إِنَّهُمْ لَنْ يُغْنُوا عَنْكَ مِنَ اللَّهِ شَيْئًا ۚ وَإِنَّ الظَّالِمِينَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ ۖ وَاللَّهُ وَلِيُّ الْمُتَّقِينَ {19}
هَٰذَا بَصَائِرُ لِلنَّاسِ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِقَوْمٍ يُوقِنُونَ {20}