read

Aya 32-37: Leo Tunawasahau

Maana

Na ikisemwa: Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli, na Saa haina shaka, nyinyi mkisema: Hatuijui hiyo Saa, tunadhania dhana tu, wala hatuna yakini.

Bado mazungumzo ya wakosefu yaaendelea. Kauli yake Mwenyezi Mungu: “Saa haina shaka,’ ni ubaiinifu na tafairi ya ahadi ya Mwenyezi Mungu. Maana ni kuwa wakosfu walipokuwa wakiwaambiwa na waumini kuwa ufufuo ni kweli na hisabu na malipo ni kweli, wao walikuwa wakisema: sisi hatuna uhakika na ufufuo wala hatuji chochote kuhusiana nao isipokuwa dhana. Basi tuleteeni.dalili yake.

Unaweza kuuliza: Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwenye Aya 24 ya sura hii, amewasimulia kuwa wao walikana ufufuo kwa njia ya mkato, kama inavyofahamisha kauli yao: ‘hapana ila maisha yutu ya duniani,’ kisha hapa Mwenyezi Mungu anawasimulia kwamba wao wanadhania na hawana yakini, yaani hawakatai moja kwa moja. Vipi tutazichanganya Aya mbili hizi?

Razi anasema dhana kubwa ni kuwa wao walikuwa vikunndi viwili: kundi liliokanusha ufufuo kwa mkato na kundi jingine walikuwa na shaka.
Lakini sisi dhana yetu kubwa ni kuwa walikuwa kundi moja tu, na kwamba maana ya Aya zote mbili ni kuwa wao hawaamini ufufuo kwa vile wanadai hawana dalili inayoyakinisha isipokuwa ni mambo yaliyo mbali na wao.

Na ubaya wa waliyoyatenda utawadhihirikia, na yatawazunguka waliyokuwa wakiyafanyia mzaha.

Duniani walipanda makosa na madhambi watayavuna matunda yake Akhera. Waliidharau Jahannam watakuwa ni kuni zake.

Na itasemwa: Leo tunawasahau kama mlivyosahau mkutano wa siku yenu hii; na mahali penu ni Motoni, wala hamna wa kuwanusuru.

Waliikana siku ya Kiyama na wakaifanyia dharau na wale wanaoiamini, Mwenyezi Mungu akawapa muda na wala hawatapata rehema ya Mwenyezi Mungu siku hiyo, bali atawaonjesha adhabu ya siku hiyo na atawaonyesha uweza wake na nguvu zake ndani ya siku hiyo waliyoitilia shaka. Umetangulia mfano wake katika Juz. 8 (7:51).

Hiyo ni kwa sababu nyinyi mlizifanyia mzaha Aya za Mwenyezi Mungu; na maisha ya dunia yakawadanganya.

‘Hiyo’ ni hiyo adhabu. Maana ni kuwa iliyosababisha adhabu yao ni kukanusha kwao siku ya mwisho, kuipinga Qur’an na kuzidharau Aya zako wanaposomewa na kujituliza kwao na dunia na strehe zake.

Basi leo hawatatolewa humo wala hao hawatakubaliwa udhuru.
‘Humo’ ni humo motoni. Maana ni kuwa wao watakaa milele humo, wala hawatatakiwa kumtaka radhi Mwenyezi Mungu kwa kauli au kitendo. Kwa sababu Akhera ni nyumba ya hisabu na malipo sio nyumba ya kuomba radhi.

Basi sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa mbingu, na Mola wa ardhi, na Mola wa walimwengu wote.

Msifuni Mwenyezi Mungu peke yake, kwa sababu Yeye ni muumba wa kila kitu.

Na ukubwa ni wake, mbinguni na katika ardhi.

Makusudio ya ukubwa wake Mtukufu ni kwamba hakuna mkubwa anayehofiwa au kutarajiwa isipokuwa Yeye peke yake. Imam Ali (a.s.) akiwasifu wanaomjua Mwenyezi Mungu kwa kusema: “Amekuwa mkubwa Muumba katika nafsi zao akawa mdogo asiyekuwa Yeye machoni mwao.”

Naye ni Mwenye nguvu, ambaye hakimshindi chochote. Mwenye hikima katikampangiliowakuumbakwake.