read

Sura Ya Arubaini : Al-Ghaafir

Ina Aya 85. Imeshuka Makka. Imesemekana Aya mbili hazikushuka Makka. Pia inaitwa Sura Mumin

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

حم {1}

Hamim.

تَنْزِيلُ الْكِتَابِ مِنَ اللَّهِ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ {2}

Uteremsho wa Kitabu umetoka kwa Mwenyezi Mungu Mwenye nguvu, Mwenye kujua.

غَافِرِ الذَّنْبِ وَقَابِلِ التَّوْبِ شَدِيدِ الْعِقَابِ ذِي الطَّوْلِ ۖ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ إِلَيْهِ الْمَصِيرُ {3}

Mwenye kughufiria dhambi na anayekubali toba, Mkali wa kuadhibu, Mwenye fadhila. Hakuna mungu ila Yeye. Marejeo ni Kwake.

مَا يُجَادِلُ فِي آيَاتِ اللَّهِ إِلَّا الَّذِينَ كَفَرُوا فَلَا يَغْرُرْكَ تَقَلُّبُهُمْ فِي الْبِلَادِ {4}

Hawabishani katika Ishara za Mwenyezi Mungu ila wale ambao wamekufuru. Basi kusikughuri kutangatanga kwao katika nchi.

كَذَّبَتْ قَبْلَهُمْ قَوْمُ نُوحٍ وَالْأَحْزَابُ مِنْ بَعْدِهِمْ ۖ وَهَمَّتْ كُلُّ أُمَّةٍ بِرَسُولِهِمْ لِيَأْخُذُوهُ ۖ وَجَادَلُوا بِالْبَاطِلِ لِيُدْحِضُوا بِهِ الْحَقَّ فَأَخَذْتُهُمْ ۖ فَكَيْفَ كَانَ عِقَابِ {5}

Kabla yao walikadhibisha kaumu ya Nuh na makundi baada yao. Na kila uma ulikuwa na hamu juu ya Mtume wao wamkamate. Na walibishana kwa upotovu ili kuipindua haki. Kwa hivyo niliwakamata. Basi ilikuwaje adhabu yangu!

وَكَذَٰلِكَ حَقَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ عَلَى الَّذِينَ كَفَرُوا أَنَّهُمْ أَصْحَابُ النَّارِ {6}

Namna hivi limewathibitikia makafiri neno la Mola wako kwamba wao ni watu wa Motoni.