Aya 56 – 63: Kuumba Mbingu Na Ardhi
Maana
Katika Hakika wale ambao wanabishana katika Ishara za Mwenyezi Mungu bila ya dalili yoyote iliyowafika, hawana vifuani mwao ila kutaka ukubwa tu, na wala hawaufikii.
Makusudio ya wanaobishana hapa ni wapenda anasa. Kwani wao wanapinga kitu kikiwa hakikubaliani na ukubwa wao. Ushahidi wa hilo ni kauli yake Mwenyezi Mungu: ‘ila kutaka ukubwa tu’ Yaani kwa sababu ya kiburi chao na kujikuza, hawaikubali haki na wanabishana. Ingelikwa bora kama wangelitubia na kukubali makosa.
Basi jikinge kwa Mwenyezi Mungu na kiburi na mwisho mbaya.
Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona, kiburi chao wana- choking’ang’ania kwa sababu ya jaha na utajiri wao. Katika Nhajul-bal- agha, imesemwa: “Jikingeni kwa Mwenyezi Mungu na majivuno kama mnavyojikinga na majanga.”
Hakika umbo la mbingu na ardhi ni kubwa zaidi kuliko umbo la watu. Lakini watu wengi hawajui.
Kila elimu inavyoendelea, ndio maana ya Qur’ani nayo yanavyozidi kwa nguvu kufunguka kwenye akili. Wataalamu wa zamani walisema: Mtu ndiye kiumbe wa ajabu ardhini na katika anga za juu na kwamba ardhi ndio kituo cha ulimwengu. Kisha ikaja elektroni na ala nyingine za elimu ya kisasa, ili ziseme:
Hapana! Mtu sio kiumbe wa ajabu wala ardhi zio kituo cha ulimwengu. Kwani ulimwengu una mamailio ya vituo na kila kituo kina mamlioni ya nyota, na kwamba hakuna yoyote asiyekuwa Mwenyezi Mungu anayejua au anayeweza kujua idadi ya vituo hivyo au idadi ya nyota na vinginevyo vilviyomo kwenye kila kituo; na ardhi katika ulimwengu ni kama chembe tu.
Hapa ndio tunapata tafsiri ya kauli yake Mwenyezi Mungu: ‘Hakika umbo la mbingu na ardhi ni kubwa zaidi kuliko umbo la watu.’ Ndio! Lakini ndani ya binadamu kuna ulimwengu wa ajabu, jinsi alivyo, hakika yake, mapendeleo yake hisia zake na matamanio yake.
Na kipofu na mwenye kuona hawawi sawa; na walioamini na watendao mema hawawi sawa na muovu. Ni machache mnayoyakumbuka.
Tofuti ni kubwa sana baina mjuzi na mjinga baina ya mwema na mfisadi na baina mwenye kufanya mazuri na mwenye kufanya maovu. Hapana! Hawawi sawa mbele ya Mwenyezi Mungu wala mbele ya watu wenye insafu mwamko. Umetangulia mfano wake katika Juz.7 (6:50), Juz. 13 (13:16) na Juz. 22 (35:19).
Hakika Saa ya Kiyama itafika, haina shaka, na itatupelekea kusimama mbele za mwenye uwezo aliye mjuzi, batilil zitaondoka, uhakika utathibiti na visababu vyote vitakatika.
Lakini watu wengi hawaamini kwamba wao watafufuliwa siku itakayokuwa kubwa na wataulizwa waliyokuwa wakiyafanya.
Na Mola wenu amesema: Niombeni nitawaitikia.
Baadhi ya wafasiri wamesema kuwa maana yake ni niabuduni nitawalipa. Wametoa dalili kuwa Qur’an inatumia neno dua kwa maana ya ibada kwa Aya ya isemayo:
إِنْ يَدْعُونَ مِنْ دُونِهِ إِلَّا إِنَاثًا {117}
Sisi tuko pamoja na wanaosema kauli hii; hasa katika Aya hii, ambapo mfumo wa maneno unarudia kwenye maana hii, pale aliposema moja kwa moja:
Kwa hakika wale ambao wanajivuna kufanya ibada yangu wataingia Jahannamu wadhalilike.
Kwa hiyo kusema kwake: ‘ambao wanajivuna na ibada yangu,’ ni tafsiri na ubanifu wa kauli yake: ‘niombeni.’ Kwa vyovyote iwavyo, ni kuwa Uislamu ni dini ya matendo sio dini ya maneno. Na Mwenyezi Mungu humruzuku mwenye kufanya juhudi na akawa na subira:
هُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ ذَلُولًا{15}
Tumezungumzia kuhusu dua (mombi) katika Juz. 2 (2: 186).
Mwenyezi Mungu ambaye amewafanyia usiku ili mpate kutulia humo, na mchana wa kuonea. Hakika Mwenyezi Mungu bila ya shaka ni Mwenye fadhila juu ya watu, lakini watu wengi hawashukuru.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 11 (10:67).
Huyo ndiye Mwenyezi Mungu Mola wenu, Muumba wa kila kitu. Hapana mungu ila Yeye; basi mnageuzwa wapi?
Vipi mnageuzwa kumtii Mwenyezi Mungu na kumwabudu na hali Yeye peke yake ndiye Muumba na Mwenye kuruzuku? Makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu: ‘Amewafanyia, Mwenye fadhila na Muumba wa kila kitu,’ ni kubainisha kuwa Yeye Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amekusanya sifa zote za uungu za ukamilifu na kwamba sifa hizo zote ziko wazi kwa mwenye macho na akili nzuri, lakini watu wengi wameghafilika na yale wanayotakiwa kuyafanya na yanayolengwa kwao.
Hivyo ndivyo walivyogeuzwa wale ambao walikuwa wakizikataa Ishara za Mwenyezi Mungu.
Kila mwenye kughafilika na kupuuza dalili zinazofahamisha ukuu wa Mwenyezi Mungu, lazima awe anaachana na ibada ya Mwenyezi Mungu na twaa yake. Kwa sababu watu ni maadui wa yale wasiyoyajua.
اللَّهُ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ قَرَارًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَصَوَّرَكُمْ فَأَحْسَنَ صُوَرَكُمْ وَرَزَقَكُمْ مِنَ الطَّيِّبَاتِ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّهُ رَبُّكُمْ ۖ فَتَبَارَكَ اللَّهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ {64}
هُوَ الْحَيُّ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ فَادْعُوهُ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ ۗ الْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ {65}
قُلْ إِنِّي نُهِيتُ أَنْ أَعْبُدَ الَّذِينَ تَدْعُونَ مِنْ دُونِ اللَّهِ لَمَّا جَاءَنِيَ الْبَيِّنَاتُ مِنْ رَبِّي وَأُمِرْتُ أَنْ أُسْلِمَ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ {66}
هُوَ الَّذِي خَلَقَكُمْ مِنْ تُرَابٍ ثُمَّ مِنْ نُطْفَةٍ ثُمَّ مِنْ عَلَقَةٍ ثُمَّ يُخْرِجُكُمْ طِفْلًا ثُمَّ لِتَبْلُغُوا أَشُدَّكُمْ ثُمَّ لِتَكُونُوا شُيُوخًا ۚ وَمِنْكُمْ مَنْ يُتَوَفَّىٰ مِنْ قَبْلُ ۖ وَلِتَبْلُغُوا أَجَلًا مُسَمًّى وَلَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ {67}
هُوَ الَّذِي يُحْيِي وَيُمِيتُ ۖ فَإِذَا قَضَىٰ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُنْ فَيَكُونُ {68}