Aya 2-3: Na Tukampa Musa Kitabu
Maana
Na tukampa Musa Kitabu na tukakifanya ni uongofu kwa Wana wa Israil, kwamba msimfanye mtegemewa asiyekuwa Mimi.
Makusudio ya kitabu hapa ni Tawrat na Israil ni Ya’qub bin Is-haq bin Ibrahim (a.s.). Maana ni kuwa Mwenyezi Mungu ameitermsha Tawrat kwa Musa ili Wana wa Israil waongoke nayo kwenye njia ya haki na ukweli na wamtegemee Mungu peke yake wala wasimfanye mwengine kuwa ni msimamizi au msaidizi wao.
Lakini wao waliyapotosha maneno ya Mwenyezi Mungu, wakaabudu ndama, wakaua mitume, na wakaijaza dunia shari na ufisadi kwa kila nyenzo waliyo nayo.
Enyi kizazi tulichokichukua pamoja na Nuh!
Nuh alichukuwa watoto wake watatu pamoja na wake zao katika Safina. Wao walikuwa ni Ham, Sam, na Yafith. (Hamu Shemu na Yafeti). Kutokana na wao kizazi kiliendelea baada ya tufani; miongoni mwa hicho kizazi ni Wana wa Israil waliokuwa katika zama za Nabii Musa. Hapa ni kuwakumbusha Wana wa Israil neema za Mwenyezi Mungu ambazo wao wanazikufuru na kuzikana.
Hakika yeye alikuwa ni mja mwenye shukrani.
Yeye ni Nuh (a.s.); yaani enyi mayahudi! Kuweni na shukrani na kukumbuka neema za Mwenyezi Mungu; kama alivyokuwa Nuh, lakini hashukuru neema ila mkweli aliye mwaminifu. Na haikujulikana kwa waisraili, tangu walipopatikana, isipokuwa uongo udanganyifu na hiyana.
Imepokewa Hadith kutoka kwa Imam Ja’far Asswadiq (a.s.) kwamba Nuh (a.s.) anapopambaukiwa alikuwa akisema hivi: “Ewe mola wangu! Hakika ninashuhudia kwamba neema ya dini au dunia iliyonipambaukia inatokana na wewe; huna mshirika; wakusifiwa na kushukuriwa kwa neema hizo kwangu ni wewe mpaka uridhie.”
وَقَضَيْنَا إِلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ فِي الْكِتَابِ لَتُفْسِدُنَّ فِي الْأَرْضِ مَرَّتَيْنِ وَلَتَعْلُنَّ عُلُوًّا كَبِيرًا {4}
فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ أُولَاهُمَا بَعَثْنَا عَلَيْكُمْ عِبَادًا لَنَا أُولِي بَأْسٍ شَدِيدٍ فَجَاسُوا خِلَالَ الدِّيَارِ ۚ وَكَانَ وَعْدًا مَفْعُولًا {5}
ثُمَّ رَدَدْنَا لَكُمُ الْكَرَّةَ عَلَيْهِمْ وَأَمْدَدْنَاكُمْ بِأَمْوَالٍ وَبَنِينَ وَجَعَلْنَاكُمْ أَكْثَرَ نَفِيرًا {6}
إِنْ أَحْسَنْتُمْ أَحْسَنْتُمْ لِأَنْفُسِكُمْ ۖ وَإِنْ أَسَأْتُمْ فَلَهَا ۚ فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ الْآخِرَةِ لِيَسُوءُوا وُجُوهَكُمْ وَلِيَدْخُلُوا الْمَسْجِدَ كَمَا دَخَلُوهُ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَلِيُتَبِّرُوا مَا عَلَوْا تَتْبِيرًا {7}
عَسَىٰ رَبُّكُمْ أَنْ يَرْحَمَكُمْ ۚ وَإِنْ عُدْتُمْ عُدْنَا ۘ وَجَعَلْنَا جَهَنَّمَ لِلْكَافِرِينَ حَصِيرًا {8}