Aya 13 – 15: Ndege Shingoni
Lugha
Makusudio ya ndege hapa ni matendo ya mtu ya kheri na shari. Waarabu walikuwa wakiona ni bahati njema ndege anayekuja upande wa kuume kwa sababu mtu anaweza kumpiga na wakiona ni kisirani ndege akitokea upande wa kushoto, kwa sababu hawezi kumpiga.
Ndio likaazimwa neno ndege kwa matendo ya heri na shari.1 Shingoni mwake ni fumbo la kuwa nayo; kama vile amefunga koja au mkufu.
Maana
Aya hizi tatu zinatofautiana kimatamshi, lakini zinashabihiana kimaana. Kauli yake Mwenyezi Mungu: Na kila mtu tumemfungia ndege wake shingoni mwake ni fumbo la kuwa mtu peke yake ndiye mwenye jukumu la matendo yake. Na kauli yake:
Na siku ya Kiyama tutamtolea kitabu atakachokikuta kimekunjuliwa.
Maana yake ni kuwa mtu kesho hataweza kuficha kitu chochote katika mambo aliyoyatenda:
يَوْمَ تَجِدُ كُلُّ نَفْسٍ مَا عَمِلَتْ مِنْ خَيْرٍ مُحْضَرًا وَمَا عَمِلَتْ مِنْ سُوءٍ تَوَدُّ لَوْ أَنَّ بَيْنَهَا وَبَيْنَهُ{30}
Kwa maelezo zaidi angalia huko.
Pia kauli yake Mwenyezi Mungu: Soma kitabu chako! Nafsi yako leo inakutosha kukuhisabu.
Hakuna haja ya shahidi wala mhasibu kesho. Kwa sababu mtu mwenyewe atajishuhudia na atajihisabu. Twabrasi anasema: “Atakuwa anajihisabu mwenyewe kwa sababu Siku ya Kiyama atakapoyaona matendo yake yote yameandikwa na kuona malipo yake pia yameandikwa kwa uadilifu, hayakupunguwa wala kuzidishiwa adhabu hata kidogo, atakiri na kukubali yeye mwenyewe, wala hatakuwa na hoja wala upinzani. Itawadhihirikia watakaofufuliwa kuwa hakuna dhulma.
Anasema Hasan: “Ewe mwanadamu! Amekufanyia insafu yule aliyekufanya ujihisabu mwenyewe.”
Anayeongoka hakika anaongoka kwa faida ya nafsi yake tu, na anayepotea anapotea kwa hasara ya nafsi yake tu.
Umetangulia mfano wake katika Juz. 8 (6: 104) na Juz. 11 (10: 108).
Wala mbebaji hatabeba mzigo wa mwingine. Umetangulia mfano wake katika Juz. 8 (6:164). Wala sisi hatuadhibu mpaka tupeleke Mtume.
AngaliaJuz.2(2:159)kifungucha‘Ubayawaadhabubilayaubainifu’
وَإِذَا أَرَدْنَا أَنْ نُهْلِكَ قَرْيَةً أَمَرْنَا مُتْرَفِيهَا فَفَسَقُوا فِيهَا فَحَقَّ عَلَيْهَا الْقَوْلُ فَدَمَّرْنَاهَا تَدْمِيرًا {16}
وَكَمْ أَهْلَكْنَا مِنَ الْقُرُونِ مِنْ بَعْدِ نُوحٍ ۗ وَكَفَىٰ بِرَبِّكَ بِذُنُوبِ عِبَادِهِ خَبِيرًا بَصِيرًا {17}
مَنْ كَانَ يُرِيدُ الْعَاجِلَةَ عَجَّلْنَا لَهُ فِيهَا مَا نَشَاءُ لِمَنْ نُرِيدُ ثُمَّ جَعَلْنَا لَهُ جَهَنَّمَ يَصْلَاهَا مَذْمُومًا مَدْحُورًا {18}
وَمَنْ أَرَادَ الْآخِرَةَ وَسَعَىٰ لَهَا سَعْيَهَا وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَأُولَٰئِكَ كَانَ سَعْيُهُمْ مَشْكُورًا {19}
كُلًّا نُمِدُّ هَٰؤُلَاءِ وَهَٰؤُلَاءِ مِنْ عَطَاءِ رَبِّكَ ۚ وَمَا كَانَ عَطَاءُ رَبِّكَ مَحْظُورًا {20}
انْظُرْ كَيْفَ فَضَّلْنَا بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۚ وَلَلْآخِرَةُ أَكْبَرُ دَرَجَاتٍ وَأَكْبَرُ تَفْضِيلًا {21}
- 1. Hata Waswahili pia hulitumia neno ndege kwa maana ya bahati njema au kisir- ani, wanasema: ndege mzuri au ndege mbaya - Mtarjumu.