Aya 22 – 25: Usiwambie Ah!
Maana
Usimfanye mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu, usije ukabaki ni mwenye kulaumiwa uliyetupwa.
Maneno haya anaambiwa kila mtu, sio Mtume (s.a.w.) kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu: ‘mmoja wao akifikia uzee naye yuko kwako au wote wawili; Na inajulikana kuwa Mtume alikuwa yatima.
Na Mola wako amepitisha kuwa msimwabudu yoyote ila Yeye tu na kuwatendea wema wazazi wawili. Mmoja wao akifikia uzee naye yuko kwako au wote wawili, basi usiwaambie Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa heshima. Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma na useme: Mola wangu! Warehemu kama walivyonilea utotoni.
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amekutanisha shukrani ya wazazi wawili na shukrani yake na akawajibisha kuwatendea wema. Kuna Hadith isemayo: “Kuna mtu mmoja alikwenda kwa Mtume (s.a.w.) akimtaka idhini ya kupigana jihadi pamoja naye. Akamuuliza: je. Wazazi wako wako hai? Akasema: Ndio. Akasema mtume: basi fanya jihad kwao.
Kauli yake Mwenyezi Mungu: ‘kama walivyonilea utotoni,’ ni ishara ya kuwa wao walijitolea nafsi zao kwa ajili yake, wakakesha usiku ili yeye alale, wakawa na njaa ili ashibe yeye na wakawa uchi ili yeye avae. Na hili ni deni shingoni mwake, ni wajibu alilipe atakapokuwa na nguvu na wao kuwa dhaifu, na kuwachukulia kwenye uzee wao sawa na wao walivyomchukulia alipokuwa mdogo, na wao wamemzidi kwa kumtangulia.
Imam Zaynul-abidin (a.s.) anasema akiwaombea Mungu wazazi wake: “Ewe Mola wangu! Ni wapi na wapi urefu wa shughuli yao ya kunilea mimi? Ni wapi na wapi shida ya tabu yao ya kunilinda mimi? Ni wapi na wapi kujinyima kwao kwa jili ya kunifurahisha mimi? Ni mbali kwa mbali kabisa na jinsi walivyotekeleza haki yao kwangu; ni mbali kwambali yote hayo na jinsi ninavyowafanyia! Wala mimi sijatekeleza wadhifa wa kuwahudumia.”
Kila mmoja kati ya baba na mama anajitolea kwa nafsi yake na pumzi zake zote kwa ajili ya mtoto, kisha hataki malipo wala shukrani yoyote. Analotamani ni kuwa mtoto wake awe ni mtu mwenye kutajika. Nimepata mtihani wa kuwa baba, lakini wazazi wangu hawakuupata mtihani huo, kwa sababu nilikuwa yatima wa baba na mama.
Ninasema nimepatwa na mtihani huo, kwa sababu mimi sioni raha yoyote katika maisha haya isipokuwa raha ya mwanangu wa kike na kiume. Tabasamu moja tu ya mmoja wao kwangu ni sawa na dunia na vilivyomo ndani yake na hasononeki yoyote kati yao ila huwa ninahisi kuna mkono unatoa roho yangu iliyo mbavuni mwangu.
Mola wenu ni Mjuzi zaidi wa yaliyo katika nafsi zenu, ikiwa nyinyi mtakuwa wema. Hakika Yeye ni Mwenye kughufiria wanaorejea kwake.
Hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anajua maazimio, kama anavyojua kauli na vitendo na kumlipa kila mmoja kulingana na nia yake. Mwenye kufanya uovu kisha akatubia sawasawa, basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghufira, mwenye kurehemu.
Hiii ni tahadhari kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa yule mwenye kuwaudhi wazazi wake na akawa anawaona ni mzigo kwake, kama ambavyo pia ni hadhari ya kuacha ikhlasi katika kauli na vitendo.
وَآتِ ذَا الْقُرْبَىٰ حَقَّهُ وَالْمِسْكِينَ وَابْنَ السَّبِيلِ وَلَا تُبَذِّرْ تَبْذِيرًا {26}
إِنَّ الْمُبَذِّرِينَ كَانُوا إِخْوَانَ الشَّيَاطِينِ ۖ وَكَانَ الشَّيْطَانُ لِرَبِّهِ كَفُورًا {27}
وَإِمَّا تُعْرِضَنَّ عَنْهُمُ ابْتِغَاءَ رَحْمَةٍ مِنْ رَبِّكَ تَرْجُوهَا فَقُلْ لَهُمْ قَوْلًا مَيْسُورًا {28}
وَلَا تَجْعَلْ يَدَكَ مَغْلُولَةً إِلَىٰ عُنُقِكَ وَلَا تَبْسُطْهَا كُلَّ الْبَسْطِ فَتَقْعُدَ مَلُومًا مَحْسُورًا {29}
إِنَّ رَبَّكَ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَنْ يَشَاءُ وَيَقْدِرُ ۚ إِنَّهُ كَانَ بِعِبَادِهِ خَبِيرًا بَصِيرًا {30}
وَلَا تَقْتُلُوا أَوْلَادَكُمْ خَشْيَةَ إِمْلَاقٍ ۖ نَحْنُ نَرْزُقُهُمْ وَإِيَّاكُمْ ۚ إِنَّ قَتْلَهُمْ كَانَ خِطْئًا كَبِيرًا {31}
وَلَا تَقْرَبُوا الزِّنَا ۖ إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَسَاءَ سَبِيلًا {32}
وَلَا تَقْتُلُوا النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّهُ إِلَّا بِالْحَقِّ ۗ وَمَنْ قُتِلَ مَظْلُومًا فَقَدْ جَعَلْنَا لِوَلِيِّهِ سُلْطَانًا فَلَا يُسْرِفْ فِي الْقَتْلِ ۖ إِنَّهُ كَانَ مَنْصُورًا {33}
وَلَا تَقْرَبُوا مَالَ الْيَتِيمِ إِلَّا بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ حَتَّىٰ يَبْلُغَ أَشُدَّهُ ۚ وَأَوْفُوا بِالْعَهْدِ ۖ إِنَّ الْعَهْدَ كَانَ مَسْئُولًا {34}
وَأَوْفُوا الْكَيْلَ إِذَا كِلْتُمْ وَزِنُوا بِالْقِسْطَاسِ الْمُسْتَقِيمِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا {35}
وَلَا تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ ۚ إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولَٰئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْئُولًا {36}
وَلَا تَمْشِ فِي الْأَرْضِ مَرَحًا ۖ إِنَّكَ لَنْ تَخْرِقَ الْأَرْضَ وَلَنْ تَبْلُغَ الْجِبَالَ طُولًا {37}
كُلُّ ذَٰلِكَ كَانَ سَيِّئُهُ عِنْدَ رَبِّكَ مَكْرُوهًا {38}
ذَٰلِكَ مِمَّا أَوْحَىٰ إِلَيْكَ رَبُّكَ مِنَ الْحِكْمَةِ ۗ وَلَا تَجْعَلْ مَعَ اللَّهِ إِلَٰهًا آخَرَ فَتُلْقَىٰ فِي جَهَنَّمَ مَلُومًا مَدْحُورًا {39}