Aya 49 – 52: Tutakapokuwa Mifupa Na Mapande Yaliyosagika
Maana
Na wakasema: je, tutakapokuwa mifupa na mapande yaliyosagika, je tutafufuliwa kuwa viumbe wapya?
Hii ndio hoja ya mwenye kutilia shaka ufufuo, tangu zamani hadi sasa, kuwa itakuwaje mtu arudi kuwa hai baada ya kuwa vumbi linalotifuka?
Jibu: Yule aliyeweza kuumba kitu na kukifanya kiwepo baada ya kuwa hakipo, basi ni wazi kuwa anaweza kukikusanya baada ya kutawanyika. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameitaja shaka hii na jawabu lake kwenye Aya kadhaa; miongoni mwazo ni ile iliyo katika sura Yasin:
وَضَرَبَ لَنَا مَثَلًا وَنَسِيَ خَلْقَهُ ۖ قَالَ مَنْ يُحْيِي الْعِظَامَ وَهِيَ رَمِيمٌ {78}
قُلْ يُحْيِيهَا الَّذِي أَنْشَأَهَا أَوَّلَ مَرَّةٍ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ خَلْقٍ عَلِيمٌ {79}
Tumelifafanua suala hili katika Juz. 13 (13:5).
Sema: kuweni hata mawe na chuma au umbo lolote mnaloliona kubwa katika vifua vyenu.
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anawaambia wale wanaokanusha ufufuo kuwa hata kama mtakuwa mawe au chuma au kitu kikubwa zaidi ya hivyo tutawaumba tu kuwa watu hai.
Anayeweza kuumba kutokana na chuma au jiwe au kitu kigumu zaidi ya hivyo, basi ni muweza zaidi wa kumrudishia uhai yule aliyempa uhai mwanzo. Kwa sababu kuvikusanya vitu baada ya kutawanyika ni rahisi zaidi kuliko kuvianzisha upya.
Kwa ufupi ni kuwa kumfufua mtu baada ya kufa ni wepesi zaidi kuliko kukifanya chuma kuwa mtu. Anayeweza hivi basi hashindwi kufanya vile.
Watasema: Ni nani atakayeturudisha tena kwenye uhaai baada ya kuwa mavumbi yanayopeperuka. Jibu la swali hili ni:
Sema: Ni huyo aliyewaumba mara ya kwanza.
Mwenye kurudisha ndiye yule aliyeanza. Kuanza na kurudisha ni kumoja tu; bali kurudisha ni wepesi zaidi, kwa sababu ni kurudisha ilivyokuwa. Tunasema hivi, kama mfano tu, tukijua kuwa Mwenyezi Mungu anaumba vichache na vingi na pia vidogo na vikubwa kwa neno.
كُنْ فَيَكُونُ {82}
Watakutikisia vichwa vyao kwa stihzai na kukadhibisha Na watasema: lini hayo? Makusudio ya swali hili ni kuona kuwa haiwezekani.
Sema: asaa yakawa karibu. Makusudio ya karibu hapa ni kuhakikika na kutokea, kwani ‘Kila lijalo liko karibu.’
Siku atakyowaita nanyi mkamwitikia kwa kumsifu.
Makusudio ya Siku ni siku ya Ufufuo, kuitwa ni kupuziwa parapanda, kuitikia ni fumbo la kutoka kwao makaburini na kumsifu ni kutii na kufuata:
وَنُفِخَ فِي الصُّورِ فَإِذَا هُمْ مِنَ الْأَجْدَاثِ إِلَىٰ رَبِّهِمْ يَنْسِلُونَ {51}
Na mkadhani kuwa hamkukaa ila muda mchache tu.
Watu watakapotoka makaburini watadhani kuwa wao hawakukaa duniani isipokuwa siku moja au sehemu ya siku:
قَالَ كَمْ لَبِثْتُمْ فِي الْأَرْضِ عَدَدَ سِنِينَ {112}
قَالُوا لَبِثْنَا يَوْمًا أَوْ بَعْضَ يَوْمٍ فَاسْأَلِ الْعَادِّينَ {113}
وَقُلْ لِعِبَادِي يَقُولُوا الَّتِي هِيَ أَحْسَنُ ۚ إِنَّ الشَّيْطَانَ يَنْزَغُ بَيْنَهُمْ ۚ إِنَّ الشَّيْطَانَ كَانَ لِلْإِنْسَانِ عَدُوًّا مُبِينًا {53}
رَبُّكُمْ أَعْلَمُ بِكُمْ ۖ إِنْ يَشَأْ يَرْحَمْكُمْ أَوْ إِنْ يَشَأْ يُعَذِّبْكُمْ ۚ وَمَا أَرْسَلْنَاكَ عَلَيْهِمْ وَكِيلًا {54}
وَرَبُّكَ أَعْلَمُ بِمَنْ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۗ وَلَقَدْ فَضَّلْنَا بَعْضَ النَّبِيِّينَ عَلَىٰ بَعْضٍ ۖ وَآتَيْنَا دَاوُودَ زَبُورًا {55}
قُلِ ادْعُوا الَّذِينَ زَعَمْتُمْ مِنْ دُونِهِ فَلَا يَمْلِكُونَ كَشْفَ الضُّرِّ عَنْكُمْ وَلَا تَحْوِيلًا {56}
أُولَٰئِكَ الَّذِينَ يَدْعُونَ يَبْتَغُونَ إِلَىٰ رَبِّهِمُ الْوَسِيلَةَ أَيُّهُمْ أَقْرَبُ وَيَرْجُونَ رَحْمَتَهُ وَيَخَافُونَ عَذَابَهُ ۚ إِنَّ عَذَابَ رَبِّكَ كَانَ مَحْذُورًا {57}