Aya 53 – 57: Waambie Waja Wangu Waseme Maneno Mazuri
Maana
Waambie waja wangu waseme maneno mazuri.
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimwamrisha Mtume wake mtukufu awaamrishe waumini au watu wote waseme maneno mazuri, watamke haki na uadilifu kwa thamani yoyote itakayokuwa. Angali Juz. 13 (14: 24 – 26).
Kwani shetani huchochea baina yao.
Shetani hutafuta makosa ya ulimi ili ayafanye ni kuni za moto wa uadui na chuki baina ya watu. Makosa ya ulimi hayawi tu kwa kutukana bali pia kwa kusifu pasipokuwa mahali pake na kwenye matamshi ya ufuska na uovu.
Hakika shetani ni adui aliye dhahiri kwa mtu.
Uadui huu aliubainisha wazi pale aliposema:
قَالَ فَبِمَا أَغْوَيْتَنِي لَأَقْعُدَنَّ لَهُمْ صِرَاطَكَ الْمُسْتَقِيمَ {16}
ثُمَّ لَآتِيَنَّهُمْ مِنْ بَيْنِ أَيْدِيهِمْ وَمِنْ خَلْفِهِمْ وَعَنْ أَيْمَانِهِمْ وَعَنْ شَمَائِلِهِمْ ۖ {17}
Mola wenu anawajua vilivyo, akipenda atawarehemu na akipenda atawaadhibu.
Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwadilifu na Mwenye hekima. Anajua hali za waja wake, yale yaliyo na masilahi nao na yale yenye ufisadi na anawachukulia kwa uadilifu wake na hekima yake.
Atamrehemu anayestahiki rehema naye ni yule anayefuata amri na mtiifu; Na atamwadhibu anayestahiki adhabu; naye ni yule muasi jeuri. Hiyo ni baada ya kuwawekea hoja kwa kuwafikishia yaliyo halali na yaliyo haramu kupitia kwa Mtume mtukufu.
Na hatukukutuma ili uwe mlinzi juu yao, bali ni mfikishaji:
فَإِنَّمَا عَلَيْكَ الْبَلَاغُ وَعَلَيْنَا الْحِسَابُ {40}
Na Mola wako anawajua vilivyo waliomo mbinguni na waliomo ardhini. Na hakika tumewafadhilisha baadhi ya manabii kuliko wengine; na Daud tulimpa Zaburi.
Mwenyezi Mungu anawajua watu wa mbinguni na wa ardhini na anajua uwezo wa kila mmoja wao. Kwa misingi hiyo ndio huwachagua wajumbe kwenda kwa mitume wake; kama vile Jibril (a.s.). Na hupeleka mitume wabashiri na waonyaji kwa watu.
Kama alivyowafadhilisha baadhi ya Malaika kuliko wengine; vilevile Mitume, baadhi amaewafadhilisha kuliko wengine.
Unaweza kuuliza kuwa Uislamu unasimama kwenye misingi ya usawa ; sasa kuna maana gani ya ubora huu kwa baadhi kuliko wengine? Kisha ubora huu utapatikana vipi kwa Malika na Mitume na hali tunajua kuwa wote ni waja wa Mwenyezi Mungu wenye kutukuzwa, hawamtangulii kwa jambo lolote na wanafanya kulingana na amri yake?
Jibu: Ndio ni kweli kuwa hakuna tofauti kwa msingi wa utiifu, isma, na utawala kama ulivyo; isipokuwa kwa upande wa sifa; kama vile dhahabu tunajua kuwa yote ina thamani, lakini kuna baadhi inathamani zaidi kuliko nyingine. Vile vile vitu vingine vizuri vinatofautiana kulingana na uzuri wake na daraja yake, sio katika kuwa kwake na hakika yake. Ndio maana ikasemwa: ‘Nuru juu ya nuru’ au ‘kheri juu ya kheri’
Swali la pili: imekuwaje Mwenyezi Mungu kumtaja Daud peke yake kuwa amempa Zaburi na tunajua kuwa Musa alimpa Tawrat, Isa Injil na Muhammad akampa Qur’an?
Amemtaja peke yake kuwarudi washirikina waliosema: vipi Muhammad atakuwa ni mtume na yeye ni yatima fukara. Njia ya kuwarudi ni kuwa Yeye Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anaujalia ujumbe wake kwa yule anayestahiki - awe yatima aliyefukara, kama Muhammad au tajiri, kama Daud. Katika vitabu vingi vya sera na tarikh, hutajwa Mfalme Daud.
Sema: Waombeni hao mnaodai badala Yake. hawawezi kuwaondolea madhara wala kuyabadilisha.
Wafasiri wengi wamesema kuwa Aya hii na inayofuatia zilishuka kwa ajili ya wale wanaoabudu malaika, Isa na Uzayr. Na kwamba wanokusudiwa hapa sio waabudu masanamu, kwa sababu Mwenyezi Mungu amewataja hao waabudiwa kwa kusema: ‘wao wenyewe wanatafuta njia ya kujikuru- bisha kwa Mola wao,’ na kutafuta nji hakuelekeani na masanamu.
Kwa hiyo maana ni kuwa ewe Muhammad! Waambie wale wanaoabudu Malaika, Isa na Uzayr: yakiwapata madhara, kama ufukara na maradhi, basi waaombeni wale manowaabudu wawaondolee, kisha muangalie, je wanaweza kuwakinga au kuwabadilishia? Hakuna mwenye shaka ya kushindwa kwao, kwa vile wao wenyewe hawawezi kujikinga itakuwaje kwa mwengine?
Hao wanawaomba, wao wenyewe wanatafuta njia ya kujikurubisha kwa Mola wao.
Yaani hao ambao mnawaabudu enyi washirikina wanatafuta kujikuruku- bisha kwa Mwenyezi Mungu kwa twaa, hawajitii kiburi kwa waja wengine, wanamtakasa na kumsujudia Mungu, sasa vipi nyinyi mnawaabudu.
Hata walio karibu miongoni mwao, na wanataraji rehema zake na wanaihofu adhabu yake.
Yaani kila mmoja kati ya Malaika, Isa na Uzayr anajitahidi, kumwabudu Mwenyezi Mungu na kumfanyia ikhlasi ili awe karibu na msamaha wake na rehema zake na awe mbali na machukivu yake.
Hiyo ni kwa vile Hakika adhabu ya Mola wako ni ya kuhofiwa.
Wanaihofia manabii na mawalii, je, wengine? Kila mwenye akili ni lazima ahofie mwisho na kuuandalia maandalizi, kwa hali yoyote atakavyokuwa na cheo na daraja; hasa ikiwa mwenye kuchukua hisabau anajua siri na yaliyofichikana.
وَإِنْ مِنْ قَرْيَةٍ إِلَّا نَحْنُ مُهْلِكُوهَا قَبْلَ يَوْمِ الْقِيَامَةِ أَوْ مُعَذِّبُوهَا عَذَابًا شَدِيدًا ۚ كَانَ ذَٰلِكَ فِي الْكِتَابِ مَسْطُورًا {58}
وَمَا مَنَعَنَا أَنْ نُرْسِلَ بِالْآيَاتِ إِلَّا أَنْ كَذَّبَ بِهَا الْأَوَّلُونَ ۚ وَآتَيْنَا ثَمُودَ النَّاقَةَ مُبْصِرَةً فَظَلَمُوا بِهَا ۚ وَمَا نُرْسِلُ بِالْآيَاتِ إِلَّا تَخْوِيفًا {59}
وَإِذْ قُلْنَا لَكَ إِنَّ رَبَّكَ أَحَاطَ بِالنَّاسِ ۚ وَمَا جَعَلْنَا الرُّؤْيَا الَّتِي أَرَيْنَاكَ إِلَّا فِتْنَةً لِلنَّاسِ وَالشَّجَرَةَ الْمَلْعُونَةَ فِي الْقُرْآنِ ۚ وَنُخَوِّفُهُمْ فَمَا يَزِيدُهُمْ إِلَّا طُغْيَانًا كَبِيرًا {60}