Aya 58 – 60: Mji Wowote
Maana
Mahdiy Anayengojewa
Hapana mji wowote ila Sisi tutauangamiza kabla ya siku ya Kiyama au kuupa adhabu kali. Haya yamekwishaandikwa kwenye Kitabu.
Dhahir ya Aya inafahamisha kuwa watu wote watatoweka kabla ya siku ya kiyama, ambapo itafika siku kwenye ardhi kutakuwa hakuna yoyote kabisa; na kwamba jambo hili limekwishaandikwa katika kadha na kadari ambayo haiepukiki. Kuna jamii itatoweka kwa mauti ya kawaida na nyingine kwa adhabu kali, lakini Mwenyezi Mungu hakubainisha wasifa wa hawa wala wale.
Hiyo ndiyo dhahir ya Aya, lakini wafasiri wamesema kuwa jamii njema itatoweka kwa mauti ya kawaida na jamii ya ufisadi itatoweka kwa adhabu kali. Lakini haya hayaafikianai na kauli yao katika kufasiri Aya za mwanzo za sura Hajj:
يَا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمْ ۚ إِنَّ زَلْزَلَةَ السَّاعَةِ شَيْءٌ عَظِيمٌ {1}
يَوْمَ تَرَوْنَهَا تَذْهَلُ كُلُّ مُرْضِعَةٍ عَمَّا أَرْضَعَتْ وَتَضَعُ كُلُّ ذَاتِ حَمْلٍ حَمْلَهَا وَتَرَى النَّاسَ سُكَارَىٰ وَمَا هُمْ بِسُكَارَىٰ وَلَٰكِنَّ عَذَابَ اللَّهِ شَدِيدٌ {2}
Tuonavyo sisi mji alioukusudia katika kauli yake hii ni mji ambao watu wake ni madhalimu; yaani jamii yenye ufisadi tu; na kwamba Yeye ataiangamiza jamii hii au ataiadhibu kabla ya Siku ya Kiyama, wala hawatabakia ispokua watu wema tu, wote wakiwa wanaishi kwenye twaa ya Mwenyezi Mungu wakiwa na amani ya nafsi zao na vitu vyao vyote.
Kuna Hadith nyingi zinazozungumzia suala hilo; miongoni mwazo ni hizi:-
Hadith iliyoko kwenye Sunan Abi Daud As-sasjsataniy, kikiwa ni mojawapo ya Sahih sita kwa masunni, Juzuu ya pili chapa ya mwaka 1952, uk. 422:
“Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.): Lau haitabaki isipokuwa siku moja ya dunia, basi Mwenyezi Mungu atairefusha siku hiyo mpaka amlete mtu kutokana na watu wa nyumba yangu (Ahli bayti). Jina lake linafanana na jina langu na jina la baba yake ndio jina la baba yangu, ataijaza ardhi usawa na uadilifu; kama ilivyojazwa dhulma baada kujazwa usawa na uadilifu.”
Hadith iliyoko katika Sunan Ibn Maja, Pia nayo ni miongoni mwa sahih sita, juzuu ya pili chapa ya mwaka 1952, Hadith namba: 4083: Amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu: “Atakuwa katika umma wangu Mahdi, utaneemeka uma wangu neema ambayo haujaneemeka mfano wake.”
Mapinduzi na kujitoa mhanga kwa kujilipua (intifada), kila mahali kwa ajili ya kujikomboa na dhulma, ufisadi, ujinga na umasikini, yana fahamisha waziwazi kuwa hilo litakuwa tu karibuni au baadaye.
Na hapana kinachotuzuia kupeleka miujiza ila ni kuwa watu wa zamani waliikanusha. Na wathamudi tuliwapa ngamia jike kuwa ni dalili inayoonekana, lakini wakamdhulumu.
Washirikina walipendekeza kwa Mtume awaletee muujiza wanaoutaka wao. Miongoni mwa waliyoyasema ni: Tuchimbulie chemchem kutoka ardhini, tuletee Mungu na Malaika, tuletee kitabu kutoka mbinguni tukisome na mengineyo.
Ndio Mwenyezi Mungu akawajibu katika Aya hii, kwamba yeye amekwishapitisha katika kadha na kadari yake, kuwang’owa kwa adhabu kila kaumu iliyokadhibisha miujiza iliyokuja kwa maombi yao.
Wathamudi walimwomba Mtume wao awapatie ngamia wa muujiza. Alipowajia na sifa zile walizozitaka, walimkanusha na wakamchinja. Ukawanyakua ukelele wakawa ni wenye kuangamia. Yametangulia maelezo ya ngamia katika Juz. 8 (7:73 – 79).
Imekwishapitisha kadari yake kutowang’oa Makuraishi, kutokana na mapendekezo waliyoyapendekeza kwa Mtume. Kwa sababu watapatikana watu watakaotubia na kuamini, watazaliwa wengine wapigania jihadi kwa Mwenyezi Mungu. zaidi ya hayo kadari ya Mwenyezi Mungu imepitisha kuwa uma wa Muhammad na sharia yake ubakie mpaka siku ya ufufuo. Kwa sababu hii na nyinginezo, Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hakuitikia maombi ya makuraishi.
Nasi hatupeleki ishara ila kwa ajili ya kuhadharisha.
Hakuna ishara yoyote inayodhihiri mikononi mwa Mtume ila ina malengo; yakiwemo:mawaidha,makaripionakuhadharishaadhabuisiyokuwana kinga wala kafara; sasa vipi wao wanaharakia kutoa maombi ya adhabu?
Na tulipokwambia: hakika Mola wako amekwishawazunguka hao watu.
Imeelezwa hapo juu kuwa makuraishi walimtaka Mtume awalete muujiza na kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) alimpa wahyi Mtume wake kuwa lau atawaitikia maombi yao na wakaasi, wataangamia.
Lakini jawabu hili halikuwakinaisha washirikina na wakamwambia kuwa lau ungelikuwa ni Mtume ungelituletea yale tunayotaka, ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia mtume wake kuwa wewe endelea tu, wala usiwajali wale wanaofanya inadi na kiburi. Sisi tunawajua zaidi watu na wanayoy- afanya na tumewadhibiti.
Katika maana ya Aya hii ni ile isemayo:
وَاللَّهُ يَعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ ۗ {67}
Na hatukuifanya ndoto tuliyokuonyesha ila ni fitna (majaribu) kwa watu.
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anasema kuwa alimuonyesha Mtume wake ndoto usingizini na kwamba ndoto yenyewe ni fitna, lakini hakubainisha ilikuwa ya aina gani wala makusudio ya hiyo fitna au majaribu.
Ndio maana wafasiri wakatofautiana katika maana yake. Akataja Razi kati- ka Tafsiri al-kabir, Abu Hayan Al-andalusi katika Al-bahrul-muhit, Muhammad bin Ahmad Al-kalabiy, katika Attas-hil na wengineo, wametaja kauli kadhaa katika tafsiri ya ndoto na fitna.
Miongoni mwazo ni mtume (s.a.w.) aliota kuwa yeye ataingia Makka pamoja na swahaba, lakini alipotaka kuingia makuraishi walimzuia katika mwaka wa Hudaybiya.
Akaingiwa na shaka mwenye shaka miongoni mwa waislamu kuhusu ndoto ya Mtume, akamwambia: “Si umesema kuwa tutaingia Makka kwa amani?” Akasema: “Ndio, kwani nimesema tutaingia mwaka huu?” Akasema: “Hapana” Mtume (s.a.w.) akasema: “Inshallah tutaingia” wakaingia mwaka uliofuatia.
Miongoni mwa kauli nyingine zinazotokana na tafsiri ni kuwa Mtume (s.a.w.) aliona kwenye ndoto bani Umayya wakiiparamia mimbari yake kama anavyoparamia nyani, akahuzunika na akawa hana raha, na hakuonekana akicheka.
Kikundi miongoni mwa swahaba wako kwenye tafsiri hii; miongoni mwao ni Said bin Al-musabbib na Ibn Abbas; kama ilivyo katika Tafsiru-rrazi. Pia Sahal bin Sa’d; kama ilivyo katika Tafsir Al-bahr al-muhit.
Katika Sahih Al-bukhari Juzuu ya tisa Kitabu Al-fitan, imeelezwa kuwa Mtume (s.a.w.) alisema: “Kuangamia kwa umma wangu kutakua mikononi mwa wafidhuli wa kikuraishi.” Riwaya hii inatia nguvu tafsiri ya ndoto kuhusu Bani Umayya.
Kwa hiyo makusudio ya Na mti uliolaaniwa katika Qur’an ni Bani Umayya. Katika Tafsiru-rrazi imeelezwa kuwa kuna kundi la wafasiri wanasema: “Mti uliolaaniwa katika Qur’an ni mayahudi.” Matukio ya Historia ya kale na ya sasa yamethibitisha kuwa mayahudi ndio mzizi wa fitina.
Na tunawahadharisha, lakini haiwazidishii ila uasi mkubwa.
Mwenyezi Mungu amewahadharisha wanafiki kwa mifumo mbalimbali, lakini haikufaa kitu; bali hizo hadhari ziliwazidishia upotevu, kwa sababu wao hawataharaki isipokuwa kwa wahyi wa masilahi na manufaa. Ama hoja, maadili na misimamo, kwao ni maneno na njozi tu.
وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ قَالَ أَأَسْجُدُ لِمَنْ خَلَقْتَ طِينًا {61}
قَالَ أَرَأَيْتَكَ هَٰذَا الَّذِي كَرَّمْتَ عَلَيَّ لَئِنْ أَخَّرْتَنِ إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ لَأَحْتَنِكَنَّ ذُرِّيَّتَهُ إِلَّا قَلِيلًا {62}
قَالَ اذْهَبْ فَمَنْ تَبِعَكَ مِنْهُمْ فَإِنَّ جَهَنَّمَ جَزَاؤُكُمْ جَزَاءً مَوْفُورًا {63}
وَاسْتَفْزِزْ مَنِ اسْتَطَعْتَ مِنْهُمْ بِصَوْتِكَ وَأَجْلِبْ عَلَيْهِمْ بِخَيْلِكَ وَرَجِلِكَ وَشَارِكْهُمْ فِي الْأَمْوَالِ وَالْأَوْلَادِ وَعِدْهُمْ ۚ وَمَا يَعِدُهُمُ الشَّيْطَانُ إِلَّا غُرُورًا {64}
إِنَّ عِبَادِي لَيْسَ لَكَ عَلَيْهِمْ سُلْطَانٌ ۚ وَكَفَىٰ بِرَبِّكَ وَكِيلًا {65}