Aya 70-72: Wanaadamu Tumewatukuza
Maana
Kwanini Mwenyezi Mungu amewatukuza wanaadamu? Kabla ya kujibu swali hili, kwanza tubainishe maana ya matamshi ya Aya.
Hakika tumewatukuza wanaadamu.
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amemtukuza binadamu kwa kumpa uwezo na ujuzi uliomfanya awe ni muheshimiwa mwenye kutukuzwa. Tutataja baad- hi ya ujuzi huu na uweza baada ya kumaliza kufasiri matamshi ya Aya.
Na tumewabeba nchi kavu na baharini.
Kubebwa huku ni baadhi ya mambo aliyomtukuzwa nayo binadamu. Ni wazi kwamba kurahisishiwa mawasiliano ni katika mambo ya kuendeleza maisha watu.
Na tumewaruzuku vitu vizuri.
Kila linalomletea mtu manufaa kwa namna moja au nyingine, basi hilo ni zuri, lenye kheri na jema; liwe la kimaada au la kimaana.
Na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tuliowaumba.
Wafasiri wengi wamesema kuwa makusudio ya wengi katika Aya ni wote. Kwa hiyo wakawaingiza Malaika. Suala hili limechukua kurasa ndefu za tafsiri; pamoja na kujua kuwa halina athari yoyote ya kiutendaji, isipokuwa kurefusha maneno.
Ilivyo hasa ni kuwa Aya iko mbali tena mbali sana na kufadhilisha baina ya binadamu na malaika. Na kwamba neno wengi linabaki kwenye dhahiri yake; kwani hakuna dharura ya kuleta taawili; bali elimu inawajibisha kubakia na dhahiri yake.
Kwani ugunduzi wa elimu umebatilisha nad- hariya isemayo kuwa ardhi ndio kituo kikuu cha ulimwengu na binaadamu ndiye bwana mkubwa wa ulimwengu wote.
Ugunduzi huu umehakikisha upotevu wa binadamu kulingana na ukubwa wa ulimwengu. Ugunduzi unathibitishwa na kukubaliwa na Qur’an, pale iliposema:
لَخَلْقُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ أَكْبَرُ مِنْ خَلْقِ النَّاسِ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ {57}
Yaani hii sayari ya ardhi ambayo anaishi binadamu ni mojwapo tu ya mamilioni ya sayari ambazo sayansi hazijui idadi yake, pamoja na kuwa imegundua mambo ambayo hayana ukomo. Zaidi ya hayo ni kwamba wataalamu wengi wanasema kuwa kuna sayari zinazokaliwa na viumbe vyenye akili pengine zaidi kuliko binadamu.
Ni kweli kuwa binadamu ni bwana mkubwa aliyetukuzwa, hilo halina shaka, lakini yeye si bwana wa viumbe vyote, bali ni mmoja tu kati ya mabwana. Hakuna jambo linalofahamisha hilo zaidi kuliko ujinga wa binadamu kwenye vitu vingi na kushindwa kwake kuvitumia. Bali hajui vitu vingi vilivyomo ardhini; sikwambii vilivyo katika sayari nyingine. Kimsingi ni kwamba sharti la kwanza la ubwana ni uwezo wa kutumia vitu.
Baada ya kufafanua matamshi ya Aya, sasa tunadokeza mambo ambayo Mwenyezi Mungu amemtukuza nayo binadamu:
1. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amemuumba mtu akalifanya zuri umbo lake na sura yake. Mwenyezi Mungu anasema:
بِنَاءً وَصَوَّرَكُمْ فَأَحْسَنَ صُوَرَكُمْ وَرَزَقَكُمْ {64}
لَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنْسَانَ فِي أَحْسَنِ تَقْوِيمٍ {4}
2. Akili. Lau si hiyo, binadamu asingekuwa chochote, bali lau si akili muumba asingejulikana. Kwayo tunajua utukufu wa Mwenyezi Mungu na ukubwa wa ulimwengu na ukubwa wa akili yenyewe vilevile.
Mmoja wa wenye akili anasema: “Ikiwa ulimwenguni kuna nyota zinazomeremeta, basi ndani ya akili kuna nyota inayomeremeta na kuangaza. Ikiwa vitu vinavyotuzunguka vimepangiliwa kwa ufundi, basi akili ni kuu zaidi. Ikiwa wataalamu wa falaki wanaona kuwa mpangilio wa ndani wa ulimwengu na ukuu wake ni dalili ya ukuu wa Muumbaji, basi kuweko mtu ni dalili kubwa zaidi ya ukuu wa Mwenyezi Mungu. Ikiwa kuangalia mbin- guni kunamfanya mtu ahisi upotevu wake, basi kujifikiria mtu kunamfanya ahisi ubingwa na ukuu wa aliyemuumba na kuumba ulimwengu wote.”
Ulimwengu ni mkuu na akili ni kuu. Kitu pekee cha kujua ukuu wa Mwenyezi Mungu, ulimwengu na mtu ni akili. Lakini usisahau kuwa sio mtu tu, peke yake ndiye aliyepewa akili.
3. Mtu ana sifa na siri nyingi: elimu na ujinga, dini na kufuru, mapenzi na chuki, upole na hasira, ujasiri na hofu, ukarimu na ubakhili, unyenyekevu na kiburi, uaminfu na hiyana, uthabiti na kuwa kigeugeu na mengineyo mengi yasiyokuwa na idadi. Sijui kama ametia chumvi aliyesema: “Binadamu sio kitu kimoja isipokuwa ni mamilioni ya vitu vilivyo na akili na vilivyo na wazimu, vilivyoendelea na visivyo na maendeleo.”
4. Binadamu huwa anatafuta kuishi kwenye maisha, hata kama tayari yuko katika maisha bora, atatafuta bora zaidi. Kuna Hadith isemayo: “Lau mtu angelikuwa na mlima wa dhahabu na mwingine wa fedha, basi atatamani wa tatu.” Ikiwa binadamu yuko hivyo, basi inafaa kwake pia kuwa na hamu kubwa ya kufikia kwenye utukufu zaidi.
5. Mtu ana sharia na misimamo, ambayo ni lazima aifuate na kuitumia. Ataulizwa na kuhisabiwa; na atakuwa mtukufu au mpuuzi.
6. Mtu anaathirika kwa waliopita na yeye anawathiri wajao, wakati huo huo akiathiriana na alio nao; wanamuathiri naye anawaathiri. Ndio maana akawa ana historia, turathi na athari, ambapo viumbe vingi havina.
7. Mtu ana maisha mengine, amabyo ni uwanja wa hukumu na malipo, kutokana aliyoyafanya katika maisha yake ya kwanza, na mengineyo katika neema alizoziashiria Mwenyezi Mungu kwa kauli yake:
وَإِنْ تَعُدُّوا نِعْمَتَ اللَّهِ لَا تُحْصُوهَا ۗ {34}
Siku tutakapowaita watu kwa Imam wao. Basi atakayepewa kitabu chake kwa mkono wake wa kulia , basi hao watasoma kitabu chao.
Imam ni yule anayefuatwa na kufutwa amri zake. Anaweza kuwa mtu, wahyi, akili au hawaa. Kuna Hadith isemayo: “Watu wataitwa Siku ya Kiyama kwa Imam wa zama zao, kitabu cha Mola wao na sunna ya nabiiwao.”
MakusudioyakitabukatikaAyanikitabuchamatendoyamtu,watuwa kuume ni watu watiifu walio wema na watu wa kushoto ni waasi walio waovu.
Maana ni kuwa mnadi atanadi siku ya Kiyama: Wako wapi wafuasi wa Mitume na wa viongozi wema? Wako wapi waliotumia akili na dini? Watakuja na watachukua kitabu cha mambo wema na thawabu zake kwa mikono yao ya kuume, wakiwa na furaha.
Vilevile atanadi mnadi: wako wapi wafuasi wa madhalimu na wasaidizi wao? Wako wapi wahaini na wafisadi? Watakuja na watachukua kitabu cha maovu na adhabu yake kwa mikono yao ya kushoto wakiwa madhalili waliohizika.
Wala hawatadhulumiwa hata chembe.
Yaani Mwenyezi Mungu atamlipa kila mtu kulingana na matendo yake, hapunguzi thawabu za mwenye kufanya wema wala hazidishi adhabu ya mwenye kufanya uovu.
Na aliyekuwa kipofu katika hii, basi Akhera atakuwa kipofu na aliyepotea zaidi njia.
Katika hii, ni dunia na kipofu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule aliyezama kwenye ujinga. Wasifu wa fasaha zaidi katika hilo ni aliyoyasema Imam Ali (a.s.):
“Amepotelewa na makusudio, mwenye uchu wa maneno ya bid’a, mwenye kulingania upotevu. Yeye ni fitna ya mwenye kufitinika na ni mpotevu wa uongofu uliokuwa kabla yake, mpotezaji wa aliyemfuata katika uhai wake na baada ya kufa kwake”.
Kwa ufupi wa maana ya Aya hii ni kwamba ambaye amali yake imekuwa mbaya katika maisha haya, basi mwisho wake huko Akhera utakuwa mbaya. Vile vile Aya hii inafahamisha wazi kuwa thawabu au adhabu kati- ka Akhera inafungamana moja kwa moja na matendo katika maisha ya dunia.
Ndiomaanaikasemwa:‘DunianishambalaAkhera.”Inatoshakuwani dalili kauli yake Mtume: “Watuwatafufuliwananiyazao.”AngaliaJuz.4(3:142).
وَإِنْ كَادُوا لَيَفْتِنُونَكَ عَنِ الَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ لِتَفْتَرِيَ عَلَيْنَا غَيْرَهُ ۖ وَإِذًا لَاتَّخَذُوكَ خَلِيلًا {73}
وَلَوْلَا أَنْ ثَبَّتْنَاكَ لَقَدْ كِدْتَ تَرْكَنُ إِلَيْهِمْ شَيْئًا قَلِيلًا {74}
إِذًا لَأَذَقْنَاكَ ضِعْفَ الْحَيَاةِ وَضِعْفَ الْمَمَاتِ ثُمَّ لَا تَجِدُ لَكَ عَلَيْنَا نَصِيرًا {75}
وَإِنْ كَادُوا لَيَسْتَفِزُّونَكَ مِنَ الْأَرْضِ لِيُخْرِجُوكَ مِنْهَا ۖ وَإِذًا لَا يَلْبَثُونَ خِلَافَكَ إِلَّا قَلِيلًا {76}
سُنَّةَ مَنْ قَدْ أَرْسَلْنَا قَبْلَكَ مِنْ رُسُلِنَا ۖ وَلَا تَجِدُ لِسُنَّتِنَا تَحْوِيلًا {77}