Aya 90-96: Kufikiria Mali
Kujipenda
Kila mmoja wetu anajipenda; awe mwana mume au mwanamke, mzee au mtoto, mwenye takua au muovu n.k. Ni binadamu gani asiyekuwa na shauku na maisha yake na kutetea heshima yake na uhalisi wake? Lau si hivyo uhai usingeendelea kuwako wala tusingeendelea. Hakuna tofauti katika kujipenda huko baina ya watu; isipokuwa tofauti iko katika aina zifutazo:-
Kuna yule anayekuwa kwenye msingi wa maumbile na akili. Hili linafa- hamika kutokana na jinsi mtu anavyoheshimu haki za wengine, kutosheka na alichoandikiwa kilichotokana na jasho lake na kusaidiana na kila mwenye kutumai kheri na manufaa ya watu kwa namna moja au nyingine; bali hata kujitolea juu ya hilo.
Kwani mwenye kutoa na kujitolea kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, atakuwa amejipenda, atake asitake, kwa sababu Mwenyezi Mungu hapotezi ujira wa mwenye kufanya wema, vile vile jamii inamsifu na kumtukuza yule mwenye kujitolea kwa ajili ya hiyo jamii.
Na kuna yule anayejipenda kwa kutumia yale yanayopituka akili, dini na uhalisi. Hili linafahamika kutokana na tamaa ya mtu ambaye haioni umuhimu wala manufaa ya mwingine isipokuwa wake.
Hili halikubaliki na mantiki yoyote; hata ya yahisia na ya kuonekana; sawa na alivyosema Mwenyezi Mungu: “Wana nyonyo, lakini hawafahamu kwazo, na wana macho, lakini hawaoni kwayo, na wanayo masikio, lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama wanyama bali wao ni wapotevu zaidi. Hao ndio walioghafilika.” Juz. 9 (7: 179). Hawa wako kila mahali na kila wakati; miongoni mwao ni wale aliowaashira Mwenyezi Mungu kwa kuli zake zifuatazo:-
1. Na walisema: hatutakuamini mpaka utuchimbulie katika ardhi hii chemchem.
wapenda raha katika washirikina walitoa pendekezo kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kuwa awachimbulie chemchem au mto, wao sio watu wengine, kwa ajili ya chumo na faida. Kuna mapokezi yanayosema kuwa vijoho na wapenda anasa walisema: Ewe Muhammad! Hii ardhi ya Makka ni finyu, basi yaondoe majabali yake na utuchimbulie chemchem ili tunufaike na ardhi.
2. Au uwe na kitalu cha mitende na mizabibu na utupitishie mito kati yake ikimiminika.
Yaani kama hutatuchimbulia chemchem, basi angalu jichimbulie wewe, ili uwe unafanana na hadhi ya juu. Lakini ukiwa huna kitu basi wewe unatakikana uwasikilize walio nacho. Kwamba mali peke yake ndiyo itakayomfanya aliye nayo awe anafaa kuwa kiongozi na bwana mkubwa. Hawakujua kuwa risala ya Muhammad (s.a.w.) ni utajiri mkubwa wa mtu, uhai wake, na kwamba Muhammad ni rehema kwa watu wa ardhini itakayowaokoa na ufukara, ujinga, dhulma na utaghuti. Wapi na wapi wanaoabudu mali na kupigana vikumbo na tamaa waweze kujua rehema na kheri?
Au utuangushie mbingu vipande vipande, kama ulivyodai, au utuletee Mwenyezi Mungu na Malaika ana kwa ana.
Walitaka wachimbuliwe chemchem yao au yake; kam sio hivyo au vile, basi awalete adhabu kutoka mbinguni au Mwenyezi Mungu mwenyewe aje na malaika kushuhudia kuwa Yeye ni Mtume.
Hii vile vile inatokana na fikra yao kwamba anayestahiki uongozi ni tajiri, sio fukara. Dalili ya hilo ni kule kuweka sharti la kumwamini Muhammad na jambo wanaloliona kuwa haliwezekani. Ni wazi kuwa kulazimisha jambo lisilowezekana maana yake ni kung’ang’ania matakwa yao ya kuchimbuliwa chemchem ardhini; sawa na kusema: Sifanyi hivi mpaka ngamia apite kwenye tundu ya sindano.
4. Au uwe na nyumba ya dhahabu.
Yaani iliyojengwa kwa dhahabu au iliyopambwa nayo. Hii vile vile inatokana na fikra ya mali.
Au upae mbinguni.
Nalo hili linafungamana na jambo lisilowezekana. Maana yake ni kung’ang’ania kuwa mali ndio kitu pekee cha kumweka mtu kwenye cheo.
Na hatutaamini kupaa kwako mpaka ututeremshie Kitabu tukisome.
Baadhi ya wafasiri wapya wanasema: “Unadhihiri utoto wa kuhafamu na kufikria; kama unavyodhihiri ukaidi wa kipumbavu.” Lakini hapana huo si utoto wala si upumbavu; isipokuwa hilo linatokana na ufisadi, kujibagua, uporaji, unyang’anyi na kuabudu mali. Kitu kinachofahamisha hilo zaidi ni kule kupendekeza na kuweka sharti la kumfuata Mtume awe na nyumba ya dhahabu kuwa ndio muabudiwa wao wa kwanza na ndio mfano wao mkuu.
Sema: Ametakasika Mola wangu! Kwani mimi ni nani, isipokuwa ni mwanadamu Mtume?
Anayefuata amri ya yule aliyemtuma na kukatazika kwa makatazo yake:
وَمَا كَانَ لِرَسُولٍ أَنْ يَأْتِيَ بِآيَةٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّهِ ۗ {38}
Na nini kilichowazuia watu kuamini ulipowajia utume, isipokuwa walisema: je, Mwenyezi Mungu hupeleka mwanadamu kuwa Mtume?
Wafasiri, akiwemo Tabrasi na Razi, wameiangalia Aya hii kuwa haiungani na Aya zilizotangulia na wakasema katika kuifasiri: Hakika washirikina wa Makka hawakumwamini Muhammad (s.a.w.) kwa sababu wao walikuwa wakiitakidi kuwa mjumbe ni lazima awe ni katika jinsia ya malaika, si katika jinsia ya watu. Lakini tafsiri hiyo iko mbali sana kutokana na njia zifuatazo:-
Washirikina wa kikuraishi walikuwa wakiamini utume wa Ibrahim na kwamba wao wanatokana na kizazi chake.
Kauli ya washirikina: ‘Hatutakuamini mpaka utuchimbulie,’ inafahamisha kuwa wanaamini risala ya binadamu; isipokuwa walitoa sharti la kuwa Mtume awe tajiri: “Na walisema: kwanini hii Qur’an haikuteremshwa kwa mtu mkubwa katika miji miwili hii” (43:31) Makusudio ya mtu mkubwa ni Walidi bin Mughira, katika viongozi wa Makka au Urwa bin Masud katika viongozi wa Taif.
Lau ingelikuwa tafsiri kama wanavyosema, basi washirikina wangelikuwa na udhuru katika kupinga kwao utume wa Muhammad (s.a.w.), kwa sababu watakuwa wanafanya lile wanaloliitakidi, na Mwenyezi Mungu amewasifu kwenye Aya nyingi kuwa wanadhihirisha yale waliyoyaficha:
بَلْ بَدَا لَهُمْ مَا كَانُوا يُخْفُونَ مِنْ قَبْلُ ۖ {28}
“Na wakazikataa kwa dhulma na kujitia uluwa na hali ya kuwa nafsi zao zina yakini nazo.” (27:19).
Kwa ufupi ni kuwa maana sahihi ya Aya ni kwamba washirikina wali- poshindwa na hoja ya utume wa Muhammad, walikimbilia ubabaishaji na kujaribu kuwapoteza wajinga wasiokuwa na akili.
Ndio wakasema kama mbinu tu za kuhadaa, kuwa Mwenyezi Mungu hamtumi Mtume binadamu, isipokuwa Malaika tu. Walisema haya wakiwa wanajua kwamba wao ni waongo. Ndio maana Mwenyezi Mungu akasema ‘Ispokuwa walisema’ na wala hakusema walidhani n.k. Hii inafahamisha kuwa kupinga kwao ni kiasi cha inadi tu ya kauli si ya itikadi.
Sema: Lau ingelikuwa duniani kuna Malaika wanaotembea kwa utulivu, Yaani wanaotembea kama wanadamu basi bila ya shaka tun- geliwateremshia Malaika kuwa Mtume wao.
Hekima ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) inataka apeleke Mtume kwa viumbe wake kutokana na jinsi yao. Wakiwa ni watu basi mtume wao atatokana na wao na wakiwa ni Malaika basi watakuwa hivyo hivyo. Kwa sababu jinsia inapendelea zaidi kwenye jinsia yake:
لَقَدْ مَنَّ اللَّهُ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ إِذْ بَعَثَ فِيهِمْ رَسُولًا مِنْ أَنْفُسِهِمْ {164}
Washirikina wanajua hilo, lakini wanafanya vitimbi na hadaa. Umetangulia mfano wake katika Juz.7 (6:9).
Unaweza kuuliza: Jibril ni Malaika naye alikuwa mjumbe wa Mungu kwa Muhammad ambaye ni mtu, imekuwaje? Jibu: baina ya hawa wawili kuna aina fulani ya kukurubiana katika jinsi; kwamba kila mmoja wao ni mjumbe kutoka kwa Mungu.
Sema: Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi baina yangu na nyinyi. Hakika Yeye anawajua vyema waja wake na anawaona.
Mwenyezi Mungu ni shahidi wa Muhammad kwa miujiza aliyoidhihirisha mikononi mwake, historia inashuhudia heri ya utu iliyopatikana kutokana naye na risala yake inashuhudia kwamba yeye ni rehema kwa viumbe na lolote katika sera ya Muhammad ni hoja tosha ya ukweli wake na utukufu wake.
وَمَنْ يَهْدِ اللَّهُ فَهُوَ الْمُهْتَدِ ۖ وَمَنْ يُضْلِلْ فَلَنْ تَجِدَ لَهُمْ أَوْلِيَاءَ مِنْ دُونِهِ ۖ وَنَحْشُرُهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ عَلَىٰ وُجُوهِهِمْ عُمْيًا وَبُكْمًا وَصُمًّا ۖ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ كُلَّمَا خَبَتْ زِدْنَاهُمْ سَعِيرًا {97}
ذَٰلِكَ جَزَاؤُهُمْ بِأَنَّهُمْ كَفَرُوا بِآيَاتِنَا وَقَالُوا أَإِذَا كُنَّا عِظَامًا وَرُفَاتًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ خَلْقًا جَدِيدًا {98}
أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّ اللَّهَ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ قَادِرٌ عَلَىٰ أَنْ يَخْلُقَ مِثْلَهُمْ وَجَعَلَ لَهُمْ أَجَلًا لَا رَيْبَ فِيهِ فَأَبَى الظَّالِمُونَ إِلَّا كُفُورًا {99}
قُلْ لَوْ أَنْتُمْ تَمْلِكُونَ خَزَائِنَ رَحْمَةِ رَبِّي إِذًا لَأَمْسَكْتُمْ خَشْيَةَ الْإِنْفَاقِ ۚ وَكَانَ الْإِنْسَانُ قَتُورًا {100}