Aya 97-100: Aliyeongozwa Na Mungu
Maana
Na anayeongozwa na Mwenyezi Mungu ndiye aliyeongoka na anayem- potoa, basi, hutawapatia walinzi wasiokuwa Yeye.
Hii ni kumwelezea aliye mwema; yaani anayekuwa hivyo mbele ya Mwenyezi Mungu; na wala sio yule watu wanayesema kuwa ni mwema. Kuna Hadith isemayo: “Dhahiri ni ya watu na batini ni ya Mungu.” Katika Nahjulbalagha imeelezwa: ”Utajiri na ufukara ni baada ya kuonekana kwa Mungu.”
Wafisadi na wapotevu hawana wa kuwanusuru wala kuwaombea kwa Mwenyezi Mungu. Umetangulia mfano wake katika Juz. 9 (7: 178). Ama adhabu ya wapotevu wanaopoteza, ameiashiria Mwenyezi Mungu kwa kusema:
Na tutawakusanya Siku ya Kiyama hali ya kukokotwa juu ya nyuso zao wakiwa ni vipofu na mabubu na viziwi. Makazi yao ni Jahannam. Kila moto ukifanya kuzimika tutazidi kuuchochea uwake kwa nguvu.
Hili ni fumbo la uchungu wa adhabu na ukali wake kwa yule Mwenye kupinga hisabu na adhabu yake mpaka ajue aliyoyapinga:
كُلَّمَا أَرَادُوا أَنْ يَخْرُجُوا مِنْهَا أُعِيدُوا فِيهَا وَقِيلَ لَهُمْ ذُوقُوا عَذَابَ النَّارِ الَّذِي كُنْتُمْ بِهِ تُكَذِّبُونَ {20}
Na hayo ni malipo yao kwamba wao walizikataa ishara zetu pamoja na ufafanuzi wa kutokea ufufuo. Walikanusha na wakapinga si kwa chochote ila ni kwa kuona ni mbali hilo.
Na wakasema: je, tutakapokuwa mifupa na mapande yaliyosagika, je tutafufuliwa kuwa viumbe wapya?
Imekwishatangulia Aya hii neno kwa neno katika Aya ya 49 ya Sura hii.
Kwani hawaoni kwamba Mwenyezi Mungu aliyeumba mbingu na ardhi ni Mwenye kuweza kuumba mbingu mfano wao? Na yeye amewawekea muda usio na shaka yoyote, lakini makafiri hawataki isipokuwa ukafiri.
Makusudio ya muda hapa ni muda wa ufufuo na kwamba huo utakuwa tu. Wameukana na hali wanaona kuumbwa kwa mbingu na ardhi huku wakikubali kuwa Mwenyezi Mungu ndiye aliyeziumba na akazipangilia vizuri kwa uweza wake, lakini wakasema kuwa Mwenyezi Mungu hawezi kuwarudisha tena baada ya kutoweka, kwa vile hilo ni jambo zito.
Ndio Mwenyezi Mungu akawaambia kuwa mwenye kuweza kukifanya kitu bila ya kitu basi ana uweza zaidi kukikusanya kitu hicho baada ya kutawanyika.
Maana ya Aya hii yamekwisha tangulia kwenye Aya nyingi. Angalia Juz.13 (13:5).
Hebu tusome kwa pamoja hoja hizi za kufunga mdomo wa mpinzani wa ufufuo, kwa mfumo usiokuwa na ushabiki; kisha useme: Ole wao wenye kukadhibisha:
“Walisema: Je, tutakapokufa na tukawa mchanga na mifupa ndio tutafu- fuliwa? Tuliahidiwa haya sisi na baba zetu zamani. Hayakuwa haya ila ni ngano za watu wa kale.”
“Sema: Ni ya nani ardhi na mbingu na vilivyomo ndani yake, kama nyinyi mnajua?”
“Watasema ni ya Mwenyezi Mungu.”
“Sema: Basi je, hamkumbuki?”
“Sema ni nani Mola wa mbingu saba na Mola wa Arshi kuu?”
“Watasema ni Mwenyezi Mungu.”
“Sema: Basi Je, hamuogopi?”
“Sema: ni nani ambaye ufalme wa kila kitu umo mikononi mwake, naye ndiye alindaye na halindwi, ikiwa mnajua?”
“Watasema ni vya Mwenyezi Mungu”
“Sema: basi vipi mnadanganywa?” 23: (82 – 89).
Huu ni ushahidi wazi kwamba itikadi ya kiislamu iko kwenye misingi ya elimu na uhuru wa akili na rai. Tazama. Juz. 7 (6:4) “Kifungu hakuna udikteta katika ardhi wala mbingu.”
Sema lau mngelikuwa mnamiliki hazina ya rehema ya Mola wangu, basi mngeliizuia kwa kuchelea kuisha.
Rehema ya Mwenyezi Mungu inaenea kwenye kila jambo, kama vile afya, ufahamu, mali na neema nyinginezo, lakini makusudio yake hapa ni kuhusu mali, kwa dalili ya kauli yake Mwenyezi Mungu (s.w.t.): “Kuhofia kuisha” na ile Aya ya 90 ya Sura hii.
Ubainifu wake ni kuwa Mwenyezi Mungu alimwamrisha Mtume wake awaambie wapenda anasa kuwa nyinyi mlitaka Mwenyezi Mungu awazidishie mali zenu na utajiri wenu kwa kuchimbua mito ardhini, huku akiwa anajua kwamba nyinyi lau mtamiliki hazina ya mbingu na ardhi ambayo haishi, basi mngeendelea na ubahili wenu na uchoyo kwa kuhofia kuisha. Hili linatilia mkazo tuliyosema kwamba wapenda anasa hawafikirii isipokuwa mali.
Na mtu ni mchoyo sana
Katika Juz. 12 (11: 9) tumesema kuwa Qur’an, haikusudii, kwa wasifu huu, kumueleza binadamu alivyo; isipokuwa ni kutafsiri tabia ya binadamu katika badhi ya hali zake. kwa maelezo zaidi rudia huko.
وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَىٰ تِسْعَ آيَاتٍ بَيِّنَاتٍ ۖ فَاسْأَلْ بَنِي إِسْرَائِيلَ إِذْ جَاءَهُمْ فَقَالَ لَهُ فِرْعَوْنُ إِنِّي لَأَظُنُّكَ يَا مُوسَىٰ مَسْحُورًا {101}
قَالَ لَقَدْ عَلِمْتَ مَا أَنْزَلَ هَٰؤُلَاءِ إِلَّا رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ بَصَائِرَ وَإِنِّي لَأَظُنُّكَ يَا فِرْعَوْنُ مَثْبُورًا {102}
فَأَرَادَ أَنْ يَسْتَفِزَّهُمْ مِنَ الْأَرْضِ فَأَغْرَقْنَاهُ وَمَنْ مَعَهُ جَمِيعًا {103}
وَقُلْنَا مِنْ بَعْدِهِ لِبَنِي إِسْرَائِيلَ اسْكُنُوا الْأَرْضَ فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ الْآخِرَةِ جِئْنَا بِكُمْ لَفِيفًا {104}