Aya 105 – 111: Kwa Haki Tumeiteremsha
Maana
Na kwa haki tumeiteremsha na kwa haki imeteremka.
Wafasiri wana kauli nyingi katika jumla mbili hizi. Yenye nguvu zaidi ni ile aliyoisema Tabrasi na Razi. Kwa ufupi wa kauli yao ni kuwa makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu: Na kwa haki tumeitremsha’, ni kwamba Qur’an imedhamini haki na makusudio ya ‘Na kwa haki imeteremka’ ni kwamba Mwenyezi Mungu kwa kuiteremsha Qur’an alitaka watu waiamini na waitumie. Hilo lilipatikana kwa hakika; ambapo waislamu waliiamini na wakaitumia wale wenye ikhlasi.
Sisi tuko pamoja na Razi na Tabrasi katika kufasiri jumla ya kwanza. Ama jumla ya pili, tuonavyo sisi ni kuwa kila walilokuwa nalo watu kabla ya kuteremshwa Qur’an na watakalokuwa nalo baada ya kuetremshwa, basi Qur’an inalikubali ikiwa ni la haki, kheri na masilahi.
Kwa maneno mengine ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) baada ya kusema katika jumla ya kwanza kuwa ameiteremsha Qur’an kwa haki kheri na masilahi, katika jumla ya pili anasema pia Qur’an inakubaliana na kila lililo haki lenye kheri na masilahi wakati wowote litakapokuwa, kabla au baad aya Qur’an.
Kuna Aya zilizo na maana ya tafsiri hii; kama vile:
وَأَمَّا مَا يَنْفَعُ النَّاسَ فَيَمْكُثُ فِي الْأَرْضِ ۚ كَذَٰلِكَ يَضْرِبُ اللَّهُ الْأَمْثَالَ {17}
يُرِيدُ اللَّهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلَا يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ {185}
Imam Ja’far As-swadiq (a.s.) naye amesema: “Kila lenye masilahi kwa watu kwa namna moja au nyingine, basi linajuzu.”
Na hatukukutuma ila uwe mbashiri na muonyaji.
Umbashirie Pepo mtiifu na umonye na moto muasi. Baada ya hapo anayetaka aamini na anayetaka na akufuru.
إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ مَنْ يَضِلُّ عَنْ سَبِيلِهِ ۖ وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ {117}
Je Qur’ani Ilishuka Kidogo Kidogo?
Na Qur’an tumeigawanya ili uwasomee watu kwa kituo.
Qur’an haikuteremka kwa Muhammad kwa mpigo; bali iliteremka kidogo kidogo, ikifiuatana na mara nyingine ikichelewa kulingana na masilahi na matukio ambayo huzuka mara kwa mara. Ama kauli yake Mwenyezi Mungu:
إِنَّا أَنْزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ {1}
Maana yake ni kuwa ilianza kuteremshwa usiku huo, kisha ikaendelea hadi kufa Mtume (s.a.w.) na kuanzia mwanzo hadi mwisho wa kushuka kwake ilikuwa ni miaka ishirini na tatu.
Mwenyezi Mungu amebainisha lengo la kufanya hivyo kwa kusema: ‘ili uwasomee watu kwa kituo;’ yaani kutoa muda ili iwe rahisi kuifahamu na kuihifadhi.
Aya hii ni dalili wazi ya kumkosoa anayesema kuwa Qur’an imeshuka kwa mara moja yote na mtume akaifikisha kidogo kidogo. Mwenyezi Mungu amemrudi mwenye kusema hivi kwa kauli yake: “Na wakasema wale waliokufuru: kwa nini hakuteremshiwa Qur’an kwa jumla moja?” (25: 32) Yaani moyo wako uweze kuwa na nguvu kuweza kufahamu maana ya Qur’an na siri zake.
Zaidi ya hayo kuna Aya kadhaa zinazosimulia visa na matukio yaliyojitokeza upya au kubainisha hukumu yake; kama vile kisa cha Badr, Uhud, Ahzab na Hunayn. Pia kisa cha Wakiristo wa Najrani na mayahudi wa Madina. Vile vile tukio la wake wa Mtume, mwanamke aliyemjadili Mtume kuhusu mumewe na mengineyo.
Amesema Sheikh Mufid: “Qur’an imeshuka kwa sababu na matukio kwa hali baada ya hali. Hilo linafahmika kutokana na dhahiri ya Qur’an, Hadith mutawatr na kongamano la maulama.”
Na tumeitermsha kidogo kidogo.
Jumla hii ni tafsiri na ubainifu wa yaliyo kabla yake.
Sema, iaminini au msiamini. Hakika wale waliopewa ilimu kabla yake, wanaposomewa, huanguka kifudifudi wanasujudu. Na wanasema: Ametakasika Mola wetu. Hakika ahadi ya Mola wetu lazima itimizwe. Na huanguka kifudifudi na huku wanalia, na inawazidishia unyenyekevu.
Kabla yake, ni kabla ya Qur’an. Wanaoambiwa ni washirikina ambao walimwekea masharti Muhammad (s.a.w.) ya kumwamini; kama ilivyoelezwa katika Aya ya 9 ya Sura hii. Kuanguka kifudifudi ni kusujudu kwa uso. Kumetajwa kusujudu mara mbili, kwa sababu kwa kwanza ni kwa ajili ya kumwadhimisha Mwenyezi Mungu na kwa pili ni kwa kuathrika na Qur’an katika nafsi zao.
Wale ambao wamepewa elimu kabla ya Qur’an ni wale waloiangalia haki katika watu wa Kitabu ambao walimwamini Muhammad (s.a.w.) na wenye maumbile safi, kama wale tutakaowadokeza katika kifungu kinachofuatia.
Wanyoofu
Mnyoofu ni yule aliyeacha batili na kufuata haki na njia yenye kunyooka. Wakati wa Jahiliya kulikuwa na watu waliopetuka mazingira yao, na kwa mamubile yao safi waliweza kutambua kwamba kuna muumba mmoja mwenye uwezo wa ulimwengu huu na kwamba baada ya mauti kuna ufu- fuo, hisabu, adhabu na thawabu.
Vile vile kwamba kuabudu masanamu ni ujinga na upotevu. Kuna baadhi ya shairi zao katika kitabu Al-aghani Juzuu ya 3 na Sirat ibn Hisham, Juzuu ya 1. Chapa ya mwak 1936:
• Je, ni Mungu mmoja au elfu miungu?
• Ni dini iliyokioja iliyogawanyika mafungu
• Lakini namuabudi Mola wangu Rahamani
• Anisamehe zangu dhambi Mola ghafuri manani
• Tawaona watu wema makazi yao Peponi
• Na makafiri madhalima kwenye sairi Motoni
Ibn Hisham anasema katika Juzuu ya 1 ya As-siratun-nabawiyya: “Walikusanyika makuraishi katika Idd yao ya masanamu waliyokuwa wakiyaadhimisha, wakajitoa watu wane ambao ni: Waraqa bin Nawfal, Abdallah bin Jahsh, Uthman bin Alhuwayrith na Zayd bin Amr. Wakaambiana: Wallah hawa watu wenu hawana chochote, wameikosea dini ya baba yao Ibrahim! Nini haya mawe tunayozungukia, hayasikii, hayaoni, hayadhuru wala hayanufaishi!
Zayd hakuingia kwenye uyahudi wala unaswara (ukiristo). Aliacha dini ya watu wake kwa kujiepusha na masanamu, mfu, damu na dhabihu zilizokuwa zikitolewa kwa masanamu. Akakataza kuwaua watoto wa kike na akawa anamwambia baba yake: “Usimuue mimi nitamgharimia malezi yake.”
Alikuwa akijasiri kuwaambia watu wake na kuwakosoa huku akiwaambia: “Mimi ninamwabudu Mola wa Ibrahim. Ewe Mola wangu! Lau ningejua namna inayopendeza zaidi ya kukuabudu ningeliifanya, lakini siijui.” Kisha anasujudi kwenye kiganja chake.
Zayd aliendela kuwasafihi maquraishi na ibada yao. Walipoona ni hatari walimtaka ami yake Khattwab, baba wa Umar bin, Alkhattab amzuie na amkataze, naye akamkataza. Lakini Zayd bado aliendelea na mwito wake. Al-Khattab akawa anawatuma vijana wahuni wa Kikuraishi, akiwemo mtoto wake Umar, kumzuia asiingie Makka. Zaidi akawa anapenye Kisiri.
Walipofahamu walimwambia al-Khattab na wakawa wanamfukuza na kumwudhi kwa sababu ya kuogopa kwao asije akawavutia watu kwenye dini yake. Baadaye Zaid akatoka kutafuta dini ya Ibrahim (as). Akawa anahangaika huku na huko katika nchi mbalimbali. Hata hivyo alipokanyaga nchi ya Lakhm, alishambuliwa na kuuawa. Rafiki yake Waraqa alimlilia na kumtungia mashairi haya:
• Hakika bin Amri meongozwa kwa wema
• mejiepusha na tanuri ya moto unaochoma
• Me mwabudu adhimu Mola aso mithili
• Ukaiacha mizimu ya matwaghuti jahili
• Rehema za Mola wake kiumbe humfikia
• Hata chini ajizike bonde sabini kungia
Zaidi aliuawa kabla ya kutumwa Mtume Muhammad (saw), lakini mtoto wake alimwamini Mtume (saw) Yeye pamoja Umar bin al-Khattab, ambaye alikuwa ni binamu yake, walimwendea Mtume na kumwuliza: Tunaweza kumuomba Mwenyezi Mungu amsamehe Zaid bin Amr?” Mtume alijibu: “Ndiyo. Yeye atafufuliwa kama mwakilishi pekee wa jamaa zake.”
Abdallah bin Jahsh, alibakia mpaka ukaja Uislamu, akasilimu na akahama yeye na mkewe, Ummu Habiba bint Abi Sufyan, kwenda Habasha (Ethiopia), akafia huko baada ya kurtadi kwa kuingia kwenye dini ya unaswara (ukiristo) ... Baadae Mtume akamuo Ummu Habiba.
Uthman bin Huwayrith, alikwenda kwa Kaizari mfalme wa Roma na akawa Mnaswara, huko alipewa cheo kikubwa na akafa Sham. Waraqa aliingia dini ya unaswara (ukristo) na akasoma vitabu vitakatifu vya dini hiyo mpaka akavifahamu barabara. Aliishi Makka, kama mtawa, akiwakataza watu wake kuabudu masanamu.
Warqa alikuwa ni binamu wa Khadija, mke wa Mtume (saw). Uliposhuka wahyi kwa mtume alikwenda naye kwa binamu yake huyo. Akamuuliza, ewe mwana wa ndugu yangu, unaona nini? Mtume alipomwambia akasema: “Huyo ndiye Malaika Mkuu amabye aliwashukia Musa. Natamani ningekuwa kijana, natamani niwe hai wakati watu wako watakapokutoa. Mtume akasema: Hivi watanitoa? Akasema ndio! Hakuna mtu yeyote kabisa aliyekuja na mfano wa jambo lako ila hufanyiwa uadui. Kama nikiwahi siku hiyo nitakusaidia sana!
Waraqa alitamka kwa wahyi wa umbile lake safi. “Ndilo umbile la Mwenyezi Mungu alilowaumbia watu” Kila mtu atakayerejea kwenye umbile lake hili atamwamini Muhammd (s.a.w.) na atamsaidia kwa sababu “Hapana mabadiliko katika uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Hiyo ndiyo dini iliyo sawasawa. Lakini watu wengi hawajui.” (30:30).
Sema, mwiteni Mwenyezi Mungu (Allah) au mwiteni Mwingi wa rehe- ma (Rahman), kwa jina lolote mtakalomwita, Yeye ana majina mazuri.
Washirikina walikuwa na masanamu mbalimbali, wakiyaita kwa majina ambayo Mwenyezi Mungu hakuyateremshia dalii yoyote.
Katika majina hayo hakukuwa na jina la Rahman. Kwa hiyo Mtume alipowalingania kumwabudu Rahman ndio wakasema, ni nani huyo Rahman? “Na wanapoambiwa msujudieni mwingi wa rehema (Rahman) wao husema: Ni nani huyo mwingi wa rehma? Je, tumsujudie unayetuamrisha wewe?” (25:60) Yaani ni wasifu gani huu ambao hauna athari yoyote kwa waungu wetu?
Kauli yake Mwenyezi Mungu: Sema, mwiteni Mwenyezi Mungu (Allah) aumwiteniMwingiwarehema(Rahman)nijawabutoshalaupinzaniwao.
Kwa sababu maana yake ni kwamba majina na matamshi ni nyenzo tu ya ibara. La kuzingatia ni yule anayeitwa. Mwiteni mtakavyo katika majina yake, yote ni mazuri. Kwa sababu yanaleta ibara ya maana nzuri nayo yako sawasawa katika uzuri.
وَلِلَّهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ وَذَرُو{180}
Kwenye Juzuu hiyo ya 9, tumefafanua zaidi katika kifungu cha ‘Je, majina ya Mwenyezi Mungu ni hayo hayo au yana kiasi.’
Wala usiisome jahara Swala yako wala usiifiche, bali tafuta njia baina ya hizo.
Makusudio ya jahara kwenye Swala ni kusoma kwa sauti kubwa na kuficha ni kusoma kwa sauti ndogo. Imam Jafar Asswadiq (a.s.) anasema katika kufasiri Aya hii: “Jahara ni kuinua sauti na kuficha ni kiasi ambacho masikio yako hayasikii. Na soma kisomo kilicho baina yake”
Na sema sifa njema zote ni za ambaye hakujifanyia mtoto wala hana mshirika katika ufalme, wala hana msaidizi kwa sababu ya udhaifu, na mtukuze kwa matukuzo makubwa.
Tunamuhimidi Mwenyezi Mungu kwa utukufu wa hisani yake na ukuu wa buruhani yake. Tunamuepusha na kuwa na mtoto kwa vile anajitosha na kila kitu, si muhitaji; na kwa kuwa mtoto anafanana na baba yake na kumrithi na Yeye hana wa kufanana naye wala wa kumrithi.
Tunamwepusha na mshirika kwa vile hiyo ni dalili ya kushindwa:
وَمَا كَانَ اللَّهُ لِيُعْجِزَهُ مِنْ شَيْءٍ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ ۚ إِنَّهُ كَانَ عَلِيمًا قَدِيرًا {44}
Kila mwenye nguvu mbele yake ni dhaifu na kila mwenye utukufu kwake ni dhalili; ndio maana inakuwa Mwenyezi Mungu ni mkubwa zaidi na Mwenye shani kiasi wasichoweza kusifu wanaosifu na kutekeleza haki yake wenye kushukuru.