read

Sura Ya Kumi Na Nane: Al-Kahf

Imeshuka Makka isipokuwa Aya moja tu; kama ilivyoelezwa katika Majmaul-bayan. Ina Aya 111

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye Kurehemu

الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي أَنْزَلَ عَلَىٰ عَبْدِهِ الْكِتَابَ وَلَمْ يَجْعَلْ لَهُ عِوَجًا ۜ {1}

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu ambaye amemteremshia mja wake Kitabu wala hakukifanya kombo.

قَيِّمًا لِيُنْذِرَ بَأْسًا شَدِيدًا مِنْ لَدُنْهُ وَيُبَشِّرَ الْمُؤْمِنِينَ الَّذِينَ يَعْمَلُونَ الصَّالِحَاتِ أَنَّ لَهُمْ أَجْرًا حَسَنًا {2}

Kimenyooka ili kitoe onyo kutoka kwake na kiwabashirie waumini watendao mema kwamba watapata ujira mzuri.

مَاكِثِينَ فِيهِ أَبَدًا {3}

Wakae humo milele.

وَيُنْذِرَ الَّذِينَ قَالُوا اتَّخَذَ اللَّهُ وَلَدًا {4}

Na kiwaonye wale wanaosema Mwenyezi Mungu amejifanyia mtoto.

مَا لَهُمْ بِهِ مِنْ عِلْمٍ وَلَا لِآبَائِهِمْ ۚ كَبُرَتْ كَلِمَةً تَخْرُجُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ ۚ إِنْ يَقُولُونَ إِلَّا كَذِبًا {5}

Hawana ujuzi wa hili wala baba zao. Ni neno kuu litakalo vinywani mwao, hawasemi ila uongo tu.

فَلَعَلَّكَ بَاخِعٌ نَفْسَكَ عَلَىٰ آثَارِهِمْ إِنْ لَمْ يُؤْمِنُوا بِهَٰذَا الْحَدِيثِ أَسَفًا {6}

Huenda utajiangamiza nafsi yako kwa kusikitikia hali yao ikiwa hawataamini mazungumzo haya.

إِنَّا جَعَلْنَا مَا عَلَى الْأَرْضِ زِينَةً لَهَا لِنَبْلُوَهُمْ أَيُّهُمْ أَحْسَنُ عَمَلًا {7}

Hakika tumevifanya vilivyo katika ardhi kuwa ni pambo lake ili tumjaribu ni nani kati yao mwenye vitendo vizuri zaidi.

وَإِنَّا لَجَاعِلُونَ مَا عَلَيْهَا صَعِيدًا جُرُزًا {8}

Hakika sisi tutavifanya vilivyo juu yake kuwa nchi iliyo kame.