read

Aya 1 – 8: Amemteremshia Kitabu Mja Wake

Maana

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu ambaye amemteremshia mja wake-Muhammad- Kitabu wala hakukifanya kombo, kimenyooka ili kitoe onyo kutoka kwake – Yeye Mungu - na kiwabashirie waumini watendao mema kwamba watapata ujira mzuri; wakae humo milele.

Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameiitaja Qur’an katika Aya zake kadhaa kwa sifa za haki uongozi na nuru. Hapa ameiita kwa sifa za msimamo na kutokuwa kombo na kwamba inambashiria mwema kupata thawabu na neema ya milele na kuwaonya wafisadi kupata adhabu na moto wa milele.

Lengo la yote hayo ni kubainisha kuwa Yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu amiteremsha Qur’an ili twende na mwongozo wake, sio tuhifadhi Aya zake na matamko yake na kusoma tajwid nzuri na tafsiri tu; kama tulivyo.

Mtume (s.a.w.) alisemana sisi ndio tulikuwa tunaambiwa - “Utakuja wakati kwa watu, dini haitabakia isipokuwa maandishi yake, wala Qur’an isipokuwa darasa yake”. Ninaapa kuwa kila ninaposoma makemeo haya kutoka Mtume wa rehema, huwa manywele yananisismka.

Ni makemeo gani yanayotisha kuliko kua miongoni mwa waliokusudiwa na wasifu huu? Sisi hatuna imani isipokuwa jina, wala uislamu isipokuwa maandishi pia hatuna Qur’an isipokuwa kuisoma tu.

Walitia ila Qur’an walioitia na wakaipinga walioipinga tangu mwanzo. Sisi tukaimaini, lakini tunahalifu hukumu zake na mafundisho yake waziwazi. Tofauti yetu sisi na wanaoipinga ni kama ile tofauti baina ya anayesema: Mimi sioni hii kuwa ni haki, lau ningeliijua ni haki basi ningeliifuata na yule asemaye: Bila shaka mimi ninakubali kuwa hii ni haki, lakini sina ulazima nayo wala siiheshimu.

Na kiwaonye wale wanaosema Mwenyezi Mungu amejifanyia mtoto. Hawana ujuzi wa hili wala baba zao.

Maneno haya yanaungana na ya mwanzo: ‘ili kitoe onyo’ onyo la kwanza ni kwa kila mwenye kuasi na kustahiki adhabu na onyo la pili linahusu aliyemnasibisha Mungu kuwa ana mtoto. Ametakata Mwenyezi Mungu na hayo kabisa.

Mara nyingi maungano ya mahsusi kwenye ujumla yanafahamisha kuzidi huyo aliye mahasusi. Mfano kuunganisha Jibril na Malaika au kuanganisha waasi na wale wanaosema Mwenyezi Mungu ana mtoto. Kwa sababu kuse- ma kuwa Mwenyezi Mungu ana mtoto ni uasi zaidi.

Razi anasema kuwa waliosema Mungu ana mtoto ni makundi matatu: “Kundi la kwanza ni makafiri wa kiarabu waliosema kuwa Malaika ni mabinti wa Mungu. Kundi la pili ni manaswara (wakiristo) waliosema kuwa Masih ni mwana wa Mungu. Kundi la tatu ni mayahudi waliosema kuwa Uzayr ni mtoto wa Mungu.”

Makusudio ya kusema: ‘Hawana ujuzi wa hili’ ni wao hawategemei dalili yoyote ya hili; bali dalili iko kinyume. Ama kusema wala baba zao ni kusisitiza shutuma tu; kama kusema: Ni mshenzi mtoto wa mshenzi au ni maluuni mtoto wa maluuni.

Ni neno kuu litakalo vinywani mwao, hawasemi ila uongo tu.

Hakuna kitu kikubwa kuliko uongo. Uwongo mkubwa zaidi ni uongo juu ya Mwenyezi Mungu na kunasibisha uhalali na uharamu kwake bila ya dalili. Na mkubwa kuliko yote ni kumnasibishia mtoto.

Huenda utajiangamiza nafsi yako kwa kusikitikia hali yao ikiwa hawataamini mazungumzo haya.

Makusudio ya mazungumzo hapa ni Qur’an, kwa mafikiano ya wote. Kuisifu Qur’an kuwa ni mazungumzo ni dalili ya kuvunja kauli ya wale wasemao kuwa Qur’an ni ya tangu zama.

Hakuna mwenye shaka kuwa Mtume anamtakia heri kila mtu bila ya kubagua; kama vile wewe uanvyomtakia heri mtoto wako na mimi ninavyomtakia heri mtoto wangu. Mtume alikuwa akihuzunika na kusononeka sana pindi mtu anapofuata njia ya upotevu na maangamizi.

Katika Aya hii Mwenyezi Mungu anamkataza Mtume wake mtukufu kuwa asijitie simanzi, akajiangamiza bure kwa ajili ya wanaopinga uongofu na kufuata haki. Akamwambia usihuzunike:

إِنَّ إِلَيْنَا إِيَابَهُمْ {25}

ثُمَّ إِنَّ عَلَيْنَا حِسَابَهُمْ {26}

“Hakika ni kwetu sisi marejeo yao na hakika ni juu yetu hisabu yao.” (88:25-26).

Hakika tumevifanya vilivyo katika ardhi kuwa ni pambo lake ili tum- jaribu ni nani kati yao mwenye vitendo vizuri zaidi.

Vipambo hapa vinakusanya cheo mali na watoto na kila lile wanalokufia watu na kuvurugana kwa ajili yake. Ghururi hizi ndizo zinazomtambulisha mwema na muovu.
Mwenye kukinai na fungu lake na akaishi kwa jasho lake basi huyo ni mwema aliye karimu.

Na mwenye kujaribu kufanya ulanguzi na kuishi kwa jasho la wengine; hata kama ni kwa kuanzisha vita na kuleta fitna, basi huyo ni muovu mwenye dhambi.

Maana ya majribio ya Mwenyezi Mungu kwa watu katika vipambo vya ardhi ni kuzidhihirisha sababu zake na vitendo vyao ambavyo vitastahiki thawabu au adhabu. Tumezungumzia hilo kwa ufafanuzi Juz. 7 (5:94) kifungu cha ‘Maana ya kujaribu kwa Mwenyezi Mungu’.

Hakika sisi tutavifanya vilivyo juu yake kuwa nchi iliyo kame.

Juuyakenijuuyaardhi.Yaanikilakilichojuuyaardhikitatowekaibaki tupu. Mwema ni yule atakyemtii Mwenyezi Mungu na muovu ni yule atakayetii hawaa yake.

أَمْ حَسِبْتَ أَنَّ أَصْحَابَ الْكَهْفِ وَالرَّقِيمِ كَانُوا مِنْ آيَاتِنَا عَجَبًا {9}

Kwani unadhani kwamba watu wa pango na maandishi walikuwa ni ajabu miongoni mwa ishara zetu?

إِذْ أَوَى الْفِتْيَةُ إِلَى الْكَهْفِ فَقَالُوا رَبَّنَا آتِنَا مِنْ لَدُنْكَ رَحْمَةً وَهَيِّئْ لَنَا مِنْ أَمْرِنَا رَشَدًا {10}

Pale vijana walipokimbilia kwenye pango wakasema: Mola wetu! Tupe rehema itokayo kwako na tutengenezee uongofu katika jambo letu.

فَضَرَبْنَا عَلَىٰ آذَانِهِمْ فِي الْكَهْفِ سِنِينَ عَدَدًا {11}

Basi tukayaziba masikio yao pangoni kwa miaka kadhaa.

ثُمَّ بَعَثْنَاهُمْ لِنَعْلَمَ أَيُّ الْحِزْبَيْنِ أَحْصَىٰ لِمَا لَبِثُوا أَمَدًا {12}

Kisha tukawazindua ili tujue ni lipi kati ya makundi mawili lililohisabu sawa muda waliokaa.