Aya 9 – 12: Watu Wa Pango
Utangulizi
Tutafisiri Aya zinazofungamana na watu wa pango (As-habulkahf) kutokana na dhahiri ya zinavyofahamisha Aya au kutokana na dalili ya mazingira; kwa mfano kusema kiulize kijiji kwa maana ya waulize watu wa kijiji. Tutaachana na rejea au ngano nyenginezo. Kwani tumesema mara nyingi kwamba matukio ya historia na mfano wake hayathibiti ila kwa nukuu ya Qur’an au kwa Hadith iliyopokewa kwa njia nyingi (Mutawatir) Na kwamba Hadith iliyopokewa kwa njia moja (Ahad) si kitu, hata kama yakisihi mategemezi yake; isipokuwa katika hukumu ya sharia.
Maana
Kwani unadhani kwamba watu wa pango na maandishi walikuwa ni ajabu miongoni mwa ishara zetu?
Makusudio ya maandishi hapa ni ubao ulioandikwa majina ya watu wa pango. La kushangaza ni kauli ya anayesema kuwa neno raqim, tuliolifasiri kwa maana ya maandishi, ni jina la mbwa wao; na hali inajulikana na ni maarufu kuwa jina la mbwa wao ni Qitmir.
Vyovyote iwavyo ni kuwa kisa cha watu wa pango kilielezwa katika vitabu vya kale na waliokisoma au kukisikia wakashangaa kuwa itakuwaje watu walale usingizi mrefu wa miaka kiasi hicho na wabaki bila ya chakula?
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akamwambia kila anayeshangazwa na kisa hiki kuwa usistaajabu na hayo, kila ishara ya Mwenyezi Mungu ni ya ajabu. Yule aliyewafanya watu wa pango ndiye yuleyule aliyeufanya ulimwengu na vilivyomo. Kwa hiyo kwake kuwabakisha vijana usingizini kwa mda mrefu kisha kuwaamsha ni jambo rahisi sana, lakini watu wengi hawajui.
Pale vijana walipokimbilia kwenye pango wakasema: Mola wetu! Tupe rehema itokayo kwako na tutengenezee uongofu katika jambo letu.
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anaishria katika Aya hii na nyingine mbili zinazofuatia kuhusu kisa cha watu wa pango kwa ujumla, kisha anaanza kufafanua. Katika Aya hii tuliyonayo anasema kuwa hapo zamani za kale kulikuwa na vijana walioacha kila kitu katika maisha haya na wakakimbilia pangoni; wakamtaka Mwenyezi Mungu awahurumie na awatengenezee mambo yao wakiwa pangoni.
Hakudokeza Mwenyezi Mungu, katika Aya, hii sababu iliyofanya vijana hao waache kila kitu na kujiingiza pangoni, huku wakimtaka Mwenyezi Mungu awaangalilie mambo yao. Tunavyofahamu, kutokana na tafsiri ya mazingira na inavyoashiria Aya inayofuatia, ni kuwa vijana waliongozwa na maumbile yao salama kuwa watu wao wako katika upotevu wa kuabudu masanamu na kwamba wao walikataa kuabudu yale wanayoaabudu wazazi wao.
Kwa hiyo kama kawaida ya wenye siasa kali walitaka kwaua vijana au kuwafitini na dini yao. Vijana walipokosa njia zote waliamua kukimbilia pangoni na kumwambia Mwenyezi Mungu kuwa tumeudhiwa kiasi hiki unachoona nasi tunahitaji sana msaada wako na huruma zako. tunaomba msaada kwako wewe tu, si kwa mwengine.
Basi tukayaziba masikio yao pangoni kwa miaka kadhaa.
Yaani tuliwalaza usingizi ambao hawawezi kusikia chochote kwa muda wa miaka kadhaa. Itaelezwa idadi ya miaka hiyo kwenye Aya ya 25.
Kisha tukawazindua yaani tuliwaamsha ili tujue ni lipi kati ya makundi mawili lililohisabu sawa muda waliokaa.
Watu walijua kisa cha watu wa pango wakiwa bado kwenye usingizi wao. Habari zikaenea na watu wakatofautiana katika muda wa kukaa kwao. Kuna waliosema muda mchache na waliosema mwingi. Mwenyezi Mungu akawainua watu wa pango. Ili makundi mawili yajue muda waliokaa waweze kuamini awazidishie imani yao kuhusu uweza wa Mwenyezi Mungu wa kuwafufua wafu. Kusema kwake Mwenyezi Mungu “ili tujue’ maana yake ni ili idhihiri elimu yetu kwa watu kiasi cha muda waliokaaa. Umepita mfano wake katika Juz 4. (3:140).
Unawezakuuliza:Watuwalijuajemudawaonahaliwenyewewalipoamka hata hawakuujua; bali walianza kuulizana, wengine wakasema tumekaa siku moja tu au nusu siku?
Jibu: Watu walijua muda wao kutokana na pesa walizokuwa nazo. Mmoja wao alikwenda mjini kununua chakula na watu wa mji walipoona ile pesa walijua ilikuwa ni wakati wa mmoja wa wafalme waliopita. Utakuja ufafanuzi wake kwenye Aya 19.
نَحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ نَبَأَهُمْ بِالْحَقِّ ۚ إِنَّهُمْ فِتْيَةٌ آمَنُوا بِرَبِّهِمْ وَزِدْنَاهُمْ هُدًى {13}
وَرَبَطْنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ إِذْ قَامُوا فَقَالُوا رَبُّنَا رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ لَنْ نَدْعُوَ مِنْ دُونِهِ إِلَٰهًا ۖ لَقَدْ قُلْنَا إِذًا شَطَطًا {14}
هَٰؤُلَاءِ قَوْمُنَا اتَّخَذُوا مِنْ دُونِهِ آلِهَةً ۖ لَوْلَا يَأْتُونَ عَلَيْهِمْ بِسُلْطَانٍ بَيِّنٍ ۖ فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّهِ كَذِبًا {15}
وَإِذِ اعْتَزَلْتُمُوهُمْ وَمَا يَعْبُدُونَ إِلَّا اللَّهَ فَأْوُوا إِلَى الْكَهْفِ يَنْشُرْ لَكُمْ رَبُّكُمْ مِنْ رَحْمَتِهِ وَيُهَيِّئْ لَكُمْ مِنْ أَمْرِكُمْ مِرْفَقًا {16}
وَتَرَى الشَّمْسَ إِذَا طَلَعَتْ تَزَاوَرُ عَنْ كَهْفِهِمْ ذَاتَ الْيَمِينِ وَإِذَا غَرَبَتْ تَقْرِضُهُمْ ذَاتَ الشِّمَالِ وَهُمْ فِي فَجْوَةٍ مِنْهُ ۚ ذَٰلِكَ مِنْ آيَاتِ اللَّهِ ۗ مَنْ يَهْدِ اللَّهُ فَهُوَ الْمُهْتَدِ ۖ وَمَنْ يُضْلِلْ فَلَنْ تَجِدَ لَهُ وَلِيًّا مُرْشِدًا {17}
وَتَحْسَبُهُمْ أَيْقَاظًا وَهُمْ رُقُودٌ ۚ وَنُقَلِّبُهُمْ ذَاتَ الْيَمِينِ وَذَاتَ الشِّمَالِ ۖ وَكَلْبُهُمْ بَاسِطٌ ذِرَاعَيْهِ بِالْوَصِيدِ ۚ لَوِ اطَّلَعْتَ عَلَيْهِمْ لَوَلَّيْتَ مِنْهُمْ فِرَارًا وَلَمُلِئْتَ مِنْهُمْ رُعْبًا {18}