Aya 13-18: Habari Zao Za Kweli
Maana
Sisi tunakusimulia habari zao kwa haki.
Kabla ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.), watu walikuwa wakielezana habari za kisa cha watu wa pango. Kikaandikwa kwenye vitabu na pia kwenye mashairi. Miongoni mwa kaswida ya Umayya bin Abu Swalat:
Hakuna isipokuwa raqimu aliye jirani watu na mbwa wao wamelala pangoni.
Mtume alikuwa akiwataka watu wamsomee shairi la Bin Abu swalat. Basi husikilza kisha anasema, huyu mtu aliamini kwa ulimi wake na akakufuru kwa moyo wake.
Watuwalitungaviganokuhusuwatuwapango;kamawalivyotungakwa watu wengine waliopita. Ndio maana Mwenyezi Mungu akamwabia Mtume wake: ‘Sisi tunakusimulia habari zao kwa haki’ amabazo hazina shaka. Na ni nani aliye mkweli zaidi wa mazungumzo kumshinda Mwenyezi Mungu?
Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kuelezea kisa chao kwa ujumla katika Aya iliyotangulia, sasa anaanza kukichambua katika Aya zinazofuatia.
Kisa hiki kinagawanyika mafungu mane: Kwanza, kuelekea watu wa pango kwa Mwenyezi Mungu. Pili, hali yao na ya watu wao pamoja na kukimbia kwao. Tatu, kuamka kwao kutoka kwenye usingizi wao mazito. Nne, kufa kwao na kujengewa. Aya tuliyo nayo imechukua sehemu ya kwanza na ya pili na Aya zinazofuatia zimechukua sehemu mbili za mwisho.
Sehemu Ya Kwanza:
Hakika hao ni vijana waliomwamini Mola wao na akawazidisha uon- gofu na tukazitia nguvu nyoyo zao.
Katika vijana wako wale ambao wamekomaa kiakili na kifikra; sawa na walivyokomaa kimwili. Aina hii ya vijana, ingawaje ni nadra kupatikana, lakini wapo, miongoni mwao ni watu wa pango. Walikuwa wakiishi katika jamii iliyojaa ufisadi na kuabudu masanamu, lakini wao walikataa na wakajiongoza kwa muwongozo wa usafi wa maumbile yao. Wakajiuliza, vipi mawe yanaweza kuwa miungu? Vipi wapenda anasa wanahodhi utajiri na nguvu na kuzitumia kwa wanyonge?
Shaka hii na maswali haya yaliwapeleka vijana hao kwenye itikadi ya tawhid na ufufuo. Mwenyezi Mungu alipoona ukweli wao wa nia na ikhlasi yao, aliwapa uthabiti katika imani yao na busara katika mambo yao.
Waliposimama.
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hakubainisha walisimama wapi. Kwa hiyo wafasiri wametofautiana. Kuna waliosema kuwa walisimama mbele ya mfalme wao Decianus aliyejifanya jabari. Wengine wamesema kuwa walisimama kutoka usingizini.
Sio mbali kuwa makusudio ya kusimama kwao ni kutoka kwao kwenye ada ya watu wao na kuasi ushirikina na ufisadi. Hii ndio nembo ya mapinduzi yao.
Wakasema: Mola wetu ni Mola wa mbingu na ardhi. Hatutamuomba Mungu mwingine badala yake. Hakika tutakuwa tumesema jambo la kuvuka mpaka. Hawa watu wetu wamefanya waungu badala yake. Kwa nini hawawaletei dalili bayana? Basi ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule amzuliaye Mwenyezi Mungu uongo?
Vijana waliamini Mungu mmoja aliye peke yake. Wakatangaza imani yao kwa watu na wakasema kuwa mataghuti katika watu wao wanamzulia Mwenyezi Mungu uongo na akili zao pia; kwa sababu wameyapa masanamu sifa ya Mungu huku wakijua kuwa hayadhuru wala kunufaisha. Wanawazuga wapumbavu kwamba hayo masanamu ndiyo yaliyowachgua wao na kuwapa nguvu juu ya watu. Na kwamba atakayewakhalifu malipo yake ni kuadhibiwa na kuuawa.
Ni kwa madai haya ndio mataghuti walitaka kuwauwa vijana hao, si kwa lolote ila ni kwa kuwa wao wamemwamini Mwenyezi Mungu na kuayakana masanamu kwa kuwaweka juu mataghuti na kuwakandamiza wanyonge.
Nilizinduka wakati nikiandika maneno haya, kwenye tafsiri ya mfano hai wa kushangaza uliojitokeza katika miji yetu. Nao ni hili jeshi kubwa la masheikh wenye vilemba ambao hawana usheikh hata chembe. Nimegundua kuwa kuna mkono mchafu unaofanya kazi kwa siri. Wanatenga mali za kuwalipa vibaraka na za kuwaingiza kwenye safu ya maulama na kuwavisha vilemba. Wanafanya hivyo kwa ajili ya kulinda masilahi ya mataghuti na wanyonyaji kwa jina la dini; sawa na walivyoyapa masananamu sifa ya Mungu ili wawambie watu mazuzu kuwa hayo masanamu ndiyo yaliyowateua wao kuwa viongozi wao na yakawapa wao mali na kuwanyima wanyonge.
Sehemu Ya Pili
Na mkijitenga nao na vile wanavyoviabudu badala ya Mwenyezi mungu, basi kimbilieni pangoni, atawafungulia Mola wenu rehema yake na atawafanyia wepesi mambo yenu.
Mataghuti waliwabana vijana waumini na wakajaribu kuwatia mtihani na dini yao. Wakaambiana kuwa hatutapona na watu madhalimu isipokuwa tuwakimbie wao na yale wanayoyaabudu na kuyafanya.
Baada ya kubadilishana mawazo na kushauriana waliafikiana wakimbilie Pangoni. Kwani walikuwa hawana pengine zaidi ya hapo. Wakaingia Pangoni na wakamwachia Mungu jambo lao; hata kama watakufa kwa njaa na kiu.
Hivi ndivyo anavyokuwa mumin wa kweli, anabakia na imani yake akiitekeleza kwa hamasa na uthabiti bila ya kujali tatizo litakalomtokea. Mtu akifikia hali hii, basi Mwenyezi Mungu anakuwa pamoja naye popote alipo na atampa faraja haraka sana; hata kama wa mbinguni na ardhini watamkalia vibaya; kama ilivyokuwa kwa watu wa pango, pale Mungu alipowachagulia raha na amani na kuwa huru na dhiki ya maisha. Akawapa usingizi usioweza kuamshwa wala kuhofia chochote.
Na unaliona jua linapochomoza linaelemea kuumeni mwao mbali na pango lao; na lipokuchwa linawahepa kushotoni na wao wamo katika uwazi wake.
Yaani uwazi wa hilo Pango. Lilikuwa ni kubwa lenye uwazi wa kupitisha hewa safi na mwanga wa jua. Miili yao haiweza kufikiwa na jua si wakati wa mawiyo wala machweo. Kwa sababu walikuwa kwenye sehemu ambayo haifikiwi na mwanga wa jua au kwa kuwa Mwenyezi Mungu alikuwa akiliepusha kwa kudura yake.
Hayo ni katika ishara zake.
Hayo ni pamoja na kutofikiwa na jua, kana kwamba ilikusudiwa kuwa hivyo. Pia kuwekwa katika hali ambayo si kuwa macho, kiasi ambacho wakati ulipita bila ya kujua; wala si mauti kwa kuwa na harakati na pumzi. Hakuna tafsiri ya haya isipokuwa uweza wa Mwenyezi Mungu na hekima yake.
Ambaye Mwenyezi Mungu anamuongoza basi yeye ndiye aliyeongoka na anayempoteza hutampatia mlinzi (wala) mwongozi.
Makusudio ya ambaye Mwenyezi Mungu anamuongoza ni watu wa pango na anayempoteza ni wale waliokusudia kuwatesa. Angalia Juz. 9 (7: 178).
Utawadhania wako macho na hali wamelala na tunawageuza kuume na kushoto na mbwa wao amenyoosha miguu yake ya mbele kizingitini.
Macho yao yalikuwa wazi kama vile yanaangalia mbele na damu inatembea mishipani, wanageuka upande huu na huo. Mbwa wao akiwa pembeni au mlangoni mwa pango kama mlinzi.
Lau ungeliwatokea bila shaka ungeligeuka kuwakimbia na ungelijazwa hofu.
Kwa sababu wako katika hali ya kushangaza isiyokuwa na mfano.
وَكَذَٰلِكَ بَعَثْنَاهُمْ لِيَتَسَاءَلُوا بَيْنَهُمْ ۚ قَالَ قَائِلٌ مِنْهُمْ كَمْ لَبِثْتُمْ ۖ قَالُوا لَبِثْنَا يَوْمًا أَوْ بَعْضَ يَوْمٍ ۚ قَالُوا رَبُّكُمْ أَعْلَمُ بِمَا لَبِثْتُمْ فَابْعَثُوا أَحَدَكُمْ بِوَرِقِكُمْ هَٰذِهِ إِلَى الْمَدِينَةِ فَلْيَنْظُرْ أَيُّهَا أَزْكَىٰ طَعَامًا فَلْيَأْتِكُمْ بِرِزْقٍ مِنْهُ وَلْيَتَلَطَّفْ وَلَا يُشْعِرَنَّ بِكُمْ أَحَدًا {19}
إِنَّهُمْ إِنْ يَظْهَرُوا عَلَيْكُمْ يَرْجُمُوكُمْ أَوْ يُعِيدُوكُمْ فِي مِلَّتِهِمْ وَلَنْ تُفْلِحُوا إِذًا أَبَدًا {20}
وَكَذَٰلِكَ أَعْثَرْنَا عَلَيْهِمْ لِيَعْلَمُوا أَنَّ وَعْدَ اللَّهِ حَقٌّ وَأَنَّ السَّاعَةَ لَا رَيْبَ فِيهَا إِذْ يَتَنَازَعُونَ بَيْنَهُمْ أَمْرَهُمْ ۖ فَقَالُوا ابْنُوا عَلَيْهِمْ بُنْيَانًا ۖ رَبُّهُمْ أَعْلَمُ بِهِمْ ۚ قَالَ الَّذِينَ غَلَبُوا عَلَىٰ أَمْرِهِمْ لَنَتَّخِذَنَّ عَلَيْهِمْ مَسْجِدًا {21}
سَيَقُولُونَ ثَلَاثَةٌ رَابِعُهُمْ كَلْبُهُمْ وَيَقُولُونَ خَمْسَةٌ سَادِسُهُمْ كَلْبُهُمْ رَجْمًا بِالْغَيْبِ ۖ وَيَقُولُونَ سَبْعَةٌ وَثَامِنُهُمْ كَلْبُهُمْ ۚ قُلْ رَبِّي أَعْلَمُ بِعِدَّتِهِمْ مَا يَعْلَمُهُمْ إِلَّا قَلِيلٌ ۗ فَلَا تُمَارِ فِيهِمْ إِلَّا مِرَاءً ظَاهِرًا وَلَا تَسْتَفْتِ فِيهِمْ مِنْهُمْ أَحَدًا {22}