read

Aya 30 – 31: Ujira Wa Watendao Mema Haupotei

Maana

Hakika wale ambao wameamini na wakatenda mema, hakika sisi hatupotezi ujira wa anayefanya mazuri.

Baada ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kuwataja madhalimu na adhabu yao, sasa anataja wema na malipo yao. Akabainisha aina hii ya thawabu kwa kauli yake:

Hao wana bustani za milele zinazopita mito chini yake, watavaa nguo za kijani za hariri na atlasi. Huku wakiegemea juu ya makochi. Ni malipo bora yalioje na mahali pazuri palioje pa kupumzika.

Katika Aya nyingine Mwenyezi Mungu anasema:

وَفِيهَا مَا تَشْتَهِيهِ الْأَنْفُسُ وَتَلَذُّ الْأَعْيُنُ ۖ {71}

“Na humo vitakuwemo ambavyo nafsi zinavipenda na macho yanavifurahia” (43:71).

Imam Ali (a.s.) anasema: “Kila neema isiyokuwa Pepo ni ya kudharauliwa na kila balaa isiyokuwa moto ni raha.” Umepita mfano wake katika Aya nyingi ikiwemo Juz. 1 (2: 82), Juz.4 (3:171) na Juz.5 (4:57).

Kauli ya kushangaza ni ile ya badhi ya masufi, kwamba makusudio ya kivazi ni tawhid, nguo za kijani ni sifa zinazoleta furaha, hariri ni vipawa, atlasi ni maadili na makochi ni majina ya Mwenyezi Mungu.

Wala hakuna ujeuri mkubwa kwa Mungu kuliko kutafsiri makusudio yake kwa njozi na mawazo au kwa hawaa na malengo mengine.

وَاضْرِبْ لَهُمْ مَثَلًا رَجُلَيْنِ جَعَلْنَا لِأَحَدِهِمَا جَنَّتَيْنِ مِنْ أَعْنَابٍ وَحَفَفْنَاهُمَا بِنَخْلٍ وَجَعَلْنَا بَيْنَهُمَا زَرْعًا {32}

Na wapigie mfano wa watu wawili: mmoja wao tulimjalia vitalu viwili vya mizabibu na tukavizunguushia mitende na kati yake tukajaalia mimea ya nafaka.

كِلْتَا الْجَنَّتَيْنِ آتَتْ أُكُلَهَا وَلَمْ تَظْلِمْ مِنْهُ شَيْئًا ۚ وَفَجَّرْنَا خِلَالَهُمَا نَهَرًا {33}

Hivyo vitalu viwili vikitoa mazao yake, wala hapana kitu katika hivyo kilichotindika. Na ndani yake tukapasua mito.

وَكَانَ لَهُ ثَمَرٌ فَقَالَ لِصَاحِبِهِ وَهُوَ يُحَاوِرُهُ أَنَا أَكْثَرُ مِنْكَ مَالًا وَأَعَزُّ نَفَرًا {34}

Naye alikuwa na mazao. Basi akamwambia mwenzake naye akibishana naye: Mimi nimekushinda kwa mali na nguvu za watu.

وَدَخَلَ جَنَّتَهُ وَهُوَ ظَالِمٌ لِنَفْسِهِ قَالَ مَا أَظُنُّ أَنْ تَبِيدَ هَٰذِهِ أَبَدًا {35}

Akaingia kitaluni kwake, naye ameidhulumu nafsi yake, akasema: Sidhani kuwa haya yataharibika milele.

وَمَا أَظُنُّ السَّاعَةَ قَائِمَةً وَلَئِنْ رُدِدْتُ إِلَىٰ رَبِّي لَأَجِدَنَّ خَيْرًا مِنْهَا مُنْقَلَبًا {36}

Wala sidhani kuwa hiyo saa (ya Kiyama) itatokea. Na kama nitarudishwa kwa Mola wangu bila shaka nitapata marejeo bora zaidi kuliko haya.

قَالَ لَهُ صَاحِبُهُ وَهُوَ يُحَاوِرُهُ أَكَفَرْتَ بِالَّذِي خَلَقَكَ مِنْ تُرَابٍ ثُمَّ مِنْ نُطْفَةٍ ثُمَّ سَوَّاكَ رَجُلًا {37}

Mwenzake akamwambia kwa kubishana naye: Je, umemkufuru ambaye amekuumba kutokana na udongo, tena kutokana na tone la manii, kisha akakufanya kuwa mtu kamili?

لَٰكِنَّا هُوَ اللَّهُ رَبِّي وَلَا أُشْرِكُ بِرَبِّي أَحَدًا {38}

Lakini Yeye Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu, wala si mshirikishi na yeyote.

وَلَوْلَا إِذْ دَخَلْتَ جَنَّتَكَ قُلْتَ مَا شَاءَ اللَّهُ لَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّهِ ۚ إِنْ تَرَنِ أَنَا أَقَلَّ مِنْكَ مَالًا وَوَلَدًا {39}

Na lau ulipoingi kitaluni kwako ungelisema, alitakalo Mwenyezi Mungu huwa (mashaallah!), hapana nguvu ila kwa Mwenyezi Mungu. Ikiwa unaniona mimi nina mali kidogo na watoto kuliko wewe.

فَعَسَىٰ رَبِّي أَنْ يُؤْتِيَنِ خَيْرًا مِنْ جَنَّتِكَ وَيُرْسِلَ عَلَيْهَا حُسْبَانًا مِنَ السَّمَاءِ فَتُصْبِحَ صَعِيدًا زَلَقًا {40}

Basi huenda Mwenyezi Mungu akanipa kilicho bora kuliko kitalu chako na kukipelekea maafa kutoka mbinguni na kugeuka ardhi tupu inayoteleza.

أَوْ يُصْبِحَ مَاؤُهَا غَوْرًا فَلَنْ تَسْتَطِيعَ لَهُ طَلَبًا {41}

Au maji yake yadidimie usiweze kuyagundua.

وَأُحِيطَ بِثَمَرِهِ فَأَصْبَحَ يُقَلِّبُ كَفَّيْهِ عَلَىٰ مَا أَنْفَقَ فِيهَا وَهِيَ خَاوِيَةٌ عَلَىٰ عُرُوشِهَا وَيَقُولُ يَا لَيْتَنِي لَمْ أُشْرِكْ بِرَبِّي أَحَدًا {42}

Yakaangamizwa matunda, akabaki anapinduapindua viganja vyake, kwa vile alivy- oyagharimia, nayo imeanguka juu ya chanja zake. Akawa anasema: Laiti nisingelimshirikisha Mola wangu na yoyote.

وَلَمْ تَكُنْ لَهُ فِئَةٌ يَنْصُرُونَهُ مِنْ دُونِ اللَّهِ وَمَا كَانَ مُنْتَصِرًا {43}

Wala hakuwa na kundi la kumsadia kinyume na Mwenyezi Mungu wala mwenyewe hakuweza kujisaidia.

هُنَالِكَ الْوَلَايَةُ لِلَّهِ الْحَقِّ ۚ هُوَ خَيْرٌ ثَوَابًا وَخَيْرٌ عُقْبًا {44}

Huko usaidizi ni wa Mwenyezi Mungu, Mkweli. Yeye ni Mbora kwa malipo na mbora wa matokeo.