Aya 32 – 44: Baina Ya Kafiri Tajiri Na Mumin Fukara.
Muhtasari Wa Kisa
Tulipofasiri Aya 27 ya Sura hii tulitaja kuwa vigogo wa kishirikina walitoa sharti la kumwamini kwao Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) kuwa awafukuze mafukara au awatengee vikao vyao ili wasichanganyike na mafakura, kwa vile wao ni mabwana na viongozi na watu wengine ni watumwa wao tu.
Aya tulizo nazo sasa zinaleta picha ya matajiri wenye kiburi, kwa mtu mmoja tajiri mwenye mali na mashamba na picha ya mafukara waumini, kwa mtu mmoja fukara asiye na chochote, lakini anajitukuza kwa maadili yake na tajiri anajitukuza kwa mali yake. Yanapita majibizano baina yao yanayowakilisha mvutano baina ya haki na batili. Hatimaye haki inashinda na batili inaanguka. Amesema kweli mwenye hekima aliyesema: “Mwenye kupigana na haki itampiga mweleka”
Kwaufupi,maanayaAyahizoni:Yuleanayejitukuzakwamaliyake, anamiliki mashamba mawili makubwa yenye miche ya ngano na nafaka nyinginezo. Pia mna miti mingi ya mitende na mizabibu. Mashamba yote mawili yana chemchem ya maji; mavuno yake ni mazuri na kamili. Ama yule anayejitukuza kwa maadili yake, hana kitu chochote.
Mwenye mashamba akamwambia yule fukara kwa kujisifu na kujinaki: Mimi nimekushinda na kila kitu – mali na jaha. Angalia mimea, miti, matunda na mito ya maji niliyo nayo. Hii ndio milki ya kudumu itakayoku- ja wafaa watoto na wajukuu; sio pepo mnayodai nyinyi masikini. Hivi baada ya mauti kweli kuna pepo na moto? Kama itakuwa ni kweli basi hadhi yangu huko itakuwa kubwa kuliko hapa duniani. Kwa sababu aliye tajiri hapa huko pia atakuwa tajiri .
Yule mumin akamjibu kwa kumjadili na kumlaumu: Hivi unasema haya kwa kumbughudhi na kumkufuru ambaye amekufanya uwe mtu? Umesahau asili yako? Wewe si umetokana na Adamu na Adam akatokana na mchanga? Hukuwa wewe ni tone la manii? Mimi mwenzako ninamwamini Mwenyezi Mungu na ninampwekesha, ninamsifu kwa kuniongoza kwenye njia yake na radhi zake. Kama ungekuwa na busara basi ungelimnyenyekea Mwenyezi Mungu na kumshukuru badala ya kujitia ujuvi kwa dhambi. Ni lipi liliokufanya ujiaminishe na mambo ya kushtukiza ya ghafla? Mungu akiwapa muda waasi kwa huruma zake huwa amewapa muda wa hasira zake na nakama yake.
Kabla ya hata kumaliza maneno yake yule mumin, mara miti ikaanza kuanguka, mito ikakauka, mimea ikateketea na kila kitu shambani kikaharibika. Mwenye shamba akasema: “Sikufikira kabisa itaharibika hii.” Baada ya kuona alivyofanya Mwenyezi Mungu na kukata tamaa ya mimea yake na miti yake alisema kwa masikitiko: “Laitani nisingemshirikisha Mola wangu na yeyote.” Lakini wapi! Hivi sasa na hali hapo mwanzo umemuasi na ukawa katika wafisadi?
Huundiomuhtasariwakisa.Namakusudioyakisahichonikuwamtu aamini kwa kauli na vitendo kuwa hakuna hila wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Mwenyezi Mungu mmoja mwenye kushinda. Na kwamba Yeye ambaye imetukuka hekima yake saa yoyote anayotaka anaweza kumgeuza mtukufu kuwa dhalili na dhalili kuwa mtukufu. Vilevile tajiri kuwa fukara na fukara kuwa tajiri na afya kuwa ugonjwa na maumivu na kinyume chake. Vile vile mtu aamini kuwa milki ya mwenye kuumbwa si chochote kadiri itakavyokuwa ila akiibadilisha katika kazi za kheri.
Baada ya muhtasari huu sasa tuingilie ufafanuzi wa na tafsiri ya Aya ingawaje nyingi ziko wazi zisizohitaji ufafanuzi.
Maana
Na wapigie mfano wa watu wawili: mmoja wao tulimjalia vitalu viwili vya mizabibu na tukavizunguushia mitende na kati yake tukajaalia mimea ya nafaka. Hivyo vitalu viwili vikitoa mazao yake, wala hapana kitu katika hivyo kilichotindika. Na ndani yake tukapasua mito.
Anaambiwa Muhammad (s.a.w.) awambie washirikina waliosema kuwa awafukuze mafukara au amwambie kila mpenda makuu mwenye kiburi. Makusudio ya watu wawili ni tajiri na fukara ambao walikuwa na majibizano.
Ni maarufu Qur’an kuwa mara nyingi inaleta mifano ya fikra na misingi ya kiujmla na kufananisha na vitu vyenye kuhisiwa; kama kufananisha imani na nuru na ukafiri na giza. Pia mara nyingine inafananisha chenye kuhisiwa na chenye kuhisiwa kingine kilichowazi zaidi na kilicho na ubainifu zaidi; kama kufananisha mwenye kurtadi na mbwa mwenye kuhema kwa nguvu.
Lengo la yote hayo ni kufafanua na kuweka wazi, kuongezea mazingatio na mawaidha:
وَعَادًا وَثَمُودَ وَأَصْحَابَ الرَّسِّ وَقُرُونًا بَيْنَ ذَٰلِكَ كَثِيرًا {38}
وَكُلًّا ضَرَبْنَا لَهُ الْأَمْثَالَ ۖ وَكُلًّا تَبَّرْنَا تَتْبِيرًا {39}
Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hapa amefananisha hali ya mataghuti wapenda makuu wenye kiburi na mtu mmoa kafiri mwenye kiburi mjinga aliye na vitalu viwiwili ambavyo ndani yake mna mto, mimea ya nafaka na miti inayobeba matunda bora ya wakati huo, ambayo ni tende na zabibu.
Mimea yote inatoa mazao kwa wakati wake kwa ukamilifu. Na akamfananisha mumin na mtu mmoja mnyeneykevu mwenye maarifa, lakini hana chochote ni fukara. Yakatokea majibizano baina ya wawili hao; kama ifuatavyo:-
Basi akmwambia mwenzake naye akibishana naye.
Aliyesema ni yule tajiri mwenye kiburi kumwambia mwenzake mumin mwenye adabu
Mimi nimekushinda kwa mali na nguvu za watu.
Aliona kuwa mali na jaha ndio kipimo cha utukufu, lakini imani na ikhlasi ni maneno matupu tu yasiyokuwa na maana. Hii ndio mantiki ya mafasiki na wovu, tangu zamani hadi leo. Thamani ya mtu kwao ni kile anachokimiliki, sio matendo mema wala elimu nzuri.
Mali ndiyo inayosababisha matatizo ya binadamu. Ndio kichocheo cha kwanza cha fitina ya silaha za maangamizi na kutumia mamilioni ya walalahoi kutengenezea silaha hizo. Wanyonyaji wanaiba mali ya wananchi na kuigeuza mabomu na maroketi kisha wayatupe kwa hao hao wananchi waliowanyanganya riziki zao na maliasili zao.
Akaingia kitaluni kwake, naye ameidhulumu nafsi yake kwa sababu aliyaitikia matamanio yake akaitia hatarini nafsi yake; sawa na anayemkubalia mwanawe mambo yatakayomdhuru na kumwangamiza.
Akasema: Sidhani kuwa haya yataharibika milele.
Razi anasema: “Vipi alisema kuwa sidhani kuwa haya yataharibika milele pamoja na kuwa hisia zinafahamisha kuwa dunia si yenye kubakia? Tunasema: alikusudia kuwa havitaharibika katika uhai wake”
Jibu sahihi ni kuwa ujinga na ghururi zilimpofusha mwenye shamba na kila kitu hata na vitu waziwazi na vyenye kuhisiwa. Anasema Mtukufu wa wasemao: “Wana nyonyo, lakini hawafahamu kwazo, na wana macho, lakini hawaoni kwayo, na wanayo masikio, lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama wanyama bali wao ni wapotevu zaidi. Hao ndio walioghafilika.” Juz. 9 (7:179).
Wala sidhani kuwa hiyo saa (ya Kiyama) itatokea.
Dhana hii haitegemei chochote isipokuwa majivuno ghururi na mambo ya kuwazia tu, kwamba neema yake ni ya milele haitaisha. Hii ndio tafsiri ya mataghuti wajivuni wanaokana hisabu na ufufuo.
Na kama nikirudishwa kwa Mola wangu bila shaka nitapata marejeo bora zaidi kuliko haya.
Kwa fikra yake anaona kuwa wapenda makuu huko pia wana nafasi. Anakisia ya ghaibu kwa ya sasa. Hajui kwamba uokovu kesho ni wa wamchao Mungu, sio mataghuti na wajivuni:
مَا أَغْنَىٰ عَنِّي مَالِيَهْ ۜ {28}
هَلَكَ عَنِّي سُلْطَانِيَهْ {29}
Mwenzake akamwambia kwa kubishana naye: Je, umemkufuru ambaye amekuumba kutokana na udongo, tena kutokana na tone la manii, kisha akakufanya mtu kamili?
Mumini alimwambia kafiri kwa kumlaumu, kuwa unamkana aliyekuumba na dalili zake ziko wazi kwako? Umepata vipi uhai pamoja na akili yake na uoni wake? Si ulikuwa si chochote?
Lakini Yeye Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu, wala si mshirikishi na yoyote.
Anaendelea kusema mumin, ama mimi nimeongoka kwa umbile langu na akili yangu kwa muumba wangu na muumba wa kila kitu na nimeamini kuwa Yeye pekee ndiye muumba mwenye kuruzuku.
Kisha muumin akamkumbusha yule kafiri neema ya Mwenyezi Mungu kwake na wajibu wa kumshukuru na kumsifu kwa kumwambia:
Na lau ulipoingia kitaluni kwako ungelisema alitakalo Mwenyezi Mungu huwa (mashaallah!), hapana nguvu ila kwa Mwenyezi Mungu.
Yaani lau ungelikuwa una busara ungelitambua kuwa kheri na fadhila ni kuongezeka ujuzi wako sio mali yako, ungeshindana na watu kwa maadili yako sio kwa jaha yako na kujua kuwa hapana hila wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Mwenyezi Mungu mmoja mwenye nguvu na kushinda.
Ni Yeye pekee ndiye anayetoa enzi na jahaa na kubadilisha utajiri kwa ufukara na ufukara kwa utajiri; alitakalo huwa na asilolitaka haliwi.
Ikiwa unaniona mimi nina mali kidogo na watoto kuliko wewe, basi huenda Mwenyezi Mungu akanipa kilicho bora kuliko kitalu chako na kukipelekea maafa kutoka mbinguni na kugeuka ardhi tupu inayoteleza; au maji yake yadidimie usiweze kuyagundua.
Mumin aliendelea kumjia juu kafiri kwa mali yake, akamwambia kuwa utajiri na ufukara unatoka kwa Mungu na wewe hujui mimi nina utajiri zaidi wa kukushinda wewe alioniwekea akiba Mwenyezi Mungu kwenye nyumba ya milele kushinda hivi vitalu vyako unavyojifaharisha navyo.
Hujui wewe kuwa Mwenyezi Mungu anaweza kunifanya tajiri mimi na kukufanya fukara wewe baina ya asubuhi na jioni.
Wewe unajigamba na mali yako, kwa sababu watu wanakusifia. Je sifa hizi ndio zitakukinga na mambo yanayofichwa na nyakati? Je, umejiaminisha na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu? Huogopi wewe na hivyo vitalu vyako kushukiwa na majanga kutoka mbinguni na ukabaki mtupu?
Yakaangamizwa matunda, akabaki anapinduapindua viganja vyake kwa vile alivyoyagharimia nayo imeanguka juu ya chanja zake.
Kupinduapindua viganja ni fumbo la kujuta. Mimea iliangamia, miti ikaanguka kila upande na maji yakauka mpaka tone la mwisho. Ardhi ikawa inateleza; kama kwamba hakukuwa na chochote.
Ufukara ukachukua nafasi ya utajiri, dhiki mahali pa faraja na udhalili na kuvunjikiwa mahali pa kujitukuza na kiburi. Haya ndio matunda ya ukafiri, dhulma na ufisadi – hasara na majuto ya juhudi na mali.
Akawa anasema: Laiti nisingelimshirikisha Mola wangu na yoyote.
Kama kwamba anakusudia, kwa kauli hii, kurudi kitalu chake, lakini wapi?
لَا يَنْفَعُ نَفْسًا إِيمَانُهَا لَمْ تَكُنْ آمَنَتْ مِنْ قَبْلُ أَوْ كَسَبَتْ فِي إِيمَانِهَا خَيْرًا ۗ {158}
Wala hakuwa na kundi la kumsadia kinyume na Mwenyezi Mungu wala mwenyewe hakuweza kujisaidia.
Kabisa! Hakuna ndugu wala rafiki au jaha wala mali, isipokuwa Mwenyezi Mungu.
قُلْ إِنِّي لَنْ يُجِيرَنِي مِنَ اللَّهِ أَحَدٌ وَلَنْ أَجِدَ مِنْ دُونِهِ مُلْتَحَدًا {22}
Huko usaidizi ni wa Mwenyezi Mungu, Mkweli. Yeye ni Mbora kwa malipo na mbora wa matokeo.
Huko ni ishara ya siku ya kiyama; yaani, ikiwa mtu katika maisha haya anapata wa kumtetea na kumsaidia, basi siku ya kiyama hatapata isipokuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) peke yake.
Na Mwenyezi Mungu yuko pamoja na wenye takua na amewaandalia ujira mwema na mahali pazuri.
وَاضْرِبْ لَهُمْ مَثَلَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا كَمَاءٍ أَنْزَلْنَاهُ مِنَ السَّمَاءِ فَاخْتَلَطَ بِهِ نَبَاتُ الْأَرْضِ فَأَصْبَحَ هَشِيمًا تَذْرُوهُ الرِّيَاحُ ۗ وَكَانَ اللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ مُقْتَدِرًا {45}
الْمَالُ وَالْبَنُونَ زِينَةُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَالْبَاقِيَاتُ الصَّالِحَاتُ خَيْرٌ عِنْدَ رَبِّكَ ثَوَابًا وَخَيْرٌ أَمَلًا {46}